Head teacher
JF-Expert Member
- Mar 10, 2012
- 1,796
- 411
Kuna gari ninataka kuinunua ina engine imeandikwa D4, ila ni 3S, mafundi wananitaadharisha nisinunue, itanisumbua. Hawaweki wazi tatizo lake. Msaada kwa wanaoifahamu, je ina matatizo gani?
Kuna gari ninataka kuinunua ina engine imeandikwa D4, ila ni 3S, mafundi wananitaadharisha nisinunue, itanisumbua. Hawaweki wazi tatizo lake. Msaada kwa wanaoifahamu, je ina matatizo gani?
Duh mkuu mbona kali hii kwenye jukwaa hili. Ngoja tuiondoe sasa hivi iende inakotakiwa
Ninachokumbuka ni kuwa hakuna mafundi wa uhakika wa gari zenye injini hiyo hapa nchini.
Hizo injin ni kama CDM unajua itakufa lakini haijulikani wakati gani. Epukana nayo kama watanzania wenye akili walivyo epukana na CDM.
Mod remove this ***** please
D4 ni (Direct injection 4 stroke engine) kwa Toyota na GDI (Gasoline Direct Engine) kwa Mitsubishi
Kampuni hizi mbili walikaa pamoja wakakubaliana kutengeneza engine yenye ufanisi mkubwa na kutumia mafuta machache na kufanya vizuri kwa spidi pia kuwa na emmision ndogo(euro 2-3),
Walichokifanya hapa ni kuruhusu injection iwe direct kama engine za diesel kwa ku-inject mafuta mengi kwa interval kwenye combustion chamber
Sasa shida inakuja watumiaji wa kwetu wanatumia mafuta ambayo si salama kwa engine husika ambayo inafanya kujaza mabaki ya carbon,wakati engine ikaperform sasa kwa kua inafanya kwa interval mafuta yanaenda kidogo kidogo inaanza kumiss na kupunguza nguvu na kwakua inatumia umeme,ikifanya hivyo mara kadhaa ina fail,ikifikia hapo lazima uivute,
sasa mafundi wetu hawajui hilo ama jinsi ya kutengeneza ikisumbua
Ushauri-usinunue
Nakushukuru kwa elimu uliyotoa na ushauri bora. Hapa ni kuachana nazo, isije ikainpata kama ilivyompata rafiki yangu mmoja mwenye gari furani, yapo machache sana hapa tz, yeye anatafuta fundi na spear, wanamwambia mafundi wapo Arusha na spear zipo nairobi, yaan ni taabu