Elections 2010 Endapo Kampeni ya kumzuia JK kugombea 2010...

Baada ya upelelezi wa kina wa muda sasa, vyanzo vyetu vimebaini kwamba, waziri wa mambo ya ndani, Mh. Lawrence Masha, akishirikiana na baadhi ya wabunge ndani ya CCM, wameanza kuandaa mikakati kabambe kumg’oa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2010.

Hadi sasa, Bw. Masha, tayari umeshaandaa viongozi katika kila Mkoa nchini watakao msaidia katika kampeni yake. Imebainika kwamba, Masha, akishirikiana na baadhi ya viongozi wanaoshutumiwa na ufisadi, wamekuwa wakikutana katika hoteli moja, nje kidogo ya jiji la Dar ili kubuni mbinu zaidi.

Wakisaidiwa na billionea mmoja, kadhalika kundi la Masha, limepanga kuwaonga wengi wa Wabunge ndani ya CCM ili kumuunga mkono, na habari za kumfilisi Mengi, ni habari za kumpiga JK changa la macho.
Mmoja wa wanakamati linaloongozwa na Masha mwenyewe kama mwenyekiti, ndiye aliyevuja hizi habari. Inasemekana huu ni mwezi wa 5 tangu hii shuguli ianze.

Kadhalika, Masha anaandaa kundi la wasomi walioko Uingereza ambao pia wanaandaa mikakati ya kujivutia ushindi dhidi ya JK. ……………….. tutawataarifuni na maendeleo zaidi.
 
Jamiiforums where we dare to talk openly!!! mafumbo ya nini? kama unamkanda weka mambo wazi hapa
 
sawa sawa kabisa,CCM Asili bado ipo ipo eeh!

Mkuu,
Vyanzo vyako wewe na nani? Kwanza hii ndiyo post yako ya kwanza.Nakuona umepost kisha umeganda hapo hapo kusikilizia.Yaani kuingia kwenye nyumba za watu tu kabla hujakaaribishwa ushaanza udaku? Au ndiyo kuvuta attention?

Kwanza nani kasema tupo tayari au tunatamani kuona CCM wakiparuana? Kwi kwi kwi!

Hata hivyo karibu sana hapa JF mkuu
 
sawa sawa kabisa,CCM Asili bado ipo ipo eeh!

Mkuu,
Vyanzo vyako wewe na nani? Kwanza hii ndiyo post yako ya kwanza.Nakuona umepost kisha umeganda hapo hapo kusikilizia.Yaani kuingia kwenye nyumba za watu tu kabla hujakaaribishwa ushaanza udaku? Au ndiyo kuvuta attention?

Kwanza nani kasema tupo tayari au tunatamani kuona CCM wakiparuana? Kwi kwi kwi!

Hata hivyo karibu sana hapa JF mkuu
tehe tehe huyu atakuwa mshikaji wake Masha wanaeshinda nae Rose garden.
 
Mkuu,
Vyanzo vyako wewe na nani? Kwanza hii ndiyo post yako ya kwanza.Nakuona umepost kisha umeganda hapo hapo kusikilizia.Yaani kuingia kwenye nyumba za watu tu kabla hujakaaribishwa ushaanza udaku? Au ndiyo kuvuta attention?

Kwanza nani kasema tupo tayari au tunatamani kuona CCM wakiparuana? Kwi kwi kwi!

Hata hivyo karibu sana hapa JF mkuu

tehe tehe huyu atakuwa mshikaji wake Masha wanaeshinda nae Rose garden

MKUU YOYOYO ULIJUAJE ???NDO ZAO KATUMWA HUYU ..KAONA WATU WAMEMKOMALIA MSHIKAJI KILA KONA.....................
 
Du hatari kweli kweli!sijui atakuwa nani at the end ila itajulikana tu maana mpira ni dk 90 ikibidi hata matuta lazima kitaeleweka tu!
 
Giving Jakaya another five years will be a disaster to the country. Kama ameshindwa hii mitano ya kwanza hiyo mingine atakuwa anaiba tu na wakina-Sinclair!! Mitano inamtosha ama sivyo ataifikisha nchi pabaya.
 
Giving Jakaya another five years will be a disaster to the country. Kama ameshindwa hii mitano ya kwanza hiyo mingine atakuwa anaiba tu na wakina-Sinclair!! Mitano inamtosha ama sivyo ataifikisha nchi pabaya.
 
Mheshimiwa Dr W Slaa alijaribu bila mafanikio kutaka bunge lijadili/lichunguze kama Waziri wa mambo ya ndani L Masha aliingilia mchakato wa zabuni ya vitambulisho vya taifa.kuna taarifa ambazo bado hazijakanushwa kwamba wabunge wa CCM walizuia kujadiliwa kwa hoja ya Mhe Dr W Slaa nje ya kanuni na taratibu za bunge,pengine wabunge wa CCM walielezwa faida za kuipiga nyundo hoja ya Mheshimiwa W Slaa ambazo watanzania wa kaiwada hatuzijui.
Mchakato wote wa vitambulisho vya taifa umejaa harufu ya rushwa tena mchakato wenyewe wala hakustahili kuwepo kwasababu mpiga chapa mkuu wa serekali alishaomba kupewa tenda kwa gharama ndogo ya shilingi bilioni 95 ikiwa ni pamoja na gharama za kununua mashine ya kutengeneza vitambulisho.
Gharama za kutengeneza vitambulisho kwa kuyatumia makampuni ya nje zitafikia shilingi bilioni 220 !.Tunahitaji mapofesa wa hesabu kutushauri tuachane na huu mradi na kama ni lazima ni kwanini tusimtumie mpiga chapa mkuu wa serekali.Mwaka 2005 watawala wetu walishinda kwa kishindo kwa kutumia EPA,mwaka 2010 watatumia vitambulisho vya taifa.
 
Mjadala mzuri. Ila mimi ningependa kuongezea tu kwenye baadhi ya post zilizowekwa na baadhi ya watu hapa.

Ukweli ni kwamba, 2010 hakuna mwana-CCM yeyote atakaeweza kumshinda JK licha ya kumng'oa kabisa asigombee kwenye uchaguzi wa ndani wa kuwania nafasi ya kugombea uRais kwa mara ya pili. Hakuna anaeweza kumshinda kwasababu, yeye ndie Mwenyekiti CCM na kiongozi wa vikao vyote vitatu vinavyochuja na hatimae kuchagua mgombea, hataweza kuachia hilo litokee.

Uwezekano pekee uliopo ni kama wananchi hawatamchagua. Hili la wananchi kutomchagua nalo si rahisi sana, japokuwa kura zitapungua sana mwaka huo kulinganisha na mwaka 2005.

Ningekuwa na uwezo, ningemuomba asigombee tena ili kulinusuru Taifa. Maana miaka mitatu imepita, na hali nzuri aliyoikuta sasa imekuwa mbaya kuliko inavyoweza kuelezeka. Inavyoelekea hakuna uwezekano wa kurekebisha hata kufikia hali iliyokuwepo (licha ya hali bora zaidi).

Baadhi ya ubaya wa hali hiyo ni kama ifuatavyo;

1. Makosa mbalimbali yanayofanywa (ya kiutendaji na kauli) na viongozi aliowateua bila yeye kuchukua hatua zozote (Upotovu wa maadili ya uongozi)
2. Inflation imekuwa kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha muda mfupi (hadi kufikia 13.5%)
3. Migogoro ya waalimu/wanafunzi, wazee wa EA, n.k. ambayo haijashughulikiwa bali imefunikwa.
4. Ufisadi uliobainika wa pesa nyingi sana za umma ambao hatua madhubuti hazijachukuliwa kukomesha na kuchukua hatua za kisheria. Hatua kidogo sana zimeshachukuliwa.
5. Migogoro ya Muungano imeshughulikiwa nusunusu na hivyo kuongeza ukali wa migogoro yenyewe (Zanzibar nchi au si nchi, Kamati butu ya kujadili masuala ya Muungano)
6. Hali duni za maisha ya kila siku ya waTanzania
7. Ahadi alizotoa hazijatekelezwa hata kidogo kwa kipindi kizima cha kwanza
8. Baraza kubwa la Mawaziri lisilo na tija n.k.

Ninavyoamini ni kwamba, atakapopitishwa tena na kuchaguliwa kuwa Rais, yafuatayo yatajitokeza;

1. Kesi nyingi za ufisadi zitafutwa na watuhumiwa kuachiwa huru
2. Marafiki zake waliopatwa na misukosuko watarudishwa madarakani na kupewa nafasi kubwa katika uongozi wa Taifa
3. Hali ya uchumi na ufisadi itazidi kuwa mbaya kwasababu ni kipindi cha kutokea, na atakuwa mgumu kuchukua hatua kali akihofia madhara yake atakapomaliza kipindi chake cha uongozi, na fisadi kuchukua nchi
4. Kigugumizi cha OIC na Kadhi Mkuu hakitakuwepo tena, hivyo ataamua (liwalo na liwe)
5. Ahadi zozote atakazo kuwa amewahi kuzitoa itakuwa ndio mwisho wake.
 
Naomba tuzungumzie yeye binafsi akikataa kugombea kwa mhura wa 2 je nchi itakaaje?
Je demokrasia itachukua mkondo wake?
 
Naomba tuzungumzie yeye binafsi akikataa kugombea kwa mhura wa 2 je nchi itakaaje?
Je demokrasia itachukua mkondo wake?

Mkuu Fidel80, endapo akikataa kugombea kwa ridhaa yake mwenyewe, sidhani kuwa kuna madhara yoyote yatakayotokea. Madhara yanaweza kutokea ndani ya CCM (tu), endapo atalazimisha chama chake kimchague mtu atakaemtaka yeye, na ambae hatakiwi na wengine wengi katika chama.

Kitaifa hakutakuwa na madhara yoyote. Ni imani yangu pia kuwa, chama kitaweza kujipanga upya na kuteua mgombea atakaekubalika zaidi, mwenye uwezo wa kufanyakazi kwa uadilifu zaidi, mwenye nia ya kuendeleza nchi vizuri zaidi, na mwenye uwezo wa kuiunganisha CCM tena. Mtu huyo atakuwa na changamoto kubwa za kuinua uchumi unaoanguka na kusimamia misingi ya utawala bora na wa kisheria vizuri zaidi. Taifa halitegemei nani anaeongoza nchi, bali anaeongoza nchi ana uwezo gani na nia gani ya kuiongoza kuelekea kwenye maendeleo yanayokusudiwa (kwa vitendo).
 
Mzee Mwanakijiji inawezekana unayosema yanabeba maji kiasi fulani. Lakini unatakiwa kutambua kuwa maneno hayo yalisemwa wakati mwalimu alipokuwa aking'atuka. Uzuri hayajasemwa wakati Mkapa amemaliza muda wake, simply kwa sababu watu wameanza kugahamu kuwa rais sio Mungu.
Sasa hivi de facto CCM imegawanyika, CCM mtandao (aka mafisadi) bado ipo na CCM asilia waliofanyiwa fitna na wanamtandao bado wapo. Kimsingi CCM sasa hizo ziko mbili. Pamoja na misukosuko yote bado tunasonga mbele na tutaendelea kusonga mbele.
CCM itakapoparaganyika ndipo wanaCCM na watanzania wengine tutakaporudi kwenye akili zetu na kutambua kuwa Tanzania ndio mama yetu na sio CCM. Ndipo maslahi ya taifa yatakuwa na maana zaidi kuliko maslahi ya CCM na watu wachache ndani yake. Na ndipo maendeleo ya kweli (sio porojo) yataanza kuonekana.
 
...JK ni mdhaifu kukiwa na kelele nyingi za namna hiyo,kwa hiyari yake mwenyewe anaweza kusema "Mimi sasa basi!! Mwanachama mwingine mwenye uwezo aendeleze kazi hii"...

JK kama akifikia maamuzi ya kutogombea hatakuwa mdhaifu. Akiacha kugombea ataacha historia kubwa sana katika uongozi, na kuondoka kwake kutaleta mabadiliko ya msingi sana katika maadili ya uongozi wa Tanzania.
Lakini, mimi naona JK kuacha Uraisi kwa hiari itakuwa ngumu kwake, hata kama anania ya kuacha amekabwa kooni. Mazingira yamekaa vibaya sana kwake, na kama anajiuliza swali basi itakuwa atachajeachaje! Usalama wake upo wapi! Akiacha anafanya nini! Atapona na vita ya ufisadi? Atakuwa nani - atapewa chamani - ama siasa ndio basi! Atajieleza nini kwa chama chake na wananchi kwinini hagombei tena?

Raisi wetu bado kijana jamani! Akijitoa kwa kashifa hata kitabu chake kinaweza kisinunulike, atafanyi nini asipokuwa Raisi? Je jamii itamuenzi ama ndio mwisho wake! Akiamua kuacha wewe mwananchi utamhukumu vipi? Lakini la ziada, anaielezea vipi nafsi yake kwamba ameshidwa kuwa kiongozi! Familia yake itamuonaje. Ni uamuzi mgumu jamani! Wananchi mtampa kifuta jasho?

Mambo ndio kwanza yamepambazuka! Sababu za kugombea kwake ni chache kuliko maswali atakayopaswa kujibu! Chama anacho! utamaduni wa chama unamruhusu, wapiga kura wake vijiji wanaweza kumpa kura! Kama binadamu wakawaida ambaye hana hakika na salama yake, lazima agombee kujilinda na kashfa na ghadhabu ya wananchi!

Lakini je akisema hagombei 2010 utamhukumu, ama kumpa shahada?
 
Kwanza mkuu hiyo kauli ya kuwa JK ni kijani si sahihi, pia hata kama ni kijana basi akili zake zimezeeka kitu ambacho ni kibaya zaidi afadhali angezeeka mwili but brain iwe safi. JK kutokugombea 2010 kwake ni afadhali zaidi kuliko kungangania mpaka 2015. I tell you what happened Madagascar ndio mwendo wa ulimwengu wa sasa and may be soon Bongo sasa kipi bora aachie ngazi 2010 or yamkute ya madagascar. Vile vile mpaka 2015 kutakuwa na mabadiliko makubwa sana ya kisiasa nchini hivyo hata akisurvive mpaka 2015 anaweza ishia segerea for the rest of his life.

Kama anamaswali kama yako namshauri aachie ngazi fast tena 2010 kwa hiari yake bila kulazimishwa. Watanzania vile vile JK akichukua form ya urais 2010 solution ni kuitisha maandamano kupinga uamzi wake hata kama ni wakikatiba.
 
Back
Top Bottom