RedDevil
JF-Expert Member
- Apr 30, 2009
- 2,367
- 1,519
WanaJF, Juzi kuna jamaa yangu katuma mzigo wake kwa mke wake kupitia EMS services na kulipia hela kibao kutoka huku ughaibuni. Mzigo umefika, mwenye kuupokea kapigiwa simu aende akachukue mzigo, alipofika pale ofisi za EMS kaambiwa alipe fedha za clearance ya hicho kifurushi, huyo bwana aliyeenda kuchukua mzigo basi akashtukia dili akakomaa hadi wakampa bila malipo yeyote.
Zamu imekuja kwangu, nimetuma mzigo kwa mchumba wangu kutoka huku ughaibuni, kama kawaida nikalipa pesa nyingi zaidi ya thamani ya mzigo, nikautuma. Cha ajabu mzigo ulifika mapema lakini hawakupiga simu hadi mimi mwenyewe nimetrack mzigo na kupata taarifa kuwa mzigo umemiss delivery. Cha ajabu kaenda kuulizia mzigo anaambiwa alipe Tsh 15900 kwa ajili ya kuhifadhia huomzigo. Ikabidi alipe baada ya kuanza kubishana kwa muda, lakini kabla ya hapo nilishawahi kutuma mizigo kibao na kupokelewa bila malipo ya ziada.
Ndugu zangu, najiuliza kuna nini siku hizi EMS - Posta au ndo ufisadi? naombeni mnisaidie kunielewesha maana hapa nawashangaa EMS badala ya kumbembeleza wateja,wao wanasema hata usipokuja.