Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 54
Recta
Wapinzani wangeibaje kura wakati wizi unategemea kushirikishwa Polisi, Jeshi na NEC? Kutokana na mfumo uliopo, Polisi, Jeshi na NEC wako upande mmoja na CCM. Ni juzi juzi tu maofisa wote wa ngazi za juu wa vyombo vya ulinzi na usalama walikuwa wanatakiwa kuwa wana CCM.
Kwani vyama vya upinzani Zambia na Kenya ni tofauti sana na vya kwetu? Mbona vimeshinda?
Swala la msingi kwa Recta na wengine hapa ni hili: Mtasemaje CCM haibi kura na huku mnakubali iliba ushindi Zanzibar 1995?
Augustine Moshi,
Mimi nadhani hili la kuiba kura halina uzito mkubwa sana ukilinganisha idadi ya viti ambavyo CCM wanavipata. Kama tutaendelea kujadili suala ni kwamba CCm wanashinda kwa sababu wanaiba kura hatuwezi kuona haya mambo katika uhalisia wake. Ni vema kama tunataka kuweka suala la kuiba kura basi ni kwamba inabidi tuje na data za uhakika ambazo zita-support hoja na kuonesha ni viti vingapi vilichukuliwa kwa kuiba kura.
kimsingi ninachotaka kusema ni kuwa kuna sababu ambazo baadhi ya wachangiaji kwa mapenzi yao kwa chama fulani au maono yao binafsi, hawataki kujadili na kukubali kuwa baadhi ya sababu nilizozitoa hapo juu ndiyo zinazochangia ushindi wa kimbunga wa CCM. Kwa mantiki hiyo basi, ni vema wale wote wanaogombea kiti na CCM wakaelewa hilo na kuwa na mikakati mdabala ya kuwawezesha walau waweze kufurukuta. Kwa mfano kule Mbeya unaweza kusema kuliibiwa kura? au Mramba aliiba kura? Tuangalie pia ni nani amasimamishwa kugombea na CCM. Baadhi ya wagombea wa upinzani kusema kweli hawauziki hata kwa senti moja, na kwa vile uchaguzi ni wa kidemokrasia basi kura nyingi hupewa yule ambaye wananchi wanamtaka.
Jambo lingine ni kwa baadhi ya vyama vyenyewe, vinakwenda kwenye uchaguzi ilihali havijui vinataka kuifanyia nini hii nchi jambo gani, kama unataka kupata kushinda, basi eleza yale ambayo kweli mtayafanya au kuyarekebisha na wala siyo kwenda kuwatisha wananchi au kupandikiza chuki wachukie serikali yao. Wananchi wanasikiliza na baadae hufanya maamuzi ambayo matokeo nadhani wote tunayajua.
Hata siku moja wapinzani wasiendelee kufanya makosa kwa kutumaini kuwa wataingia madarakani kwa huruma ya wananchi, no way. Na wala wasitegemee ikifika wakati wa uchaguzi CCM itawaonea huruma, no way.