Email from James - Jeddah

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
21,229
36,245
Habari za mwisho wa wiki mabibi na mabwana wa MMU,

Leo nawasimulia kisa kilichonitokea kuanzia wiki iliyopita………….

Jumanne iliyopita ya tarehe 2/02.2016 saa nne asubuhi, Kasie nilipokea barua pepe kutoka kwa mwanajeshi aliyejitambulisha kwa jina la James kuwa yeye ni mtanzania anayeishi Jeddah (sijajua vizuri Jeddah ni nchi ya kiarabu au laah hata sikujisumbua kuitafuta kwenye mtandao (gugo).

Alikuwa ananiuliza habari za kikazi maana mie asili ya kazi ninazofanya ni kuhudumia wateja, baada ya kumalizana na kumhudumia kwa njia ya barua pepe nikajua vimeishia pale maana huwa nahudumia wateja wengi. Kwenye barua pepe yangu nimeweka saini ya jina langu, anuani, na namba ya simu ya mkononi na ya mezani ya ofisini. James kumbe akaihifadhi namba ya ngu ya simu ya mkononi na kuanza kuniangalia kupitia mtandao wa whattsapp. Kumbuka shida yake iliisha siku ile ile jumanne ya tarehe 2 kwasababu alijibu name nikajibu hadi tulipoelewana na kuridhika kuwa shida yake imeisha.

Alhamisi jioni nikapokea simu iliwa haina namba wala jina na hata ile application ya caller identity haikufanya kazi kuniletea jina kuwa huyu ni flani. Nilipokea simu ile na sauti ilikuwa uuuuuh maashaalaaaah!!!!

Mazungumzo yakaanza na alijitambulisha kwangu na moja kwa moja akasema shida yake anaomba urafiki na mimi. Nikamjibu nina mpenzi wangu akasema sihitaji kuwa mpenzi wako naomba urafiki na wewe. Nikaguna akasema najua hunielewi ila naomba uniruhusu niwe rafki yako na hutojutia.

Kwakuwa sikuwa na mpango nae nikamwambia sawa ili niachane nae, ijumaa asubuhi ya tarehe 5.02.2016 akaanza mawasiliano ya whattsapp mmmmmmmmmmmmmhhhhhhhhh, ………………………………. Hadi sasa hivi nilichokigundua ni kuwa kuna vitu sio vya kujaribu maana ukiingia huwezi kutoka hata uwe mgumu vipii.

Hapa nilipo leo nimetoka kupata breakfast na James Kempisk na Lunch pia tulipata hapo hapo Kempisk Hotel zamani Kilimanjaro Hotel. James amekuja jana na amefikia hotel hiyo yaani mtihani nilionao ni weekend hii ntapona kweli…………………………..

James ni mwanajeshi yuko Jeddah kikazi na anaishi huko, alioa na akaachana na mkewe na wana watoto 2 ambao wanaishi na mama yao. Sijelewi hadi dakika hii kuwa itakuwa ni CRUSH kama crush nyingine zilizopita, one night stand au ndo nimetumbukia tundu bovu……………………..

Hapa ndo najiandaa kutoka kazini maana kasema dinner pia kwake hapo hapo Kempisk ila nikamwambia ntarudi kulala kwangu lakini hata sijui kitakuweje.

Nawapenda sana MMU hata sielewi elewi naogopa hata kunywa wine………

HINT: James ni msukuma…………..

Ntawataarifu kilichojiri mkiona kimya mjue nimekuwa terrorized au nimenyoywa damu na mumiani James. Ikitokea sitatokea tena hapa jukwaani mjue kuwa nawapenda sana na laah sina la kusema. Sina mume, wala mtoto wala shosti wa kunisindikiza ila nyie ndo watu wangu wa karubu nimeona niwaelezee ili mkisikia loote muwe na pa kuanzia.

Nawapenda mnooo wana MMU,


Kasie.
 
Kama nakuona vile unavyotamani hii thread members wasiione au ifutike bahati mbaya bwana James.

Ah wapi!

Nshazoea.

Kuna wengine wanaamini mimi naitwa Richard Mugizi na 'ushahidi' wanao.

Wapo wanaoamini mimi ni nina miaka 59, 62, 69, na kadhalika, na 'ushahidi' wanao.

Wengine wanaamini mimi namiliki 'ma apartments' huko Msasani, Masaki, na Mtwara huko kwa Dangote' na ushahidi wanao.

Hivyo kusema ukweli nshazoea.

Ngoja tu nitulie nione kitachojiri ingawa nina wasiwasi tayari nimesha ki-preempt.....
 
Wala usiogope we nenda Kamuhudumie mteja(James) kama ulivyokuwa unavyoWahudumia hao wateja wengine
 
Nimerudia tena kusoma na nimefurahishwa na uandikaji wako [@Kasinde] wa Kiswahili bila kuchanganya sana na Kiingereza.

Hapo kwenye 'breakfast' na 'lunch' ungetumia 'staftahi' na 'chakula cha mchana' basi ningekupa 98% kati ya 100% ambayo ni A+.
 
Ndugu Zako Umewaambia?
Waje Kuchukua Bloodless And Lifeless Body Of Yours Hapo Kempinski Should It Happen.
Kama Bado Basi Ungeanza Na Wao Ndo Uje Ku-Show Ofd Hapa.
KUDOS!
 
umeanza na breakfast,,. lunch..utaeda badae kupata dinner,...askari yeyote anajua kuna kitu inaitwa UP..hapo huchomoki lazima ukakione kitanda chake then muoneshane uchi
 
Mambo vp mkuu?
Naona upepo upo upande wako this time.

Hoist your colors
 
Mambo vp mkuu?
Naona upepo upo upande wako this time.

Hoist your colors

Paw hapo umemsalimia nani sasa?

Au umemsalimia mtu niliyemsweka kwenye 'ignore list' yangu ndo maana sioni uliyemnukuu [kama umemnukuu mtu]?
 
Back
Top Bottom