Elimu yetu itashuka mpaka serikali ya CCM mtakapoamua kuwajali walimu

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,667
1,566
Jana baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha nne ambapo katika matokeo hayo ufaulu umeonekana kushuka kwa zaidi ya asilimia moja.

Pia katika matokeo hayo, hakuna shule yoyote ya serikali iliyoingia katika shule kumi bora zilizofanya vizuri.

Najua watakuja na sababu nyingi, watatueleza mengi zaidi. Kinachonikera mimi ni kuukwepa ukweli na kutoa sababu ambazo hata wao wanajua kwamba ni uongo.

Watatuambia labda ni mabadiliko ya mfumo wa utunuku wa alama, uchache wa walimu w sayansi nk.

Ukweli ni kwamba walimu wa taifa hili wamesuswa, walimu wa taifa hili wanamigomo yao ya rohoni, wanafanya kazi wakiwa na vinyongo vingi moyoni.

Mwalimu wa diploma anayeanza kazi anaanza na Mshahara TGTSC ambapo ni shilingi 532,000 (basic salary) ambapo baada ya makato mwalimu anapata 430,000.

Mwalimu wa ngazi ya cheti (primary school) anaanza na TGTSB ambapo ni sawa na 389,000 (basic salary) ambapo baada ya makato anapata 287,000.
Hii ni mifano tu, kwa hali hiyo mwalimu anaishi vipi. Mwalimu anatakiwa alipie nyumba, usafiri, nk.

Tuache kuzunguka, iwapo serikali ya CCM, wanataka kuinua kiwango cha elimu basi tujali walimu kwanza.

Tutoe hata teaching allowance kila mwezi kwa walimu walau laki mbili kwa kila mwezi.
 
Wasipowakumbuka walimu hakuna la ziada... if course wapo kwenye mgomo baridi
 
Kama mimi ningekuwa magufuli, walimu wangekuwa ni kipaumbele changu cha kwanza. Kwa kuwa walimu ndiyo wanaotuzalishia rasilimali watu
 
Nakubaliana kabisa na mtoa mada. Ni ndoto nchi kupata maendeleo makubwa ya kweli bila elimu nzuri kwa wananchi wake inayofundishwa na waalimu wanaolipwa vizuri. Waalimu katika taifa hili wamepuuzwa kwa muda mrefu sana. Maslahi duni yamewaondolea ari ya kufundisha na kufanya elimu yetu kuwa duni.

Ikiwa tunataka kupata wataalam wazuri watakaoliletea taifa letu maendeleo endelevu lazima tuwathamini waalimu. Tunaweza kununua maendeleo kwa raslimali tulizonazo lakini hayo si maendeleo endelevu. Maendeleo tuyatakayo yatoke vichwani mwa watz walioelimika. Hii inaanzia kwa waalimu wanaothaminiwa kwa kulipwa vizuri. Mimi si mwalimu ila natambua mwalimu ndo kila kitu.
 
Jana baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha nne ambapo katika matokeo hayo ufaulu umeonekana kushuka kwa zaidi ya asilimia moja. Pia katika matokeo hayo, hakuna shule yoyote ya serikali iliyoingia katika shule kumi bora zilizofanya vizuri.
Najua watakuja na sababu nyingi, watatueleza mengi zaidi. Kinachonikera mimi ni kuukwepa ukweli na kutoa sababu ambazo hata wao wanajua kwamba ni uongo. Watatuambia labda ni mabadiliko ya mfumo wa utunuku wa alama, uchache wa walimu w sayansi nk.
Ukweli ni kwamba walimu wa taifa hili wamesuswa, walimu wa taifa hili wanamigomo yao ya rohoni, wanafanya kazi wakiwa na vinyongo vingi moyoni.
Mwalimu wa diploma anayeanza kazi anaanza na Mshahara TGTSC ambapo ni shilingi 532000 (basic salary) ambapo baada ya makato mwalimu anapata 430000.
Mwalimu wa ngazi ya cheti (primary school) anaanza na TGTSB ambapo ni sawa na 389000 (basic salary) ambapo baada ya makato anapata 287000.
Hii ni mifano tu, kwa hali hiyo mwalimu anaishi vipi. Mwalimu anatakiwa alipie nyumba, usafiri, nk.
Tuache kuzunguka, iwapo serikali ya ccm, wanataka kuinua kiwango cha elimu basi tujali walimu kwanza.
Tutoe hata teaching allowance kila mwezi kwa walimu walau laki mbili kwa kila mwezi.
sasa tunaambiwa waalimu watakuwa wanasafiri bure, je ni dar tu, au tanzania nzima? kweli hapo kuna kukurupuka
 
Ninyi waalimu, hembu acheni kulalamika lalamika. Hivi huo mshahara unaosema mdogo, ni mdogo ukilinganisha na taaluma ipi?. Sasa wewe ni mwalimu wa ngazi ya certificate, unataka upate mshahara shilingi ngapi? Jamani hembu tuache huu ubinafsi na tuzingatie hali halisi. Umefuatilia watu wa taaluma nyingine walioajiriwa halmashauri wanalipwa shilingi ngapi?, au mmekalia kulalamikia mambo ambayo mnaujua ukweli bali mnajifanya mnatizama mbali ya huo ukweli?
Wewe kama ni mwalimu wa Certificate, nenda shule upate Diploma, na kisha nenda shule upate Degree. Sasa umekaa unalalamika, ukiambiwa uende ku re-seat mtihani hutaki, halafu unakaa unalalamika na kumuonea wivu mtu alietaabika kusoma PCB, akaenda akasoma udaktari 5YRS, kisha akaenda Internship 1 yr. Au engineer aliyesoma aliyekomaa na PCM, kisha 4 yrs at the COET. Huo unakuwa ni wivu usiokuwa wa maendeleo, Kabla hujalalamika, hembu kwanza fikiria una sifa gani? na ufaulu wako upoje? halafu kisha ndipo either uamue kukaa kimya au kulalamika. Sawa ndugu zangu waalimu?
 
Hata uingereza shule za serikali zipo chini kidogo ya binafsi,,nyie wadau mmefanya nini kusaidia watoto wenu kielimu na elimu kwa jumla
 
Jana baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha nne ambapo katika matokeo hayo ufaulu umeonekana kushuka kwa zaidi ya asilimia moja. Pia katika matokeo hayo, hakuna shule yoyote ya serikali iliyoingia katika shule kumi bora zilizofanya vizuri.
Najua watakuja na sababu nyingi, watatueleza mengi zaidi. Kinachonikera mimi ni kuukwepa ukweli na kutoa sababu ambazo hata wao wanajua kwamba ni uongo. Watatuambia labda ni mabadiliko ya mfumo wa utunuku wa alama, uchache wa walimu w sayansi nk.
Ukweli ni kwamba walimu wa taifa hili wamesuswa, walimu wa taifa hili wanamigomo yao ya rohoni, wanafanya kazi wakiwa na vinyongo vingi moyoni.
Mwalimu wa diploma anayeanza kazi anaanza na Mshahara TGTSC ambapo ni shilingi 532000 (basic salary) ambapo baada ya makato mwalimu anapata 430000.
Mwalimu wa ngazi ya cheti (primary school) anaanza na TGTSB ambapo ni sawa na 389000 (basic salary) ambapo baada ya makato anapata 287000.
Hii ni mifano tu, kwa hali hiyo mwalimu anaishi vipi. Mwalimu anatakiwa alipie nyumba, usafiri, nk.
Tuache kuzunguka, iwapo serikali ya ccm, wanataka kuinua kiwango cha elimu basi tujali walimu kwanza.
Tutoe hata teaching allowance kila mwezi kwa walimu walau laki mbili kwa kila mwezi.
Wapo wanaofikri vitisho na sheria kali ndizo zitakazombana mwalimu...Hao hujikita kukagua andalio la somo na mpango kazi wa mwalimu wa mwaka. Inawezekana ni muhimu lakini mimi naamini inamchango mdogo sana. Mwalimu ni anacheza na akili za binadamu ambao wanatofautiana uwezo wa kuelewa. Ili afanikiwe ni lazima ajitume na awe tayari kutumia hata njia za ziada ikibidi hata mda wake wa ziada. Hata ukikaa nyuma kumkagua bado haisaidii labda ukae kila siku.

Wakuu wa shule wengi kazi yao ni kusafiri ili wajipatie pesa. Utaratibu uliandaliwa unaotwa shirikishi wa matumizi ni shida kwa maana ya kuwa shirikishi huwa ni tata "PARADOX OF PARTICIPATION". Ni lazima serikali iangalie upya manufaa na nafasi ya mwalimu. WALIMU WENGI HAWAPO SAWA KISAIKOLOJIA. HIVYO WANAUMWA( rejea maana ya health ya WHO). Serikali tibuni walimu.
 
Jana baraza la mitihani Tanzania limetangaza matokeo ya kidato cha nne ambapo katika matokeo hayo ufaulu umeonekana kushuka kwa zaidi ya asilimia moja. Pia katika matokeo hayo, hakuna shule yoyote ya serikali iliyoingia katika shule kumi bora zilizofanya vizuri.
Najua watakuja na sababu nyingi, watatueleza mengi zaidi. Kinachonikera mimi ni kuukwepa ukweli na kutoa sababu ambazo hata wao wanajua kwamba ni uongo. Watatuambia labda ni mabadiliko ya mfumo wa utunuku wa alama, uchache wa walimu w sayansi nk.
Ukweli ni kwamba walimu wa taifa hili wamesuswa, walimu wa taifa hili wanamigomo yao ya rohoni, wanafanya kazi wakiwa na vinyongo vingi moyoni.
Mwalimu wa diploma anayeanza kazi anaanza na Mshahara TGTSC ambapo ni shilingi 532000 (basic salary) ambapo baada ya makato mwalimu anapata 430000.
Mwalimu wa ngazi ya cheti (primary school) anaanza na TGTSB ambapo ni sawa na 389000 (basic salary) ambapo baada ya makato anapata 287000.
Hii ni mifano tu, kwa hali hiyo mwalimu anaishi vipi. Mwalimu anatakiwa alipie nyumba, usafiri, nk.
Tuache kuzunguka, iwapo serikali ya ccm, wanataka kuinua kiwango cha elimu basi tujali walimu kwanza.
Tutoe hata teaching allowance kila mwezi kwa walimu walau laki mbili kwa kila mwezi.
sisi kina gogo la shamba tulishasema waalimu wa nchi hii hawana tofauti na masheikh Ubwabwa ubongo wa samaki kama alivyowai kusema Karume
 
elimu yetu haiwezi kukaa vema mpaka watoto wa kina ndalichako, magufuli, samia, na majaliwa watakapoanza kusoma kwenye shule za serikali kama zamani. Tuwe nao mle Tambaza, Jangwani, Tabora na kwingineko.

pia zamani mchujo wa kuingia form one haukuwa wa mchezomchezo
 
Sasa hiv hata tution makufuli kafuta ....walim wanaisoma namba ...maisha magum na ccm inaendelea wadharau
 
Back
Top Bottom