Elimu yangu imegeuka kero mtaani.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,828
Nimesoma kwa shida na taabu nyingi, misukosuko na dhoruba ndizo zinazo endelea kunisonga tangu nikiwa mdogo, labda rabsha hizo kwa kizungu ndio huitwa challenges.
Mtaa ninaoishi ni wa hali ya chini, namshukuru Mwenyezi Mungu nilisha wahi kuvaa joho na kikofia, pia kushikana mkono no rais kwenye mahafali (majaoho huvaliwa hata kwenye graduu za chekechea, lakini wahadhiri hawahudhurii)
Sipendi watoto wa leo wapite mapito niliyopitia, kwa hiari nimeamua kuwa MWALIMU WA HIARI MTAANI.
Kama mjuavyo, maduka ya Uswahilini kama sio la Mpemba basi ni la Mchaggah.
Leo nilikuwa nikimuuliza mtoto wa Mchagga muuza duka hesabu za mara a.k.a tebo a.k.a hesabu za kuzidisha.
Baba na mama muuza duka wakanijia juu, kwa nini namuuliza mtoto wao maswali wakati sichangii katika ada wala hela ya daftari?
Nimeporomoshewa matusi hadi nimekoma, sijui ni wapi tunalipeka hili taifa.
Wazazi wamewaka eti naringia degree yangu, wamesema degree yangu ni ya kuunga unga, sijui kusoma wala kuandika.
Wanajinadi hili taifa limeuzwa kwa wenye hela, ukiwa na hela unafanya utakalo.
Waweza kununua cheti kuanzia cha msingi hadi cha chuo , hata kama mwanao hajui kusoma wala kuandika.
Kwenye udhia penyeza rupia.
Baada ya kusikia maneno hayo nikasikia kuzimia.
Hakika Elimu na mwamko wangu wa kuelimisha jamii vimeniponza mtaani.
 
Watu hawajakuelewa tu.....................Afadhali wewe umeona umuhimu wa kuhakikisha wenzako hawapiti kwenye magumu uliyoyapitia.............Kuna wengine kwanza ndio wangekuwa wanawasimanga wenzao.
 
Juzi alikuja na store ya kuaga kwenda kujisaidia kumbe kaishia baa
hadi akalishwa nyama ya mbwa,
leo kaja na

"kwa hiari nimeamua kuwa MWALIMU WA HIARI MTAANI"

Ole wako nyie waalimu vizee wa tuisheni mna tabia ya kula
watoto wa shule ole wako na ndipo utakapojua hata lile
joho lako la kuunga unga siyo mali.

But pole sana mkuu buji.

.
Is this a real story?? napata shida kuiamini
 
Hahaha! Hicho chuo ulichosoma lazma cha wasabato. Kadigrii ka kwanza na ka pili huwezi shikwa mkono na mgeni rasmi bwana! Labda ka-phd!

Sasa ww sio mhaya wala mndukulukudusucho, utakuwa mwana ccm! Kwa kuuliza hesabu za table ndo unaokoa maisha ya hao jirani uswazi? Huna tofauti na anaehubiri maisha bora kwa kila mdanganyika na kumgawia kilemba na khanga nyepesi!
 
Mmmh Shem, huna kabila lingine la kuulizia ?
Mbona waulizia hilohilo ?
Una allergy nalo nini ?
Shem una vituko! Unakumbuka hata mie uliniuliza same quiz!

Hahah Judgement, sio hivyo..koz kama mshkaji mhaya nadhani anajifagilia tu hapa kama ilivyo hulka yao.
 
Last edited by a moderator:
Nimesoma kwa shida na taabu nyingi, misukosuko na dhoruba ndizo zinazo endelea kunisonga tangu nikiwa mdogo, labda rabsha hizo kwa kizungu ndio huitwa challenges.
Mtaa ninaoishi ni wa hali ya chini, namshukuru Mwenyezi Mungu nilisha wahi kuvaa joho na kikofia, pia kushikana mkono no rais kwenye mahafali (majaoho huvaliwa hata kwenye graduu za chekechea, lakini wahadhiri hawahudhurii)
Sipendi watoto wa leo wapite mapito niliyopitia, kwa hiari nimeamua kuwa MWALIMU WA HIARI MTAANI.
Kama mjuavyo, maduka ya Uswahilini kama sio la Mpemba basi ni la Mchaggah.
Leo nilikuwa nikimuuliza mtoto wa Mchagga muuza duka hesabu za mara a.k.a tebo a.k.a hesabu za kuzidisha.
Baba na mama muuza duka wakanijia juu, kwa nini namuuliza mtoto wao maswali wakati sichangii katika ada wala hela ya daftari?
Nimeporomoshewa matusi hadi nimekoma, sijui ni wapi tunalipeka hili taifa.
Wazazi wamewaka eti naringia degree yangu, wamesema degree yangu ni ya kuunga unga, sijui kusoma wala kuandika.
Wanajinadi hili taifa limeuzwa kwa wenye hela, ukiwa na hela unafanya utakalo.
Waweza kununua cheti kuanzia cha msingi hadi cha chuo , hata kama mwanao hajui kusoma wala kuandika.
Kwenye udhia penyeza rupia.
Baada ya kusikia maneno hayo nikasikia kuzimia.
Hakika Elimu na mwamko wangu wa kuelimisha jamii vimeniponza mtaani.
nilijua hicho kifront fromt ni huku jf tu kumbe unakipeleka mpaka mtaani tena shukuru hao waliokutunana wakakuacha wengine wanakuzungusha mtaani ukiongea kingereza wee mwishowe unalaa jalalani .Pole bujibuji
 
Hadi vijijini siku hizi wanajua nini maana ya elimu
hao wanaofokea mtoto wao kufundishwa sijui akili zao zimejaa matope?
 
buji unatafuta kurogwa?

Back
Top Bottom