Elimu ya Tanzania na Education for ignorance! Kweli hawa nao ni wasomi au makapi?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
6.jpg
Hilo ni bango mojawapo kati ya yale yaliyobebwa na wanaoitwa wasomi wa vyuo Tanzania! Inasikitisha licha ya kukera. Je hawa ni wasomi kweli au waganganjaa wanaoweza kutumiwa na fisadi yoyote awe mtu au chama kufikia malengo yake. Usomi maana yake ni uasi siyo ukondoo, ukuku wala upunda.
 
Mkuu hawa vijana vijana wana haki kikatiba ila inasikitisha kwamba wapo kusikostahili. Nadhani ni njaa tu zinawasumbua hawa vijana wetu. Nadhani wanamaanisha kuwa wale waliohama ccm ndo magamba. Kama ndivyo nadhani wanakosa uelewa maana hakuna ushahidi kuwa ni magamba na wala hakuna vithibitisho. Kwa kuwa ni falsafa ya wachache kuwa kila anaehama ni gamba basi ha hawa vijana wamo kwenye huo mkumbo wa kuchafua wengine kwa majibu mepesi.
 
Kusoma na kupata elimu ni vitu viwili tofauti. Unaweza ukasoma na usipate elimu, si unakumbuka mwaka 2010 kule UDOM baadhi ya wanachuo walichangishana pesa ili kumsaidia JK achukue fomu ya kugombea urais baadae kidogo wakaanza kuandamana kudai mkopo wakaambulia mabomu. Kweli funzo la mjinga ni tabu.
 
Back
Top Bottom