Elimu ya sasa ya sekondari na ya enzi za mwalimu,ipi bora

BUMIJA

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
5,818
11,001
Viongozi wengi waliosoma kipindi cha nyuma ndo wengi wana vyeo,kazi nzuri je unathani Elimu ya kipindi hicho ilikua bora kushinda sasa
 
Viongozi wengi waliosoma kipindi cha nyuma ndo wengi wana vyeo,kazi nzuri je unathani Elimu ya kipindi hicho ilikua bora kushinda sasa

Bila shaka ilikuwa poa, maana vijana wa dot kom mkimpeleka ikulu atagoma, ukimpa ukuu wa mkoa atagoma, ukimpeleka kwenye bongo F ndio mwake, maana ni kizazi migomo.
 
Nzowa nimekupata,hasa dent wa ud ukimpeleka ikulu ni fujooooo,wakorofi cjui kwa nini+
 
Hilo halina ubishi ingawa waliopata fursa walikuwa wachache. Sababu za ubora zilitokana na haya yafuatayo:

1) Waalimu walioiva kitaaluma, wenye maadili ya ualimu na wanaojituma.
2) Idadi mufaka ya wanafunzi katika darasa: Enzi hizo darasa lilikuwa halizidi wanafunzi 45.
3) Upatikanaji wa vifaa vya kufundishia hasa masomo ya sayansi: Enzi hizo hata shule za msingi zilikuwa na vifaa vya kufanyia majaribio, kama test tube, beakers, n.k.
4) Mitaala iliyoimara na isiyobadilikabadilika: Enzi za mitihani ya Cambridge syllabus ilikuwa ya Afrika Mashariki nzima. Hata miaka ya mwanzo baada ya Uhuru mambo yalikuwa mazuri mpaka walipoanza kujichanganya na mabadiliko ya mara kwa mara.
5) Waalimu kutoka nje: Walisaidia kuimarisha taaluma. Mimi binafsi nilifundishwa na waalimu kutoka Uingereza, India, Russia na Marekani (peace corps) kwa nyakati tofauti.
6) Huduma za serikali: serikali iligharimia karibu kila kitu. Zamani hizo hakukuwa na ada wala michango. Pia kulikuwa na hati inaitwa 'waranti' ambayo mwanafunzi alipewa shuleni na ilimuwezesha kusafiri bure kwenye mabasi na treni. Serikali baadae iliwalipa wasafirishaji.
7) Huduma nzuri mashuleni: Chakula, malazi, vitabu, maktaba, n.k. vyote vilikuwa vinaridhisha.
8) Ukosefu wa udanganyifu: hakukuwa na udanganyifu katika mitihani wala kughushi vyeti.
9) Labda na mabaya yalikuwepo lakini nadhani kulinganisha na sasa wakati ule ilikuwa kama mbingu.
 
Kila Elimu ni bora kutokana na zama zake tusidanganyane.
 
Back
Top Bottom