Elimu ya Msingi ya Tanzania ina Msingi gani??

Revolutionary

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
456
86
Tumezoea kwamba elimu ya msingi ni Darasa la kwanza hadi la saba. Lakini katika hali halisi Elimu ya msingi kwa msingi wake na mane yake yaani basic or foundational education na ukitazama hali halisi ya mfumo wetu wa elimu., kwangu mimi elimu ya msingi ni darasa la kwanza hadi form Six. Ingawa bado mfumo wenyewe una changamoto nyingi.


Elimu ya msingi wa msingi wake ni kumuaandaa mtu kabla hajaanza kusoma elimu ya kitaaluma (professional) ili aje kuwa mtaaluma Fulani mfano Daktari, muhasibu, mchumi, mwanasheria n.k.


Kwa kuongezea elimu ya msingi ndiyo inayomuandaa mtu kabla hajaanza kupata mapokeo hayo makubwa makubwa na kwa kumjengea msingi thabiti wa kuweza kuielewa vizuri elimu ya juu.


Enzi za Mwalimu nyerere, elimu ya msingi, yaani darasa la kwanza hadi la saba ililenga kuondoa UJINGA .Period. Ili watu wajue kusoma na kuandika. Sekondari ilitumika kumuandaa mtu kitaaluma ili aweze kuitumikia nchi na kupata msingi mzuri kwa ajili ya elimu ya juu.


Na ndio maana wengi waliomaliza kidato cha nne au cha sita walikuwa na nafasi nzuri kupata kazi serikalini na kuchangia uchumi wa taifa kinyume na sasa ambapo elimu sawa na hiyo bado mtu anakua hana vigezo vinavyokidhi haja za changamoto za uchumi na hali ya dunia sasa. Hiyo ni kutokana na kuwa na mfumo wa elimu usioendana na changamoto za wakati huu ukilinganisha na sera za elimu ya ujamaa na kujitegemea enzi za Mwalimu (aliyetukuka).


Vijana wanaomaliza darasa la saba siku hizi bado wengi wana ujinga. Na kwa mtazamo wangu elimu ya sekondari sasa ni kama inatumika kutoa watu ujinga badala ya ile ya msingi na ndio maana utakuta bado watu wanamaliza kidato cha nne na wanapata kiwango cha sifuri (division zero). Hii inamaanisha mfumo huu wa elimu unazalisha (produces) watu ambao hawana tija na ambao hawana taaluma (profession) kwa kuwa hawana vigezo vya kuajirika na nafasi na uwezo wao kuchangia katika uchumi wan chi ni mdogo sana.


Kwa hayo niliyoyaainisha, changamoto tunazozikabili za mabadiliko ya kasi ya dunia na mfumo wetu wa mgando elimu (our stagnant education system) yafaa tukubali kuwa darasa la kwanza hadi kidato cha sita zote ni elimu za msingi (primary education) na ni kwaajili ya kutoa ujinga tu kwa kuwa hauwaandai watu kuwa wachangiaji katika kukuza uchumi na kutokana na udoro wake.


Tutakapobadili mfumo wetu na kuwa wa kuwaandaa watu kitaaluma na kuwajenga waweze kuchangia uchumi haraka ndipo tutakuwa sahihi katika tafsiri halisi ya elimu kwa msingi wake. Kwani uliopo ni mrefu, usio na tija na usioendana na changamoto za sasa.
 
Kuna ukweli ndani yake ila ungeipeleka kwenye jukwaa la elimu. Labda Mods wakimaliza kunywa kahawa watakusaidia kuihamisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom