Elimu ya msingi sasa mwisho darasa la sita

Baada ya hilo, watizame elimu ya Upili ambayo inachukula miaka 6. Huku kwetu sisi tuko na 8,4,4.
 
Wasogee hadi secondary, iishie form two kwa kuwa ndio wengi huwa wanachemka. ! (just mockin)
 
Nadhani suala kubwa hapa ni "ELIMU YA MSINGI"
kumekuwa na wito kwa mda mrefu sana kuwa tupitie upya Elimu yetu.
Kama huu ndio mwanzo wa mapitio haya ili kufuta dhana kuwa "Elimu ya msingi ni msingi wa kwenda sekondari" kama mapitio haya hayatakuwa na lengo la kubomoa dhana hyo hapo, basi tuendelee kupalilia bomu ambalo saiv linampa ngazi ya umaarufu Lowassa!
 
Mimi naona ni bora wapunguze jamani lol!! Tunasoma miaka mingi mno jamani....angalia hii;
  1. Elimu ya msingi miaka 7 plus chekechea 1 year=8
  2. O-level miaka 4
  3. Advanced level miaka 2
  4. Elimu ya juu miaka 3 or 4 or 5
Total 17 or 18 or 19
Jamani miaka 17 unasoma tu? Na kibaya zaidi mfano elimu ya o-level na Advanced level hakuna tofauti sana.Nadhani cha msingi ni kuboresha elimu yetu katika mitaala yetu ili kuboresha elimu yetu...

Nakubaliana na ww kwa asilimia kubwa kumbuka pia kuna life expectancy ya mtanzania ni vitu vya kuviconider maana kama muda mwingi utatumika kwa elimu ni lini mtu huyu atapata experience ya kazi na kufanyakazi...lini atatengeneza familia yake...!
 
Nakubaliana nao kupunguza miaka shule za msingi,wangefanya mtoto kuanzia miaka 4 aende nursery 2yrs after that primary ni miaka 5 tu then secondary iwe moja kwa moja form 1 up to 4m 3 unapiga pepa ya mchujo kama ya form 2 ukifaulu unaenda form 4 up to 4m 6 unapiga pepa kuingia chuo
 
Wadau wa JF,
muda mchache uliopita nimesikia ktk kipindi cha magazeti redioni(rfa) kuwa serikali inabadilisha mfumo wa shule za msingi kwa kiwango cha juu cha elimu ya msingi mwisho kuwa ni darasa la sita. Utaratibu huu unaanza effective mwakani. Wenye access na magazeti ya leo amwage data zaidi hapa jamvini..

Kwa shule za english medium, mfumo huu hauna madhara yoyote kwani kwa sasa watoto wanasoma miaka kumi yaani Nursery school 3 yrs + primary 7 years. Elimu ya pre-unit inazidi class II ya shule za kawaida. Madhara ni kuwa shule za kawaida UNLESS iwe ni lazima watoto wote kupitia shule za awali ingawaje shule za awali serikalini (Montisori) ni miaka miwili hivyo bado wa English Medium watawazidi hawa wa shule za kawaida kwa miaka ya kukaa shuleni kati ya mwaka mmoja mpaka mitatu
 
Tuna hesabu za kuchagua jibu sahihi kwenye mtihani wa darasa la saba.Nafikiri kwenye mpango huu tutakuja na hesabu za kuandika True and False.
 
Ikiwa miaka 7 ya sasa inatoa watoto wasiojua kusoma, kuandika au hesabu za kiwango cha darasa la pili, je miaka 6 itatoa nini?

Ni vyema elimu ya msingi ikaishia darasa la pili maana miaka mingine yote ni kuwapotezea muda vijana
 
mimi naona ni bora wapunguze jamani lol!! Tunasoma miaka mingi mno jamani....angalia hii;
  1. elimu ya msingi miaka 7 plus chekechea 1 year=8
  2. o-level miaka 4
  3. advanced level miaka 2
  4. elimu ya juu miaka 3 or 4 or 5
total 17 or 18 or 19
jamani miaka 17 unasoma tu? Na kibaya zaidi mfano elimu ya o-level na advanced level hakuna tofauti sana.nadhani cha msingi ni kuboresha elimu yetu katika mitaala yetu ili kuboresha elimu yetu...
hakuna tofauti!???
 
Swali kwa Mheshimiwa waziri wa Elimu:

Ukiwa na suruali ukiikata inakuwa bichikoma aka Pensi,

Ukiwa na bichikoma aka pensi na kuikata utabakiwa na nini?

Elimu ya msingi ya miaka saba tunayotoa haikidhi hata matarajio ya kawaida ya elimu ya msingi ukipunguza mwaka mmoja basi watoto watakuwa mbumbumbu ile mbaya.
 
A good start nilikuwa nimeshachoshwa na muda mrefu tunaoutumia kwenye elimu tena ambayo haimuandai kikamilifu kijana kupambana na soko la ajira
 
Back
Top Bottom