Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,265
- 105,432
Ndugu yangu nashukuru kwa maoni yako haya.Lakini naomba ukumbuke kwamba sio watanzania wote wana uwezo kama wako,ambao sijui umeupata wapi mpaka unakua na kiburi kiasi hicho.Na hata kama wangekuwa nao, bado serikali ina wajibu wa kushiriki kawa njia moja au nyingine katika elimu ya watu wake.Hata nchi zinazojiita tajiri zinatoa mikopo ya elimu kwa vijana wake,sembuse Tanzania?Wewe unayetoa mawazo hayo potofu, inawezekana umesomeshwa na hela za kifisadi au na Mchonga.Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.Lakini la msingi zaidi ni kwamba na kuhurumia kwa vile umeshindwa kabisa kujua ajenda halisi ya tamko hilo.Si shangai lakini kwa vile watanzania walio wengi hatuko diagnostic.
Tikera sijui hukusoma sehemu hii hapa chini katika bandiko langu, au hujaelewa tu.
Kwa kifupi mimi nina advocate a centrist position, ambapo serikali inachukua wajibu kidogo na mwananchi anachukua wajibu kidogo.Hamna upande uanaobeba mzigo wote, kwani serikali yetu ina mambo mengi na wananchi wetu wengi masikini.
Hebu soma tena hapa
Elimu ya juu kwa nchi iliyo na challenges za kufanya resource allocation kama yetu bado ni privilege, itatolewa kwa wachache walioonyesha uwezo au wenye fedha, tuache kuifanya serikali kama baba tajiri ambaye atalipa kila bili yetu.
Na serikali nayo iache ubahili wa ajabu na mifumo ya ukiritimba wa kikoloni katika kusaidia wananchi wasiojiweza kupata elimu ya juu.
Ni katika kufuata misingi hii tu ndipo tunaweza kupata suluhishi la kati, lisiloegemea sana kwa upande wa serikali kubeba mzigo wa gharama zote za elimu, wala kwa mwananchi kubeba gharama zote.
Lazima kuwe na mlinganyo wenye uwiano unaowezesha taifa letu kujikwamua kiuchumi kwa kutumia elimu bila kuipa serikali wala mwananchi mzigo mkubwa isivyostahili.