Elimu na pesa bora nini?

Pure nomaa

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
1,158
1,382
Wakubwa naomba mnisaidie hii mada kidogo,ELIMU na PESA bora nini maana unaweza kusoma vyuo vikuu hata zaidi ya mia lakini ukaacha chuo ukaenda kuomba kazi je kuna umuhimu kama leo hii ukizaliwa uokote fuko la pesa ili usisome?
 
Elimu inakuongezea maarifa ya jinsi ya kutumia hizo pesa...vyote ni muhimu,ila elimu kwanza.
 
Ukikosa elimu utashindwa kumliki pesa yako. Kuna elimu ya maisha, na ile ya masomo, but elimu ni muhimu.
 
Elimu haileti pesa.
Elimu inaleta maarifa.
Ni vizuri kuwa na elimu na pesa kwa wakati mmoja manake elimu itakupa maarifa ya kutumia pesa!
 
bila pesa utasoma?
Sijasema lazima kusoma, nimesisitiza kuna elimu ya masomo na ya maisha. Kuna watu hawakusoma ila wanafanya biashara yao au wanalima kilimo chao na kuyapeleka maisha kuliko hata walio soma. Ila all in all bila elimu (at least elimu ya maisha) huwezi kufika mbali na gunia lako la dollars.
 
ooh! Elimu ya maisha inapatikana wapi hiyo?
 
Kwakuwa niliamini nasoma ili nipate pesa ivyo kusoma sikuoana umuhimu.mwokozi nitoe roho niepuke ili balaa!maisha nilichezea leo hii nalala na njaa!chemshabongo kabla ujapagwa uja chachawa*2-Profesa J.
 
bora ngoswe, maana ndio kitovu cha uzembe
kuna watu hawana elimu na pesa lakini they are happily ngosweanaring
 
Haaaaaa,wachaga kibao mikoani hawana elimu but wanapesa,walks za na ujambazi wakafungwa wakatoka wakapata pesa wakajenga Kwao wakapata heshima,hata hawaulizwi vidato........alex m
 
Ukikosa elimu utashindwa kumliki pesa yako. Kuna elimu ya maisha, na ile ya masomo, but elimu ni muhimu.
mtaani kwetu kuna jamaa alimwambia mzee wake sitaki kusoma hakuna kinachoingia akilini nikiwa class,
akapewa mtaji na mambo yake ni mazuri,sasa hapo itakwaje?
 
Wakubwa naomba mnisaidie hii mada kidogo,ELIMU na PESA bora nini maana unaweza kusoma vyuo vikuu hata zaidi ya mia lakini ukaacha chuo ukaenda kuomba kazi je kuna umuhimu kama leo hii ukizaliwa uokote fuko la pesa ili usisome?

Hapo kwenye Red nafikiri haliwezekani. Kwa mtizamo wangu, Elimu ni muhimu kuliko hizo pesa, kwani hata hao ambao wamefanikiwa kuwa na pesa nyingi, kwasasa wengi wao kama si wote wanawatumia wenye elimu ili wafanikiwa ktk biashara yao. Lakini, pia kuna Formal Education na Informal Education katika maisha. Na yote haya yanategemea huyo mtu anahitaji elimu gani ili imsaidie katika yale anayotaka kufanya. Na katika wale wengi waliofanikiwa ni hakika wengi wao wana INFORMAL EDUCATION ya kile wanachofanya (shughuli/biashara wanayofanya). Kwahiyo suala hapa ni Elimu gani huyo mtu anahitaji na kwa level gani ili afanikiwe ktk malengo yake. Tuna watu wengi sana ktk jamii zetu walioona kwamba Pesa ni muhimu sana kuliko Elimu, hivyo wakazembea kupata vyote Formal na Informal Education kwa kiwango ambacho kingewasaidia katika kufanikisha yale wanayoyafanya. Mimi naamini kwamba wote waliofanikiwa wana elimu, inaweza kuwa Formal au Informal lkn wote wana Elimu ambayo imewasaidia kuwa na uelewa ktk kile wanachofanya na kujua ni wapi wanapaswa kuelekea. Tunapoongelea Informal Education tuna maana pana zaidi ikihusisha vitu kama kujifunza kutokana na mahitaji ya mazingira husika, kujifunza toka kwa wazazi, ndugu, marafiki ,n.k. Na ndiyo maana tunafikia kipindi tunaamini kwamba URITHI PEKEE UNAYOWEZA KUMWACHIA MWANAO ILI AWEZE KUWA SALAMA NI Elimu kuliko Pesa.
Nawakilisha.
 
Elimu haileti pesa.
Elimu inaleta maarifa.
Ni vizuri kuwa na elimu na pesa kwa wakati mmoja manake elimu itakupa maarifa ya kutumia pesa!

Ktk red na kutengeneza hiyo pesa, ngoja niongeze na kaneno!! most likely and importantly most wisely!!!
 
Back
Top Bottom