Elimu katika ndoa

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,974
1,400
Nampenzi wangu amenizidi elimu yeye ni mwanamke ana masters of chemical engineering na mie ni mwanume elimu yang form six... Sasa tunataka kuoana, kwenye ndoa huyu mwanamke hawezi kunisumbua kwa sababu ya kigezo cha elimu yake??
 
Kama mnapendana na kuheshimiana na kila mtu anajua wajibu wake,uwe na amani,ndoa itakuwa ya furaha na isiyo na usumbufu,changamoto za hapa na pale hazikosekani,Mungu umuombe na kumtegemea.
 
Ndio atakusumbua....
BTW: Kuna wanandoa wasiosumbuana?
 
Kama amesoma kweli na ana akili za kuzaliwa sio za kutumia madesa walizonazo wasomi wengi wa siku hizi...naamini hawezi kukusumbua. La muhimu upime kwanza kama anakupenda kweli... Ila na wewe mzee jimudu kidogo...form six na masters match yake yaweza kuwa ndogo kwa baadae...hujachelewa
 
Hata kama hajakuzidi elimu wewe ndo umemzidi usumbufu uko pale pale.

Kuta nne zina siri yake!!!! We zione hivyo hivyo
 
issue ya nani kasoma kuliko nani kwenye ndoa cdhani km ipo applicable
hapo ni mapenzi ya kweli na kuaminianat tu
 
ndoa inajengwa na mapenzi/upendo, maelewano, kuaminiana na kuvumiliana. nyote wawili mkizingatia haya, basi haijalishi nani ana elimu na ma degree na hana. hivyo usisite hata kidogo chukua jumla. mbona hata familia yenu itajikwamua kiuchumi, vile mama msomi LOL
 
Issue inaweza kuanzia kwako ukianza kuwa na inferiority, solution na wewe anza kujiendeleza kielimu
 
mwanajamiione, mwanajamii... jamii01... halafu FL na FL1

haya bana... tuna acid, hydrochloric sijui na nani tena
 
Cheki majibu, wanawake wengi watakuambia "haisumbui" kwa sababu wengi wanaishi kwenye 'ndoto'.

Mie nakwambia itakusumbua kwa sababu nature ya mwanamme hawezi kuwa mwanamke amzidi. Mwanzo mapenzi yakiwa moto moto haitasumbua baada ya muda itaanza kukukera kidogo kidogo.

Oaneni lakini jiendeleze kielimu kama hilo haliwezikani (huna interest) basi hakikisha una kitu cha kumzidi sana mkeo. Kama si pesa basi japo elimu ya kiroho.
 
Wewe tafuta hela tu. Ukiwa nazo zitafidia elimu aliyokuzidi.
Ila cha muhimu zaidi na zaidi ni upendo na kuheshimiana baina yenu.
 
nashukuru sana kwa ushauri wenu..kwa sababu kuna rafiki zangu wamenikalia koo nisimwachie huyo dada kwasababu ananijari mpaka kapitiliza..
 
Kama amesoma kweli na ana akili za kuzaliwa sio za kutumia madesa walizonazo wasomi wengi wa siku hizi...naamini hawezi kukusumbua. La muhimu upime kwanza kama anakupenda kweli... Ila na wewe mzee jimudu kidogo...form six na masters match yake yaweza kuwa ndogo kwa baadae...hujachelewa

umeongea point sana nadhani azingatie sana hili
 
Cheki majibu, wanawake wengi watakuambia "haisumbui" kwa sababu wengi wanaishi kwenye 'ndoto'.

Mie nakwambia itakusumbua kwa sababu nature ya mwanamme hawezi kuwa mwanamke amzidi. Mwanzo mapenzi yakiwa moto moto haitasumbua baada ya muda itaanza kukukera kidogo kidogo.

Oaneni lakini jiendeleze kielimu kama hilo haliwezikani (huna interest) basi hakikisha una kitu cha kumzidi sana mkeo. Kama si pesa basi japo elimu ya kiroho.

Habari yako Gaijin.....
Well said...
Mwanaume ni kiongozi....na kiongozi anapaswa kuwa juu....kuona mbali zaidi ya anaowaongoza......
 
Nampenzi wangu amenizidi elimu yeye ni mwanamke ana masters of chemical engineering na mie ni mwanume elimu yang form six... Sasa tunataka kuoana, kwenye ndoa huyu mwanamke hawezi kunisumbua kwa sababu ya kigezo cha elimu yake??

Muombe Mungu kwanza, kama huyo ni mke uliyepewa na Mungu haijalishi kama unamzidi elimu au anakuzidi elimu, mapenzi yakiwa ya dhati hayabagui. Nina rafiki yangu mpendwa ana degree ya law, ameolewa na mume wake ana form four chafuuuuuu, lakini wanaishi kwa amani coz wanapendana sana, na ukifika kwao huwezi ukagundua hata kidogo. Ukimuomba Mungu atakupa kama ni mume au mke wa kwako, ukioa mke wa mwingine ndio usumbufu hauishi kila siku!!!!!!!!!!!!! pray again and again God will answer your prayer. Pia ushauri wangu kwako usibweteke na elimu uliyonayo, baada ya kuoa na wewe nenda shule ikiwezekana hata PHD
 
Cheki majibu, wanawake wengi watakuambia "haisumbui" kwa sababu wengi wanaishi kwenye 'ndoto'.

nimecheka sana na uliotoa comment hiyo
 
shule nitapiga kimtindo kwa sababu dada mwenyewe huwa ananimbia kwa mbali ..anajua nitachukia sipendi kupiga shule zaidi ya business ila yeye kila mara ananimbia anataka akafanye Ph D Germany..Ndicho kisa cha kuniganda mpaka basi..
 
Back
Top Bottom