Elimu inakuwa au tunaiua?

Mwalimu Mkuu

Member
Dec 26, 2010
62
39
ni mara nyingi nimekuwa nikijiuliza juu ya kiwango cha elimu kinachotolewa hasa katika taasisi zetu za elimu ya juu kama vyuo vikuu. kumekuwepo na idadi kubwa ya uandikishaji (addmission) jambo ambalo ukiliangalia kwa haraka unaweza kuona ni jema, kwani hata watoto wa maskini wanaweza kupata elimu walau ya chuo kikuu.
jambo linaloshangaza ni product inayotolewa na vyuo hivi sasa, juzi nilikuwepo eneo fulani ambalo watu walikuwa wanafanya usaili wa wafanyakazi, ilikuwa ajabu kabisa kwamba wanafunzi waliotoka katika vyuo kama UDSM ama UDOM hawakuwa na kipaumbele katika jopo la usaili, kwani wanadai wanafunzi hao wanaweza kuwa na GPA hata za point 5 lakini kiukweli ni wabovu katika fild walizosomea. kwa maan hiyo walipendelea kupata wanafunzi kutoka katika vyuo binafsi ambavyo kwa sababu binafsi sintovitaja.
hoja ni kuwa kweli vyuo vyetu hivi vilivyokuwa na heshima ulimenguni kama chuo cha Dar es salaam kinaweza kuwa na picha hii iliyopo kwa jamii? tunakuza elimu au tunaiua, vyuo havina vyumba vya mihadhara vya kutosha, osteli za wanafunzi zenye mahitaji muhimu, matatizo ya mikopo inayoandamana na migomo ya wanafunzi kwa kutaja machache
je elimu inakuwa au tunaiua?
 
Mkuu Peter,
Nadhani hii haina ukweli, yawezekana hao uliokuwa nao kwenye usaili wako biased kama wewe na vyuo ulivotaja. Nasema hivi make hata mi ilinitokea nikawa kwenye usaili uliokuwa na wakuu supporters wa vyuo ulivotaja, ukweli walikuwa biased na candidates from private and other colleges. So ni fikra chafu ambazo zimewajaa watu wengi na zinachochewa zaidi na mijadala kama hii ambayo mara nyingi haiko objective.
Kwa sasa nasoma huku Europe niliattend career day hapa chuoni kwangu matatizo wanayotaja waajiri kuhusu graduates from Europe almost ni kama TZ tu. Msitake kulazimisha mtu agraduate na awe na uwezo wa kufanya kazi kama wenye 10yrs experience. Pamoja na mapungufu yaliyopo ktk vyuo vyetu si kweli kuwa elimu yetu ni mbaya kwa kuangalia sababu ndogo kama hizo au majungu na biaseness za watu.
Na pia graduate mmoja akiwa mbaya dont generalize. Ingetokea hiyo interview akashinda wa vyuo ulivotaja wala usingeleta hii taarifa.
 
ukweli ni kwamba Elimu imeshuka sana Tanzania tena sio Vyuo vikuu tu zaidi mno hata kwa mashule ya secondary na A'LEVEL's .
Nakumbuka wakati tunamaliza sisi mtu ilikuwa kuingia MHIMBILI lazima uwe na div 1 ,ukikosa basi walau uwe na div 2 nzuri esp kwa males.
Lakini leo nenda pale mhimbili ukawaulize watakwambia kuwa hadi div 3 ya mwisho wanachukuliwa sababu watu wenye div One kwa masomo hayo wamezidi kuwa wachache sana. Na juzi juzi tu nilikuwa naongea na jamaa yangu aliyepale akawa ananipasha na kusema mmmhh yaani hapa siku hizi Criteria sio za mhimu sana.
Sasa unategemea nini? kama huwezi kuwa strict on academic credibility? je hao unaandaa madaktari wa kiasi gani? si maanishi kuwa wakiwa na div 3 au 4 hawawezi kuwa madaktari, la hasha ila nataka kuweka hali halisi ilivyobadilika , na hili liko karibu vyuo vyote ambavyo vilikuwa na sifa kubwa kwa sasa vinazidi kuporomoka.
 
Si kweli kwamba elimu imeshuka, isipokuwa opportunities zimeongezeka kwa hiyo watu wengi wanapata admission. Kwani sifa za kuingia chuo kikuu ni zipi? Zamani watu walikuwa wanachaguliwa wachache kwa sababu nafasi zilikuwa chache. Kwa hiyo hata wenye sifa waliachwa kwa sababu ya ufinyu wa nafasi! kwa taarifa yako mtu anayepata admission ya chuo ina maana anaqualify.
 
una uhakika na unachokiongea lakini?

Nina uhakika, kwani sifa za kujiunga na chuo zimebadirika? Ukweli ni kwamba zamani zile watu walikuwa na sifa za kujiunga na chuo lakini kwa sababu ya ufinyu wa nafasi walikosa. Kwa hiyo ule ufaulu wa form six ulitumika kama chekecheo. Kama ni vigezo vya kujiunga na chuo ni vilevile tu havijabadirka isipokuwa vyuo vimeongezeka na watu wengi wanapata nafasi . Pia kumbuka kuna TCU ambao wanadhibiti ubora wa elimu itolewayo nchini.
 
Huyo aliyekuambia muhimbili ameingia kwa div 3 ni muongo ama la amehonga ukimtoa mbele aeleze hata thubutu ng'o!!!! Hivyo vyuo unavyosema vya private vyenye uwezo wa kutoa graduates wanaokubalika ni vipi tanzania hii jamani? Msifanye vyuo vyetu kama vya nchi za Scandinavia graduates wa vyuo vingi vya serikali wakitoka wanafanya kazi vema baada ya muda mfupi. Unapoajiriwa lazima ujifunze organisation politics, stucture, priorites and so so sio kukurupuka tu. Sidhani kama interviews tunazozifanya kama zinaweza kuidentify uwezo wa mtu katika utendaji, sanasana yatakua maongezi mazuri kingereza kizur nk.
 
pole sana kama hujui kuwa kwa sasa kuna wanafunzi wengi tu wala sio mmoja walio na division 3 na wamepokelewa mhimbili ,kama hujui jaribu kufatilia utajionea mwenyewe , Kila siku tunaona matokeo yalivyobadilika na kupolomoka form 4 hadi 6 leo unasema wanachukuliwa kwa vigezo sawa Mmh ,ndio maana hapo juu nilimuuliza jamaa kuwa jetliners anafamilia uhakika na anachoongea .
 
@ Mallaba
nashukuru kwa comment yako, sidhani kama binafsi niko bias kama ulivyosema kwani katika huo usaili sikuwa miongoni mwa wajumbe wa bodi, nilikuwa namsubiri mmoja miongoni mwa wajumbe alipotoka ndo alinishirikisha. hata mimi nikashtuka na hali hiyo nikaamua kuposti wazo hilo.
ki ujumla nililazimika kufanya kautafiti kidogo kwa kuwasiliana na wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya umma na wale wa binafsi. sijamaliza utafiti ila so far matokeo yanaoonesha hali si nzuri sana katika vyuo vyetu.
admission ni kubwa hasa katika kozi za ualimu, biashara na uchumi. vitengo vya science kidogo havipati malalamiko makubwa kama kwingine. mzigo mkubwa unawaelemea wahadhiri na si rahisi kufanya kazi kwa kiwango kilichokuwa miaka kadhaa hapo nyuma, pia bado pamoja na ongezeko hilo wahadhiri wengi wanafundisha chuo zaidi ya kimoja, ukosefu wa vitabu, uchache wa computer, vifaa vya kujifunzia elimu kwa vitendo, ni miongoni mwa malalamiko ya wanavyuo wengi.
anyways nadhani hata bila kuwa bias kuna changamoto na ni lazima tukubali kukabiliana nayo. vinginevyo elimu ya juu inaweza kuwa kama mpango wa "mkukuta" "mkurabita" "kilimo kwanza" ni kama slogans nzuri zisizofika katika kilele chake. ni maoni yangu tu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom