Naomba ushauri jaman!nimemaliza kidato cha sita HKL na nimepata DIV 4 YA 19 .je nifanye nini sasa?naomba mnisaidie.
nilikuwa kwiro high schoolUsiwe na hofu huo siyo mwisho wa maisha..tulia mwombe Mungu, He always has a plan 4u, Jeremiah 29:11...
Kuna stori nyingi sana za watu waliofeli form 6 na sasa wamefanikiwa academically and in life...wala usiwe na hofu mdogo wangu!!!
* one of the options ni kutumia vyeti vyako vya form four uanze certificate uendelee na life..
* au, kama unaona, unajua, na una uhakika kuwa imetokea kwa bahati mbaya, labda hukuwa tayari kimaandalizi, as in u r very sure...then i suggest u resit the examinations..lakini hii ni kama una uhakika wa sababu iliyokufanya upate matokeo hayo!!!
Ulikuwa shule gani mdogo wangu!??
nilikuwa kwiro high school
nashukuru kwa ushauri mzuri,nitaufanyia kazi.pia nta ku pm ili unijuze zaid.nimekata tamaa kabisa.ki ukwel nlikuwa fit sana'Pole Tizo1. Ukweli ni kuwa bado una nafsi kubwa sana ya mafanikio katika maisha. A-level huwa ina suprises zake na mazingira ya usomaji mara nyingi ni magumu. Miongoni mwa mambo ambayo huwa yanatatiza ni kuulizwa maswali na watu wa mtaani kuhusu matokeo yako na pia inauma pale unapoona wenzako wanaenda vyuo vya elimu ya juu na kukuacha. Hili ni jambo la kawaida.
USHAURI:
Jipe moyo, maumivu ni lazima yawepo kwa muda fulani na ni lazima yaishe. Ila ni rahisi maumivu kuisha kama utajua nini hatua ya kuchukua baada ya matokeo haya. Tuko pamoja na Mungu akubariki.
- Usijaribu kuzuia maumivu ya kufeli. Kwa kipindi fulani ni lazima na ni halali pia kupata maumivu. Usifanye kazi kubwa sana kujaribu kuzuia maumivu, yataisha yenyewe. Maumivu huisha kama utakuwa na altenatives. Ukishapata jibu juu ya hatua za kuchukua utashangaa ghafla maumivu yanaanza kuisha.
- Soma kwa hatua. Kwa kutumia cheti chako cha Form 4 unaweza kuapply vyuo vinavyotoa certificates then diploma then degree n.k. Ni sawa tulikuwa tunataka kwenda chuo kikuu, lakini matokeo hayaturuhusu. Katika mazingira kama haya tufe? Hapana maisha ni lazima yaendelee, hata kama watu watakucheka, vumilia. Katika kuchagua certificates angalia courses za mambo unayoyaweza au kuyapenda, pia ni vizuri kuangalia soko la ajira la courses hizo Tz (kama unawaza kuajiriwa).
- Kama unadhani umefeli kwa bahati mbaya unaweza ku-resit, japo ku-resit na kufaulu ni kitu kigumu sana. Angalia uhalisia wa uwezo wako.
NB. Kama utakuwa unahitaji ushauri wa ziada au ushauri private waweza kunitumia private message.
asante kwa ushauri.Hakuna haja ya pole na wala usikubali yeyote akupe POLE. Panga stratergy yako upya, naamini ulikuwa una ndote, malengo, you wanted to be(come) somebody. Hebu fanya assessment kama umeharibu sana au kuna uwezekano wa ku-make up.
There's still a life for you.
Nilikuwepo ile Kwiro ya Makunja, sisi ndo tulianzisha combi za arts mahali hapo. Natumaini Mama Ngapo bado atakuwepo!
nashukuru kwa ushauri mzuri,nitaufanyia kazi.pia nta ku pm ili unijuze zaid.nimekata tamaa kabisa.ki ukwel nlikuwa fit sana'
Asante sana kwa ushaur mzuri.UMENITIA MOYO na kunipa mwanga!nilikuwa na uwezo mzuri sana!hakuna wasi ntajitahd kufanya hivyo!we mbona hujafeli! kufeli ni kupata division 0.. kuna vyuo vingi unaweza kuapply usome remedial course then unaunga degree mwaka huu huu. fuatilia st. augustine university mdogo wangu, usikate tamaa.
Asante sana nazid kufarijika na wana JF nilipo wengi si wasomi na wanafikiri kufel nh uzembe!kwel hiki ni jukwaa la elimu tayari naanza kupata mwanga na kuona si mimi pekee niliyefeli maishaHuna haja ya kujilaumu kivile, ni kweli unaokosa kufikia malengo yako unaumia, lazima kila kitu kiende mbele, Naunga mkono wote wanaosema kuwa tumia cheti chako cha fom4 (kama unahitaji kuendelkea na elimu ya juu) unaweza kuanza na dip na kama inashindikana kabisa anzia cheti. Vyuo vilivyo chini ya Nacte vinasaidia sana katika hili, vipo vingi mfano ni IFM, CBE, Mwalimu Nyerere na TIA, USTAWI,
Ningekushauri tembelea USTAWI MNMA utapata zaaidi
Halafu (SIRI YAKO) unaweza kucope na stress ulizonazo kwa kuangalia mifano ya watu walioanzia na elimu za UPE lakini leo ni madaktari, mfano mmoja ni Dr Kadeghe Maiko:A S 39:
asante sana angalau nimepata mwanga fulani hivi!JF ni msaada tosha jamaniasante sana TIZO1...asanteni wadau wote mliotoa ushauri wa kujenga.....hapa sasa napata faraja na maana ya kukaa JF....it is a building block, nikiwa mdau mkubwa wa elimu nashawaishika kusema dogo TIZO1 kujgundua tatizo au kushirikisha watu tatizo lako tayari umeshalitatua 50%... yaani umeshafika nusu ya jibu la tatizo lako
Shule zipo nyingi kufikia malengo yako ..japo ile njia uliyokuwa unaiona haikidhi haja!
rejea ibada kwa kasi mpya
asante sana TIZO1...asanteni wadau wote mliotoa ushauri wa kujenga.....hapa sasa napata faraja na maana ya kukaa JF....it is a building block, nikiwa mdau mkubwa wa elimu nashawaishika kusema dogo TIZO1 kujgundua tatizo au kushirikisha watu tatizo lako tayari umeshalitatua 50%... yaani umeshafika nusu ya jibu la tatizo lako
Shule zipo nyingi kufikia malengo yako ..japo ile njia uliyokuwa unaiona haikidhi haja!
rejea ibada kwa kasi mpya