Elimu bure, matibabu bure kuanzia kilimanjaro 2010-2015

Ndugu angalieni tusiweke ukabila, kinachotakiwa ni kwamba elimu bure iwe kwa watanzania na si Kilimanjaro, kumbukeni kodi zote za watanzania zisaidie watanzania wote, Tukiungana pamoja twaweza daima.

Tuhimizane kuwa na maendeleo kwa wote maana watoto ni wetu sote, Kenya wameweza kwanini sisi tusiweze?

Soma post kwanza na kisha uilewe, siyo unarukiarukia tu utakujapata mimba mangi
 
kuna watu wanasema chama hiki ni cha (kabila) mkoa fulani...! KUNA UKWELI JUU YA HILI?
 
na kwa mujibu washeria za nchi yetu CHADEMA ndio watakaounda serikali ya mkoa huu kwa hiyo ni moja kwa moja kuwa ILANI ya chama itaanza kutekelezwa mkoani kilimanjaro,

Kuna serikali ya mkoa kweli ...... au unamaana ya kuunda council ya eneo.... na sidhani kama chadema.... ikla wilaya ina serikali yake na council yake .... moshi mjini ndio chadema wataunda coucil ya manispaa na sio kilimanjaro.... sawa kaka
 
Kwa kuwa chama cha CHADEMA ndicho kilichopata viti vingi vya ubunge na udiwani ktk mkoa wa kilimanjaro, na kwa mujibu washeria za nchi yetu CHADEMA ndio watakaounda serikali ya mkoa huu kwa hiyo ni moja kwa moja kuwa ILANI ya chama itaanza kutekelezwa mkoani kilimanjaro, kwa hiyo ni mategemeo yangu kuwa elimu na hospitali zitakuwa ni bure, labda kama nimekosea mwenye uelewa zaidi anipe mwongozo.

Ehe, subiri kwanza rudi nyuma kidogo. Mkoa wa kilimanjaro una wilaya 7 na majimbo 9 ya uchaguzi. Katika haya majimbo, manne tu ndio yaliyochukuliwa na upinzani (cdm 3 na tlp 1) na pia halmashauri walizoshinda nadhani ni moshi mjini, sasa unapozungumzia mkoa kuchukuliwa na cdm unazungumzia nini. Pili, kuna mapato yatokanayo na makusanyo ya serikali za mitaa na serikali kuu. Nisichoelewa ambacho pia nawe ndicho usichoelewa ni kuwa haya mapato yakusanywayo na serikali za mitaa ndio hutumika kuendesha serikali hizo? Kama ndivyo basi wataweza, na kama sivyo hawataweze kutimiza hayo katika halmashauri wanazoziongoza kwani hawatakuwa na fungu la kutosha. Ila wataweza kufanya mambo mengi yaliyokwenye urefu wa kamba yao.
 
kuna tax za serikali kuu na za halmashauri.
mapato ya serikali kuu
1. vat 2. income tax 3.corporate tax 4. fuel duty 5. mirahaba ya kampuni za madini 6. % kutoka makampuni ambayo yana hisa 7. hela za misaada

mapato ya halmashauri
1. kutoka serikali kuuu
2. parking fees
3. kodi za majengo/viwanja
4. advert fees (mabango)
5.business licence
6. kodi za masoko
7. maeneo ya jiji yaliyokodishwa
8. kodi ya machinjio (kama eneo lina machinjio)
9. kodi mbalimbali za makampuni kama vile usafi (ie breweries, barrick lazima wawe wanalipa polution)

halmashauri ziko responsible kwa
1. primary school education
2. usafi
3. local roads (mitaa)
4. zahanati
5. maji safi na taka
note: wafanyakazi wa hizi sehemu wanalipwa na central govt

kwa hiyo utaona kuwa central govt ndio wanakusanya tax kubwa, local govt wanategemea sana central govt kwa mapato
 
shukrani kwa data...
ungeweka source tu ili tuweze kuhakiki ingekuwa fresh!!
 
Kwa kuwa chama cha CHADEMA ndicho kilichopata viti vingi vya ubunge na udiwani ktk mkoa wa kilimanjaro, na kwa mujibu washeria za nchi yetu CHADEMA ndio watakaounda serikali ya mkoa huu kwa hiyo ni moja kwa moja kuwa ILANI ya chama itaanza kutekelezwa mkoani kilimanjaro, kwa hiyo ni mategemeo yangu kuwa elimu na hospitali zitakuwa ni bure, labda kama nimekosea mwenye uelewa zaidi anipe mwongozo.

Mfano mzuri hapa ni kwa hospitali ya Mawenzi. Huyu mbunge kabadilisha vitu vingi sana, mpaka hospitali sasa inaeleweka na watu hawalalamiki.
kwa hiyo kwa kipindi hiki kingne ni kwamba watafanya kila namna kupata kipato ili elimu na hospital ziweze kuwa bure.
 
Inawezekana ikiwa tu central government itaacha mapato ya Moshi kwa kiasi kisichopungua 60%
 
chadema wamepata majimbo 3 mkoani kilimanjaro yaani moshi mjini,hai na Rombo.wamekosa jimbo la moshi vijijini,vunjo,same mashariki,same magharibi na mwanga.sasa nashindwa kukuelewa unavosema chadema imechukua majimbo mengi kilimanjaro wakati imechukua majimbo 3 kati ya name.Labda utueleze zaidi ulichukua hatua gani.
 
Watakachofanya ni kusaidia kutekeleza kwa ufanisi ilani ya ccm kwani wao ndio wako madarakani na si zaidi ya hapo.
 
Back
Top Bottom