EL; RA & AC Wamtunishia Misuli JK: Wagoma Kujibu Barua

Some Info. Dogo Nape amezibwabwaja Channel 10 Asubuhi hii . . .

You can check a separate thread . . .

Respect.
 
Hongera sana Rais Kikwete kwa kuwang'oa mafisadi CCM. Usirudi nyuma.Hatakama mafisadi watawatumia upinzani.Msimamo ubaka pale pale 90 days.No retreat no surrender. The determination should remain in force i.e 90 days. Nauye endelea kuwaumbua mafisadi wanaoitafuna nchi.Usiogope vitisho.Nchi ipo nyuma yako.We must purify our party which was doomed to die because of Mafisadi. Let the mafisadi go. Really, Kikwete you have left a legacy!

Kujivua gamba kwa staili ya kufukuza mafisadi CCM kulihitaji utashi kama aliokuwa nao sokoine ,nyerere au kawawa...waliomshuri JK hii strategy beleave me wanataka aanguke kama MBEKI .....read this date...utakuja kuniambia.....,nadhani hata kikaoni ilizusha walakini ,lakini kwa kuwa JK alishatekwa nyara na kundi linalotaka kulipiza kisasi na kujipanga kwa mwaka 2015 ,na kwa kuwa huwa hana msimamo akashindwa kubaini...

Tujiulizeni kitu kimoja unapovua gambaa kwa kashfa ambazo zinamuhusu RAIS ,marafiki zake na familia yake ..unamtakia mema rais au unataka kumuengua>>>>ina maana ndani ya siku 90 rais nate ajiengue ..kwa kuwa naye wananchi wanamtuhumu pia...

Kwa wasomi wa historia huwa zinajirudia ,ndio maana hata kwenye sheria ,hukuma za zamani zinatumika....angalieni hili lililotoke ANC karibuni.....,ili kummaliza ZUMMA kisiasa ..mkuu wa usalama wa taifa pale akishiriikiana na mbeki na THE SCROPION ...walimpa zumma kesi ya kifisadi ya rushwa ya silaha...na kesi ya aibu ya kubaka...kwa miaka miwili na zaidi nyumbani kwake kukawa mahakamani ..lakini guess what ...mkutano mkuu wa ANC uliofuatia pale Palakwane,PRETORIA...ulimuengua MBEKI kama rais....na nchi ikawa chini ya caretaker president ......Kgelema Motlanthe.....

Wana CCM WENGI wanadanganywa kuwa CHADEMA ndie adui yao[NI kweli CHADEMA ni wapinzani wakubwa lakini upinzani wao hauna madhara makubwa kwenye PRESIDENCY..unlike upinzani wa ndani ambao at any given time unaweza kusababisha technical coup] ...hii ni ku divert attention ..na kuwaacha huru maadui wa kweli wa Kikwete ndani ya CCM wakiendeelea na mipango yao..tatizo la kikwete ameweka makundi .....mawili makuu ...moja la wapambanaji na lingine linaitwa la mafisadi[yeye akiwamo]......alichotakiwa kufanya ni kuwamwaga wote ....aje na watu huru kabisa wasioegemea upande wowote...lakini kwa sasa ni wazi amecheelewa na kundi la mafisadi wanalo FAILI JEUSI la JK........
Tayari watanzania ambao walikuwa hawamfahamu jk wanaaza kuambiwa kuwa yeye alishakula rushwa ya IPTL ..Enzi akiwa waziri wa nishati..moja ya rushwa ya mwanzo ya nishati,rushwa ya Saclair...,na kuwafukuza wachimbaji wadogo wa madini,[wanasema alikuwa anatafuta pesa ya kugombea urais mwaka 1995], na ushahidi wanao nafikir wapinzani wameshapatiwa,rushwa ya pesa za ubalozini,..[Luhanjo anajua alikuwa PS wake Aliyehama naye].....EPA ..[kupata pesa za kugombea 2005],stimulus package, kuna list ndefu ya makampuni ambayo ana hisa au anamiliki ..,[inafanyiwa kazi]..,mwanaye ana malori mengi sana ya kupeleka mafuta ..na anachukua advantage lakupasuka mara kwa mara kwa bomba la TAZAMA ...isivyokaawaida...Congo connection..,kwa kifupi kuna uchafu mwingi sana sana ..ambao ina maana waliokuja na hii hoja ya kujivua gamba waatakuwa na kazi moja kubwa ya kuondoa mafuta kwenye maji...ili waweze kumwaga maji....wakikosea tu watamwaga na mafuta...

Uchaguzi mkuu wa ndani wa CCM mwaka 2012 ..utakuwa muhumi mno ku determine future ya hichi chama kikongwe na urais wa Kikwete ...na hata uwezo wake wa udhibitu kuelekea mwaka 2015.

Hii post nimeandika kama Mtanzania mzalendo ambaye nina uwezo wa ku analyse mambo kwa undani...sitegemei mtu aijibu kisiasa...mfikishieni!!!!
 
  1. Tayari watanzania ambao walikuwa hawamfahamu jk wanaaza kuambiwa kuwa yeye alishakula rushwa ya IPTL ..
  2. Enzi akiwa waziri wa nishati..moja ya rushwa ya mwanzo ya nishati,rushwa ya Saclair...,na kuwafukuza wachimbaji wadogo wa madini,[wanasema alikuwa anatafuta pesa ya kugombea urais mwaka 1995], na ushahidi wanao nafikir wapinzani wameshapatiwa,
  3. rushwa ya pesa za ubalozini,..[Luhanjo anajua alikuwa PS wake Aliyehama naye]
  4. .....EPA ..[kupata pesa za kugombea 2005],
  5. stimulus package, kuna list ndefu ya makampuni ambayo ana hisa au anamiliki ..,[inafanyiwa kazi]..,
  6. mwanaye ana malori mengi sana ya kupeleka mafuta ..na anachukua advantage lakupasuka mara kwa mara kwa bomba la TAZAMA ...isivyokaawaida...
  7. Congo connection..,
kwa kifupi kuna uchafu mwingi sana sana ..ambao ina maana waliokuja na hii hoja ya kujivua gamba waatakuwa na kazi moja kubwa ya kuondoa mafuta kwenye maji...ili waweze kumwaga maji....wakikosea tu watamwaga na mafuta...

Uchaguzi mkuu wa ndani wa CCM mwaka 2012 ..utakuwa muhumi mno ku determine future ya hichi chama kikongwe na urais wa Kikwete ...na hata uwezo wake wa udhibitu kuelekea mwaka 2015

Mkuu PM;

Very well presented. Technically Analysed.

Na penye Red hapo ndo kinachomnyima usingizi JK na yuko very uncertain about his future ingawa yuko madarakani.

Waliotaka kuleta hoja CC ya kutenganisha kofia wanajua kuwa JK hayuko karibu na wanachama wake na kazi hiyo walikuwa wakiifanya wengine. Anayo kazi ya ziada kama ni kweli anataka mabadiliko ya kweli. Unless kama anaongelea Cosmetic Changes ambazo hizo amezizoea sana.

Kwa ujumla huwa mara zote wanakuja na majibu mepesi kwa maswali magumu.

Respect.
 
Hao wanaotaka kuandamana amewalipa shilingi ngapi ili wamsaidie. MCHUNGAJI KWELI HII IMEKAA KISHIGONGOSHIGONGO VILE!

Waliomchague awe mbunge huyo (EL) aliwapa shilingi ngapi? na Kule Igunga RA aliwapa Shilingi ngapi? Mabaya ya EL unayoyaona wewe wengine hawayaoni. Mbona hii haiitaji reasoning kubwa. We unadhani kila mtu anamchukia EL?
 
Wakuu wangu, unajua yule mkubwa wa magogoni ni mtu wa ajabu ajabu, nadhani kaupeo kake ni tatizo. Mtu serious hawezi kusema kama kweli Chama cha Magamba kinataka kupunguza magamba ni kuanza na mwenyekiti. Jamaa anashindwa kabisa kutofautisha yeye kama kijana wa kikwere na yeye presidenti. Presidenti lazima afanye kazi kwa mujibu wa katiba na sheria, lakini cha ajabu jamaa anatoa ahadi bila kuangalia sheria zinasemaje.
Kutoa Magamba kama ni kweli gamba la juu ni yeye mwenyewe, ajiuzuru tuanza upya tuweke CDM, wao watakuwa wanapata gamba jipya. Ukijiuliza kama ni richimondi si ilipitishwa na baraza la mawaziri, na kama mikataba mibovu mingine alisaini yeye.
Nitoe mifano
Alisema lazima ajenge barabara kupitia serengeti, akasahau ama hajui kuwa ni eneo nyeti, ndio maana wakubwa wa nje wanaliita maajabu ya dunia. Sasa keshasema, wataalamu wanamwambia sheria inagomba, umeshasaini mikataba mingi ya kimataifa ambayo inatubana, anatoka na jibu jepesi ni wakenya hawataki. Jibu jamaa gurumeti anajenga hoteli, uwanja wa ndege , na ndio Mungu wa Serikali. Nawambia wanajamii akishajenga tu ule mbarabara ambao utapita zaidi ya kilomita 50 hakuna kiumbe , Serengeti ecosystem yake inashikiliwa na nyumbu, Lakini yote ya yote si huo ni mpango wa EL kujenga hiyo ili mahoteli yao na Rost isiyo Tamu yapeleke wageni wao.
Kimsingi kuna uvunjaji wa sheria makusudi na anatoa maagizo yanayopinga na katiba, sheria, taratibu na ndizo zimesaidia kukuza ufisadi, kwa hiyo anayepaswa kutoka ni JK, ambalo ndilo gamba la juu, vingine ni kama magamba madomadogo.
Na mimi ningekuwa JEI KEI ningejiuzuru kupisha watu wanostahili kukaa magogoni sehemu takatifu na nikaanzisha mifuko ya Hisani kama vile kuchangia YANGA waweze kujenga uwanja, kutoa zawadi za kwa watoto walio katika mazingira magumu kipindi chote cha mwaka na siyo sikukuu tu, ili hali wanasota mwaka mzima, kuanzisha vikundi vya bongo fleva nk

Zidumu Fikra za Chama Cha Mapinduzi?
 
Kama hizi taarifa ni za kweli, sioni uwezekano wa mtu kugeuza mwelekeo wa mambo, na matokeo ya mwelekeo huu lazima yatokee na yataumiza wengi. Kama yakitokea kweli, huu utakuwa uthibitisho kwangu, kuwa
  1. si kila mtu anaweza kuwa kiongozi
  2. uongozi hauhitaji kiongozi mwenye hila bali hekima
  3. uongozi unahitaji kiongozi mwadilifu na sio fisadi
  4. huwezi kutawala watu kwa kuwadhulum haki siku zote, kuna siku watakataa...hata wakiwa wanyonge, dhaifu na wajinga wasio na elimu
  5. pesa na mtandao sio mtaji mzuri wa kuwa kiongozi mwenye mafanikio ....
Kwa dalili hizi yawezekana CCM ikagawanyika kama siyo kufa kabisa. Ili kuepusha matokeo hayo, inategemea Kikwete na njia atakazotumia kuepusha chama kufarakana. Kama atawekeza nguvu nyingi katika maridhiano na huyo dada Rachel ili kumzuia asimwage mboga, atafanya hivyo kwa ghalama ya kuvunja maridhiano na wananchi anaowatawala. Wananchi wataamua kusikiliza zaidi maelekezo ya vyama vya upinzania. Hivyo kuna uwezekano mkubwa sana Serikali yake ikashindwa ama ikafika mwaka 2015 kwa shida na misukosuko mingi kuliko awamu zote. Na kama ikitokea hivyo, naomba Mungu atunusuru tusiingie kwenye vurugu na mapigano yanayotokea nchi zingine.
 
Kujivua gamba kwa staili ya kufukuza mafisadi CCM kulihitaji utashi kama aliokuwa nao sokoine ,nyerere au kawawa...waliomshuri JK hii strategy beleave me wanataka aanguke kama MBEKI .....read this date...utakuja kuniambia.....,nadhani hata kikaoni ilizusha walakini ,lakini kwa kuwa JK alishatekwa nyara na kundi linalotaka kulipiza kisasi na kujipanga kwa mwaka 2015 ,na kwa kuwa huwa hana msimamo akashindwa kubaini...

Tujiulizeni kitu kimoja unapovua gambaa kwa kashfa ambazo zinamuhusu RAIS ,marafiki zake na familia yake ..unamtakia mema rais au unataka kumuengua>>>>ina maana ndani ya siku 90 rais nate ajiengue ..kwa kuwa naye wananchi wanamtuhumu pia...

Kwa wasomi wa historia huwa zinajirudia ,ndio maana hata kwenye sheria ,hukuma za zamani zinatumika....angalieni hili lililotoke ANC karibuni.....,ili kummaliza ZUMMA kisiasa ..mkuu wa usalama wa taifa pale akishiriikiana na mbeki na THE SCROPION ...walimpa zumma kesi ya kifisadi ya rushwa ya silaha...na kesi ya aibu ya kubaka...kwa miaka miwili na zaidi nyumbani kwake kukawa mahakamani ..lakini guess what ...mkutano mkuu wa ANC uliofuatia pale Palakwane,PRETORIA...ulimuengua MBEKI kama rais....na nchi ikawa chini ya caretaker president ......Kgelema Motlanthe.....

Wana CCM WENGI wanadanganywa kuwa CHADEMA ndie adui yao[NI kweli CHADEMA ni wapinzani wakubwa lakini upinzani wao hauna madhara makubwa kwenye PRESIDENCY..unlike upinzani wa ndani ambao at any given time unaweza kusababisha technical coup] ...hii ni ku divert attention ..na kuwaacha huru maadui wa kweli wa Kikwete ndani ya CCM wakiendeelea na mipango yao..tatizo la kikwete ameweka makundi .....mawili makuu ...moja la wapambanaji na lingine linaitwa la mafisadi[yeye akiwamo]......alichotakiwa kufanya ni kuwamwaga wote ....aje na watu huru kabisa wasioegemea upande wowote...lakini kwa sasa ni wazi amecheelewa na kundi la mafisadi wanalo FAILI JEUSI la JK........
Tayari watanzania ambao walikuwa hawamfahamu jk wanaaza kuambiwa kuwa yeye alishakula rushwa ya IPTL ..Enzi akiwa waziri wa nishati..moja ya rushwa ya mwanzo ya nishati,rushwa ya Saclair...,na kuwafukuza wachimbaji wadogo wa madini,[wanasema alikuwa anatafuta pesa ya kugombea urais mwaka 1995], na ushahidi wanao nafikir wapinzani wameshapatiwa,rushwa ya pesa za ubalozini,..[Luhanjo anajua alikuwa PS wake Aliyehama naye].....EPA ..[kupata pesa za kugombea 2005],stimulus package, kuna list ndefu ya makampuni ambayo ana hisa au anamiliki ..,[inafanyiwa kazi]..,mwanaye ana malori mengi sana ya kupeleka mafuta ..na anachukua advantage lakupasuka mara kwa mara kwa bomba la TAZAMA ...isivyokaawaida...Congo connection..,kwa kifupi kuna uchafu mwingi sana sana ..ambao ina maana waliokuja na hii hoja ya kujivua gamba waatakuwa na kazi moja kubwa ya kuondoa mafuta kwenye maji...ili waweze kumwaga maji....wakikosea tu watamwaga na mafuta...

Uchaguzi mkuu wa ndani wa CCM mwaka 2012 ..utakuwa muhumi mno ku determine future ya hichi chama kikongwe na urais wa Kikwete ...na hata uwezo wake wa udhibitu kuelekea mwaka 2015.

Hii post nimeandika kama Mtanzania mzalendo ambaye nina uwezo wa ku analyse mambo kwa undani...sitegemei mtu aijibu kisiasa...mfikishieni!!!!

PM thanks for proving my hypothesis huu ulikuwa mtihani wangu wa PhD ya unabii ambapo proposal niliidefend three years ago; nadhani degree yangu karibu naiweka mkononi bado niko kwenye mwaka wa mwisho kabisaa na imebaki defence tu! I said hii ngoma hakuna wakuipangua iko well articulated kiasi kwamba hata wasiojua kuwa wako vitani wamekamata silaha ndogo ndogo na wako wamemweka adui (Ufisadi) katikati. Niliwasaidia na theory lakini inaonekana luga nayo iongea ina very high pitch kiasi kwamba wengi wanasikia kelele tu they can not perceive what I mean.

There is no way fisadi yeyote atakatiza hii ni tsunami mathematics hapo hakuna forumula itakubali nimesimama kabisa na miguu yangu yote grounded kwamba hakuna mvua kunyesha mpaka kwa neno langu kama Elija aliweza who am I to fail to do the same? Hapa anayeweza kupambana na mimi katika haya ni the opposite way ni labda Yahaya na wale wenye weak powers like him ambao nyote nimashahidi these days nimetoboa macho yake na kung'oa antena zake zote anaona chenga chenga tu kwenye tv zake zote na watazamaji wake wanamuuliza mzee vipi mbona picha imekataa kucheza?

Mbaya zaidi nimesha mwaga na petrol kwenye nyumba yao hapo sasa mwenye kuweza kuchomoka kupitia madirisha yenye gril ajaribu kama siyo wote wataangamia kwakukanyagana wakigombea kutokea mlango ambao ndiko petrol ilikoanza kuwashwa. I belong to neither camp ila ile inayopinga ufisadi kwa nguvu zao zote akili yao yote na kwa mioyo yao yote. And by this Taifa litaanza upya baada ya michanganyo mingi and come up with a gud governance ambayo haijalishi is from which party! Ningekuwa mimi ndiyo ninyi ningejiuunga kuimba praises and worship songs ili Alfa na Omega bwana wa vita amalizie kazi aliyoianza; Glory and honour be to our God the almighty whom I am not ashamed to be called his Prince. This is the word from your gospel preacher!
 
Mkuu;

Katika ile report ya Mzee Mwinyi ambayo Msekwa na Kinana; AK47 alitaka Mafisadi watoswe. Piusi Msekwa aka PM alitaka wabaki. Hawakufukuzwa. Sasa hivi katika CC iliyomalizika PM aliwataja Mafisadi kwa majina na AK47 ndiye aliyetoa wazo CC yote ijiuzulu.

AK47 alikuwa walikuwa na JK jeshini na ndiko walikofahamiana na yeye ndiye aliwakutanisha JK na EL. AK47 ana makazi Arusha ambako inawezekana ndiko alikokutana na EL akiwa pale AICC.

AK47 na EL wamesoma wote sekondari.......nadhani Old Moshi kama sikosei
 
AK47 na EL wamesoma wote sekondari.......nadhani Old Moshi kama sikosei

Ambako AK aliondoka na devision 0....akatoka kwenda kuwa activist wa TYL na baadaye jeshini ..akaja kuwa officer...na El alienda high school na badaye mlimani for BA ambako pia alikutana na JK....baadaye aliingia kwenye system kama msaidizi wa Sokoine ..later akawa kwenye moja ya directorate wa ofisi ya waziri mkuu,director AICC,mbunge.....waziri ofisi ya waziri mkuu[malecela]....etc etc.....
Ninasikia lowasa alipata millitary training kufikia cheo cha Luteni....beside JKT lakini ,sina uhakika nalo sana ..unless wenye kujua zaidi waseme..
 
Tunahitaji kuwa makini sana hapa!

Mi naamini huu wote ni mchezo wa kuigiza, mkuu wa kaya alishakubaliana na hawa jamaa wakae pembeni kwa muda. Hivi wataondoka ila wanabisha kidogo ili kunogesha mchezo ionekane CCM imefanya kazi kubwa kuwaondoa! Wakiondoka haraka watu watashtuka!

Vinginevyo kama ni kweli dogo Nape anatumika basi namwonea huruma, watamtosa wakishamaliza kazi naye kama Sitta alivyotumika kumng'oa Lowassa kwenye Richmond then wakamtosa.

Mwisho uchafu wa CCM is much much more than these three! ni mfumo mzima uliooza wa chama. Hakiwezi kusafishika kwa kuwaondoa watu wachache.
 
Hongera sana Rais Kikwete kwa kuwang'oa mafisadi CCM. Usirudi nyuma.Hatakama mafisadi watawatumia upinzani.Msimamo ubaka pale pale 90 days.No retreat no surrender. The determination should remain in force i.e 90 days. Nauye endelea kuwaumbua mafisadi wanaoitafuna nchi.Usiogope vitisho.Nchi ipo nyuma yako.We must purify our party which was doomed to die because of Mafisadi. Let the mafisadi go. Really, Kikwete you have left a legacy!

Kusema ukweli Raisi Kikwete amekoroga mchoro wa hii agenda na amejitengenezea kitanzi chake,pamoja na kwamba simpendi sana kwa jinsi ameifanya Tanzania ikawa ni Failed State lakini namuonea huruma kwa vipi atabaki salama na akaivusha nchi mpaka 2015 kama sio kunq'atuliwa kwa nguvu.
Kwa kipindi kirefu amekuwa akituhumiwa kujihusisha na uhujumu wa rasilimali za nchi kwa kupitisha na kuweka sahihi mikataba tata ikiwemo ya IPTL
Amewahi kutuhumiwa kwamba alitumia fursa ya vikwazo vya umoja wa mataifa kwa Ruanda kunyimwa fursa za kibiashara kwa yeye kuanzisha kampuni ya malori ya kupeleka mafuta Ruanda akishirikiana na Rostam

Amewahi kutuhumiwa kwamba alimtishia Mangula na Mkapa kulazimisha chama na serikali watafute fedha za uchaguzi 2005 na EPA ikazaliwa

Akiwa wizara ya Fedha ,fedha nyingi zilitoweka bila maelezo maalumu,ni vipi sasa yeye atachagua baadhi ya watu wachache akasema ni mafisadi huku akiacha msululu wa watu kibao nyuma akiwemo yeye mwenyewe,mwanaye na mtoto wa Mwinyi Dr Mwinyi, wanachama wa CCM wafanyabiashara wakubwa wanaotumia mwanya wa kupata tender miradi ya serikali kujinufaisha
Hana maelezo ya kutoa ruhusa ya stimulus package wakati yeye mwenyewe na govana wa benki kuu waliwahi kuthibitisha kwamba mtikisiko usingeweza kukumba Tanzania
hili ni goro,anataka kuyumbisha nchi na sasa amechanganyikiwa sana atashindwa kutimiza ahadi zake kama alivyotuahidi sasa hivi anakazana kuhakikisha hao mapacha watatu hawamzidi kete,na wao wanajua wakiachia ngazi wenyewe ni kwamba watafikishwa mahakamani na kesi zitapelekeshwa haraka ili wafungwe ukweli na wao hawatakubali kuondoka wenyewe wakati walikuwa kwenye syndicate ya umafia wakiwa pamoja na yeye,nadhani wamekurupuka kwenye strategy yao walitakiwa wawatose papo hapo
lakini unapotaka wajitoe wakati minutes za vikao za chama hazisemi hivyo si Jakaya na sekretariati ya chama chake wanajichimbia kaburi
Hii ni aborted operation na imeiweka mahali pabaya sana CCM ,ukweli ni kwamba wanaelekea kwenye safari ya mwisho watazikwa bila Sanda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom