Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,571
Waswahili nao pia wamo, pegamon waliopo pale Msasani kwa Nyerere ni kampuni ya wazalendo ila wao nao na uzalenndo wao sijui ni uzalendo gani kwani mashine zao wanauza bei ghali kuliko kwa wahindi hivyo kuwaforce wateja masikini kuendelea kuwakumbatia na kuwafaidisha wahindi badala ya wazalendo wenzetu!.Ndo maana hii biashara imejaa wahindi !
Nimetaka kununua EFD ya Incotex 500F wao wanaagiza direct toka kwa manufacture bei yao ni US $ 2000!, mhindi pale Freedom Electronics waliopo JM Mall anaagiza kupitia kwa agent, yeye anakuuzia the same machine kwa US $ 1,400!, wewe utanunua kwa nani?. Diference ya 600 US $ sio mchezo!.
Bahati tuu mimi niliweka mbele uzalendo nikachukua quotation ya mhindi ikionyesha US $ 1,400 na kumpelekea yule mswahili wangu wa Pegamon na kumuonyesha eti nae ndio angalau akakubali kushuka mpaka US $ 1,600 na nikanunua kwa uzalendo tuu kwa sababu kwa mhindi ningesave $ 200!.