Eeh MUNGU tusaidie!

snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,708
23,637
Mungu Baba,
najua mimi si mkamilifu kiasi cha kusogea mbele yako
najua sina utakatifu wa kuisogelea meza yako
lakini baba katika udhaifu wangu na wa wenzangu
twaja mbele yako tukiomba msaada wako
Baba ndoa nyingi zimekuwa ni vidonda .baba wanao tumekata tamaa
Baba wanao hatuna tena uwezo kwa nguvu zetu hizi za kibinadamu
tumefunikwa upofu hatuoni tena la kufanya kunisuru ndoa zetu
Baba hakuna lingine tunaweza fanya kama taasisi hii haiko sawa baba
tunajifariji kuwa tuko ok lakini ukweli ni kwamba mioyo yetu ni mitupu na nafsi zetu hazina urazini
hatuna amani kwenye familia zetu,hatuna furaha
Baba tuliowaamini na kuwakabidhi miili na mioyo yetu ndio wamekuwa visu vya kutuumiza
na mishale ye kututoboa,dhamiri zetu ni mfu si hai tena
ndoa nyingi Baba zimepoteza uelekeo,tunatembea kwenye ubatili,tunatembea kwenye uzandiki na ufedhuli
hakuna kujaliana tena kwenye ndoa Baba,maumivu ya wenzetu yamekuwa si yetu tena
ule umoja katika uwili tulioapa kuuishi sasa hauna maana tena
ndoa nyingi zimekuwa ni kwa ajili ya ridhiko la nje la mwanadamu zaidi ya ridhiko la ndani kabisa
nyama katika nyama zetu hakuna tena
damu katika damu zetu hakuna!\
Baba tupe busara tuzipende ndoa zetu
Baba tupe busara tuamini katika kupendwa na kupenda tena
Baba tupe busara ya kutimiza wajibu wetu tukiwa ni wake au waume
Baba tujalie roho ya msamaha na kuamini katika kusamehewa
Baba tuondolee roho ya kisasi maana ulisema kisasi si kazi yako KISASI NI KWA MUNGU!
Baba vita iliyopo dhidi ya ndoa mwanadamu na macho yake ya nyama hatuwezi kuipigana Baba
VITA HII NI YAKO NA HAKIKA MIKONONI MWAKO NAIKABIDHI
UKAWAJAZE KINAMAMA NA KINABABA WOTE NEEMA YA UPENDO NA KUCHUKULIANA
UKAWAPE BUSARA YA MALEZI WANANDOA WOTE MAANA KATIKA HILI LA NDOA ZILIVYOKOSA THAMANI NA MALEZI YANATUSHINDA BABA!
UWABARIKI WATOTO WETU! NYUMBA ZETU! WAUME ZETU! WAKE ZETU!
 
True love does nt look on externals with true love na dedication kati ya wapenzi,kumujumuisha Mungu katika mapenzi yenu,kuombeana hakika ndoa itadumu na itakuwa na furaha pia tukumbuke its was blessed for us. Ndoa ni takatifu

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Katika Jina La Yesu,tumeomba na kuamini..Amen. Mungu akubariki.

nawe pia ubarikiwe mamii!mi leo nimeamka nimepitia hizi thread humuu nimepitia za huku nakule,nimepitia jukwaa la sheri kule nako nakuta msaada wa kisheria unaombwa kwa kiasi kikibwa ni kuhusu ndoa(actually talaka),nikijumlisha na real life situation tunazokutana nazo kama story na zinazotuhusu nikaamua nisali tu maana nahisi hali ni mbaya zaidi tunavyofikiri!
 
True love does nt look on externals with true love na dedication kati ya wapenzi,kumujumuisha Mungu katika mapenzi yenu,kuombeana hakika ndoa itadumu na itakuwa na furaha pia tukumbuke its was blessed for us. Ndoa ni takatifu

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums[/QUOTE/] tena na ni KITU CHEMA!
 
nawe pia ubarikiwe mamii!mi leo nimeamka nimepitia hizi thread humuu nimepitia za huku nakule,nimepitia jukwaa la sheri kule nako nakuta msaada wa kisheria unaombwa kwa kiasi kikibwa ni kuhusu ndoa(actually talaka),nikijumlisha na real life situation tunazokutana nazo kama story na zinazotuhusu nikaamua nisali tu maana nahisi hali ni mbaya zaidi tunavyofikiri!

yani nakwambia, huyu mdudu anaekula ndoa za watu huyu!dah maana shetani amegandia kweli kuvuruga ndoa, wababa ndo wanatusumbua kila siku..wamama wanasumbua kaka zetu, vijana majizi kuchitiana ktk izo ndoa bubu za kila cku, yan mi natamani ingekuwa mtu kama cyo mtu wako alokupa Mungu, nanhii inagoma kata kata kuonekana,af kw wenye ndoa ukitoka nje inapotea. Ila majaribu yapo Mungu atuongoze tuyashinde.
 
Amina
Kweli snowhite tuna vita kubwa sana kwani vita hii si ya flesh na blood bali ni vita ya kiroho.

Tunahitaji kupingana roho zote za betrayal, roho za cheating, roho za ubinafsi, roho za wasiwasi na kutojiamini, roho za uchonganishi n.k.

Stratergy ya shetani, ni kuharibu kanisa la kwanza ambalo ni familia; the rest come easly.

Nguvu ya Mungu ikae nasi. Amina!
 
Last edited by a moderator:
:lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol:

hav a nice weekend
 
natamani ningekupatia kitabu kimoja kinaitwa 'kuponya majeraha katika familia zetu', kimeandikwa na Padre Baptisti Mapunda.

Ukikisoma hutatoka hivi hivi.
 
Ndoa ya kweli huwa haivunjiki...
Sababu kubwa ya ndoa kuvunjika ni kutokana na watu kuoa au kuolewa kwa kufuata tamaa za miili yao na wala sio unganiko la nafsi, roho na miili yao.
Watu huoana kwa kuangalia uzuri, mali, familia, kazi n.k....
Ukweli ni kwamba ndoa ya kweli hutoka kwa Mungu maana yeye ndio chimbuko la ungano baina ya nafsi mbili Me na Ke...
Hivyo basi wakati pekee muhimu ambao Mungu humsaidia mwanadamu kupata mwenzi bora ni kabla ya ndoa, kosa likifanyika hapo awali, mchawi wa matatizo atakuwa ni wewe mke na wewe mume na wala tusisukume hilo zigo la matatizo kwa Mungu...

"Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake, na hayo mengine yote mtazidishiwa..."
 
i am so scared lol
naona MMU Women mmegeuka wachungaji.....

na jinsi mlivyo good na ya dunia pia,its scary lol
 
i am so scared lol
naona MMU Women mmegeuka wachungaji.....

na jinsi mlivyo good na ya dunia pia,its scary lol

ukijua huu wenzio wanajua ule,kwa hiyo mbinu zote zinatumika ili MMU men muwe waumini wetu tu!na si wa wa wengine!
 
hili kanisa si la kitoto lol....

umeona enh manake tumeambiana kuwawekea udi weee mbado
tumeona tulegeze sauti weee mbado
tufundishane kupika weee mbado
tupeane unyago kwa PM weee mbado
tuwazalie watoto wee mbado kila siku watu wanalia humu
tuwapigie magoti wee mbado tu watu wanatafuta nje cup
sasa bora tu tufungue kanisa la maombi watu warudi kwenye mstari
yani mi kwa kweli huwa naumia kweli haya mambo yanayopostiwa humu ndani The Boss.shida ni kubwa rafiki yangu!ndoa nyingi sana mambo ni hovvyo hovyo!ukijumlisha na huku uraiani,maofisini bs dag!wacha tu MMU WOMEN tuwe wachungaji!
 
kuna mvurugano mkubwa mno
nafikiri inaaanza na watu kushindwa kujua
'how to live happily wenyewe'
kabla ya ku share that happiness na wengine
so mtu yuko miserable anasambaza misery tu kwa wengine
 
kuna mvurugano mkubwa mno
nafikiri inaaanza na watu kushindwa kujua
'how to live happily wenyewe'
kabla ya ku share that happiness na wengine
so mtu yuko miserable anasambaza misery tu kwa wengine
yaah ni kweli kabisa watu hatujui jinsi ya kuwa na furaha wenyewe ili tuwape furaha wengine
mi huwa nasema najipenda,nayapenda mapenzi,nafurahia kutoa mapenzi,nafurahia kupokea maoenzi
with this theory kusema ukweli naweza kabisa kusimama kifua mbele na kumwambia mwingine mapenzi si laana wala maumivu!si kwamba sina migogoro ndani ya penzi langu lakini kwa kuitanguliza theory hiyo mambo mengi sana mabyo mtu analiona ni tatizo kuubwa sana mi huwa linakuwa jepesi sana kulitatua!
hili la wengine kushindwa kwenye mahusiano na kwenye ndoa zao na kuwaaminihsa wengine kuwa ndoa ni mateso nafkiri ni aina tu ya hulka ya mwanadamu kutafuta unafuu!vinginevyo dah!so saad kwa kweli!
 
Ameen dada snowhite, lakini haya yote yalitabiriwa katika biblia. nyakati za mwisho upendo wa wengi utapoa na ndivyo inavyotokea katika ndoa na maisha kwa ujumla. Amani imetoweka, shetani anajua wakati wake ni mfupi sasa anajitahidi kuvunja nguzo kuu za amani ambazo ni imani (dini) na ndoa. kwani ukiwa na imani thabiti ndoa yako itakuwa imara. sasa anaamua kuvuruga imani za wengi then hofu ya Mungu inatoweka na wanandoa wanafarakana. Ee Mungu utusaidi kusimama imara katika imani . . . Amen!
 
AMEEEN! charminglady si unajua nguzo ya familia ikiparaganyika ndo kila kitu mpaka taifani ni tatizo.kweli kabisa shetani amezikamia familia jamani!angalia jinsi migogoro mingi inavolipuka wakti wa maandalizi ya harusi?simply becoz hataki watu waoane,na matokeo yake wakioana anawaandama kwenye ndoa mpaka inakosa thamani!watu siku hizi kuachana au kutengana baada ya mwaka tu ni kama kawaida na wala jamii haistuki!hili tatizo ni kubwa sana basi tu kutokana na mazoea yetu ya kutokuzungumza,ndo mana tawimu sahihi zinakosekana!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom