Edward Moringe Sokoine 1938-1984 | Historia na wasifu wake

katika nchi inayojali haki na usawa majeshi hayana budi yawe ni chombo cha kulinda haki na maslahi ya walio wengi.NA KAMWE HAYARUHUSIWI KUWA NI CHOMBO CHA WACHACHE WENYE KUJALI NAFSI ZAO NA KUSAHAU MASLAI YA WALIO WENGI.
 
Wakati Moringe anauwawa pale dakawa-dumila cdm ilikuwepo? huna haya! wakati Karume anauwawa cdm kilikuwepo? huna akili! wakati wasomi wazalendo walikua na mitazamo kingano walipotimuliwa nchini kama kina Fundikira cdm ilihusika? huna uzalendo! komboa fikra zako! cdm si mpinzani wa Tanzania wala mtanzania ila ni mpinzani wa mfumo gandamizi wa mtumwa na mtwana.

Mawazo yako yanafana na Chama chako cha kigaidi.
 
Mkuu miaka hiyo wote tuliitana Ndugu, ila Sokoine alikuwa kiboko. Nakumbuka baada ya kutangaza vita dhidi ya wahujumu uchumi wahujumu walitupa baharini na makaburini magunia ya sukari na vitu vingine vingi ili wasikamatwe. Nakumbuka katika makaburi ya Kisutu zilitupwa hela na watu waliogopa kuziokota kwa kujua watakamatwa.
 
1983 Mwalimu akiwa Mapumzikoni Butiama Comrade Moringe alianzisha Operation kamata wahujumu Uchumi, Akawatia ndani Familia ya John Rupia ( mfadhili na Mmoja wa waanzilish wa Tanu), Mwalimu aliahirisha mapumziko kuja kumuokoa Ndugu Rupia), kwa viwango vya ujasiri na uzalendo Sokoine alimzidi hata Nyerere!
 
jamii inapaswa kumuenzi sokoine kwa vitendo na si maneno record sote tunazijua ila vitendo vyake nani anajalibu atakufanya?
 
Sokoine ni kiongozi mwenye ujasiri kuwai kutokea katika nchi hii mungu ailaze roho yake mahala pema peponi amina.
 
wandugu, napenda sana kupata machapisho yanayomhusu kiongozi huyu! nimejikuta ktk wakati mgumu nilipokuwa nafanya maswali yanayohusu Transformational leaders nakujikuta namtolea mfano Edward Moringe Sokoine ila sina facts za kutosha...napenda ningepata vitabu au paper zinazomhusu.

Msaada tafadhali...
 
1609985_445731172237363_694304353_n.jpg


"Vijana wengi wana mali zaidi kuliko wazee waliofanya kazi miaka thelathini hadi arobaini. Lakini wanaitaka Serikali ndiyo iwaulize mali hiyo wameipata wapi. Hivi kwa nini mzazi asimuulize mwanaye; mali hii umeipata wapi.?"

Edward Moringe Sokoine.
Waziri Mkuu wa Zamani.
23rd October 1983.


 
Alizimika kama mshumaa kwa ajali mbaya ya gari akitokea Dodoma kwenda Dar
Ni kipindi ambacho alikuwa kwenye kipindi cha mapambano magumu ya kupambana na rushwa na wahujumu uchumi
Tunapokaribia kuadhimisha miaka 30 ya kifo chake je tuna lolote la kujivunia ?au tumefanya juhudi gani kuzienzi na kuziendeleza zile juhudi zake za kupambana na wahujumu uchumi na wals rushwa ?
 
He was a man of people, Sokoine hana wa kufananishwa naye kwa leo hii, ukitaka kuamini kuwa alikuwa threat, nenda Wami Sokoine - Dakawa utapata picha kama kweli waliopo madarakani wana nia ya dhati ya kuenzi juhudi zake, kiasi cha fedha zilizokuwa zinatajwa kwenye vifungu kuwa zinaelekezwa kutengeneza eneo alilofia ili iwe kumbukumbu yake ni tofauti na thamani ya kazi iliyofanyika pale na hakuna anayehoji wala kuchukua hatua,
 
He was a man of people, Sokoine hana wa kufananishwa naye kwa leo hii, ukitaka kuamini kuwa alikuwa threat, nenda Wami Sokoine - Dakawa utapata picha kama kweli waliopo madarakani wana nia ya dhati ya kuenzi juhudi zake, kiasi cha fedha zilizokuwa zinatajwa kwenye vifungu kuwa zinaelekezwa kutengeneza eneo alilofia ili iwe kumbukumbu yake ni tofauti na thamani ya kazi iliyofanyika pale na hakuna anayehoji wala kuchukua hatua,
Nchi ya kitu kidogo...! Maccm hapa wamepita kimyakimya ila ingekuwa uzi wa kuikandia CDM pangefurika
 
Ukweli ni kwamba vichwa kama vile havizaliwi tena.Zaidi ni uwepo wa watu walio geuka kuwa mawakala,madalali,manamba na vibarua wa rasilimali za nchi kwa walafi wachache.Hakuna wa kumuenzi sokoine.
 
Back
Top Bottom