Edward Lowassa on ITV!-Dakika 45 Part II!.

I have changed my attitude towards Lowassa,this guy is brilliant.He spoke to our issues.One thing which touched me is his concerns on the recent skyrocketing of unemployment rate among youth and the mechanisms on how to curb it.For the first time I do agree with Lowassa that we should end this political circus and focus on renewing our Economy.

Even JK said so in 2005. The problem is HOW? Can he walk the talk?
 
Pasco,
Tuliopitwa na kipindi unawezaje kutusadia ku-summarize yale aliyosema?
Vinginevyo atahukumiwa kama Lowasa bila kujua amesema nini.
Je inatosha kusema nakubali au kumkataa 100%
 
Pasco EL amechelewa,amechafuka sana nafuu yake ni kumchana JK mbele ya Press conference ili ajisafishe na dowans maana mpaka sasa tulipata uhondo kidogo tu wake kwakuwa wewe ni mtu wake wa karibu muambie mh atiririke kuhusu jk alivyohusika na dowans from a to z,mwambie taifa kwanza urafiki baadae!
 
Pasco,
Hivi zile sababu za mwaka 1995 zilizomwondoa kwenye kinyang'anyiro cha Urais mapema tu kabla hata kupigiwa kura zimefutwa? Kuna siku alisafishwa? Na nani? Na kikao gani? Utakumbuka sababu kama hizo zilimwandama JSM alipojaribu tena mwaka 2005.
Alikuwa makini jana alipojibu swali la Urais kwa kifupi tu kwamba "atavuka daraja" atakapolifikia. Na mimi naamini kwa CCM hii hata hilo daraja hataliona. WATANZANIA hatuko tayari tena kuiweka sokoni nafasi hii.
 
Pasco Heshima mbele!
Naomba unijuze kama kweli CCM watakuwa tayari kumsimamisha EL kuwa mgombea wao wa nafasi ya urais!
Mkuu Skills4ever, hili ni swali zuri kwa sababu linahusu utayari wa CCM kumsimamisha EL,

1. Kwa kuanzia, naomba kwanza nisisitize kuwa CCM kama chama tawala, ndicho kimelifikisha taifa letu hapa lilipo, CCM yenyewe tuu is not an entity, hivyo CCM haina matatizo, wenye matatizo ni viongozi wa CCM, hivyo wabaya wetu waliotufikisha hapa sio CCM bali ni viongozi wa CCM na hao ndio tutakao waadhibu kwa kuwachapa bakora vilivyo, come 2015!. Lakini pamoja na ubaya wote wa viongozi hawa wa CCM, miongoni mwao, bado kuna watu safi CCM, watu wenye impecable integrity ya kuliongoza taifa hili kwa uadilifu wa hali ya juu na kuondoa uoza wote uliomo ndani ya chama chao!.

2. Hakuna ubishi CCM kama chama tawala, kimechokwa, Watanzania wanalijua hilo na CCM wenyewe pia wanalijua hilo, tena in fact kilichokwa siku nyingi, na udhibitisho ni idadi kubwa ya Watanzania wanaojiandikisha kupiga kura halafu hawapigi kura kutokana na kukata tamaa na CCM lakini pia kulikuwa hakuna any serious mbadala kwa upande wa bara, hivyo CCM imekuwa ikiendelea kuchaguliwa kwa mazoea tuu, kwa 2015, Chadema inaonyesha seriousness zake, hivyo kwa kuchaguliwa tena kwa CCM 2015 sio kwa mazoea tena, lazima ifanyike kazi, tena kazi kubwa na sio ile ya t-shirt, kofia na shibe ya siku 1!.

3. Ni kwa kuzingatia hayo, mgombea wa CCM 2012, lazima awe ni mgombea powerful, mwenye uwezo usiotia shaka kuwa akisimama, wapinzani watany'ongonyea, ndani ya CCM hakuna mwingine yoyote mwenye uwezo huo zaidi ya EL, hii inamaani CCM watake, wasitake, they have one and only option ya kumsimamisha EL, ila kiukweli, kufuatia afya yake kuwa mgogoro, kwa jinsi nilivyomuona akizungumza, anatoa maneno makali kwa sauti yenye fire on hisi ayes, and fear is the weapon on his heart, hivyo body language isaonekana wazi, "he is a sick man"!, hivyo hawezi kuhimili mikiki mikiki ya 2015, hivyo CCM kulazimika kumsimamisha Membe, na itamlazimisha EL avunje kambi yake na kuihamishia kwa Membe!.
 
Lowassa,,,,,its tym to rest baba,,,,,eeenh,,,pia anayesema Lowasa ni waziri mkuu mstaafu ana akili kweli?????
 
Nafasi hii ya URAIS wa JMT 2015 tuipeleke ZANZIBAR kwa Shamsi Vuai Nahodha. Huku bara watu wamepigana ngeo vibaya sana. Hakuna dalili kwamba majeraha haya yatapona kabla ya 2015. Hili JK na CC yake ya CCM wanaliweza kwani waliweza kuweka sharti linalofanana na hilo kwenye USPIKA wakamudu. Sitta akashindwa kubadili jinsia yake na sasa yuko kule kwenye Cabinet akirusha vijembe vya hapa na pale!
 
Mboan 2015 mbali sana?
Sio mbali Manyi. Jamaa wanavyohaha kuitafuta nafasi hii ni balaa. CCM na vyama vingine wangefungua milango tukawajua wanaoutaka URAIS ili tupate muda wa kutosha kuwajadili na kuibua mapungufu yao. Wanapowabana hadi dakika za mwisho inabidi mapesa yatumike kwa wingi.
Nawaonea wivu jirani zetu KENYA ambao wameliweka wazi sana suala hili na sioni kama lina madhara yoyote kwa utendaji wa serikali yao. Wameweza sana kutenganisha SIASA na DOLA.
 
Ndahani,
Kikwete alianguka jukwaani kesho yake akapigiwa kura 80% akawa Rais. Nchi hii ukizungumzia afya za hawa wanaSIASA wetu hakuna atakayestahili kuwa Rais. Si uliona walivyomiminika kule kwa Babu wa Loliondo kupata kikombe?

Nimekuelewa ingawa wasiwasi wangu kama ni kiharusi, that damn thing could be terrible. Na hizi stress za kuongoza nchi kama hii ndo kabisa
 
nami nimejiuliza huyu mtu ana akili???anayemwita Lowassa waziri mkuu mstaafu?????
Mkuu Bajabiri, kama hivyo ndivyo alivyoandikwa kwenye protocali, anakuwa addred hivyo na analipwa mafao yake yote, tumwiteje?, Mwenyeakili ni yupi kati ya yule anaye muasdress mtu anavyoandikwa au ambae hana namna nyingine yoyote ya kumu adress mtu lakini anaumia kila anapoitwa jina lake stahiki!.
 
Anasema Angekuwa Rais angechukua mamia ya wanajeshi apande mahecta ya michikichi tungepata mafuta mengi tungejenga kiwanda Iyo ni mbinu moja na anazo Mia moja
hehehe! anauhakika itakuwa kwa kuwa anajua kutengeneza mvua!
 
....[/QUOTE]
Mkuu nadhani ana kiharusi, kule kutetema na uso kuchoka, kunatokana na Black Label!, akiacha kutaacha!.
 
Back
Top Bottom