Edward Lowassa na mvua toka Thailand

Wanadai huyo ndo rais wetu ajaye bongo kila kitu kinawezekana unaunda deal unakabidhiwa fungu halafu unazuga watu wanasahau hakuna mtu atakuja kukuuliza na hilo fungu sijui lilitoka kwenye budget gani hivi CAG mambo kama hayo huwa hana authority nayo kufanyia auditing au ndo fungu la ikulu lisilokuwa audited kuficha ubadhirifu kweli hatuna viongozi.
 
Lowassa akatuambia kuwa ili Mtera ijae tungehitaji mvua km za elnino vinginevyo kwa mvua za kawaida basi ni lazima mvua zinyeshe mfululizo kwa miaka mitatu, hivyo mvua za Thailand zilikuwa ni lazima. Mungu hachelewi kumwumbua mnafiki, mvua ikanyesha kwa wiki mbili tu bwawa la Mtera likajaa mpaka wakafungulia maji. Hii ndio bongo!
 
Tatizo letu kubwa ni kushambulia mtoa hoja badala ya kuchangia kwa hoja kulingana na ulivyoifahamu mada. Kama huna taarifa za kutosha kuhusu mada husika bora kutojiingiza kwenye mjadala na kusababishia watu kutapika. Teknolojia ya mvua za aina hiyo ipo na inatumika sehemu nyingi duniani kama baadhi ya wachangiaji walivyosema. Nilichohoji mimi, kama mpango huo ulikuwa umeshafanyiwa research na analysis ukaonekana unafaa kwanini haukuendelezwa baada ya Lowassa kuachia ngazi kwa kashfa ya Richmond? Je, kulikuwa na madudu yale yale kama ya Richmond ndiyo maana haukuendelezwa? Au labda haukuendelezwa kwa sababu ya kuhofia kumjenga jamaa kisiasa? Hayo ndiyo ya kujadiri.
 
inawezekana sana, mitambo hii inatumika sehemu nyingi duniani mfano Saudi Arabia. Mitambo hii inafaa kwa Dar kwa sababu bahari ipo jirani na tunazalisha thermal power kutoka gas asilia. Tatizo tumezoea "cutting corners" bila kuzingatia best practices.
kwa hiyo hakuna uhalali wa nchi kama zenji kule kukosa maji ya kunywa?? maana nachojua maeneo mengi ya baharini hayana maji na tatizo ni miundombinu na technology....
 
Utata mtupu lakini watanzania wa sasa kwa nongwa we acha
Ukiahidi jambo wanalo hilo mpka wazae na wewe chezea Bongo wewe
 
kwa hiyo hakuna uhalali wa nchi kama zenji kule kukosa maji ya kunywa?? maana nachojua maeneo mengi ya baharini hayana maji na tatizo ni miundombinu na technology....

If and when nchi ya Zenj itaamua kuzalisha umeme kwa kutumia gas asilia, basi technology hii itasaaidia kuzalisha maji safi pia. Mfano mradi wa Ummalnar Abu Dhabi unazalisha 1500 mw pamoja na maji safi 94 million gallons daily sawa na ujazo takriban 400,000 cubic metre daily(zaidi ya daily water demand ya jiji la Dar) www.power.mottmac.com/projects2/thermalanddesalinationprojects/ummalnar/
 
If and when nchi ya Zenj itaamua kuzalisha umeme kwa kutumia gas asilia, basi technology hii itasaaidia kuzalisha maji safi pia. Mfano mradi wa Ummalnar Abu Dhabi unazalisha 1500 mw pamoja na maji safi 94 million gallons daily sawa na ujazo takriban 400,000 cubic metre daily(zaidi ya daily water demand ya jiji la Dar) www.power.mottmac.com/projects2/thermalanddesalinationprojects/ummalnar/
Mkuu hii technology ni kiboko......kuna vitu hpa natamani kuelewa
1) Gharama zake zikoje upande wa INITIAL COST na ONGOING COST??
2)Vipi upande wa technology yake iko advanced sana au ni ya kawaida tunaweza kuitumia hata sisi 3rd world countries
3)Kama process ni distillation vipi kuhusu kuyarudisha madini muhimu kwenye maji??
 
Ni kweli alichosema Mtoa Mada, hata mm wakati nasoma kidato cha Pili kuna Dada nilikuwa nampenda sana sema akazingua, nikaona isiwe kesi nikamtafuna rafiki yake
 
weka video ikionyesha hayo maneno nione
Dodoma.Suala la mvua za kutengeneza kutoka nchi ya Thailand maarufu kwa jina la ‘Mvua za Lowassa’ liliwagonganisha mawaziri wawili wa Serikali bungeni jana.
Ubishi mkali ulizuka baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, Dk Terezya Huvisa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi waliokuwa wakivutana juu ya ukweli kuhusu teknolojia hiyo.
Wakati Waziri Huvisa akisema kwamba hakuna utaalamu wa aina hiyo, Lukuvi alisimamia kumpinga na kusisitiza kuwa jambo hilo lipo.
Suala la mvua hizo lililetwa nchini na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa mwaka 2007, baada ya kufanya ziara Thailand ambako alivutiwa na utaalamu wa kutengeneza mvua na kuahidi kuuleta nchini.
Kutokana na mvutano wa mawaziri hao, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alipewa dakika moja na Mwenyekiti wa Bunge, Jenister Mhagama kutoa ufafanuzi ambapo aliunga mkono hoja ya Lukuvi.
Malumbano hayo yalisababishwa na swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo ambaye alihoji mpango wa kutengeneza mvua ulipoishia kwa kuwa Serikali imekuwa kimya.
“Sasa ni miaka takriban sita au saba tangu Serikali ilipokuja na mpango wa kutengeneza mvua ambao iliuchukua kutoka nchi za wenzetu, mpango huo umefikia wapi?” aliuliza.
Akijibu swali hilo, Waziri Huvisa alisema: “Mimi ni Rais wa Mazingira wa Afrika, nasema hakuna kitu kama hicho, si Marekani wala Malaysia ambao wanaweza kutengeneza mvua, hayo ni mabadiliko ya tabianchi tu.”
Waziri Lukuvi alionyesha kutokuridhishwa majibu hayo, ndipo aliposimama kutoa ufafanuzi na kusema Lowassa alikwenda Thailand ambako kuna utaalamu huo na kusisitiza kwamba upo na bado unaendelea kutumika hata Ujerumani wanakotumia mitambo ya kijeshi kusambaratisha mawingu.
Alisema kilichokwamisha mpango huo nchini ni ufinyu wa bajeti ya Serikali.
Baada ya majibu hayo, Lowassa alisimama akitaka kutetea wazo lake. Hata hivyo, kabla ya kumruhusu, Mhagama alimwomba akae chini kwanza ili atoe maelekezo.
“Mheshimiwa Lowassa, yeye siyo waziri na hivyo hastahili kutoa majibu ya Serikali, lakini kwa kutumia kanuni zetu bungeni kuhusu kutengeneza utaratibu mzuri wa kuongoza Bunge, naomba Lowassa usimame sasa walau kwa dakika moja au mbili utoe ufafanuzi,” alisema Mhagama.
Aliposimama Lowassa alizungumza kwa ufupi; “Nakushukuru Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kukazia tu kuwa jibu lililotolewa na Mheshimiwa Lukuvi ndilo jibu sahihi.”
Majibu hayo yalisababisha Bunge kulipuka kwa shangwe.
Mara baada ya majibu ya Lowassa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza naye alisimama akitaka kutoa maelezo. Hata hivyo, Mhagama alisema inatosha na kuwaagiza mawaziri hao kukutana kuliangalia jambo hilo badala ya kuwa na majibu kinzani.
Awali, katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Rachel Mashishanga alitaka kujua ni kwa nini Serikali isirasimishe utaalamu wa kuleta mvua kutoka kwa waganga wa jadi walioko Mikoa ya Katavi na Rukwa ili maeneo yanayokabiliwa na ukame yapate mvua?
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, alipinga mpango huo na kusema hakuna kitu kama hicho isipokuwa wapo watu wenye utaalamu wa kuangalia mawingu yanayoendana na mvua.
Alisema watu wote wanaosema kuwa wanaweza kutengeneza mvua kwa imani za kishirikina ni waongo na hivyo hawapaswi kuaminiwa.
Alisema siyo wakati mwafaka kwa Serikali kushinikizwa kurasimisha utaalamu huo wa kuleta mvua kwa kuwa hakuna tafiti zozote zilizofanyika na kuthibitisha kuwapo kwake.
 
Back
Top Bottom