Edward Lowassa aumbuka Arumeru Mashariki

Nguvu ya Lowasa iko kila mahali kuanzia humu JF. Ndio maana hatuishi kumtaja karibu kila siku. Kila TAASISI au KIKAO cha CCM Lowasa ana nguvu ya peke yake. Nilikwenda Bungeni kikao cha bajeti mwaka jana, Wabunge wengi wanamwabudu na kumsujudia Lowasa.

ndio tumebadili katiba ili kuwapa nafasi waheshimiwa wabunge wetu akiwemo yeye wachague kutumikia ubunge ama chama(ujumbe wa nec),bonge la mtego ambalo linawatesa watu huko wanakunywa "wiski" usiku kucha usingizi haupatikani,unajua wabunge wengi walikua wanaamini jamaa atakua rais sasa kila mtu akawa anajipendekeza kumzuga tu ili akifanikiwa asiwasahau kwenye ufalme wake,baada ya mabadiliko ya katiba ya ccm haya juzi uende bungeni tena kama mtu atakua na time nae zaidi ya wapambe wake wa kudumu wa miaka yote kama peter labd na yule mama chilolo anaekaa nae karibu pale kwenye kiti chake bungeni
 
Mkuu WildCard ingawa ni vizuri kuelimisha na kutoa maarifa kwa wengine lakini sidhani kama KK anakupata kwasababu hamko ktk viwango vinavyolingana! Pole sana mkuu wangu.
 
Mkuu WildCard ingawa ni vizuri kuelimisha na kutoa maarifa kwa wengine lakini sidhani kama KK anakupata kwasababu hamko ktk viwango vinavyolingana! Pole sana mkuu wangu.

Huyu lazima mwanachama wa chama cha vinega huyu,vipi we kinega iko chama chenu bado tu hakimtabui rais au?
 
Takukuru Leo wameamua kumgeuka Edward Lowasa na vibaraka wake katika marudiano ya uchaguzi wa Arumeru. Katika sakata Hilo katibu wa uvccm wilaya ya Monduli ndugu Ezekiel Mollel ametupwa rumande Mara baada ya kukamatwa na simu yake ilipo pekuliwa na kukutwa na mesej alizokuwa Akiwasiliana na Lowasa kuhusu kuchukua hela kwa askofu na mathius manga kwa Lengo la kwenda kuwahonga wajumbe wa arumeru Mashariki.

Katibu huyo amekiri kupewa maelekezo hayo na Lowasa na kuomba asamehewe k
 
Iwapo yaliyosemwa ni kweli basi hali ya nchi ni tete. Askofu gani huyu anayetajwa? Kwa nini wasiwakamate watoa fedha sawa na wasambaza fedha? Hawa takukuru ni genge jingine la uhalifu nchini. Sina imani nao hata kidogo kwani baada ya mida mtasikia waliokamatwa wameachiliwa kwa uchunguzi au ushahidi wa takukuru haujitoshelezi. Wizi mtupi!

ni mfanya biashara maarufu wa tanzanite AR
 
Kwanza mi naombea EL ndio angewekwa lupango. Ila hapo waliowekwa lupango ni watu tofauti..
Sioi na EL wapo wanatanua mtaani, hata hawajahojiwa.

Endapo stori hii ni ya kweli.....basi sioni ni kwa vipi EL nae asiwekwe ndani! Meseji hazikatalika no matter what unless kama alikuwa anatumia namba maaulumu ambayo aliinunua kwa muda kwa shughuli maalumu....na kwa jinsi nchi hii watu walivyo wazoefu wa uhalifu basi sina shaka kwamba ni kweli hiyo ni namba maalumu ambayo hata kusajiliwa haijasajiliwa!
 
Hii habari kama ni ya ukweli basi hapa kuna ngoma mbili ambazo zinachezwa! Kwanini? ieleweke kua mpaka sasa hivi kuna kambi mbili ndani ya CCM ambazo zinashindana katika uchaguzi huu, kambi ya kwanza CCM nikutoka kwa EL na kambi ya pili inatoka kwa JK ieleweke pia TAKUKURU hii ndio ilyobaini michezo michafu katika chaguzi zilizopita mfano hata hapa Arusha mjini kwenye kura za maoni kwenye uchaguzi wa Uraisi na Madiwani na Wabunge Takukuru hii ilimshika Filex Mrema kwenye kura za maoni na rushwa Ready Handed! Lakini Takukuru hawa wakuchukua hatua zozote na siye yeye tu ni wengi kwenye nchi hii! Sasa tunachokiona hapa Arumeru Mashariki ni kua Kambi rasmi kutoka ndani ya CCM inapambana na kambi ya EL kwakua kila kambi inataka kumuweka mtu wake ndio maana utaona JK aliamuru uchaguzi urudiwe tena kwakua kuna mchezo mchafu unaendelea ndani ya kwao wao wenyewe CCM! Iweje leo Takukuru hawa kujifanya eti wanawajibika? Hii ndio hali halisi kutoka Arumeru Mashariki.
 
stori za kijanja-kijanja....!mbinu-mbinu...!maarifa-maarifa...!
 
Bado Jacob Zuma mpaka kufa kwangu ndio atakuwa Mwalimu wangu wa siasa hizi za majitaka za kiafrika, Lowasa nina kila sababu ya kuamini ndio Jacob Zuma wa Bongo, kinachowatofautisha tu ni kwamba huku kwetu Lowasa wanamuogopa kumpeleka Mahakamani maana wataumbuka wao kama Costa Mahalu anavyowaumbuwa sasa hivi.

Mahalu alidai kuwa katika mazungumzo hayo, Kikwete alimuuliza mama huyo, "Hivi ni kwanini kunakuwa na mikataba miwili? na mama huyo alimjibu kuwa hiyo ni kawaida kwa Italia ukitaka kununua jengo kwa bei nafuu.

Profesa Mahalu aliendelea kudai kuwa baada ya kupewa jibu hilo, Kikwete hakuzungumza tena zaidi ya kucheka na kwamba mwenye jengo alimkumbusha kuhusu malipo ya awali ya Dola za Marekani milioni moja ambapo aliafiki na kuahidi kuwa zingelipwa kabla ya mwisho wa mwaka.
 
mzee issue hapa tunataka utuoneshe zilipo nguvu za lowassa hutuonyesha unatapa tapa tu mara utupeleke ukada mara uturudishe kwenye remote ya batteries mpya,tuonyeshe nguvu za lowassa alizobaki nazo,mimi kukurahisishia ntataja alizokuwa nazo ambazo sasa hana tena..

-alikua waziri wetu mkuu kwa miaka isiyozidi mitatu,sasa sio waziri mkuu tena wala hayuko kwenye cabinet
-alikua mjumbe wa kamati kuu sasa hayuko tena huko
-alifight sana kurudi kwenye baraza la mawaziri hakuweza kurudi
-yeye kupitia kwa wapambe wake kina bashe waliapa kwamba ubunge wa igunga unaenda upinzani wakashindwa vibaya sana
-alipenda sana suala la kujivua gamba lizimwe na nec lisiende kamati kuu akashindwa licha ya kulilia sana aonewe huruma na mwenyekiti eti kwa kuwa na yeye mwenyekiti aliwahi kuonewa huruma na mkapa haikumsaidia sana
-aliomba nape aadhibiwe kwa kumpulizia vuvuzela ambalo hapendi kulisikia masikioni hakuna aliyemsikiliza
-kwenye nec ya juzi aliwatumia wapambe wake kingunge na peter serukambaa wapinge mabadiliko ya katiba yatakayomchinja yeye kwenye uchaguzi ujao wa ccm lakini wajumbe wa nec ileile ambayo huwa tunaambiwa ana nguvu wakasema hapana mzee tunamuunga mkono mwenyekiti akiimarishe chama,akashindwa tena kwa mar nyingine ndani ya nec yake
-Na sasa kuna hili mkwewe kugombea ubunge arumeru ndio watu wake wamekamatwa na jina lake kwa mara ya kwanza limetajwa na vyombo vya usalama...
Haukujibu swali langu KK! Haya unayoyaeleza hapa hayajampunguzia nguvu Lowasa. Na mengine yamemfanya kuwa na nguvu zaidi. Narudia swali langu: Kwa nini kura za maoni CCM kule AruMeru zinarudiwa?
 
Takukuru Leo wameamua kumgeuka Edward Lowasa na vibaraka wake katika marudiano ya uchaguzi wa Arumeru. Katika sakata Hilo katibu wa UVCCM wilaya ya Monduli ndugu Ezekiel Mollel ametupwa rumande Mara baada ya kukamatwa na simu yake ilipo pekuliwa na kukutwa na mesej alizokuwa Akiwasiliana na Lowasa kuhusu kuchukua hela kwa askofu na mathius manga kwa Lengo la kwenda kuwahonga wajumbe wa arumeru Mashariki.

Katibu huyo amekiri kupewa maelekezo hayo na Lowasa na kuomba asamehewe kwa kuwa Lowasa ni kiongozi mkubwa yeye asingeweza Kuwa na ujasiri wa kumkatalia. Hadi wakati huu Ezekiel Mollel na Askofu wapo rumande.

Pia katika tukio lingine Fred Lowasa amethibitika kumhonga ticket ya ndege Elirehema kaaya ili amsaidie Sioi aweze kushinda. Kwenye simu ya elirehema Kaaya zimekutwa mesej Kuwa nakulipia ndege pamoja na kukupa lile fungu la kuwapelekea wajumbe. Kwa ushahidi huu hadi sasa elirehema Kaaya yupo rumande.

Wakati wowote mambo haya yatapelekea wahusika kupelekwa mahakamani.

Wana Arumeru mashariki wafanye uchaguzi kwa amani na utulivu na tena wasiwe na hofu yoyote.

Ya kweli haya uliyoanadika mba imekaa kiudaku sana!?????????
 
Kama haya ni ya kweli nasubiri kuona na kusikia yafuatayo:

1. Takukuru na Jeshi la Polisi watasema nini,

2. Chama cha Mapinduzi na hasa CC, watasema nini kwa hili.
 
ndio tumebadili katiba ili kuwapa nafasi waheshimiwa wabunge wetu akiwemo yeye wachague kutumikia ubunge ama chama(ujumbe wa nec),bonge la mtego ambalo linawatesa watu huko wanakunywa "wiski" usiku kucha usingizi haupatikani,unajua wabunge wengi walikua wanaamini jamaa atakua rais sasa kila mtu akawa anajipendekeza kumzuga tu ili akifanikiwa asiwasahau kwenye ufalme wake,baada ya mabadiliko ya katiba ya ccm haya juzi uende bungeni tena kama mtu atakua na time nae zaidi ya wapambe wake wa kudumu wa miaka yote kama peter labd na yule mama chilolo anaekaa nae karibu pale kwenye kiti chake bungeni
Badiliko hili wala halina TIJA kwa CCM. Ni mjinga tu atakayeacha UBUNGE akagombee U-NEC wa CCM. Ni moja ya mabadiliko ambayo yanahanikizwa na nguvu nyingi walizonazo baadhi ya watu kuliko CCM na vikao vyake. Subiri tu kuonyeshana nguvu kutakakojitokeza ya MNEC wa CCM na Mbunge wa CCM.
 
Loh!!! TZ inahitaji roho mtakatifu ili tubadilike..., kama ubunge haulipi sasa hao kwanini mpaka waonge hayo mapesa yote mpaka waupate!!!. Nadhani siri wanaijua wenyewe!!!.
 
Badiliko hili wala halina TIJA kwa CCM. Ni mjinga tu atakayeacha UBUNGE akagombee U-NEC wa CCM. Ni moja ya mabadiliko ambayo yanahanikizwa na nguvu nyingi walizonazo baadhi ya watu kuliko CCM na vikao vyake. Subiri tu kuonyeshana nguvu kutakakojitokeza ya MNEC wa CCM na Mbunge wa CCM.
Don't waste ur time Man, CCM ni chama ambacho kimeshakufa kinachofanyika sasa ni postmortem ya kuhalalisha sababu ya kifo cha marehemu.
 
Back
Top Bottom