EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,483
- 15,308
Haya yalikuwa ni matangazo ya moja kwa moja kutoka Uwanja wa taifa mjini Dar es salaam kupitia redio Tanzania Dar es Salaam,"Mpira unatoka katika lango la timu ya Dar Yanga Afrikans kuelekea katika lango la timu ya Simba "Taifa Kubwa", Golikipa wa Yanga Steven Nemes anaupiga mpira vizuri kabisa hukuuuuu anauchukua Said Mwamba Kizotaa Kizotaa anampasia Method Mogella Mogella pembeni kabisaaaa anampelekeaaa kwakeeee Salum Kabunda Kabundaa Kabunda kwakeee Constatine Kimanda Kimandaaa anapeleka mpira kwa Ken Mkapa Ken Mkapa Mkapa Mkapa anatoa pasi ndeeeefuuuuu kwake Lunyamila Lunyaamiilaaaaaa Lunyamilaaaa chenga ya kwanza chenga ya piliii Lunyamila bado Lunyamilaaaa Lunyamilaaaa hatari katika lango ya timu ya Simba lalalalalalalal gooo lalaa goooo alalalalal Gooooooooooooooooooooooooo!!!
Umenikumbusha mbali aisee. Enzi hizo jumamosi kabla ya mechi ya Simba na Yanga, betri zinatolewa kwenye redio asubuhi na kuanikwa juani mchana wote na kurudishwa kwenye redio saa tisa tayari kusubiri ngoma.
Baada ya sijui taarifa ya habari na matangazo ya kifo (ambayo yalikuwa yanamaliza charge za betri tuu), unasikia, "Sasa tunajiunga na Uwanja wa Taifa kusikiliza matangazo ya mpira kati ya timu za Yanga na Simba. Watangazaji wetu huko ni Charles Hilary na Omar Jongo.
Mara "Asante sana asante sana kutoka studio, karibuni katika matangazo ya mpambano mkali wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya Mambigwa watetezi Young Africans na Simba Sports club. Mimi ni Charles Hilary nikiwa na mwenzangu hapa Omar Jongo tayari kabisa kuwaletea matangazo ya mpambano huu moja kwa moja kutoka Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam. Hali ya hewa ni nzuri kabisa, mashabiki wamefurika pande zote kweli kweli wakiwa tayari kabisa kushughudia mpambano huu. .... Kabla ya kuwatajia lineup ya timu zote mbili turudi kwanza studio kuwasikiliza wadhamini wetu" Shiiiiiiiit.
Wakirudi uwanjani, tunatajiwa line up za timu, ambazo wote tulikuwa tunazijua anyway. Halafu ngoma inaanza, mara dakika ya tatu tuu Yanga wanafunga, na mfungaji ni yule yule aliyetufunga mwaka jana, Said Sued "Scud". Baada ya hapo wiki nzima ni kama vile vile vile mtu unaumwa maleria kali.
Siku hizi jamaa wanatangaza Ligi Kuu ya Uingereza na bado wana madoido yale yale.
[video=youtube_share;Nr76ngQzv4w]http://youtu.be/Nr76ngQzv4w[/video]