Econonomic Planners wetu vipi?

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259
Wana JF inaelekea Economic Planners wetu wako likizo.
Umeme unaozalishwa Tanzania ni mdogo sana, karibia 800Megawatts lakini planning yake kiuchumi inaelekea hakuna.Sisi tunashindwa hata ku-plan uzalishaji endelevu.
Afrika ya Kusini unakaribia kutengeneza zaidi ya 42,000Megawatts kwa ajili ya uchumi wake.
Kilimo kwanza ndio imeanza, viwanda vya Kilimo vyote vimekufa .Ni historia kusikia UFI-ZZK(Ubungo Farm Implements) au ZZK-Mbeya(Zana za Kilima Mbeya).Mafisadi wana pigana vikumbo kupata tenda za kuleta matrekta.
Kipato cha Serikali kinaiishia kununua mashangingi na matumizi yasiyo ya lazima, kama samani toka Malaysia.
Hivi pamoja na Maprofesa wa ukweli na wale feki, tumeshindwa kujipanga kiuchumi?
Wana JF,Great Thinkers tuchangie , hasa wachumi na planners.
 
Back
Top Bottom