Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
Ukweli husemwa:
Mbona watu wanapiga sana kelele hapa. Kama ni kutaka kujua mali za Mh Lowassa si wanaweza kwenda kwenye Baraza la Baadili ya Viongozi wa Umma na huko watajua kile ambacho Mh Lowassa ana miliki. Na kama hakujaza hizo fomu, basi atakuwa amekiuka sheria namba 13 ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambayo inawataka kuwasilisha tamko la rasilimali na madeni yao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Kuhusu jinsi alivyoupata utajiri. Well, Watanzania wajanja ambao karibu wote kwa sasa ni Matajiri wakubwa wamenufaika na kipindi ambacho Nchi ilikuwa inapitia kipindi cha mpito kutoka ujamaa kuelekea ubepari ambapo sheria nyingi za umilikaji kiharali wa raslimali hazikuwa imara na nyingine ndiyo zilikuwa katika mchapuo wa utungwaji ili kuziba mianya ya rushwa na uporaji wa maliasili.
Nitashangaa kama atapatikana mfanyabiashara yeyote ambaye hakufanya usanii katika kipindi hicho ili kumiliki kibinafsi rasilimali za nchi. Ndiyo maana watu wajanja kama kina Rejinald Mengi hawataki kujiingiza kwenye siasa kwa vile wanajua siasa ni sehemu ambayo madudu mengi huchimbuliwa na kuanikwa kwa jamii.
Ukiangalia nchi karibu zote duniani ambazo zilikuwa na siasa za kijamaa na kuamua kufuata siasa za kibepari(USSR-Russia, China na nchi za ulaya ya mashariki(Poland, Romania, Croatia nk). Kipindi hicho cha mpito kimenufaisha watu wajanja wachache ambao kipindi hicho kiliwakuta wako katika nafasi ya nzuri kisiasa na kiuchumi aka Roman Abramovich.
Ningefarijika sana kama pia nchi ingekuwa na sheria inayomtaka kiongozi anayetaka kuongoza nchi lazima aweke mapato yake wazi na aeleze katika jamii ni jinsi gani alivyopata hicho kipato badala ya kuitaja tu kama inavyofanyika sasa. Tatizo ni nani atakayethubutu kumfunga paka kengele. Na wabunge wetu ndiyo hawa wapokeaji na watoaji wazuri wa rushwa.
Ninachombeza tu...
Ukishasema kwamba mtu alinufaika kwa kutumia fursa ya economic system transition basi mtu huyo si mwaminifu kwani hawezi ku-resist temptation ya kujinufaisha apatapo fursa.Disqualification number one!
-Kuhusu fomu za maadili hata kama amejaza,katika wimbi hili la tuhuma za rushwa dhidi yake kwa nini asitoke hadharani kutangaza source ya utajiri wake kama anaamini kwamba anaonewa?Kukaa kwake kimya ni kutoa taswira hata akiongoza taasisi haiwezi kuwa transparent kama ameshindwa kuwa honest na assets zake
-Hawezi kulinganishwa na Nyerere ambaye alikua na fursa za kujitajirisha kwa hila
-Hawezi kulinganishwa na Dr.Slaa ambaye hata posho yake kwa mwezu inajulikana au Zitto Kabwe ambaye kwa uwazi
-Narudia tena,je ni crime kwa yeye kutangaza mali alizoorodhesha mbele ya tume ya maadili hata kama hakuna sheria inayoazimisha?
-Hayo maswala ya Nyumba za kariakoo ilikua ni wajibu wake,kwani angefanya nini tofauti na hilp?