Economical/Business/Investments activities za Lowassa ni zipi?

Nampongeza mtoa mada na wachangiaji kwa umahili na hoja zao. Watanzania tunaitaji kujua Rais ajaye ni mtu wanamna gani na anauwezo gani wakuongoza watu.

Propaganda chafu na matumizi ya fedha kwenye chaguzi viongozi ngazi zao juu ndo imetufikisha hapa tulipo.

EL anajua Watanzania ni maskini na kupitia chaguzi za ndani ya chama chao tayari ameona anaweza kufunika kombe. Kazi kubwa ya Watanzania wanaoipenda nchi yao nikwenda zaidi ya mitandao na kuingia vijijini waliko wapiga kura na kuwaeleza EL alivyo na wengine kama yeye.
 
Acheni kuishi kwa hisia eti kwenye kila chaguzi za CCM anayeshindwa akilalamika kuwa rushwa imetumika basi huyo ni mtu wa EL. kuna kikundi cha washindani wake kisiasa kinatumia kila njia kumchafua kila kukicha, EL anawaacha hoi pale anapokaa kimyaa ,kwenye list of shame EL aliorodheshwa kwa kuwa alivunja mkataba wa City Water .ambao walikimbilia mahakamani na serikali ikashinda. matumizi makubwa ya fedha anayotoa , EL ni MKULIMA MKUBWA, MFANYABIASHARA MKUBWA, MFUGAJI MKUBWA, NA MWANADIPLOMASIA MKUBWA, ametoa misaada mingi ya fedha kwa uwazi sasa wasionacho huongozwa na hisia mbaya oooh mwizi, fisadi, anataka urais jamani ukiwa na fursa ya kuweza kutajirika jitume tumia fursa zako acha anasa, wivu, choyo na husuda . 
 
Lowassa ni tajiri.sio tajiri uchwara km maige.huyu ni tajiri hasa.utajiri wake kaupata kwenye nyadhifa alizokuwa akishikiria.mfano mdogo tu kipindi alipokuwa waziri wa mifugo...alitwaa 70% ya ranchi za taifa na kujimilikisha.sasa fikiria...ranchi moja ina ng'ombe zaidi ya 10000...!!!ana hoteli za kifahari dubai, sauzi,london n.k., hivi vihotel vya arusha ni vidogo vidogo tu...maghorofa makubwa unayoyaona yanamea kama uyoga ni riz1 na lowassa..wanashindana!!King maker Rostam Aziz alimuuzia Lowassa shares zake alizokuwa nazo vodacom.alikuwa na 20% ya shares za voda na zote alimuuzia EL..sasa imagine..km voda imetengeneza faida ya 100 billion na wakatenga 60 billion for dividends Lowassa atanyakua 12 billion kwa mwaka...haya Alphatel inamuingizia zaidi ya 30 billion kwa mwaka..haya shares zake TBL nazo zinamuingizia fedha nyingi..ana shares kwenye makampuni yote makubwa Tanzania..ana utitiri wa majengo..hotels..magari n.k.kwa ufupi anapata zaidi ya 100 bil kwa mwaka!!! kuna mama mmoja tunafamiana..ni mnono..aliwahi kupewa 6 million na EL kwa kufanya mapenzi naye usiku mmoja tu!!!TAFAKARI!!
 
Swali lako bado gumu, ingawa baadhi ya wachangiaji wanamsafisha kwa biashara lakini nadhani ukitoa pesa nyingi hivyo kwenye mzunguko wako wa biashara lazima ufikisike. Hesabu pesa alizochangia makanisa, chaguzi mbalimbali tangu 2009, na zile anazohonga wapambe wake.

Bado swali halijajibiwa, anatoa wapi pesa zote hizo
 
Niliwahi kupewa Story na Meneja mmoja wa Kampuni ya Tours hapa Arusha kwamba huyu jamaa akiwa Prime alikuwa hapokei Hongo ya Chini ya Dolla 100,000 yaani wazungu waliokuwa wanataka Vitalu vya Uwindaji na Maeneo ya Kuweka Camp ili aongee nao ADA ya kumona ilikuwa ni Dolla laki moja yaani hapo ndo minimam,

Na niliwahi kupewa tena story na mmasai mmoja wa Monduli kwamba, baadhi ya wamasai walisha mshutukia huyu jamaa kwani kuna Baadhi ya Maeneo Lowasa ameyagawa kwa wawekezaji na hivyo wamasai kukosa maeneo ya Kuchungia na kwa hapa ili kwenda kuonana nae kuhusu kupata eneo la Kuwindia shariti ujenge Darasa moja la Secondary, ila kwenye kukabidhi anawaambia amejenga kwa pesa yake

Unaambiwa kule Monduli huyu jamaa hajawahi fanya Project ya Maendeleo kwa pesa yake mwenyewe, ila anacho fanya ni kutafuta watu mbali mbali wanato taka miteremko fulani na kuwabana, Mfano ni Mabwawa ya maji, hapa ili upate unafuu fulani pamoja na kumpa yeye pesa shariti jingine ni wewe kwenda kuchimba Bwawa la Maji huko Monduli, Ila kwenye sherehe ya Kukabidhi utasikia anasema amechimba kwa pesa yake

Huyu jamaa Arusha wanamfahamu vyema make Vitega Uchumi vyake vingi viko Arusha, Na kuna siku nilkuwa Handeni nilionyeshwa Eneo lake kwa kweli niliishiwa Nguvu, ni zaidi ya Hekari 10,000
 
Sasa kama ana hela zote hizi, huu Urais anaouhitaji ni wa nini??
Mbona ana juhudi kubwa sana kuutafuta? Maana watu wanatumia Urais wapate hela, yeye anatumia hela aoate Urais.

Maana Rushwa ni illegal, sasa anatumia illegal ways kuupata urais tutaamini vipi kama ni for the good purposes? Yaani ahonge kupata cheo ili akitumie kuwasadia/kuwakomboa watu kama wafuasi wake wanavyotuaminisha??
 
Acheni kuishi kwa hisia eti kwenye kila chaguzi za CCM anayeshindwa akilalamika kuwa rushwa imetumika basi huyo ni mtu wa EL. kuna kikundi cha washindani wake kisiasa kinatumia kila njia kumchafua kila kukicha, EL anawaacha hoi pale anapokaa kimyaa ,kwenye list of shame EL aliorodheshwa kwa kuwa alivunja mkataba wa City Water .ambao walikimbilia mahakamani na serikali ikashinda. matumizi makubwa ya fedha anayotoa , EL ni MKULIMA MKUBWA, MFANYABIASHARA MKUBWA, MFUGAJI MKUBWA, NA MWANADIPLOMASIA MKUBWA, ametoa misaada mingi ya fedha kwa uwazi sasa wasionacho huongozwa na hisia mbaya oooh mwizi, fisadi, anataka urais jamani ukiwa na fursa ya kuweza kutajirika jitume tumia fursa zako acha anasa, wivu, choyo na husuda . 

Well,umekuja vizuri.
Anatoa misaada kwa uwazi.Ofcourse ni lazima afanye hivyo attention seeker yeyote anayetafuta madaraka kwa udi na uvumba.

Sasa ujasiri huu wa kutoa misaada kwa uwazi ningetegemea angeutumia kuweka wazi vyanzo vya mapato ukizingatia ana tainted image kwa jamii.Kama logic hii tu imemshinda wakati huu anaotaka kuaminisha umma kupitia makanisa kwamba yeye ni mtu mwema na anastahili dhamana atawezaje akiingia ikulu?
-Kuna watu kama akina Mengi na Bakhresa wanajulikana biashara zao na kila kitu kiko wazi na watanzania wanajivunia wazawa hawa.Huyu ninavyojua alivyo mroho kama kusingekuwa na shaka katika utajiri wake na anavyotafuta sifa ya uadilifu kwa udi na uvumba angekuwa ameshatangaza mali zake na kuyabatiza maamuzi magumu.Come on buddy,gimme a break!
 
Lowassa ana utajiri mkubwa wa kurithi na pia wa kutafuta mwenyewe. Kumbukeni Lowassa ni mjasiriamali mbunifu sana. Nitafurahi sana akiwa rais wetu 2015 .

wakati tunapata uhuru 1961 matajiri weusi wazalendo tanzania walikua wachache sana na wote wanajulikana akina Marealle, Bomani, Rupia, labda Mbowe, hamna mmasai aliyekua tajiri kiasi cha kuja kumrithisha mtoto wake utajiri mkubwa na kutokana na sera za kikoloni na serikali ya kizalendo iliyofuata matajiri wengi walitokana na mazao ya chai na pamba (wachaga na wasukuma) na kulikua hakuna tajiri wa mifugo hapa tanzania. Hii myth ipo kwenye dustbin

utajiri wa Lowassa hadi 95 ni myth kubwa. Tunajua kua ana akili za kupenda kujiendeleza kibiashara ikiwemo kushirikiana na watu kibiashara, lakini haingii kichwani mtu tu apate mtaji mkubwa wa kuweza kufanya biashara kubwa kubwa nchini kote toka kwenye madini hadi bandarini, ingia kwenye telecom yupo hadi utalii, miradi ya ujenzi na uwekezaji wake hadi ranchi za wanyama, mashule, dry cleaners n.k haya yote yanahitaji uanzie na mtaji mkubwa ili uzalishe zaidi uongeze zaidi na ujitanue zaidi chini ya miaka 10 (AICC 1989, 1995 Lowassa tayari ni tajiri mkubwa), hamna akili wala urithi mdogo unaomwezesha mtu kuja kumiliki na kufanya haya yote kwa ufanisi na mafanikio makubwa kiasi hiki ndani ya kipindi kifupi.

Tajiri yetu Bakhresa alianza kuuza mikate miaka ya mwanzoni ya 70's kufika muda wa soko huria wa Alhaj Mwinyi "akanunua" national milling corporation na mali nyingine za serikali na misamaha kadhaa wa kadhaa ya kodi ndiyo iliyomfikisha alipo. Mengi tunajua kilichotokea NBC, sasa EL kulikoni? na unataka kua Kiongozi wetu mkuu wa nchi wakati uongozi kitu cha kwanza ni uadilifu.
 
Lowassa ni tajiri.sio tajiri uchwara km maige.huyu ni tajiri hasa.utajiri wake kaupata kwenye nyadhifa alizokuwa akishikiria.mfano mdogo tu kipindi alipokuwa waziri wa mifugo...alitwaa 70% ya ranchi za taifa na kujimilikisha.sasa fikiria...ranchi moja ina ng'ombe zaidi ya 10000...!!!ana hoteli za kifahari dubai, sauzi,london n.k., hivi vihotel vya arusha ni vidogo vidogo tu...maghorofa makubwa unayoyaona yanamea kama uyoga ni riz1 na lowassa..wanashindana!!King maker Rostam Aziz alimuuzia Lowassa shares zake alizokuwa nazo vodacom.alikuwa na 20% ya shares za voda na zote alimuuzia EL..sasa imagine..km voda imetengeneza faida ya 100 billion na wakatenga 60 billion for dividends Lowassa atanyakua 12 billion kwa mwaka...haya Alphatel inamuingizia zaidi ya 30 billion kwa mwaka..haya shares zake TBL nazo zinamuingizia fedha nyingi..ana shares kwenye makampuni yote makubwa Tanzania..ana utitiri wa majengo..hotels..magari n.k.kwa ufupi anapata zaidi ya 100 bil kwa mwaka!!! kuna mama mmoja tunafamiana..ni mnono..aliwahi kupewa 6 million na EL kwa kufanya mapenzi naye usiku mmoja tu!!!TAFAKARI!!

he he he 100 bil kwa mwaka na halipi tax (kwa sababu kitilya anamuogopa) duh!, ila 6 mil hela ndogo kwa EL kuna vijana mtaani wanaweza weka dau zaidi ya hilo kwa usiku mmoja.
 
wakati tunapata uhuru 1961 matajiri weusi wazalendo tanzania walikua wachache sana na wote wanajulikana akina Marealle, Bomani, Rupia, labda Mbowe, hamna mmasai aliyekua tajiri kiasi cha kuja kumrithisha mtoto wake utajiri mkubwa na kutokana na sera za kikoloni na serikali ya kizalendo iliyofuata matajiri wengi walitokana na mazao ya chai na pamba (wachaga na wasukuma) na kulikua hakuna tajiri wa mifugo hapa tanzania. Hii myth ipo kwenye dustbin

utajiri wa Lowassa hadi 95 ni myth kubwa. Tunajua kua ana akili za kupenda kujiendeleza kibiashara ikiwemo kushirikiana na watu kibiashara, lakini haingii kichwani mtu tu apate mtaji mkubwa wa kuweza kufanya biashara kubwa kubwa nchini kote toka kwenye madini hadi bandarini, ingia kwenye telecom yupo hadi utalii, miradi ya ujenzi na uwekezaji wake hadi ranchi za wanyama, mashule, dry cleaners n.k haya yote yanahitaji uanzie na mtaji mkubwa ili uzalishe zaidi uongeze zaidi na ujitanue zaidi chini ya miaka 10 (AICC 1989, 1995 Lowassa tayari ni tajiri mkubwa), hamna akili wala urithi mdogo unaomwezesha mtu kuja kumiliki na kufanya haya yote kwa ufanisi na mafanikio makubwa kiasi hiki ndani ya kipindi kifupi.

Tajiri yetu Bakhresa alianza kuuza mikate miaka ya mwanzoni ya 70's kufika muda wa soko huria wa Alhaj Mwinyi "akanunua" national milling corporation na mali nyingine za serikali na misamaha kadhaa wa kadhaa ya kodi ndiyo iliyomfikisha alipo. Mengi tunajua kilichotokea NBC, sasa EL kulikoni? na unataka kua Kiongozi wetu mkuu wa nchi wakati uongozi kitu cha kwanza ni uadilifu.
Una uhakika kuwa Bakhressa katajarika kwa mtaji wa mikate miaka ya 70? Lowassa anatokea Arusha mji wa Pesa, Utalii na mengine na zamani ilikuwa hata zaidi ya Dar, unadhani kwa mitaji ilioko Arusha mtu mikate Bakhressa angeweza lakini wa Utalii Arusha angeshindwa? nikikupa tetesi za kuwa utajiri wa ghafla wa Bakhressa umetokana na pesa alizokuwa anamshikia kwa siri Shiekh Amri Abeid Karume Rais wa Kwanza wa Zanzibar? haya sema na Fida Hussein (Ali Hassan Mwinyi) alipata wapi pesa za kumfanya tajiri namba moja Tanzania? nae Pamba?
 
soma vizuri elewa ndiyo ujibu. ukikataa kuelewa nilichoandika haswa kuhusu statement ya bakhresa basi haina haja ya kunisumbua nikujibu
 
Watanzania waogopeni sana watu kama akina lowasa tumefika hapa tulipo kwa sababu yao.Naombeni tuwakatae popote pale watakapogombea.Watoto wa vigogo wote tuwakatae waziwazi kama watagombea popote.
 
kwa hiyo bora Mtikila sio? au Lipumba na Cuf yake (aka uamsho)
 
RA yuko kwenye background ya timu yake and yes he hasnt gone away na sasa hivi RA yupo zaidi kenya anashuhulikia uchaguzi wa kenya akimaliza huko anarudi hapa mtamuona sana 2015, kumbukeni EL sio mtu mmoja ni taasisi
 
wakati tunapata uhuru 1961 matajiri weusi wazalendo tanzania walikua wachache sana na wote wanajulikana akina Marealle, Bomani, Rupia, labda Mbowe, hamna mmasai aliyekua tajiri kiasi cha kuja kumrithisha mtoto wake utajiri mkubwa na kutokana na sera za kikoloni na serikali ya kizalendo iliyofuata matajiri wengi walitokana na mazao ya chai na pamba (wachaga na wasukuma) na kulikua hakuna tajiri wa mifugo hapa tanzania. Hii myth ipo kwenye dustbin

utajiri wa Lowassa hadi 95 ni myth kubwa. Tunajua kua ana akili za kupenda kujiendeleza kibiashara ikiwemo kushirikiana na watu kibiashara, lakini haingii kichwani mtu tu apate mtaji mkubwa wa kuweza kufanya biashara kubwa kubwa nchini kote toka kwenye madini hadi bandarini, ingia kwenye telecom yupo hadi utalii, miradi ya ujenzi na uwekezaji wake hadi ranchi za wanyama, mashule, dry cleaners n.k haya yote yanahitaji uanzie na mtaji mkubwa ili uzalishe zaidi uongeze zaidi na ujitanue zaidi chini ya miaka 10 (AICC 1989, 1995 Lowassa tayari ni tajiri mkubwa), hamna akili wala urithi mdogo unaomwezesha mtu kuja kumiliki na kufanya haya yote kwa ufanisi na mafanikio makubwa kiasi hiki ndani ya kipindi kifupi.

Tajiri yetu Bakhresa alianza kuuza mikate miaka ya mwanzoni ya 70's kufika muda wa soko huria wa Alhaj Mwinyi "akanunua" national milling corporation na mali nyingine za serikali na misamaha kadhaa wa kadhaa ya kodi ndiyo iliyomfikisha alipo. Mengi tunajua kilichotokea NBC, sasa EL kulikoni? na unataka kua Kiongozi wetu mkuu wa nchi wakati uongozi kitu cha kwanza ni uadilifu.
Mharakat,
Watu hawa hawataki logic kwa kuwa ni mkakati maalum.Ila tunawaahidi kwamba tutawasimamisha na hatuogopi vitu vizito au vyenye ncha kali!
 
RA yuko kwenye background ya timu yake and yes he hasnt gone away na sasa hivi RA yupo zaidi kenya anashuhulikia uchaguzi wa kenya akimaliza huko anarudi hapa mtamuona sana 2015, kumbukeni EL sio mtu mmoja ni taasisi

Their days are numbered!
 
bro, SAANANE, nashukuru tumekubaliana kuwa anatoa misaada kwa uwazi, ila unataka akufahamishe vyanzo vyake vya mapato , siku zote vingozi kila mwaka hujaza fomu zinazotolewa na tume ya maadili kuelezea mali ulizonazo bila shaka EL hufanya hivyo, tukubaliane nchi hii ukiwa kiongozi fursa za kutajirika kihalali ni kubwa mno ukiwa mbunifu na kutumia vzr fursa ulizonazo[ nasikia huyu bwana ana mashamba ya maua anauza nje ya nchi,kwa kuwa ni mwanasiasa mkubwa ktk nchi ndani na nje ya nchi fursa yake kupata soko bora ni ya juu.vilevile mji wa Arusha ukiwa na majengo bora utapata wapangaji watakao kulipa vzr EL nilimsoma kwenye gazeti la rai 1995 akithibitisha kuwa anazo nyumba na moja ya wapangaji wake ni balozi ya SA tutakubaliana pia wapangaji wake pia watakuwa ni wale wanao mlipa vzr, vile vile aliendelea kuelezea kuwa anayo mifugo mingi saaana. baada ya kuondolewa Azimio la Arusha kiongozi azuiliwi kuwa na hisa ktk makampuni kwa fursa aliyonayo na uwezo wa kifedha ni rahisi kupata/kushawishi/kushawishiwa kufanya ubia na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na yy kujipatia kiasi kikubwa cha fedha. EL akiwa waziri wa ardhi aliwashauri wakazi wa kariakoo kutokubali kuuza nyumba zao bali waingie mikataba na hao wanunuzi wao watoe ardhi, mnunuzi atoe mtaji wafanye biashara. hiyo ni vision baada ya kuona wananchi wanahadaika na fedha kidogo za uuzaji majengo yao. watu wanadai amenunua ranchi nyingi za taifa jiulize amenunua kwa gilba au kwa uwazi je ni kosa kwake yy kununua ? mwisho mapendekezo ya katiba mpya fomu za mali za viongozi zisiwe SIRI.
 
Ukweli husemwa:

Mbona watu wanapiga sana kelele hapa. Kama ni kutaka kujua mali za Mh Lowassa si wanaweza kwenda kwenye Baraza la Baadili ya Viongozi wa Umma na huko watajua kile ambacho Mh Lowassa ana miliki. Na kama hakujaza hizo fomu, basi atakuwa amekiuka sheria namba 13 ya Maadili ya Viongozi wa Umma ambayo inawataka kuwasilisha tamko la rasilimali na madeni yao kwa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kuhusu jinsi alivyoupata utajiri. Well, Watanzania wajanja ambao karibu wote kwa sasa ni Matajiri wakubwa wamenufaika na kipindi ambacho Nchi ilikuwa inapitia kipindi cha mpito kutoka ujamaa kuelekea ubepari ambapo sheria nyingi za umilikaji kiharali wa raslimali hazikuwa imara na nyingine ndiyo zilikuwa katika mchapuo wa utungwaji ili kuziba mianya ya rushwa na uporaji wa maliasili.

Nitashangaa kama atapatikana mfanyabiashara yeyote ambaye hakufanya usanii katika kipindi hicho ili kumiliki kibinafsi rasilimali za nchi. Ndiyo maana watu wajanja kama kina Rejinald Mengi hawataki kujiingiza kwenye siasa kwa vile wanajua siasa ni sehemu ambayo madudu mengi huchimbuliwa na kuanikwa kwa jamii.

Ukiangalia nchi karibu zote duniani ambazo zilikuwa na siasa za kijamaa na kuamua kufuata siasa za kibepari(USSR-Russia, China na nchi za ulaya ya mashariki(Poland, Romania, Croatia nk). Kipindi hicho cha mpito kimenufaisha watu wajanja wachache ambao kipindi hicho kiliwakuta wako katika nafasi ya nzuri kisiasa na kiuchumi aka Roman Abramovich.

Ningefarijika sana kama pia nchi ingekuwa na sheria inayomtaka kiongozi anayetaka kuongoza nchi lazima aweke mapato yake wazi na aeleze katika jamii ni jinsi gani alivyopata hicho kipato badala ya kuitaja tu kama inavyofanyika sasa. Tatizo ni nani atakayethubutu kumfunga paka kengele. Na wabunge wetu ndiyo hawa wapokeaji na watoaji wazuri wa rushwa.

Ninachombeza tu...
 
Back
Top Bottom