Ebu angalia jinsi Tz tunavyotofautiana na world trend on Electricity productions vs its Cost

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,711
2,226
Mbali ya gharama, umeme kutokana namakaa ya mawe ndio wenye kutegemewa zaidi na mataifa duniani (base load) ambapotakwimu zilizopo zinaonyesha kuwa makaa ya mawe yanachangia asilimia 41 yaumeme unaozalishwa duniani, maji asilimia 16, gesi asilimia 20, nyukiliaasilimia 15 na mafuta asilimia sita.

Miongoni mwa wategemezi wakubwa waumeme uzalishwao kwa makaa ya mawe duniani ni pamoja na Afrika Kusini asilimia93, Poland asilimia 92, China asilimia 79, Australiaasilimia 77, Kazakhstan asilimia70, India asilimia 69, Israel asilimia 63, Jamhuri ya Czech asilimia60, Moroccoasilimia 55, Ugiriki asilimia 52, Marekani asilimia 49 na Ujerumani asilimia 46.

Viwango vilivyotolewa hivi karibunina kuwasilishwa kwenye vikao mbalimbali vya majadiliano likiwamo Baraza laMawaziri na vile vya Wabunge, vinaonyesha kwamba umeme wa makaa ya mawe utauzwakwa senti 12 tu za Kimarekani, upepo senti 13 hadi 14, gesi senti 14, mafutamazito (HFO) senti 20 hadi 22 na dizeli senti 30 hadi 33.


Source:Raia Mwema

MY TAKE: Naona sisi tuko kinyumetwashabikia umeme wa kutumia mafuta ambao is the most expensive.Ila sishangai sana bse iyo yote inakuwabacked up na 10%.
 
Nchi hii kidhungudhungu, we acha tu.
Hivi ule wimbo wa kinyumenyume wa mchizi mox si unaakisi uhalisia kabisa?
 
Mkuu nakuunga mkono kwamba mikakati ya kuendeleza miradi uzalishaji wa umeme kwa kutumia mafuta ambayo ni 100% imported ni udhaifu mkubwa katika sera zetu.

Hata hivyo dunia tuliyo nayo haisapoti sana miradi mipya ya makaa ya mawe kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazingira. Ni vema tukazidisha juhudi katika miradi ya maji kama Stigler gorge na ya upepo pamoja na mionzi ya jua..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom