Easy Finance matapeli?

Unakwenda mwenyewe EF kuomba mkopo, unaambiwa masharti ya mkopo na unayakubali. Unapewa mkataba kuusaini baada ya kutimiza masharti ya mkataba huo unausaini unachukua bulungutu lako na kwenda kufanyia shughuli uliyoitarajia kama ni biashara, kumsomesha mtoto au mwenyewe au kuhudumia nyumba ndogo n.k. Ikija kwenye kuanza kurudisha mkopo huo unang'aka na kuruka juu kama vile masharti ya mkopo huo hukuyabukali na wala huyajui na kuanza kuwaita EF matapeli!!!! Wabongo bwana!!! Kazi kweli kweli!!!!
 
Anaitwa Isack Kasanga,ni mlezi wa umoja wa vijana wa CCM(sikumbukitawi/wilaya ya Kinondoni),aliichangia CCM Tshirt,Kofia kipindi cha uchaguzi mkuu na ilirushwa kwenye luninga.Watanzania tufungue macho,kuna ufisadi mwingi zaidi ya ule wa EPA unaendelea Tanzania,kanuni ni mwenye nacho anaongezewa na asiyekuwa nacho/mwenye kidogo ananyang'anywa!
 
Basi naomba kurekebisha kauli yangu na isomeke hivi......"INASEMEKANA kwamba wamiliki wa Easy Finance ndio wenye Travel Mate"

Halafu, mbona wengine mnakuwa wakali sana humu? Au mna hisa Easy Finance nini?

Anaitwa Isack Kasanga,ni mlezi wa umoja wa vijana wa CCM(sikumbukitawi/wilaya ya Kinondoni),aliichangia CCM Tshirt,Kofia kipindi cha uchaguzi mkuu na ilirushwa kwenye luninga.Watanzania tufungue macho,kuna ufisadi mwingi zaidi ya ule wa EPA unaendelea Tanzania,kanuni ni mwenye nacho anaongezewa na asiyekuwa nacho/mwenye kidogo ananyang'anywa!

Kwenye uongozi huu wa serikali ya CCM, maovu tunayoyafahamu ni mfano wa ukubwa wa kigae; hatujaona paa lenyewe.

Siku Kikwete akiona ghorofa, atafanya mara mbili ya yaliyofanywa na Mkapa.

.
 
Kwenye uongozi huu wa serikali ya CCM, maovu tunayoyafahamu ni mfano wa ukubwa wa kigae; hatujaona paa lenyewe.
Siku Kikwete akiona ghorofa, atafanya mara mbili ya yaliyofanywa na Mkapa.
.

Kweli binadamu ana sura nyingi. Kuna watu humu huwa wako msitari wa mbele kwa kuwashikia mabango MAFISADI kama wa EPA,IPTL,Kiwira n.k. - lakini leo hii wanatetea Easy Finance inayoongozwa na "fugitives" wa Standard Charter !! Apendaye chongo huita kengeza, mmh.

Hivi nani analazimishwa kununua madawa ya kulevya, nani analazimishwa kuua albino, nani analazimishwa kucheza upatu n.k. Kwa nini tunakuwa na serikali in the first place - ni regulation kwa upana wake la sivyo Shylock angepata kilo yake ya nyama.
 
Unakwenda mwenyewe EF kuomba mkopo, unaambiwa masharti ya mkopo na unayakubali. Unapewa mkataba kuusaini baada ya kutimiza masharti ya mkataba huo unausaini unachukua bulungutu lako na kwenda kufanyia shughuli uliyoitarajia kama ni biashara, kumsomesha mtoto au mwenyewe au kuhudumia nyumba ndogo n.k. Ikija kwenye kuanza kurudisha mkopo huo unang'aka na kuruka juu kama vile masharti ya mkopo huo hukuyabukali na wala huyajui na kuanza kuwaita EF matapeli!!!! Wabongo bwana!!! Kazi kweli kweli!!!!
Mazee mimi niliongea na mtu ambaye alipata mkopo kutoka kwa hawa Easy Finance na kutokana na maelezo yake hawa watu ni matapeli kutokana na jinsi mikopo yao wanavyoifanya, wanachokifanya ni kuwa-trap watu. Mtu anaanziwa kusainishwa vitu mwanzo na inabidi a-sign kabla ya kwenda process inayofuata na hapo ndio unakuta mtu at the end anaambiwa baadhi ya conditions za huo mkopo ambazo hakuelezwa mwanzo na inakuwa ni sawa na ujambazi au Ufisadi tu.
 
Mimi pia nawafahamu watu wengi waliochukua mikopo midogo midogo mpaka ya 50 millioni toka EF na walifurahia huduma za EF na kamwe hawatasita kurudi tena kama wakiwa na shida ya mkopo mwingine. Kwa hiyo shilingi ina pande mbili labda hao wanaolalamika hawasomi kwa makini hayo masharti ili wayafahamu vizuri na matokeo yake wakija kutakiwa kulipa wanawashikia bango EF kwamba ni matapeli.
 
The guys want a "POUND" of flesh from desperate Tanzanians so fittingly we can call them "SHYLOCKS"
 
Jamani kabla ya kuwasema sana hao EASY Finance ebu tuangalie MoneyMart rates huko North America ni ngapi?? Hizo Payday Loans nazo si 30% per month Huko America??

Jamani sasa hizi si ndio subprime zenyewe?? Kwa hiyo tuombe watanzania watafute collateral waende Barclays kama huna usilalamike ukipewa 30% per month rate ambazo unakubali mwenyewe.

Sishabikii wizi kama upo, lakini huwezi kulalamika eti rates kubwa, nenda kwenye rates ndogo then.
 
Hawa jamaa ni matapeli hasa, mimi kuna mtu ninamfahamu alitaka mkopo wa Tsh 3m for two weeks, walimzunguusha 1 week, wakati walimwambia atapata mkopo ndani ya 3 days.

1. alitakiwa kujaza form ya Shs 20,000 non-refundable, kabla ya kuuona mkataba, na form yenyewe ilikuwa inaulizia jina, mtaa yaani vitu personal tu.

2. Next day wakamwambia inabidi achangie stationary Shs 100,000 (non-refundable)akatafuta akawapa

3. Aliporudisha form kwa ajili ya makubaliano ya mkopo, masharti yalikuwa aweke kadi ya gari, Alipopeleka kadi wakamwambia gari yako inabidi iwe imekatiwa comprehensive insurance na kumtaka atoe Shs 300,000 wamkatie, akawapa na hawakumpa hiyo insurance

4. Alipoonana na mkurugenzi anayejukana kama Hamis Faraji kwa ajili ya kusign mkataba akaambiwa interest rate ni 30% kwa mwezi, akawaambia kama inawezekana kupunguziwa kwa kuwa yeye alitaka kwa wiki 2 wakakataa. Hivyo akaona kama ni hivyo basi bora aache kwani wiki ilikuwa imeisha, wakamwambia hawatamrefund pesa yoyote aliyotumia kama ataacha process ( yaani ni Tshs 420,000), ikabidi akubali kuendelea na mchakato, Lakini siku ya kwenda kuchukua hiyo pesa wakamwambia tena katika account aache Ths 150,000 hivyo akapata mkopo wa 2,850,000 badala ya 3M,

After 1 week aliporudisha wakamwambia arudishe 3,900,000 out of (420,000 +150,000) hapo sasa akawajia juu na kuwapa Tshs 3,600,000 only

Ukiangalia ni kwamba kwa mkopo wa Tshs 2,850,000 within 1 week walipata extra 1,320,000 ambayo ni sawa 46% of interest in 1 week. Sasa kama huu si wizi na utapeli ni nini?

My Take
Watu kama hawa easy finance wanadidimiza wananchi na kuiba jasho la wananchi masikini huku vyombo vya kuregulate na ku-oversight financial sector vikiwa havina habari. Huu ni wizi uliohalalishwa ambao ni sawa na ufisadi. Unatarajia mjalisiamali atajikwamua na maisha katika mazingira kama haya.
 
Mimi pia nawafahamu watu wengi waliochukua mikopo midogo midogo mpaka ya 50 millioni toka EF na walifurahia huduma za EF na kamwe hawatasita kurudi tena kama wakiwa na shida ya mkopo mwingine. Kwa hiyo shilingi ina pande mbili labda hao wanaolalamika hawasomi kwa makini hayo masharti ili wayafahamu vizuri na matokeo yake wakija kutakiwa kulipa wanawashikia bango EF kwamba ni matapeli.

Wewe una hisa EF si bure, na kama unayoongea ni kweli basi EF unayoiongelea wewe ni ya US si ya Bongo tunayoijua sisi iliyokuwa Kinondoni Mwanamboka na Sasa imehamia Burundi Street
 
Unakwenda mwenyewe EF kuomba mkopo, unaambiwa masharti ya mkopo na unayakubali. Unapewa mkataba kuusaini baada ya kutimiza masharti ya mkataba huo unausaini unachukua bulungutu lako na kwenda kufanyia shughuli uliyoitarajia kama ni biashara, kumsomesha mtoto au mwenyewe au kuhudumia nyumba ndogo n.k. Ikija kwenye kuanza kurudisha mkopo huo unang'aka na kuruka juu kama vile masharti ya mkopo huo hukuyabukali na wala huyajui na kuanza kuwaita EF matapeli!!!! Wabongo bwana!!! Kazi kweli kweli!!!!

BAK

Tatizo linakuja kwenye upande wa Watanzania kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu haya mambo ya mikopo. Na huu udhaifu ndio watu kama EF wanautumia kwa sababu wanaujua vyema.

Watu wachache sana huwa wasoma vipengele vyote vya mkataba achia mbali kuelewa kuwa hata koma inacount.

Wale jamaa pale watakuaonyesha yale masharti nafuu ili kukuvutia wakukombe pesa zako. Kwa mfano unaomba mkopo wa millioni tano. Watakuambia riba ni asilimia kumi na tano na utarudisha baada ya muda kadhaa na kila mwezi utakuwa unakatwa kiasi kadhaa. Utaenda home utacalculate vizuri kabisa. Utasign makatasi yako. Tayari kwa kwenda kwenye kuchukua mkopo instantly.

Ukifika huko unapewa breakdown unajikuta jumla utawarudishia say 5.8 millions. Wao wanapata faida ya laki nane toka kwako. Juu ya hivyo wakati unachukua mkopo, unaweza kuambiwa tunakata elfu hamsini au lakini kama loan application fee. Mwanzo hawakukuambia kwamba kuna hiyo application fee. Kwa hiyo mkopo wako ni 4,950,000/= lakini kwenye interest ukatwa based on 5,000,000/=. Chururu si ndondondo.
 
Njia pekee ya kukwepa mfumuko wa bei na mikopo yenye interest rate ya juu ni kuziba mianya ya wezi na ufisadi na kuachia soko huria lifanye kazi na kuleta ushindani, rate zitashuka na mashariti yatakuwa nafuu.
lakini kwa nchi zenye mfumuko wa bei kama za dunia ya tatu, loan nyingi ni high risk loan, hivyo zinabebwa na high interest return rate.

Tanzania bado mabenki hayajafanya kazi zake viruri, ajira shida na Serikali haipo, hakuna wa kumfunga paka kengele.
 
BAK

Tatizo linakuja kwenye upande wa Watanzania kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu haya mambo ya mikopo. Na huu udhaifu ndio watu kama EF wanautumia kwa sababu wanaujua vyema.

Watu wachache sana huwa wasoma vipengele vyote vya mkataba achia mbali kuelewa kuwa hata koma inacount.

Wale jamaa pale watakuaonyesha yale masharti nafuu ili kukuvutia wakukombe pesa zako. Kwa mfano unaomba mkopo wa millioni tano. Watakuambia riba ni asilimia kumi na tano na utarudisha baada ya muda kadhaa na kila mwezi utakuwa unakatwa kiasi kadhaa. Utaenda home utacalculate vizuri kabisa. Utasign makatasi yako. Tayari kwa kwenda kwenye kuchukua mkopo instantly.

Ukifika huko unapewa breakdown unajikuta jumla utawarudishia say 5.8 millions. Wao wanapata faida ya laki nane toka kwako. Juu ya hivyo wakati unachukua mkopo, unaweza kuambiwa tunakata elfu hamsini au lakini kama loan application fee. Mwanzo hawakukuambia kwamba kuna hiyo application fee. Kwa hiyo mkopo wako ni 4,950,000/= lakini kwenye interest ukatwa based on 5,000,000/=. Chururu si ndondondo.

Hivi hakuna regulations kwa vyombo vya fedha nchini kwetu? What is BoT up to?
 
Ninavyoelewa mimi ni kwamba ukiomba mkopo bila good credit history au ukaomba mkopo ambayo ni non secure (kwamba hauhitaji collateral) basi hapo lender ana uhuru wa kukucharge interest rate ambayo ni ya juu kwa sababu ya risk anayochukua katika kuazima hela yake. Sasa nyumbani, hakuna njia ya ku determine credit worthness, na pia sidhani kama kuna financial institution yeyote ile ipo willing to lend money bila collateral.
Hata Easy Financial wenyewe sidhani kama wanatoa mikopo yao bila kuona kwamba kuna mali ambazo ni rahisi kuzi liquidate incase borrower ata default malipo ya mkopo.
Naona watu wanaoitetea Easy Finance wanasahau kuwa majority ya watu wanaokwenda Easy Finance ni walalahoi ambao hawana other means na wanahitaji hiyo capital kwa sababu really wana shida na they can not cope na njoo kesho na other bureaucracy za conventional lending institutes. Naona mnasahau kwamba ukiwa na connections unaweza kukata corner kwenye financial systems zetu za Bongo. Mfano mzuri ni ule watu kama akina Mzindakaya aliyechukua personal loan BoT kwa ajili ya mradi wake wa nyama I think. Je ni kweli kwamba mimi as a mere citizen naweza tu kwenda Benki kuu hata kama nina jina na collateral kuchukua personal loan? Jiulize.
Pia mnasahau kuwa hizi "hidden fees" either hazionyeshwi mwanzoni mteja anapo make first contact ama zipo kwenye "fine prints" ama zimeandikwa kwa lugha ambayo mtanzania wa kawaida asiye na elimu na ambaye haelewi mambo ya amortization na hizi adjustable rates, na kwa sababu ya shida mtu anaenda kukupoa hela ndogo tu lakini kwa ajili ya kubandikiwa li package la ma fees..lile deni lina balloon...linashindwa kulipika. Interest rate ya 30% kukopa hela baada ya kuweka collateral ni ya juu mno. Na hizo fees za ku apply na other BS ni wizi tu.
Huu ni ulafi kwa sababu once you screw people over...guess what wanaenda kuwaambia watu 10..unlike ukifanya jambo jema ataambiwa mtu 1 au wawili. What do I mean? Kwenye ulimwengu wa biashara watu (wateja) wanategemea kuwa treated right...
 
Wewe una hisa EF si bure, na kama unayoongea ni kweli basi EF unayoiongelea wewe ni ya US si ya Bongo tunayoijua sisi iliyokuwa Kinondoni Mwanamboka na Sasa imehamia Burundi Street

Sina hisa lakini kuna watu ambao nawafahamu kwa karibu katika mazungumzo wameniambia wamechukua hapo EF mikopo kiasi cha 50 millioni watu hawa wamejiajiri wenyewe na ni ni watu maarufu tu na kwa maoni yao wakihitaji mkopo tena hawatasita kurudi EF.

Sasa kama nimeambiwa hivi na wahusika sioni sababu yoyote ya kuficha ukweli eti kwa kuogopa kuambiwa nina hisa EF. Sina hisa EF wala sina mpango wa kununua hisa huko bali nasema nilichoambiwa na baadhi ya wakopaji waliofaidika na mikopo ya EF. By the way I am talking about Tanzania's EF and I know nothing about US' EF.
 
Mkuu Bubu...tuseme ukweli tu...hivi interest rate ya 30% and above kwa short term loans...na hizo fees tutaendelea mkuu? Hao wanaokopeshwa si inabidi wakauwe "albino" ili waweze kurudisha hizo hela??
 
Mkuu Bubu...tuseme ukweli tu...hivi interest rate ya 30% and above kwa short term loans...na hizo fees tutaendelea mkuu? Hao wanaokopeshwa si inabidi wakauwe "albino" ili waweze kurudisha hizo hela??

Buyer beware!! ni kweli kabisa hizo interest charges na fees ni kubwa mno kwa Watanzania walio wengi labda ni watanzania wachache sana ambao wanaweza kuhimili riba na fees kubwa kiasi hicho. Cha kushangaza BoT imekaa kimya kabisa katika hili la riba kubwa na masharti magumu mno ambayo yanakuwa kikwazo kikubwa kwa Watanzania kujipatia mikopo ili kukidhi shida zao mbali mbali ikiwemo mitaji.

Sasa hivi serikali inaimba sana kuhusu Watanzania kujiajiri wenyewe lakini wengi hawana mitaji ya kufanya hivyo. Hivyo basi kuna umuhimu mkubwa wa Serikali na BoT kuhakikisha masharti magumu ya kupata mikopo yanapunguzwa na pia riba zinakuwa na nafuu kubwa ili Watanzania wengi waweze kunufaika na mikopo hiyo.
 
Hivi hakuna regulations kwa vyombo vya fedha nchini kwetu? What is BoT up to?

Hili ndio la ninajiuliza pia ingawa sijapata majibu ninahisi BoT wamelala au wanajikongoja. Huu sio muda wa kulala wala kujikongoja.
 
Wakuu this is how we play ktk Ubepari!.. mnataka regulations za nini ikiwa mikopo inajieleza wazi..Nchi zote za Kibepari kuna watu (mashirika) kama hawa wanaotoa mikopo yenye masharti madogo kwa wale wasiokuwa na good credit..ili mradi tu unawezeshwa kujiendeleza, hizo hesabu utapiga mwenyewe!

Na sio kweli unalipa asilimia 30 ya 1,000,000 kila mwezi kwa mwaka mzima, isipokuwa asilimia 30 inapigwa hesabu fedha iliyosalia ktk deni kila mwezi..Kwa mfano ukichukua hizo 1,000,000 kabla ya mwezi kwisha ukalipa 300,000 utatoa asilimia 30 ya fedha iliyobakia ktk mkopo..

Wakuu zangu hakuna mtu aliyefungwa kamba na hii mikopo ni sawa kabisa na mikopo nchi yetu huchukua toka hayo mashirika makubwa ya IMF ambayo sisi wote tumefungwa kamba za shingo kuyalipa..Na kama mlivyosema hawa jamaa wametumia mfumo wa Benki ya Standard Bank kukopesha. Hawa wote Matapeli tu hakuna haki ktk utoaji mikopo duniani.

Hawa vijana wametoka Standard Bank na uzoefu wa mikopo na Utapeli wa Kibepari ambao Wadanganyika wengi hamnazo - wamejua wapi kuna makosa huko banki kama vile Watanzania wengi hawana credit line, acha mbali hiyo good credit record..hawana hata account banki..
Wengi hawana fedha lakini wana mashamba, majumba na mali walizorithi kutoka kwa wazee wao...Kama nilivyokwisha sema mara millioni kuwa ikiwa unataka kuanzisha kitu chochote hasa ktk biashara mambo mawili tu ya kutazama - WATU na MAZINGIRA. Ukishinda hapo ni lazima utawafanikiwa...

Kizazi hiki kipya kinataka njia za mkato kupata fedha za mtaji wakati wazee wetu walifanya kazi miaka 40 chini ya mfumo mgumu wa maisha - Ujamaa na wakaweza kujenga hivyo vibanda vya Kariakoo...
Sisi ndio kwanza tunaamini kabisa kuwa bila mtaji mtu huwezi kuishi mjini..utafanya kazi miaka 40?... Noooway! -
Well Ubepari unakuja na mengi, Wachezaji tofauti lakini Mchezo ni huo huo!
 
Hamisi F. na Gonzaga

Kaka ZANAKI taratibu. Huko unakoingia ni kubaya kuliko chumbani kwa LOWASA. Wacha mjadala uendelee na wenye kutaka kuelewa wataaelewa bila ya haja ya kutafuniwa chakula chote. Inaelekea unaijua vizuri hii team....

Tanzanianjema
 
Back
Top Bottom