East African Federation (EAF) public Views

i ask again,

why is this site censoring my reply?the incovinient truth i utter?you cannot take facts and figures from a kenyan who is here to give his 2 cents?this just proves your legacy,you want to perpetuate kenyan hatred without leveling the palying field.i gave statistics from impeccable resources but the moderators deleted them.the more you censor my posts the more i will post.
 
wa TZ watu wa ajabu sana. Leo hii uchumi uko mikononi mwa kaburu, wanamiliki kila kitu watanzania wako pale mchikichini. Kama ni kupoteza tayari kwa hilo la uchumi.

Ajira: Wa-tz wenye makampuni yao wanapendelea kuwaajili wa Kenya, sio siri. Nenda pale St Mary's Mkenya aliyemaliza form two huko kwao anapata mshahara mara mbili ya graduate wa TZ kwasababu ya lugha na kasumba ya kuthamini wa Kenya.

Tujiunge basi ili nasi tupate akili, tuamke na tushindane. wanaosema tu-protect, nini wakati uchumi huo RSA na nafasi tayari akina mazee wanachukua na sisi ndo tunawapa?
 
I think TZ should be left out of the EAC. I think Tanzanians in terms of cosmopolitan sophistication are far behind Kenya, Rwanda and Uganda. Tanzania should be left to forge some kind of alliance with Burundi, they have more in common.
 
Unregistered said:
Tanzania does not like EAC yet they have become a backyard South African supermarket


Kenya is also selling lots of goods here, after SA, without a federation! We want it to remain that way for now until we iron out costs and benefits. You see, even in EU, there are compensatory measures that are guaranteed to some members from the more progressive ones. The way I see things going in EA, there is this blind rush to Fed. that may cost us dearly in future!

As I said before, EU started negotiations about fifty years ago and they are not even at it yet. So, much as it may bring prosperity in future, how we start matters a lot to a balanced future development.
 
Mbunge Kenya awatoa hofu Watanzania

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Wabunge wa Kenya anayemaliza muda wake, Kadis Motela, amewataka Watanzania waache kuwahofu wenzao katika Afrika Mashariki, kwamba mipaka ikifunguliwa ajira zao zitapokonywa na wageni.

Alisema badala yake nafasi za ajira zitaongezeka kwani kufunguliwa kwa mipaka kunaenda na kumiminika kwa rasilimali kutoka nje ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Motela alisema hayo, alipokuwa anazindua kitabu cha ‘Politics of Partnership' kilichotungwa na Mbunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Dk. George Nangale kueleza siasa ya Muungano wa nchi hizo tatu, kwa kutumia uzoefu wa miaka mitano aliyotumikia bunge hilo.

Hafla hiyo, ilifanyika juzi jioni katika ukumbi wa Karimjee na kuhudhuriwa na baadhi ya wanasiasa na wasomi maarufu kama vile, Dk. Pius Ng'wandu, Zitto Kabwe, Paul Rupia, Hulda Kibacha, Dk. Harrison Mwakyembe, Kate Kamba na Profesa Raphael Mwalyosi.

Hulda na Kate walikuwa na Dk. Nangale, katika Bunge la Afrika Mashariki.

Pia, Motela alizungumzia suala la ardhi akitaka iwekwe sera nzuri za kusimamia ardhi nchini, ili kufungua milango kwa wawekezaji kuja kuendesha shughuli zao nchini na kupanua nafasi za ajira na uzalishaji kitaifa.

"Mtu akizalisha kahawa Tanzania itakuwa kahawa ya Tanzania, acheni ardhi iwe ya Watanzania. Woga huu unatuchelewesha kuendelea," alisema Motela na kuongeza: "Kinachotakiwa, tengenezeni sheria nzuri ziwalinde vizazi vijavyo."

Kuhusiana na kitabu kilichotungwa, Motela alisema ni cha kipekee, kwani kitakuwa cha manufaa kwa wanasiasa na watu wa Afrika Mashariki na kuwa mtunzi amefanya jambo la kipekee kati ya wabunge wote wa Afrika Mashariki.

Dk. Nangale kwa upande wake, alisema baada ya uzinduzi atazunguka katika vyuo vikuu mbalimbali vilivyo Afrika Mashariki na kupata mawazo zaidi ili afanye mapitio ya kuboresha kitabu hicho.

Pia, Dk. Ng'wandu aliyejitambulisha kama baba wa ukoo wa Dk. Nangale, alimshauri mtunzi kufanya uzinduzi wa kitabu katika miji mbalimbali nchini na nchi nyingine za Afrika Mashariki ili kukipatia umaarufu.

Baadhi ya waliopewa nafasi ya kuzungumza, akiwemo mbunge Kabwe na Profesa Mwalyosi, walielezea kuvutiwa na kazi nzuri ya mwansiasa huyo.

Chanzo: Gazeti la Uhuru la tarehe 28 Oktoba 2006
 
So, The United States of America has enacted a law to construct a wall along its border with Mexico! Hahaaa hahaa, who said Tanzania is xenophobic? Perhaps Tanzania should also construct a wall along its borders particularly with Kenya and Rwanda.It is very expensive though.

I read somewhere that about 1.2 milion illegal immigrants from Mexico are streaming into USA yearly. The mexicans are not only grabing jobs, but it appears in forty years to come or even less than that USA will have a president of mexican origin or Hispanian. Is this a tall story?

By the way how many Kenyans are streaming into Tanzania yearly? Is there a possibility of having a Tanzanian President of kenyan origin in twenty or even thirty years to come?

Tanzania is a land of opportunities isn't? If not why some of our neighbours are "fighting" to come into Tanzania? If there is nothing in Tanzania why should they be yearning to come here?
 
Unregistered said:
Nadhani mumemsikia au kumsoma wenyewe namna mkenya alivyo "arrogant". Anasema Kenya ni super power ya Afrika Mshariki. Anasema kuwa watanzania kazi yetu ni kukaa chini ya minazi kusubiri ruzuku ya serikali kama ilivyokuwa wakati wa vijiji vya ujamaa. Anasema kuwa katika eneo hili la Afrika mashariki inayofahamika ni Kenya tu iwe michezoni na kadhalika. Huyo ni Mkenya halisi na lugha yao siku zote.

Lakini Mkenya huyo hakusema upande wa pili kwamba wao pia ni wezi; kwamba katika jiji la Nairobi pamoja na kuwepo mjumba mazuri ya ghorofa pia kuna nyumba za maboksi; ambapo watu huweka vinyesi kwenye mifuko ya plastiki kwani hawana vyoo; kwamba wizi wa Kenya pia upo katika fikra zao ambapo ukipanda Kenya Airways unapoingia Tanzania huwa hawasemi kuwa sasa unaingia Tanzania isipokuwa utasikia tu upande ule wa kushoto au kulia kuna mlima Kilimanjaro ili abiria wafahamu kuwa Mlima Kilimanjaro upo Kenya.

Mkenya huyo licha ya kuikashifu Tanzania hajazungumzia umaskini mkubwa uliopo Kenya. Hao ndio Wakenya wanaotaka Shirikisho la Afrika Mashariki kwa manufaa yao ya kiuchumi na kibiashara.

Je, mnawataka Wakenya hao? Hiyo ndiyo sura yao halisi. Lugha ya jeuri na majivuno kwamba wao wamesoma sana na kwamba watanzania hupeleka watoto huko Kenya. Ni kweli watanzania hupeleka watoto wao huko Kenya na pia Uganda, kwa hiyo kwa Wakenya hiyo ni sifa tosha kweli kweli. Wao ni Super Power.

Nawathibitishieni wao ni super power katika wizi na "arrogance". Vipi Kijeshi? Sina hakika na hilo, pengine pia ni Super power. Labda siku moja wakati wa Shirikisho tutakuja ona ni nani super power kati ya tanzania na Kenya, kwani kwa maoni yangu kama ndio tabia hii ya wakenya ya kuwadharau watanzania itaendelezwa ndani ya shirikisho ni lazima litajitokeza jambo na hapo ndipo super power wa kweli atakapofahamika. Wakenya hao waje, Tanzania na watamke lugha hiyo vijijini ndani ya Tanzania waseme nyie watanzania hamjasoma, hapo ndipo watatambua maana ya kuzuia ulimi wao.

mzalendo halisi

usiskizi huyo mkenya, huyo ni jamaa mjinga sana, mimi ni mkenya na nime soma ile mumeandika hapa chini. mimi ningependa tukua na EAC lakini sikua nime fkiria vile ita afect watanzania mbeleni mbaka nika soma hizi problem zote mume taja. Shida zote mumataja ni za concern ya ukweli lakini kama wa bongo najua 80% ya izo shida muna weza overcome.

1-Hio mabo yakuangalia nini ilifanyika 1977 haiwezi saidia leo, Kama Germany na England wanaweza sahau shida zao mbona Kenya na tanzania wasisahau shida zetu.

2- Mambo ya viwanda sio problem kwasababu sisi wote tutakua inchi moja kwahivio hakuna kitu kama viwanda za kenya au za tanzania, viwanda ni zetu sis wote kama wa E, Africa.

3- Siasa ya ukabila nyinyi ndio muta saidia kenya kumaliza, najua hata nyinyi hamufurahii kuona wakenya na ukabila, mseveni pia sio shida kwani nyinyi muta mpigia kura, hakuna mtu hatampigia kura.
 
Let's face it, the Tanzania media is not being very neighbourly
By CHARLES ONYANGO-OBBO

As East African leaders met to give the political federation a shot in the arm, regional observers were focused on the surprising and increasing hostility towards the East African Community from Tanzania.

For many years, the Tanzania of Julius Nyerere was the Mecca of Pan-African politics in Africa. The Organisation of African Unity's Liberation Committee was based there, and from the late 1960s through to the early 1980s, nearly every progressive liberation movement in sub-Sahara Africa was either headquartered or had significant representation in Dar es Salaam.


Tanzania is still internationalist, witnessed by its role in brokering the Burundi peace, and the attempts to heal the rift between Presidents Yoweri Museveni and Paul Kagame after the Ugandan and Rwanda armies fought over the spoils of occupation in the eastern Congo jungles six years ago.

However, outside the statements of President Jakaya Kikwete and a few of his ministers, popular Tanzanian attitudes toward the Community seem to be growing decidedly hostile. The country is unique in the Community in that a Tanzania website, www.habaritanzania.com, actually hosts a running hate campaign against other East Africans.
An exasperated columnist in Rwanda's New Times complained about how; "It is filling Nyerere's land with the most xenophobic venom imaginable." Meanwhile, sections of the Tanzania media take exception to even the most mildly critical articles and cartoons on Tanzania appearing in the Kenya and Ugandan press - especially the former. These articles invite sharp responses, and calls to expel Kenyans.

On the other hand, I have not read a single article in the Ugandan and Kenyan media rebutting unflattering stories about them in the Tanzania media - and there are a lot. One reason is that Kenyans and Ugandans are part-time patriots and only rally to defend their countries when a European or American criticises them. They tend to be quite tolerant of, and often even to agree with, criticism by other Africans.

Kenya has simply too much to lose economically if the Community goes up in smoke, so it would seem there's an informal strategic agreement not to do anything that gives the xenophobes in Tanzania ammunition.

In Uganda, because of Tanzania's much-appreciated role in ousting the dictator Idi Amin in 1979, but also because it's a landlocked country, there's a general consensus about the East Africa Community across the political divide. Therefore, it's just not fashionable to rail publicly against Tanzania (or Kenya for that matter). There now seems to be a belief in Kenya and Uganda that Tanzania could walk away from the EAC, and therefore a creeping elite consensus that you can criticise any country in the world, but you can't ruthlessly challenge the erroneous views about the Community that one sees in the Dar es Salaam media because it could provoke a crisis.

THE RESULT IS THAT MANY regionally-minded Tanzanians (and the tens of thousands of them who send their children to Kenya and Ugandan schools) aren't getting enough support for their worldview. But also because the rest of East Africa isn't screaming foul, the Tanzanian government is able to get away with not dealing with this problem. Even more surprising is that the radical intellectuals in Tanzania have retreated so much, they hardly speak out against the demonisation of other East Africans.

Because of this silence, by the time EAC governments put pressure on Dar es Salaam, it will be too late. Today, the vocal ultranationalists in Tanzania don't want the rest of East Africa. Tomorrow, they might just have their wish. The rest of East Africa might not want to touch a xenophobic Tanzania. Someone has to say these things.

Charles Onyango-Obbo is Nation Media Group's managing editor for convergence and new products. E-mail: cobbo@nation.co.ke
 
Charles Obbo Onyango namfahamu kwa muda mrefu amekuwa mtu mwenye mawazo hasi kuhusu Tanzania na Watanzania na hilo linajionyesha katika moja ya article zake alizotoa baada ya kifo cha Baba wa Taifa,mWALIMU jk Nyerere okotba 1999.Yeye,kama walivyo nyang'au wengi wanachotaka ni ardhi na rasilimali bikira zilizo Tanzania na wala si kitu kingine chochote
 
Mind you, the writer of the article is a Ugandan, not a Kenyan, even though he is writting for the East Aftican, a paper owned by the Kenyan Nation Media Group. Let us use proper language when discussing other countries. I think there are legitimate reasons to question the speed with which our leaders want us to join the East African Federation.

Let us address these issues without calling each other names. Insulting each other, or attempting to show that other countries are very bad compared to us will take us no where. I know that many Kenyans admire Tanzania for peaceful way that we change our governments.Some politicians in Kenya consider Tanzania as a good example of unit among people of different ethnic groups.

Not long ago, Lee Njiru, a spokesperson of Moi wrote an article in the Standard extolling the virtuals of Tanzania's lack of Tribalism. During the Bomas discussion, Tanzanian arrangement of having a President and Prime Minister was considered by many as ideal. Museveni, perhaps picking a leaf from Tanzania is trying hard to make Kiswahili a national language of Uganda. Following Tanzania, the Ugandan army is called Uganda's People Defence Forces, similar to TPDF.Let us also look for the good things from Uganda and Kenya and extoll them and imitate them.

Kenya for example is very entraprising. Uganda's private schools are considered to be the best. Our drive should be to form a federation based on the positive strength of each individual country. And we can only do that by respecting each other.Let us discuss the issue of Federation in terms of pooling only the best that each country can offer, and each has so much to offer, and we have so much to learn from each other.
 
Shukran kwa makala nzuri ya kuufumbua macho umma wa Watanzania.Waswahili husema, HERI LAWAMA KULIKONI FEDHEHA. Natumaini Charles Obbo Onyango amezipata salaam.
 
Nimesoma makala zote kuhusu ugogoro wa jumuia ya afrika mashariki. Mie ni mkenya mswahili wa Mombasa. Yaliyosemwa yana ukweli juu yetu sisi wakenya ambao twabaguana wenyewe kwa wenyewe.

Ndugu zetu wa bara hawataki kusikia neno mswahili. Waweza ona hata jinsi wajibuvyo. Laiti ingekuwa amri yetu siyo subhana tusingetaka kuwa katika Kenya kusema lile la ukweli.

Hao wanoona waonewa waulize kama kwa mfano mkikuyu kenya anae rafiki? Na kama anaye muulize kamfanya nini? Anotaka kujua aje Mombasa aone tunavyoparurana nao tokana na tamaa na ubinafsi wao.

Anotaka kujua kenya tuna shari ende kisumu awaulize wajaluo. Wanafahamu wanavyodhalilishwa na kuchukia kisa eti hawakupata sunna (tohara). Kusema lile la ukweli wakenya kama hatubadiliki hatutafaa mtu hata sie wenyewe.

Tuache kichwa ngumu na ujanja ujanja. Kwanini kila siku tujione twafaa wakati siyo? Tungekuwa twapendana tusingekuwa na flying toilets ambapo mtu bila kujali mwenzie hurusha kinyesi kimdondokee mwenziwe! Hayafanyiki Nairobi haya? Nenda Dar au ndoo mambasa uone kama utakuta vitu hivi.
hayo ndiyo yangu.

Khalidi Maitha
Mishomoroni
Mombasa
Kenya.
 
Ndugu raisi na Watanzania wengine kwa ujumla muungano huu hauna maana kwe2 na 2siukubali kwa hali na mali,muungano huu una nia ya kutuumiza cc Watanzania na mali ze2 kiujumla,hatuutaki c kwa Kenya na Uganda hata nchi yoyote kwanza kinachotakiwa ni cc tuweze kujiendesha wenyewe bila kutegemea muungano wowote.

Wakenya/Wauganda/Wanyarwanda na Waburundi ni wabaguzi,washenzi na wa2 wasiofaa kuwa na umoja nao hata kidogo,waganda wana nini ili tuwe na urafiki nao?wakenya wana nini ili tuwe na urafiki nao? ukiwa na gari usikubali hata cku moja kuwa na urafiki na m2 mwenye baiskeli hatokusaidia ukipata matatizo ni sawa na cc kujiunga na hao wakenya na wauganda hawatotusaidia kivyovyote kubali au kataa.

Sisi Watanzania wa kweli hatuutaki huo muungano ,namalizia kwa kusema
MUUNGANO WA EAST AFRICA SU9-87#@#K
 
Claud Gwandu said:
Charles Obbo Onyango namfahamu kwa muda mrefu amekuwa mtu mwenye mawazo hasi kuhusu Tanzania na Watanzania na hilo linajionyesha katika moja ya article zake alizotoa baada ya kifo cha Baba wa Taifa,mWALIMU jk Nyerere okotba 1999.Yeye,kama walivyo nyang'au wengi wanachotaka ni ardhi na rasilimali bikira zilizo Tanzania na wala si kitu kingine chochote

Gwandu umenena kweli. Ila hawa waheshimiwa ndugu zetu hawataki kuambiwa ukweli. Na isitoshe wanachotung'ang'ania ni nini kama siyo mali zetu. Kama mchumba anasema hakutaki kwanini ulazimishe na kukereka. Je Kenya iko tayari kuungana na Ethipia na Somalia? Ruksa na haraka maana wanafanana kuliko sisi na wao.

Hata wangesema vipi, mwandishi anaonewa. Kama kosa basi ni la viongozi kulazimisha mambo kwa ajili ya faida yao. Ndugu zetu wakenya, kubalini ukweli hata kama unauma. Mnapotusakama utadhani tumewaibia sasa tutawezaje kuwaamini na kuungana nanyi wandugu?
 
Safi sana!Mimi nipo Kenya, wakenya wanataka afrikaMashariki kwasababu wanashida kubwa sana ya ajira. Wanaona tanzania ndiyo nchi pekee ambayo inarutuba.Suala la Afrika Mashariki watanzania tusipokuwa macho litatufanya tuwe watumwa katika nchi yetu. Otherwise lazima kuliangalia kwa kina sana. Viongozi wetu wapo leo, kesho hawatakuwapo mbona ni binadamu, hivi wasitupeleke pabaya.Afrika mashari kwa Tanzania ni hatari sana.Kila mtu aishi kwake.

Mi napinga kwa nguvui zote suala hili la Afrika Mashariki, kwa sababu naishi Kenya hivi nafahamu athari zake.Wakenya wanajiona ni supperpower wa EatAfrica yote, kumbe sivyo kabisa.Afadhari ya Rwanda,Burundi, Uganda kuliko Kenya.
Asante!
 
Nimesoma kwa makini makala na majibu na mawazo ya wasomaji mbali mbali. Nimejifunza kitu kimoja. Kwanza kuwa watu wana utaifa wa kila mtu kuvutia kwake.

Pili kuwa watu wa ama Tanzania au Kenya hata Rwanda kumbe tulikuwa hatuelewani kwa undani!

Ajabu mwandishi ametupa changamoto ya kuweza kujuana kwa undani,tunaitumia kukanusha na kutishana.
Kama mtaalam wa sanaa na fasihi,nampongeza mwandishi kwa kuweza kutupa mpira yeye akakaa kando akizidi kuturushia kunga.

Hivyo basi kuna haja ya kuanza kuelezana tulivyo badala ya kukanusha au kutishana. Ajabu hata waandishi mahiri wameingia mtego wa mwandishi. Kama tutatumia sayansi ya sanaa,tutakiri kuwa mwandishi katupa uwanja wa kuogelea na kitendawili kinachohitaji hekima zaidi ya lawama. Kwa michango iliyokwisha tolewa ni vizuri tukaanza kuelimishana juu ya sisi ni nani kama wahusika. Vinginevyo kama ungekuwa mtihani tumeambua kapa.

Picha niliyoiona ni kwamba ima wakenya,wanyarwanda au watanzania waliwajua wenzao tofauti na walivyo. Hakuna jamii yenye wema tu au wabaya tu.

Hivyo tulikabili changamoto la mwandishi kwa hekima na subira. Acha nimkariri mwandishi"Heri kusikia lawama za mwenye hekima kuliko wimbo wa mpumbavu"
Kazi njema
 
Makala hii nzuri. Nimeipenda. Nayachukulia maoni ya Onyango kwa namna tofauti kidogo. Ni wazi kuwa Watanzania tunapaswa kufahamu matatizo yaliyoko katika nchi hizi zinazotegemewa kuunda hii jumuia ya Afrika mashariki. Kenya, wanamatatizo na Raisi wao na uongozi wa juu katika serikali, Uganda kadhalika.

Tanzania tunayo neema na tunamshukuru Mungu kwa hilo. Ila sasa, hata kama ni ubinafsi, nafikikiri jambo la msingi hapa ni Utaifa wetu na umoja wetu. Mengine yote yanafaa kuangalia katika namna ambayo, yamkini sisi na utaifa wetu na baraka alizotujalia Mola, tunafaidika vipi na Jumuia hii hata kama itakuwa inajumuisha Burudi na Rwanda au haitakuwa inazijumuisha. Miezi kadhaa iliyopita nilikuwa naongea na Mkenya mmoja, na kilichojiri ni kwamba; na kwa maoni yake "Watanzania tumelala, na Wakenya wamekuwa wakituchukulia kazi zetu, na kwamba baada ya hiyo Jumuia, watachukua Ardhi yetu pia kwa vile tuna sheria zilizo dhaifu juu ya wageni umiliki wa ardhi".

Sasa kwa Watanzania wenzangu, kuna mambo ya kuangalia juu ya kukubali Jumuia hii. Faida na Hasara. Jinsi watanzania walivyojiandaa. Kiwango cha elimu tulichonacho Tanzania, ukilinganisha na nchi zinazotaka kujiunga, na Uwezekano wa kupoteza au kupata ajira. Hao wakubwa wanaoshabikia jumuia, wanaweza kuwa wanatafuta maslahi yao.

ILA CHA MSINGI-KAMA SISI KATIKA NCHI TARAJIWA ZA JUMUIA HII HATUJAFIKIA KIWANGO CHA JUU CHA DEMOKRASIA, itawezekana kweli kuwa katika jumuia pasipo kupatwa na matatizo? Umwagaji damu nk? Ni bora tukaonekana wa binafsi, ni bora akina Onyango wakatufikiria watakavyo, la msingi ni kuangalia maslahi yetu kwanza na ukubali wa Watanzania waliowengi juu ya jumuia hii na pia juu ya nani awemo au asiwemo.

ILA TAHADHARI INAHITAJIKA
 
Thanks for being so bold, and articulate in bringing what you consider essential for consideration before anymore steps are taken in that direction.

I hope you wont only deal with EA Federation agenda, but other similar incidents both within and outside TZ, i.e extension of contract for the Container Handling Company in the DAr Port, Presidential Jet saga, Kigamboni Ferry menace, Muhimbili National Hospital state, patient refferal system to India etc!
 
Enhee kumekucha! Ngoma sasa inaanza kunoga maana ndugu zetu wakenya sasa wanaanza kupeana ukweli. Poa kabisa. Nimefurahishwa na mawazo ya Maitha, huo ndiyo ukweli unaotakiwa na siyo kanusha kanusha.

Wanaosema wamevuliwa kofia mbona watavuana nguo wenyewe kwa wenyewe! Ukweli mzuri hata kama wauma yakhe.

Jamani wabongo tusilale jitokezeni tuwatia aibu watawala wetu wanaozamilia kutuuza.
Kafu
 
Mwishoni mwa mwaka 1999 nilikuwa ninaishi Afrika Magharibi. Kuna bwana mmoja aliandika habari moja ambayo mpaka sasa sijaisahau. Kwamba baada ya uhuru viongozi wa Tanzania walisajiri umasikini kwa wananchi wa Tanzania. Ndio maana baadala ya kujenga nchi na kujishughurisha na kutokomeza umaskini wetu. Nguvu zote na rasilimali zetu zilielekezwa kwenye ukombozi wa kusini mwa Afrika, pamoja na mambo mengine ambayo umeyataja hapo juu.

Ninashangaa bado viongozi wetu wanaendelea na mtindo uleule, Mtanzania yeye umasikini ni halali yake: Ndio maana kazi hakuna wageni wanazichukua wao wanaangalia tu. Nimeisoma habari ya Ndugu Charles Onyango, kuna sehemu kakubali ukweli kuwa " Kama hii jumuiya haitafanikiwa basi Kenya watathirika sana kiuchumi" hii ina maana anakiri ukweli kuwa Tanzania hatuna mengi ya kunufaika zaidi ya kugeuzwa soko la bidhaa za nchi jirani.

Ndugu zangu watanzania ushauri wangu ni kuwa kufuatana na historia yetu, mfumo wetu wa elimu ambao ni wana siasa hao hao walio uchanganya, ndio maana tuna onekana sio washindani sana kwenye soko ukilinganisha na wenzetu. Shikisho hili haliwezi kutusaidia. Japo tupo Afrika mashariki lakini tunatofautina sana na hawa wenzetu. Kihistoria, kisiasa na kiutamaduni. Kwa nini tusibaki kama tulivyo? Kwa nini wapo moto sana?

Wanatutamani jinsi tunavyo ishi na lengo lao kuja kutuharibia maisha yetu. Watanzania angalieni vingineveyo umasikini utaendelea kusajiriwa kwenu ili kuwanufaisha wengine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom