East African Countries' Budgets

Kuthibitisha hoja iweke? Kurasa nne tu maana hata muhutsari wa kikao unazidi kurasa nne sembuse bajeti?! Sibishi lakini naona uiweke kuondoa utata.

Mkuu ni bora ungeuliza kurasa nne za karatasi ya size gani?
 
Uhuru Kenyata ni very bright sishangai hata kama ilikuwa kurasa moja ,,hili la kwetu ni tabulalasa yaani hotuba ndefu ka anasoma kanuni za TANU
.
Bajeti ya nchi haiandikwi na mtu binafsi, bali ni mchakato unaowahusisha watu wengi, ila yeye kwa wadhifa wake ndiye anayeisoma bungeni!
 
Believe or not kenyan wako mbele compare to sisi. Picha zinajieleza vizuri.These guys they're well-groomed in using technology.

Waliandaa BUDGET SYSTEM na wakaweka online 7 days before kwa watu woote waone kabla haijatangazwa na ilikuwa the big opportunity kwa wananchi kuikosoa na serikali kujua ni wapi pa kulekebisha.

BUDGET SYSTEM

Final Touches
249442_223949814300246_148874415141120_914078_4588312_n.jpg

Making final touches on the Budget Speech with PS. Kinyua
247902_223949884300239_148874415141120_914080_580034_n.jpg


very hard working officials heading to Bunge
248615_224155840946310_148874415141120_915554_4382830_n.jpg


walk to parliament to give a speeech,hana Briefcase mkononi ana IPAD....
uhuru.jpg

A jovial Mr Kenyatta held a black iPad, Ms Koimett had her clutch-bag, while Dr Oburu had some loose papers.
 
Ripoti iliyosomwa ya Bajeti ya Tanzania ina kurasa 126 wakati ile ya Kenya ina kurasa 32 na kwa hesabu ya haraka haraka ni kuwa bajeti ya Kenya imeandikwa kwenye karatasi ROBO (1/4) ya karatasi zilizotumika kuiandika Bajeti ya Tanzania

Kwa mtindo huo huenda hata muda uliokolewa.
 
Kwa kweli hichi ni kichekesho sana. Lakini kwa kukusaidia napenda nikwambie kuwa Bajeti hatuhesabu kurasa zake bali yale mambo muhimu sana kwa maendeleo ya jamii yaliyomo ndani ya bajeti hiyo.

Pole sana
 
Maana ya bajeti ni nini? maana nadhani ile anayosoma waziri sio bajeti nzima bali ni ripoti tu. Bajeti nzima inajadiliwa baada ya hapo kwenye vikao vinavyofuata. nadhani hapa tunaongelea swala la ripoti kuwa deep au shallow. Ya kenya wanaweza wakawa wametoa summary na ya TZ wameweka kila kitu!!
 
Kuna siku nilisikia BBC kua katika east Africa ni Rwanda,kenya na unganda katika order hiyo
ndizo zimewekeza sana katika Technolojia na mawasiliano kwa ujumla!

Tanganyika tumewekeza kwenye majungu na wizi,....
I wish i was a kenyan,....there is no hope in Tanganyika
 
Jamaa kachemka, Bajeti ya kenya ina kurasa 32 wakati ya Uganda ni kama kurasa 18 hivi... Lakini kuna tofauti ya FONT SIZE kati ya bajeti hizo, font size ya bajeti ya Tanzania ni kubwa kuliko font size ya bajeti za Uganda na Kenya.... Hata hivyo, zingekua na font size zinazofanana bado bajeti ya Tanzania ingekua kubwa zaidi kuliko bajeti hizo zingine ambazo inawezekana zingefanana kwa ukubwa!?

Wengi wa kurasa sio issue. What matters is contents.

Anyway kwa kufauta utamu wa hoja mimi nadhani urefu wa bajeti ya Tanzania unachangiwa pia na lugha ilitumika ya Kiswahili. Kule Kenya zamani walikuwa wanasema acha Kiswahili murefu ya Tanganyika.
 
Kuna siku nilisikia BBC kua katika east Africa ni Rwanda,kenya na unganda katika order hiyo
ndizo zimewekeza sana katika Technolojia na mawasiliano kwa ujumla!

Tanganyika tumewekeza kwenye majungu na wizi,....
I wish i was a kenyan,....there is no hope in Tanganyika
mkuu wakenya wamekuwa hivyo sababu waliitengeneza kenya yao wenyewe, Hata sisi tunaweza kuitengeneza Tanganyika yetu wenyewe!
 
Huwa nashindwa kuelewa tunapoongelea tofauti zilizopo kati ya wakenya na watanzania alafu ukamwona mtu anajifanya kupingapinga..lakini kadri mda unavyopita tutakuwa tunatambua ukweli huu,Kenyans are so incomparable in almost every compound that constitutes their life
 
wakenya wanaendesha uchumi wao wenyewe sisi tunategemea wakenya waje wawekeze hapa kwetu sasa unatarajia nn?
 
Wazembe wote hawatakiwi maofisini, Lakini hilo bongo ndo vice-versa. Utakuta jitu from no where, ni mkurungezi mara sijui Officer mipango ukifuatilia jamaa kaunga unga vitu baadae kapiga debe wakati fulani kaukwaa uofisa. Sikatai kuwa hizo hazipo, lakini wapige kazi na wawe tayari kurekebishwa siyo kung'anga'nia mambo ya 1970's wakati watu tunafikiria 2050 kutakuwaje.

Serikali ifanye uamzi mgumu tena wa haraka kufyeka fyeka wavivu au watu wasiokuwa na ubunifu wowote kufanya kazi zao.
 
Kwa kweli hichi ni kichekesho sana. Lakini kwa kukusaidia napenda nikwambie kuwa Bajeti hatuhesabu kurasa zake bali yale mambo muhimu sana kwa maendeleo ya jamii yaliyomo ndani ya bajeti hiyo.

Pole sana
Kweli content muhimu lakini yetu imejaa mambo ya kisera ya wizara.hebu soma ya kenya uone walivyo absorb yote ya msingi lakini sisi tunapiga domo na sera za kuongeza mvuto wa kisiasa kwa kutaka kutaja na kusema kila kitu ili kila mtu aone kaguswa.its big challenge kwakweli page 32 kwa 102
 
mkuu wakenya wamekuwa hivyo sababu waliitengeneza kenya yao wenyewe, Hata sisi tunaweza kuitengeneza Tanganyika yetu wenyewe!

Mkuu,wamefika hapo walipo kwa sababu walipewa nafasi
ya kuonesha uzalendo kwa nchi yao,Tanganyika ukiwa mzalendo utakufa mapema
kweli tena bila kufikia ulicho taka kufanya!

Tuna chagua maraisi kuongoza watanganyika lakini maraisi wenyewe kumbe
hakuna hata mmoja ambae ni Mtanganyika,Nani yule alikua
mzanzibari,mwingine akawa Mzulu (wa afrika kusini),huyu wa sasa ni mmarekani,...
Tutapata lini raisi wa "kitanganyika" kweli kweli?

Wakenya wamesha wekeza tanganyika kama vile kila kitu ni chao,tafuta
sehem hata moja afu unambie hawaja wekeza hapo,....hadi kalamu tunatumia
kama sio za kenya ni za china,...nambie sasa,tuitengeneze Tanganyika kwa kwenda
kuwekeza wapi?
kwa kipi tulicho nacho cha kuwekeza huko?

Waganda wana kiwanda cha kusafisha dhahabu lakini hawana dhahabu,...
wana nunua dhahabu Tanganyika,wanasafisha kwao then wanauza nje,...
nambie,tukawekeze nini na wapi?

Nasikia serengeti imenunuliwa na bush,tuna cha kuwekeza bado?

Tuki kimbilia kwenda kutafuta riziki kwenye madini,kwenye migodi yetu,kwenye
ardhi tuliyo zaliwa tuna uliwa kama sisimizi,hakuna hata kiongozi mmoja wa serikali
anae ongelea hili,.... "Rejea hapo juu nimekwambia hatuna raisi wa kitanganyika"

Kenya,na nchi zingine zinazo jali raia wake,akiuliwa kizembe hivi utasikia kama
sio raisi basi kiongozi mkubwa wa serikali anakemea na kuruhusu uchunguzi,umewahi kulisikia hilo
Tanganyika?

kwanini kujenga nchi ambayo hakuna anae kujali?
hakuna anae thamini ubinadamu wako kama Mtanganyika ila rangi ya "mzungu"?

Kwanini nisitamani kua mkenya ambapo ukionesha talent yako basi
uta saidiwa na serikali katika uvumbuzi wa kitu unacho fanya (rejea kijana alogundua umeme wa biogas kenya)

Wakati Tanganyika nasikia kuna kijana alivumbua jinsi ya kurusha matangazo
ya redio nadhani mpaka leo yuko jela,...kisa,..."ana haribu mawimbi ya radio zingine"?

Kwanini nitembee nje ya Tanganyika nikiwa najivunia kua mtanganyika
wakati kila raia wa nchi nyingine anajua kua Tanganyika haiongozwi na watanganyika?

ooops,bora nisikize mziki mie
 
Kenya wamebadilisha jinsi wanavyosoma budget yao. Hii wameiita 'ministerial statement'. Ndio maana nimewauliza maana ya budget ni nini?
Angalia hii video mpate somo. Ndio result ya new constitution hiyo.

 
Last edited by a moderator:
Huwa nashindwa kuelewa tunapoongelea tofauti zilizopo kati ya wakenya na watanzania alafu ukamwona mtu anajifanya kupingapinga..lakini kadri mda unavyopita tutakuwa tunatambua ukweli huu,Kenyans are so incomparable in almost every compound that constitutes their life

You guys are inferior and pathetic...do you have to compare every lil thing with a poor neighbouring county? what is Kenya? how big is their budget $13B compare to $10B ??..both of the two are still very tiny economies in the global scale...:lol:
 
Back
Top Bottom