Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
EAC wajadili mchakato sarafu moja Monday, 17 January 2011 20:13
Mussa Juma, Arusha
NCHI za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), jana zilianza mchakato wa kuanza matumizi ya sarafu moja kwa nchi hizo , ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya jumuiya hiyo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, Balozi Juma Mwapachu, akizungumza katika kikao hicho, alisema wajumbe tisa katika nchi tano za jumuiya hiyo wamechaguliwa kushughulikia suala hilo.
Alisema umoja wa fedha katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki utasaidia sana kukuza uchumi na kuimarisha mahusiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara.
" Leo tumeanza na kikao cha kwanza cha kuanzisha mchakato wa kuwa na umoja wa fedha, hadi kufikia mwezi Machi nadhani tutakuwa katika hatua nzuri,"alisema Mwapachu.
Alisema hadhani kama kutakuwa na ugumu wa kufikia kuwa na umoja wa fedha kwani tayari itifaki mbalimbali za jumuiya hiyo zimesainiwa na kuwa na mafanikio.
"Tulikuwa na itifaki ya umoja ya forodha , tukaja soko la pamoja sidhani kama hili la umoja wa fedha litakwama"alisema Mwapachu.
Katika majadiliano hayo ya umoja wa fedha, kimsingi jana wawakilishi wa nchi zote wanachama wa jumuiya hiyo, walikubaliana kuanza majadiliano ya kufikia hatua ya kuwa na sarafu moja.
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki hadi sasa ni Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi ambao ndio wanashikilia nafasi ya Uenyekiti wa jumuiya hiyo.