Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,319
- 33,122
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, zimeazimia kujenga mtandao wa reli utakaoziunganisha kwa lengo la kuimarisha usafirishaji wa kikanda ili kukuza uchumi na maendeleo ya jamii.Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Stergomena Tax, aliyasema hayo jana katika mkutano uliokutanisha wizara yake na Wizara ya Miundombinu kuelezea kuhusu kongamano la kanda ya EAC litakalofanyika siku mbili mfululizo kuanzia leo jijini Dar es Salaam.
Kongamano hilo linatarajia kufunguliwa na Rais Jakaya Kikwete na litahusisha nchi zote wanachama, wadau wa maendeleo, wawekezaji binafsi pamoja na wadau wa usafiri wa reli ili kujadili kwa pamoja namna ya kuboresha, kuendeleza reli na gharama itakayotumika.
Tax alisema mkutano huo utajadili mpango kamambe wa reli wa nchi za EAC na namna utakavyotekelezwa.
Alisema hatua hiyo imetokana na maagizo ya wakuu wa nchi za EAC ambao walikaa mwaka 2004 na kukubaliana kuandaa mpango kamambe wa ujenzi wa miundombinu.
"Wakuu hawa walitambua kwamba bila kuandaa mpango huu nchi zote katika ukanda huu zitabakia kutokuwa na ushindani kutokana na gharama kubwa za usafirishaji na uchukuzi kuliko sehemu nyingine duniani," alisema.
Tax alisema katika mkutano huo wa mwaka 2004 wakuu wao waliguswa na tatizo la kudidimia kwa huduma za uchukuzi wa reli na mchango wake katika usafirishaji wa mizigo na kuharibika kwa miundombinu ya barabara katika ukanda huo kutokana na usafirishaji wa mizigo mingi.
Aidha, alisema kutokana na maagizo ya wakuu hao, Sektetarieti ya EAC ilimteua mshauri mwelekezi ambaye ni CPCS Transcom ya Canada, kufanya kazi ya kutayarisha mpango kamambe wa reli ya Afrika Mashariki (EARMP) ambaye aliikamilisha Januari, mwaka jana.
Alisema mshauri huyo aliukabidhi mpango huo kwenye kikao cha mawaziri wa sekta ya uchukuzi, mawasiliano na hali ya hewa ambao nao walipendekeza kufanya mabadiliko na kuongeza njia nyingine mpya za reli ambazo zilisahaulika kwenye mpango huo.
Tax alisema kutokana na tatizo la miundombinu ambayo ndio itakayoweza kufungua fursa nyingi za kufanya biashara wameamua kukutana leo ili kuona namna ya kuziboresha.
Naye Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo, alisema ndani ya mpango huo, Serikali ya Tanzania imekusudia kutekeleza miradi miwili muhimu ya kimataifa.
Chambo alisema wamekusudia kujenga reli ambayo itajumuisha nchi tatu ya Tanzania, Rwanda na Burundi ambayo itakuwa na umbali wa kilomita 1651.
"Reli hii itaanzia Dar es Salaam-Isaka Kigali/Keza-Gitega -Musongati ambapo kati ya umbali huo kilometa 970 ni za kuboresha reli ya kati ya kutoka Dar es Salaam hadi Isaka, kilomita 494 ni ujenzi wa reli mpya ya kati kutoka Isaka hadi Kigali, Rwanda na kilomita 197 ni ujenzi wa reli mpya ya kati kutoka Keza hadi Musongati Burundi," alisema.
Chambo alisema hivi sasa upembuzi yakinifu umeshakamilika na kazi inayofuata ni kufanya usanifu wa kina na kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa reli hiyo.
Kadhalika, alisema wanatarajia kujenga reli mpya ya Arusha hadi Musoma itakayojumuisha nchi za Tanzania na Uganda yenye umbali wa kilomita 573.
Alisema kutokana na umuhimu wa miundombinu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya jamii wizara yake imeweka miradi hiyo kwenye programu ya miaka 10 ya uwekezaji.
Alisema pamoja na utekelezaji wa ujenzi wa reli, serikali inaendelea kutekeleza miradi ya barabara kwa kujenga barabara kutoka Arusha, Namanga hadi mto Athi kwa urefu wa kilomita 240.
"Barabara nyingine ni Arusha, Holili hadi Voi kwa kilomita 260, barabara ya Malindi, Lungalunga, Tanga hadi Bagamoyo kwa kilomita 400 na uanzishwaji wa Vituo vya Pamoja vya Mipakani (OSBP)," alisema.
Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Balozi Juma Mwapachu, alisema kutokana na kuwepo kwa hali mbaya ya miundombinu, Rais wa Benki ya Dunia alipowatembelea Marais wawili wa EAC, aliomba kuharakishwa kwa kongamano hilo ili waweze kutazama tatizo la mfumo wa reli moja au kuongeza zaidi.
CHANZO: NIPASHE