Dynamic Productivity; Tija na Maarifa

Nyani, "unatuvamia";)

Kwanza huanza mawazo, kisha maneno na halafu vitendo. Tunafikiri binafsi, tunazungumza kama gumzo kufundishana na kisha huchukua mbinu bora zilizotokana na mwazo na mazungumzo na kuzifanya vitendo; Kuchapa Kazi.

Natamani sana Tanzania tukipata watu 10,000 katika nyanja za Uongozi na utendaji ambao watakuwa kama Mzee Ben Mulokozi aliyekuwa Utumishi!

Ni kweli hivyo huanza. Lakini vitendo huja lini...? Sitaki uniambie tumekuwa huru kwa miaka sijui 46 au 47....no no no!! Dunia iliumbwa wakati mmoja na Mungu...at least tunajua hivyo. Sasa sisi vitendo vyetu nitakuja lini..? We are so slow....dang...
 
Jokakuu,
Unayoyasema ni marudio ya mada iliyopita kuhusu Nyerere. Tatizo letu hatupendi kukubali kwamba mapungufu sio maazimio wala mfumo wa siasa kwani zipo nchi zilizokuwa na siasa mbaya kuliko yetu leo hii wamefanikiwa, Kwa nini sisi tusiwe kati ya nchi hizo?..
.
Kuendelea kulaumu Ujamaa ni moja ya udhaifu wetu, kwa sababu kizazi hiki wengi wenu hawafahamu kabisa Ujamaa ulikuwa ni kitu gani zaidi ya kusimuliwa.
Kuna mahala Bin Maryam alisema kwamba Vilipokuja vijiji vya Ujamaa wananchi wengi hawakuupenda na wengi hawakushiriki. Hapo hapo tunapata jibu rahisi kuwa sisi Ujamaa kwetu ulishindikana kutokana na wananchi wenyewe tofauti na nchi kama China, Urusi ama Ethiopia.
Halafu basi kwa hulka hiyo hiyo tumeshindwa hata kuungana sisi wenyewe nchi za nje. Kila nchi utakayo kwenda hakuna jumuiya ya Watanzania iliyosimama zaidi ya siku za matukio iwe Kifo ama Harusi nje ya hapo kila mtu na mzigo wake. Hivyo basi ikiwa Ujamaa watu waliukataa wakitegemea mfumo asili wa - Kila mtu atabeba mzigo wake!.. haishangazi kuona tumeshindwa hata kuunda jumuiya zetu nje isipokuwa kwa makundi tofauti na mataifa mengine ambao wamweza fanya mengi sana kupitia jumuiya zao.

Kisha basi ni nchi ngapi Afrika zilichukua mkondo huo wa Ujamaa..hazijai hata mkononi lakini bado maendeleo yameonekana kuwa ni shida tupu. Nchi nyingi kama zilivyoachwa na Mkoloni bado zinaendeshwa kwa miundombinu ile ile tena naweza sema afadhali hata sisi..
Kwa hiyo mkuu, tutazame deep swala hili, Watanzania hao hao wako China, Amerika Urusi Uingereza leo wanafanya kazi kama wenzawazimu inakuwaje nyumbani wali/wanashindwa? Je, shina la kuzembea huku kunatokana na kitu gani haswa!.Asili ya Utumwa maanake hata Zaire, Benin nana sehemu zilizoathirika sana na Utumwa hawana imani ya Umoja. Na kama kweli wangekuwa na Umoja toka enzi hizo za Utumwa wangeweza kum over power mwarabu mmoja mwenye gobole.. something is very wrong!

Swali kubwa hapa ni kitu gani kinaweza kutuondoa ktk shina hili la Upuuzaji na uzembe!.. Ni nchi kama zetu ati unakuta kuna kundi kubwa la watu wanaitwa Wazururaji, I mean jamani hawa sio kati ya unemployed ila Wazururaji, wanaweza fika asilimia 20 au zaidi na wanaipenda kazi yao ya kuzurura - huwaambi kitu...
 
Rev.Kishoka,

..matatizo yetu yanatokana na MINDSET. chanzo cha mindset hiyo ni siasa za ujamaa na umilikaji mali wa umma.

..wakati wa Ujamaa viwanda na mashirika vilikuwa mali ya umma. matokeo yake tukaajiri watumishi wengi kupita uwezo, na vilevile tukashindwa kufukuza wale wazembe.

..Meneja aliyejaribu kufukuza kazi wazembe, au kudhibiti ajira, alionekana mbaya mbele ya jamii. Alionekana kama mtawala anayejaribu kuhodhi mali ya umma, na kuzuia wananchi kufaidi matunda ya uhuru wao. Mameneja wa aina hiyo waliandamwa na wanasiasa, jumuiya za wafanyakazi, na hata kwenye vipindi vya redio kama mikingamo.

..Kutokana na kushindwa kudhibiti ajira, na kuhimiza uwajibikaji na tija, viwanda na mashirika yakashindwa kuzalisha. Matokeo ya kushindwa kuzalisha na ajira zilizozidi uwezo yakasabisha watumishi walipwa ktk viwango visivyokidhi mahitaji ya lazima.

..Hili tatizo litaisha kwa kuondokana na dhana ya mali za umma. Wengi bado tunalilia mashirika ya umma, lakini tunasahau kwamba utendaji ktk mashirika ya umma ulikuwa ni aibu ya kutisha kwa taifa letu.

..Hata kama tutakuwa na mashirika ya umma, basi kipaumbele kiwe ktk kutengeneza faida na siyo kutoa huduma.

..Vilevile mashirika na idara yajielekeze ktk kuajiri wafanyakazi wachache, wenye nidhamu, na wanaolipwa mafao ya kutosha. Mameneja wawe na nguvu za kuamuandika mtu kazi, au kumfukuza bila kuingiliwa.

..My observation ni kwamba wale ambao ajira zao zinawapatia vipato vinavyokidhi mahitaji muhimu wanachapa kazi kama vile wako nchi za magharibi.

..Tatizo lingine ni huu utaratibu wa watumishi, haswa serikalini, kuishi kwa kutegemea posho za safari na vikao. Kwa kweli ktk safari na vikao watu wanajituma kwelikweli. Hii ni tofauti kabisa na wanapokuwa ktk majukumu yao ya kawaida. Serikali inapaswa iliangalie hilo kwa umakini mkubwa.

..Kwa upande mwingine naamini wakulima wa Tanzania ni wachapa kazi. Wajomba na shangazi zangu wanaamka saa 10 asubihi kwenda shambani. Wanapumzika kidogo tu jua linapokuwa kali. Wengine hurudia hata usiku ikiwa kutakuwa na mbalamwezi kwa shughuli ndogo ndogo.

..Vilevile mama wa nyumbani kijijini anafanya kazi ngumu,kwa muda mrefu, ktk mazingira magumu kuliko wafanyakazi ktk nchi za magharibi.

..Tatizo la wakulima ni vitendea kazi na kutokuwepo kwa incentives za kuwafanya wazalishe ziada.

..Katika maeneo ambapo mkulima akizalisha ziada anakuwa na nafasi ya say, kupata mtaji wa duka, au kujenga nyumba bora, au kupeleka wanae shule, basi utaona wakulima wanajituma zaidi.

..Hoja hiyo hapo juu inakurudisha ktk kuhoji na kuchunguza mahusiano kati ya serikali/chama na wakulima, wafigaji, na wavuvi.

JokaKuu,

Ujamaa ulikufa baada ya Mwinyi kuingia, this make it 22 years even though efficial years are from 1992 after azimio la Zanzibar. The question becomes what have we done since then to rid bad practices?

On Ukulima, yes, watu wanaamka saa 10 asubuhi, lakini kwa kutumia jembe la mkono na kujilimia vieka vidogo kwa ajili ya chakula kutumia siku nzima? Yes they put the efforts but using primitive methods hence low yields and continue to be peasants and create subsistance agroeconomy!

Bottom line we are not making drastic efforts to rid of old bad habits to be progressive.

On the otherside of this discussion, may be some of us who are always pushing and asking for more to better our country are too over zelous not acknowledging the fact that perhaps that is what Watanzania want and they are comfortable with their livelyhood!
 
Ni kweli hivyo huanza. Lakini vitendo huja lini...? Sitaki uniambie tumekuwa huru kwa miaka sijui 46 au 47....no no no!! Dunia iliumbwa wakati mmoja na Mungu...at least tunajua hivyo. Sasa sisi vitendo vyetu nitakuja lini..? We are so slow....dang...

Que Sera Sera, Ndivyo tulivyo, what ever will be will be! Watanzania ndivyo tulivyo, tangu Adamu na Hawa!;)
 
  • Halafu basi kwa hulka hiyo hiyo tumeshindwa hata kuungana sisi wenyewe nchi za nje. Kila nchi utakayo kwenda hakuna jumuiya ya Watanzania iliyosimama zaidi ya siku za matukio iwe Kifo ama Harusi nje ya hapo kila mtu na mzigo wake. Hivyo basi ikiwa Ujamaa watu waliukataa wakitegemea mfumo asili wa - Kila mtu atabeba mzigo wake!.. haishangazi kuona tumeshindwa hata kuunda jumuiya zetu nje isipokuwa kwa makundi tofauti na mataifa mengine ambao wamweza fanya mengi sana kupitia jumuiya zao.
  • Swali kubwa hapa ni kitu gani kinaweza kutuondoa ktk shina hili la Upuuzaji na uzembe!.. Ni nchi kama zetu ati unakuta kuna kundi kubwa la watu wanaitwa Wazururaji, I mean jamani hawa sio kati ya unemployed ila Wazururaji, wanaweza fika asilimia 20 au zaidi na wanaipenda kazi yao ya kuzurura - huwaambi kitu...
Mkandara,

Wiki kadhaa nilikwenda kutafuta Family Physician, jirani na nyumba yangu nikaenda kuna Clinic, Daktari Mkuu mwenye clinic ni Mnigeria, nikapewa referal kwa Urologist, naye ni Mnigeria, nikabidi kwenda kwa vipimo vya lab nako ni kwa Mnigeria, mwishowe nikaenda kwenye imaging centre leo kwa CAT scan, 2 head associates/partners ni Wanigeria!

Sasa pamoja na kuzubaa kuona muungano wao pamoja na kuwa wanatoka makabila tofauti(Yoruba, Hausa, Igbo) lakini wanashirikiana kupelekeana biashara, nikajiuliza hii ni kweli au ni 419 scheme?

I wish Watanzania we had such solidarity and unity and not Vilio na Matanuzi as you said!

On Uzururaji, nenda George's Grill, Texco, RoseGarden, Maliasili, Utamaduni, Lango la jiji na vimigahawa vyote maarufu, tangu wafungue kwa biashara asubuhi mpaka wanafunga usiku wa manane, vijiwe vimejaa watu, mpaka unajiuliza, hivi hawa watu wanatoa wapi pesa na kazini wanakwenda saa ngapi?
 
Que Sera Sera, Ndivyo tulivyo, what ever will be will be! Watanzania ndivyo tulivyo, tangu Adamu na Hawa!;)

And too bad neither you nor Mwanakijiji can change it!! Mtaandika mimakala yenu lakini mimi hadi nione matokeo ndio nitaamini. Maneno nimeshayasikia hadi nimechoka.
 
[/LIST]Mkandara,

Wiki kadhaa nilikwenda kutafuta Family Physician, jirani na nyumba yangu nikaenda kuna Clinic, Daktari Mkuu mwenye clinic ni Mnigeria, nikapewa referal kwa Urologist, naye ni Mnigeria, nikabidi kwenda kwa vipimo vya lab nako ni kwa Mnigeria, mwishowe nikaenda kwenye imaging centre leo kwa CAT scan, 2 head associates/partners ni Wanigeria!

Sasa pamoja na kuzubaa kuona muungano wao pamoja na kuwa wanatoka makabila tofauti(Yoruba, Hausa, Igbo) lakini wanashirikiana kupelekeana biashara, nikajiuliza hii ni kweli au ni 419 scheme?

I wish Watanzania we had such solidarity and unity and not Vilio na Matanuzi as you said!

On Uzururaji, nenda George's Grill, Texco, RoseGarden, Maliasili, Utamaduni, Lango la jiji na vimigahawa vyote maarufu, tangu wafungue kwa biashara asubuhi mpaka wanafunga usiku wa manane, vijiwe vimejaa watu, mpaka unajiuliza, hivi hawa watu wanatoa wapi pesa na kazini wanakwenda saa ngapi?

Mmmhh...wewe kwa Urologist ulienda kutafuta nini....nini kinakusumbua...? Sitaki hata ku-guess....mweee!!!!
 
Mmmhh...wewe kwa Urologist ulienda kutafuta nini....nini kinakusumbua...? Sitaki hata ku-guess....mweee!!!!

Uzee! Ukisikia ngiri, kifuko cha uzazi na mkojo unauma, inabidi uende kupimwa. Si siri wala aibu, Prostate Cancer runs in the family, I am close to the age and I am black!
 
Uzee! Ukisikia ngiri, kifuko cha uzazi na mkojo unauma, inabidi uende kupimwa. Si siri wala aibu, Prostate Cancer runs in the family, I am close to the age and I am black!

Yeah I heard it somewhere that just by virtue of being black we are more likely to get it...dunno why...

Nahisi kama vile na wewe ulienda kutafuta prescription ya cialis kama nanihino....kwikwikwiiii
 
Yeah I heard it somewhere that just by virtue of being black we are more likely to get it...dunno why...

Nahisi kama vile na wewe ulienda kutafuta prescription ya cialis kama nanihino....kwikwikwiiii

Weye Kunkoma Nyani Giladi acha mzaha bwana, tayari mzee kanywea kusikia atapigwa msasa ule wa mduara wa Brown Ring kupiga chabo la uzibuaji! Sina raha!:rolleyes:
 
Back to subject enogh na uvamizi!

Sasa wewe Nyani what are you suggesting? you always ask questions but never offer some sort of solution or "win-win situation" as Kikwete says! Tupe basi japo mtazamo wako yakinifu, what do we need to do to become an economic giant by utilizing the resources in hand and change our attitudes towards Uzalishaji mali?
 
Ni kweli hivyo huanza. Lakini vitendo huja lini...? Sitaki uniambie tumekuwa huru kwa miaka sijui 46 au 47....no no no!! Dunia iliumbwa wakati mmoja na Mungu...at least tunajua hivyo. Sasa sisi vitendo vyetu nitakuja lini..? We are so slow....dang...

Sipendi kutumia nadharia sana kwenye habari hii ila ni muhimu nikakupinga kidogo kuwa japo Mungu aliiumba dunia kwa wakati mmoja lakini bado hakuweka ulinganifu katika kusambaza RIZIKI.

Kuna bwana mmoja mtalamu wa mambo haya anaitwa DARWIN na ana nadharia aliyoiita NATURAL SELECTION.

Ukiiangalia sana hii nadharia kwa kina utakubaliana na mimi kuwa katika ugawaji wa Riziki Mungu haku-balance.Huwa nakaa na kujiuliza bila kupata jibu kuwa kwa nini kila sehemu yeyote ya nchi ama dunia ama eneo ambalo ni Northern huwa ni tajiri ama lina madini kuliko Southern??Nakosa jibu.Mfano ukichukua Northern America na southern America,ama Northern Tanzania na Southern Tanzania ama Northern Africa na Southern Africa ama kwa kijiji kwetu Majita au kijijini kwenu au jijini Dar au mwanza utagundua kuwa northern ni tajiri kuliko southern.
Basi inabidi tu tukubaliane kuwa hii ni natural selection.Na mungu uliyesema ameumba dunia siku moja anajua kwa nini ilitokea hivyo.

Naamini na nina uhakika kuwa kama Wazungu nao wangekuwa Watumwa wa WAAFRICA,basi ni lazima nao wangekuwa masikini kama Africa ilivyo sasa.Swali linakuja,Je! kwa nini weusi (mostly) ndio walikuwa watumwa wa weupe na haikuwa weupe kuwa watumwa wa weusi????Jibu Natural selection.

Huwa nasikia habari za huko Marekani kuwa wana train ya chini ya ardhi(Sub-way).Siku moja niliiota hiyo sub way.Ni vigumu kuisimulia ilivyo kwani siyo tu kuwa huko chini inapita train tu bali kuna hadi masoko,maduka na watu wanaendelea na maisha as if wako juu ya ardhi huku juu yake watu wakiendea na maisha huku majengo na kila kitu kikiendelea.Lakini nani alifanya maajabu haya jibu ni Watumwa tena Waafrica.Kwa nini??Darwin's theory.

Hivyo basi kwa sauti moja nasema kuwa umasikini wa sasa wa Mwafrika mtanzania unatokana na "Natural selection" anayoiongelea Darwin.Sijui kiswahili kizuri cha maneno hayo.

Kuna mjumbe mmoja kule nyuma amesema kuwa Mtanzania wa kima cha chini hawezi kumudu maisha.Ni kweli.Ila nabishana nae anaposema kuwa Marekani mtu wa kima cha chini anaefanya kazi kwa masaa 40 kwa wiki anayaweza maisha.Hapa nasema NO.
Ukiwa na masaa 40 kwa marekani huku ukilipwa dola 10 kwa saa,ina maana kwa wiki una $400 na kwa wiki una $1600 hapo ni bado hujatoa tax ambayo kwa namna yeyote ile huwezi kuikwepa.Baada ya hapo toa bili ya appartment say $700,gas say $100,Umeme na maji,simu,Chakula,bado Insurances kama za Afya,gari nk bado mkopo wa gari hujamaliza $800.HAKIKA HUTABAKI NA KITU CHOCHOTE MWEZI unaofuata,so ndo maana watu hufanya kazi mbili. Swali je kwa nini Tanzania watu hatuna mwamko wa kufanya kazi mbili??Napata kigugumizi.Je niseme Darwin???Ok ngoja nisimseme.Je kuna uwezekano watu kufanya kazi 2 TZ???Je WaTZ wako tayari?? Jamani hapa namuongelea mtu wa chini na Siyo mafisadi coz mafisadi wao wana kazi nyingi tuuu.

Najua wadau hapa tutampinga Darwin ila nakaribisha challenges na solutions ili tuone tutanyanyuka vipi.

Tanzania ilizaliwa mwaka 1961 na ina miaka 47 tu.Marekani ilizaliwa mwaka 1776 na ina miaka 232.Je tutaweza kulinganisha watu wawili hao kwa Maendeleo??Uingereza sijui ina miaka mingapi.Mimi naamini kuwa kuna siku ile Natural selection itaikumba TZ na sisi tutakuwa kama Marekani ya leo.Kuna mzee mmoja aliniambia kuwa Dar ya leo ni kama ilivyokuwa New York miaka 150 iliyopita.So tusubiri.Mungu anajua.
 
Afrika Kusini sikujua kama iko kaskazini!
Na sijui ilizaliwa mwaka gani...1910 au 1994...?
 
Afrika Kusini sikujua kama iko kaskazini!
Na sijui ilizaliwa mwaka gani...1910 au 1994...?

Mkuu ni kweli usemavyo.Ila ninachosema mimi ni Southern Part na Norther part.Sidhani kama Southern Part ya Africa ni Africa kusini pekee.Hebu igawe Africa katika vipande viwili vya Southern na Northern then linganisha,utaona maana yangu iko wapi na wapi Tajiri.
 
Afrika Kusini sikujua kama iko kaskazini!
Na sijui ilizaliwa mwaka gani...1910 au 1994...?

By the way Africa Kusini haikupata Uhuru wake 1994. Africa kusini ilipata uhuru wake mwaka 1910,hiyo ya 1994 hatuongelei Uhuru.Hapo ni habari nyingine kabisa.Sidhani kama Mandela ndo Rais wa Kwanza wa Africa Kusini.
Pia hebu igawe hiyo Africa kusini katika anga za kaskazini na kusini uone Darwin kalalia wapi.Thanx
 
Mimi naona unproductivity inaanzia na malezi ya nyumbani ama siasa mbovu za nchi.
Ukiwapa chakula au msaada wajomba, wakwe, mashemeji, washikaji au watoto wakubwa, nk hakikisha unawapa maneno yao ili nao wajitegemee kwa kufanya kazi ama hakikisha wanakufanyia kazi kwa misaada unayowapa. Kama tunashindwa kuwasema kwa kupenda dezo, uzururaji wao ama kutofanya kazi basi moja kwa moja tunakua tunapunguza productivity yao. Kata msaada wasipokubali kufanya kazi.
Je tunaweza kubadilika, maana mimi naona tuna hizo mila/taboo za kuendeleza unproductivity. Fikiria mama atavyosema ukimsema mjomba nk.
 
Rev.Kishoka, Mkandara,

..I wont mention ujamaa again. I think every time i do that ppl dont read my entire response.

..Tatizo hapa ni wafanyakazi kulipwa mafao ambayo hayakidhi mahitaji. Sasa lazima waende mjini kutafuta vipato vya ziada.

..Maeneo mengi, kuanzia bosi mpaka mtu wa chini kabisa hali ni hiyo hiyo. Mazingira hayo yanasababisha kutokuwepo kwa usimamizi na uhimizaji ktk maeneo ya kazi.

..Nimeelekeza kwamba ktk maeneo ambayo wafanyakazi wanalipwa mafao mazuri, basi uchapakazi wao hauna tofauti na watumishi ktk nchi za magharibi.

..Wakulima tatizo lao ni kukosa incentive ya kuzalisha ziada. Kuna maeneo mengi ambako wakizalisha ziada mazao yanaozea shambani au kwenye maghala.

..Kuna maeneo ambayo yana infrastracture nzuri[barabara,masoko], na wakulima wako exposed kwa wafanyabiashara. Maeneo hayo wakulima wanaona manufaa ya moja kwa moja ya kuzalisha ziada. Kwa mfano mkulima akizalisha zaidi anapata pesa za kujenga nyumba bora, kupeleka watoto shule, au kuingia ktk biashara. Mazingira kama hayo yanafanya wakulima wajitume zaidi.

..Naamini kabisa tukiweza kuunganisha kilimo na commerce basi wakulima wetu watajituma zaidi.

NB:

..Labda ktk kupanua mjadala tujiulize wafanyakazi wanapotoroka makazini wanakwenda kufanya shughuli gani? Je, serikali ina habari zozote na shughuli hizo?

..Zaidi, tujiulize wafanyakazi wanaishi namna gani, ukizingatia kwamba mishahara wanayolipwa ni kama kumdhihaki mtu?

..Definetely kuna fedha ambazo zina-seculate nje ya mfumo rasmi wa fedha. Je, kuna uwezekano wa serikali kurasimisha shughuli hizo, kama ni halali, ili zitozwe kodi?
 
Jokakuu,
Unayoyasema ni marudio ya mada iliyopita kuhusu Nyerere. Tatizo letu hatupendi kukubali kwamba mapungufu sio maazimio wala mfumo wa siasa kwani zipo nchi zilizokuwa na siasa mbaya kuliko yetu leo hii wamefanikiwa, Kwa nini sisi tusiwe kati ya nchi hizo?..
.
Kuendelea kulaumu Ujamaa ni moja ya udhaifu wetu, kwa sababu kizazi hiki wengi wenu hawafahamu kabisa Ujamaa ulikuwa ni kitu gani zaidi ya kusimuliwa.
Kuna mahala Bin Maryam alisema kwamba Vilipokuja vijiji vya Ujamaa wananchi wengi hawakuupenda na wengi hawakushiriki. Hapo hapo tunapata jibu rahisi kuwa sisi Ujamaa kwetu ulishindikana kutokana na wananchi wenyewe tofauti na nchi kama China, Urusi ama Ethiopia.
Halafu basi kwa hulka hiyo hiyo tumeshindwa hata kuungana sisi wenyewe nchi za nje. Kila nchi utakayo kwenda hakuna jumuiya ya Watanzania iliyosimama zaidi ya siku za matukio iwe Kifo ama Harusi nje ya hapo kila mtu na mzigo wake. Hivyo basi ikiwa Ujamaa watu waliukataa wakitegemea mfumo asili wa - Kila mtu atabeba mzigo wake!.. haishangazi kuona tumeshindwa hata kuunda jumuiya zetu nje isipokuwa kwa makundi tofauti na mataifa mengine ambao wamweza fanya mengi sana kupitia jumuiya zao.

Kisha basi ni nchi ngapi Afrika zilichukua mkondo huo wa Ujamaa..hazijai hata mkononi lakini bado maendeleo yameonekana kuwa ni shida tupu. Nchi nyingi kama zilivyoachwa na Mkoloni bado zinaendeshwa kwa miundombinu ile ile tena naweza sema afadhali hata sisi..
Kwa hiyo mkuu, tutazame deep swala hili, Watanzania hao hao wako China, Amerika Urusi Uingereza leo wanafanya kazi kama wenzawazimu inakuwaje nyumbani wali/wanashindwa? Je, shina la kuzembea huku kunatokana na kitu gani haswa!.Asili ya Utumwa maanake hata Zaire, Benin nana sehemu zilizoathirika sana na Utumwa hawana imani ya Umoja. Na kama kweli wangekuwa na Umoja toka enzi hizo za Utumwa wangeweza kum over power mwarabu mmoja mwenye gobole.. something is very wrong!

Swali kubwa hapa ni kitu gani kinaweza kutuondoa ktk shina hili la Upuuzaji na uzembe!.. Ni nchi kama zetu ati unakuta kuna kundi kubwa la watu wanaitwa Wazururaji, I mean jamani hawa sio kati ya unemployed ila Wazururaji, wanaweza fika asilimia 20 au zaidi na wanaipenda kazi yao ya kuzurura - huwaambi kitu...

Mkandara:

Naona unam-miss sana babu. Kwa bahati nikiwa Ulaya nimepiga dai waka nchi mbalimbali. Na katika dai waka hizo nilikutana na vijana wengi wa kitanzania walitoka DSM, Zanzibar, Mwanza, Arusha na miji mingine. Vijana hawa wengi hawakuwahi kufanya kazi za shambani na kazi za mitulinga.

Pamoja na kuwa hawakuwahi kufanya kazi za mitulinga wakiwa bongo, vijana wengi waliweza kufanya kazi kwa uzalishaji, tija na maarifa.

Niliwahi kumuuliza kijana mmoja kwanini juhudi za kazi anazofanya akiwa uingereza hajawahi kuzionyesha akiwa Tanzania. Kwa uzuri tulikuwa super-market na kunijibu swali langu akanionyesha TV moja kubwa ya Paundi 400. Akaniambia kuwa akifanya kazi yake na kuongezea OT, katika kipindi cha wiki mbili anaweza kununua hiyo TV kwa kutumia pesa zake za mfukoni.

Kwa miaka mingi wanafalsafa wetu na viongozi wa juu wanachukulia kuwa kazi za maendeleo ni struggle. Na kwamba tukitaka kufikia nchi zilizoendelea itabidi tu-struggle sana.

Ukweli wa mambo wananchi wengi wanaangalia kazi kama kijana niliyekutana naye uingereza. Wanafanya kazi kutimizi malengo yao kwanza. Na kama kazi wanazofanya zitakuwa zinalipa basi watazifanya kwa juhudi zote ili ufanisi upatikane. Hata yule ambaye hakuwahi kulima kwa kutumia jembe la mkono, kama kazi ya jembe la mkono italipa zaidi atakuwa tayari kujifunza kazi hiyo na kumpita yule aliyezaliwa akiwa na mpini mkononi.

Kwa ujumla kazi za Tanzania hazilipi na hazina matumaini yoyote. Na kinachofanyika ni kwa waajiri kuigiza kuwa wanawalipa wafanyakazi wao na wafanyakazi kuigiza kuwa wanafanya kazi (A.K.A USANII).
 
Bin Maryam,

Hivyo motisha kwa Watanzania wengi ni mahitaji ya sasa, yakishatimizwa basi liwalo liwe? Je inawezekana kabisa kuwa mind set zetu ni kuridhika na kile haba tulichnacho na kukipata na si kutafuta ziada? Tumekomaa falsafa za Ujamaa na Ujima kiasi kuona kuwa kuongeza au ziada ni dhambi hivyo hata uwajibikaji na uchapa kazi wetu ni kwa kiasi a si ziada?
 
Mchungaji,
Hakika uvivu ni mojawapo ya sababu za umaskini wa mtu mmoja mmoja,jamii na taifa.
Waumini wako watakumbuka neno hili,toka katika hekima za mfalme Suleiman;
How long wilt thou sleep,
O sluggard?
when wilt thou arise out of thy sleep?
Yet a little sleep,
a little slumber,
a little folding of the hands to sleep:
So shall thy poverty come as one that travelleth,
and thy want as an armed man
.(Mithali 6:9-11)

Yamkini wafanyakazi wa viwandani na maofisini nchini kwetu wengi waaangukia katika nadharia X ya mtaalam Douglas McGregor ambaye alipata kusema hivi;
Some managers assume that
employees are inherently lazy
and will avoid work if they can.
Because of this,
workers need to be closely supervised and comprehensive systems of controls developed.
A hierarchical structure is needed with narrow span of control at each level.
Employees will show little ambition without an enticing incentive program
and will avoid responsibility whenever they can
.(McGregory,1960)
Kama ndivyo tulivyo,wakati umefika tutambue kwamba kwa uvivu au kutega kazi hatumkomoi mwajiri bali sisi wenyewe,wanaotutegemea na taifa letu kwa ujumla.

Lakini mimi bado najiuliza swali, asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima.Kule vijijini wanadamka alfajiri,wanaenda mashambani, jua lao,mvua yao,ukame wao,n.k, wakiwa wamepinda migongo na jembe la mkono, hawa nao waambiwe sababu ya ufukara wao ni uvivu?
 
Back
Top Bottom