Duuu...! Enzi hizo...bora turudi zamani...!

gango2

JF-Expert Member
Aug 31, 2011
1,941
2,251
Duuu,

leo nimekaa nimefikiria sana enzi za zamani kwa kweli nimetamani turudi enzi hizo, enzi za zamani, kila kitu kilikuwa poa, upendo amani yaan raha sana zamani kuliko sasa!!

nimekumbuka enzi hizo tunajiendea HOSPITALINI bureee yaani ukifika manesi wanakupokea kwa furaha wanakuhudumia, na unapewa dawa bureeee.....duuu enzi hizo jamani ilikuwa raha saaaana

nimekumbuka enzi hizo kweli ukisikia mwanafunzi kafaulu darasa la saba au form four ujue kweli ni kichwa tena balaaa, yaani wale vichwa wa juu walikuwa wanapatikana MZUMBE, ILBORU, KILAKALA, MSALATO..ifunda, iyunga ....teh teh jamani jamani enzi zetu.safi sana.

nakumbuka enzi izo ukitaja UDSM basi unataja hapo MUHIMBILI, ARDHI, DUCE, IJMC na ilikuwa mtu ili aende chuo kikuuu kweli inaitaji usomeee, kwanza kulikuwa hakuna migomo kabisa. lakini sasa

nakumbuka enzi za makamba dar es salaam, teh teh kina matonya, bongo ilikuwa burudani sana, wanafunzi wa sekondari dar wanavaa vikaptula...teh teh jamani enzi hizo ilikuwa bomba eeeh

.......!!!!
 
Enzi hizi pamoja na kuwa umepata division one form six ili uende chuo (UDSM) lazima ufanye mtihani (MALTICULATION) teh teh sijui huu mtihani uliishia wapi
 
Enzi hizo tulikuwa tunafanya kazi bila komputer masaa nae, tunatumiana barua kwa posta, tunapanda UDA bila foleni barabarani, tunakula mikate ya siha, tunaangalia sinema za bure Drive In, kuna treni kila siku kwenda Mwanza na Kigoma na mara kadhaa kwa wiki kwenda Arusha, tunalala chuma kimoja watu wawili na tunajifungulia chai na maziwa kweye vibomba UDSM, tukipikiwa wali maharage lazima litoke tangazo kutuomba radhi pale UDSM, tunaheshimu wanasiasa, tunaandamana siku kuu za sabasaba na kushona (sio kununua) nguo mpya, tunapangiwa kazi hadi Uganda na Kenya tkiwa shirika la East African au customs, raisi na mawaziri wakitembelea mikoani tunaenda kuwapokea na matawi ya miti mikononi!

Yaani, basi tu!

Mwisho wa mambo mazuri bwana ilikuwa Idd Amin alipochukua nchi Uganda na Arap Moi alipochukua nchi Kenya.

Tukapigana vita Uganda

Tukaanza kupanga foleni ya unga na sukari, tukajua kuna mwendo wa kuruka, tukaujua ugali wa yanga, tukawa na maduka ya kaya, zikaingia dala dala, tukaanza kununua bia na soda kwa vibali, ice cream zikapotea, Blue Band za Kenya zikapotea, tukaanza kununua Colgate na kanga toka Kenya kwa magendo, tuaka tunatakiwa kuwa na kibali kuleta debe moja ya mchele toka Mbeya kuja Dar, tukawa tukienda ulaya tunafanya shopping ya colgate, sabuni Imperial na viatu vya kukimbilia (raba mtoni), suruali za Jeans na kodurai zikawa mali adimu sana, tukawa tunakosa usafiri wa kwenda mikoani kwa sababu mabasi ya Relwe na Kamata na Kwacha yamejaa mwezi mzima.

Mmh, kweli mambo hubadilika.
 
... enzi hizo hakukuwa na ukimwi na kondomu zilifahamika kwa Wasomi wachache! Miji yote mikubwa Dar, Mwanza, Arusha, n.k. na baadhi ya Miji midogo ilikuwa na Mitaa maalumu kwa huduma ya ngono ya kununua (Red Streets). Kwa Mwanza ilikuwa Lumumba Street na Mlango Mmoja. Tofauti na siku hizi Shule na Vyuo ndo maeneo rasmi ya mawindo!

Enzi hizo za"Afro", Pekozi, Raizoni na Shati Slimu-fiti!

Dah, enzi hizo!!
 
ninacho kikumbuka ni kuwa enzi hizo hata mtihani wa la saba ulikuwa siku moja ufaulu alama 125/150 na siyo leo 50/250
 
Enzi hizo pale UDSM kulikuwa na mzee PUNCH! Alikuwa akifanya kazi kama mzuka! Nashangaa sijui alipotelea wapi!
 
Enzi hizo ukianza shule ya msingi, unakwenda wewe tu ukiwa umevaa shati jeupe, kaptura bluu aina ya jinja, viatu aina ya chachacha au raba aina ya DH, kama familia imepotea kabisa unavaa kandambili. Madaftari na kalamu ilikuwa ni bure tu!
 
Enzi hizo ukianza shule ya msingi, unakwenda wewe tu ukiwa umevaa shati jeupe, kaptura bluu aina ya jinja, viatu aina ya chachacha au raba aina ya DH, kama familia imepotea kabisa unavaa kandambili. Madaftari na kalamu ilikuwa ni bure tu!

Dah Kaka! Kwenda Shule na raba tena DH nyeupe! Wewe itakuwa ulikuwa wa "uzunguni" aisee! Wengine siku pekee za kutokelezea na DH ilikuwa Kanisani Jumapili (pea 1 madogo wavaaji watatu), siku ya Kipaimara, Mtihani wa "la Saba" na kwenye Pati ya LY. Unakumbuka LY Mkuu?

Surely, those were good old days!
 
Dah Kaka! Kwenda Shule na raba tena DH nyeupe! Wewe itakuwa ulikuwa wa "uzunguni" aisee! Wengine siku pekee za kutokelezea na DH ilikuwa Kanisani Jumapili (pea 1 madogo wavaaji watatu), siku ya Kipaimara, Mtihani wa "la Saba" na kwenye Pati ya LY. Unakumbuka LY Mkuu?

Surely, those were good old days!

Nakumbuka DH zimeingia miaka ya tisini,,,,
 
Enz izo mtu akiingiza CM nyumban kwake anaogopwa,,,,cm unaunganshwa kama umeme,!

Enz izo kupiga cm mpaka pista,,,!
Enz izo tv hakuna,,,!

Nakumbuka kwa mara ya kwanza TV niliiona mwaka 86 kwa jiran etu alikua tajir mnooo!
 
Naliaaaaa mieeee. Kweli tumepitia mengi mazuri. Miji/mitaa ilikua safiiiiii. Hospital safiiii, shule safiii, wanafunzi wachache mnafundishwa mnaelewa haswa. Walimu wana upendo kama wa wazazi wetu.
Wapiiiiiii..... Ndo kushnehi.
 
Enzi hizo ukimtongoza msichana anaangalia chini huku akichora-chora kwa dolegumba chini au kukata kata kinyasi ; siku hizi bana ni Live!! acha longo-longo sema una sh gapi...?

Zamani mambo ya Telex na Telegram Money order na si Mpesa zenu za sasa.
 
Kweli enzi hizo ilikuwa raha, mambo mengi yalikuwa shwari tofauti na na siku hizi kila kitu afadhali ya jana lol!

Wapi mwl Jirabi, Gilala walimu wa hesabu Kirumba/Nyakabungo s/m, enzi hizo ukifaulu kweli wewe kichwa, mtaani wanakuheshimu...leo sasa!!!!! lol!
 
enzi hizo nakumbuka,tunalipa nauli wanafunzi tsh 25/= afu shule zote za secondary tunapiga kampula dsm
 
Enz izo mtu akiingiza CM nyumban kwake anaogopwa,,,,cm unaunganshwa kama umeme,!

Enz izo kupiga cm mpaka pista,,,!
Enz izo tv hakuna,,,!

Nakumbuka kwa mara ya kwanza TV niliiona mwaka 86 kwa jiran etu alikua tajir mnooo!
hehehe na kupokea simu ilikuwa dilii....simu ikiita tu watoto mnatoka ndukii kuwahi kupokea...
 
Enzi hizo ukimtongoza msichana anaangalia chini huku akichora-chora kwa dolegumba chini au kukata kata kinyasi ; siku hizi bana ni Live!! acha longo-longo sema una sh gapi...?

Zamani mambo ya Telex na Telegram Money order na si Mpesa zenu za sasa.

Enzi hizo story za denda zilikuwa dili, vitu kama hug na kisses sio kisaaana, mambo mtwango tu, lakini sasa vijana dhaifu mbwembwe nyingi issue kidogo.
 
Back
Top Bottom