Pure nomaa
JF-Expert Member
- Dec 10, 2011
- 1,158
- 1,382
Kuna mzee mmoja alikuwa anashangaa sana maana kila akiweka whisky yake kwenye fridge akija kuiangalia baadaye anaikuta imepungua,siku moja akiwa pamoja na mkewe akaamua kumuuliza house boy wao ambaye alikuwa jikoni anapika;mzee akauliza nani anayekunywa whisky yangu humu ndani house boy akajibu sisikii,mzee akaita tena hb,hb akaitika naam mzee akauliza tena nani anayekunywa whisky yangu humu ndani ,hb akajibu sisikii,mke akaingilia kati hb mbona mzee anakuuliza swali hutaki kujibu,hb akajibu ukiwa jikoni halafu mtu akauliza swali humsikii kama mnabisha mmoja wenu aende jikoni halafu mi niulize swali nione kama atanisikia,basi mzee akaamua aende yeye jikoni,hb akaita mzee ,mzee akaitika naam,hb akauliza nani anatembea na house girl humu ndani mzee akajibu sisikii,hb akaita tena mzee akaitika naam akauliza swali lile lile tena mzee akajibu sisikii,basi mzee akatoka jikoni huku akisema kweli nimeamini mtu ukiulizwa swali ukiwa jikoni huwezi kulisikia.
ukiwa jikoni
ukiwa jikoni