Durusuni Somo Hili, Kazi kwenu Mabingwa.

Junius

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
3,181
139
DURUSUNI SOMO HILI.
Durusuni somo hili, Kwanini hamdurusu?
Somo hili Kiswahili, kingereza hakihusu,
Durusuni msifeli, somo lote siyo nusu.
v
Somo kaleta Mwalimu, Pamoja na mtihani.
Wanafunzi kufahamu, imekuwa tafurani.
Wamebaki kulaumu, tatizo hawalioni.
v
Mwanena ngumu topiki, eti hamuoni ndani!
Kudurusu hamutaki, mutajuwa kitu gani?
Kufeli mukidiriki, lawama zende kwa nani?
v
Munakhiyari “twisheni”, hiyo ndo suluhu gani?
Mnakesha vikaoni, darasa mnalikhini.
Somo lipo vitabuni, sasa mwajadili nini?
v
Somo hili tangu kale, limekuwa tatanishi.
Kila kukicha kelele, vineno neno havishi.
Huyu akitaka vile, mwengine huwa mbishi.


v
Musizinge ukakasi , hebu rudini durusi.
Hakuna haja matusi, vitisho na usabasi.
Somo lenyewe rahisi, wa nini tena uasi!
v
Someni na durusuni, waiteni wadarisi.
Herufi zote piteni , musiwache sentensi.
Nahau dadavueni, semanti na sintaksi.
v
Chambueni tamathali, za semi na viambishi.
Msisahau methali, na sarufi patanishi.
Na kanuni za usuli, nomino na viambishi.
v
Nahitimisha tamati, somo nakuwachieni.
Junius ninaketi, narejea darasani.
Mabingwa na wenye viti, kazi kwenu durusuni.
v
Junius,
24/7/2009
 
wasomi wakipuuza kitabu na wakiendelea na porojo tu, somo si lazidi kuwa gumu????
 
Back
Top Bottom