Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

Hoja ya Pili
Kuhusu upendeleo
Hili nalo linapaswa kuangaliwa kwa upana. Kwanza, malalamiko ya Sanders kuhusu upendeleo yalijikita katika maeneo makuu mawili
1. Kuruhusu chaguzi ziwe open kwa vile Sanders alionekana kufanya vizuri ingawa takwimu hazikubali
2. Kupelekea uchaguzi kwenye mkutano mkuu kwa kutohesabu super deleagates

Hapa kulikuwa na tatizo, kwamba, Sanders alipoingia katika uchaguzi alijua sheria zinazotumika
Ni zile zilizomuengua Hillary alipogombea na Obama. Kumbuka Obama alikuwa na super delegates wachache waliomuunga mkono. Kadri muda ulivyosonga walibadili mweleko na kumuunga mkono

Kwavile Demokrasia yao ni pana, Democrats walikataa maombi hayo. Kwamba, kama ipo haja basi sheria hizo zibadilishwe muda ujao na si sasa. Ni sawa na kutaka sheria za mchezo zibadilike wakati mchezo unaendelea. Demokrasia yao ikasema hilo hapana.

Kuhusu emails, hata Democrats wanakiri yalikuwepo maneno mabovu ndani yake.
Hata hivyo, wanachosema ni kuwa hakuna ushahidi kuwa katika sanduku la kura kulikuwa 'rigged'
Ndio maana Sanders na wafuasi wake hawana mahali pa kusema, wapi palikuwa na rigged elections

Kuhusu Demokrasia ya kujiuzulu, mara baada ya leak za habari Debbie Wasseman Schult wa Dem ametakiwa ajiuzulu nafasi hiyo mapema. Kinachosema ni tatizo ni kuwa wakati Sanders analalmika, ilikuwa wakati mufaka wa Debbie kujiuzulu ili kutoa nafasi kutokuwa na malalamiko

Tujuiulize, je hapa kwetu tumefanya hivyo hata kama ni kwa kuchelewa?
Waliosababisha mauza uza wamepongezwa , ndipo tofauti kati yao nasi inapoonekana

Hoja ya Tatu inafuata
 
3. FBI kuchunguza

Kinachofanywa na FBI si kuchunguza nani ametoa habari kama unavyosema

Wao wanachunguza nani amefanya 'hacking' wakitaka kujua nani ameingilia mawasiliano

Kumbuka Hacker wakiweza kuingia Dem, wanaweza kuingia hata katika military

Tofauti na 'Polisi', FBI wanatafuta root cause,effect, nani anafanya na kwa masilahi gani

FBI wanataka kujua kama nchi ipo salama katika zama hizi za Cyber War.

Hawatafuti nani ame leak information za Dem kama unavyoeleza.

FBI hawajasema ni Russia, waliosema ni kampeni ya Clinton.
FBI hawafanyii kazi madai, wanachunguza,kuna suala la usalama kwa upana wake

Kuwa FBI wanachunguza nani ame leak si kweli.

Wanachokifanya ni kazi kitaaluma kujua chanzo, nani anahusika na kwa masilahi gani.

Ikiwa ni ISIS utawezaje kusema nchi ni salama dhidi ya magaidi ukiacha majasusi.

Hapa kuna majasusi ambao ni china, Russia na Marekani wenyewe au nchi nyingine.

Kuna magaidi ambao sote tunawajua
 
Hoja ya nne

CCN: CNN wanajadili habari zilizotoka kwa muda huo
Wanatathmini possibility zote,kweli au uongo, wanajulikana kama Political pundits

Kauli zao si hukumu hata siku moja, ni maoni yao.
Hakuna mahali wamethibisha Russia wamefanya hivyo.

Ikiwa itatokea, watanukuu vyanzo kama walivyonukuu FBI na taarifa ya emails za Clinton

Kusema wamesema ni Russia, ni kuwahukumu kwa wasichosema.
Hawajathibitisha, bali kujadili kauli za viongozi wa Kampeni ya Clinton

Unaweza ona upana wa Demokrasia yao, kwamba, mambo yanajadiliwa bila vikwazo

Sisi tunaweka sheria za kuzuia watu wasijadili mambo yanayowahusu.
 
Hoja tya Tano

Kuhusu kubadili matakwa ya Marekani walio wengi
Kwanza, huu ni uchaguzi wa vyama,wingi wa matakwa ya Wamerkani si sahihi kusema

Pili, hakuna mahali wagombea walilalamika kuhusu matokeo
Trump alishinda ingawa wengi wa Republican hawamtaki.

Kwa ukubwa wa Demokrasia yao hakuna 'aliyefukuzwa hata robo' waliruhusiwa kuimba never Trump. Sisi ukiimba 'robo hawabaki'

Kura za Democrats zinaonyesha nani ameshinda wapi.
Na wagombea walikubali ilipotokea, si Sanders au Clinton.

Walijua Demography ya uchaguzi na walijua matokeo mapema kabisa

Kwa mfano, uchaguzi ulipokuwa middle west, ulikuwa ni caucus na weupe wengi.
Sanders aliandaa mikutano siku ya matokeo kwa kujua eneo lake.

Clinton hakuwa na mikutano.
Matokeo yakaonyesha Sanders ameshinda caucus 7 kwa mpigo

Ilipokwenda south, Clinton alijua ni eneo la watu wa rangi.
Aliandaa mikutano ya siku za matokeo, Sanders hakuandaa

Ilipokuwa New York, wote walijua wanaweza kushinda, waliandaa mikutano

Sanders haku kampeni Indiana, Clinton alijua ni eneo lake.
Clinton haku kampeni Wisconsin Sanders alijua ni eneo lake n.k

Ninachosema ni kuwa uchaguzi wao ni wa kisayansi si kiviazi.
Mgombea anajua ana nguvu wapi ni dhaifu wapi aelekeze rasilimali wapi.

Utashangaa matokeo wanayasikiliza kutoka kwa watu wao na katika TV
Ndiyo maana huwa wanaosubiri projections za TV na hapa nakuja katika hoja ya sita
 
NI HII 'DEMOKRASIA' YA DEMOCRAT YA MAREKANI TUHIMIZWAYO KUIFUATA?
TUJITEGEMEE, nadhani Nguruvi3 amekupa majibu murwa zaidi ila sina hakika kama ulifuatilia thread iliyotangulia hii kwa makini na namna wagombea wateule wanavyopatikana ndani ya vyama...hakuna anayetoswa na uongozi wa chama, hilo jukumu ni la mgombea na idadi ya kura anazopewa na wananchi katika majimbo yote 50 ya Marekani.

Hebu pitia hapa; Uchaguzi Marekani

Uchaguzi Marekani hupitia hatua nyingi hadi kumpata anayeitwa Presumptive Nominee wa chama. Kwa Republicans wagombea waliojitokeza walikuwa 17 na kwa Democrats walikuwa 4...hakuna aliyetolewa na Uongozi wa hivi vyama, ni wao wenyewe walichukua jukumu la kujiondoa moja baada mwingine walipoona nafasi zao za kushinda ni finyu.

Donald Trump hakupendwa na establishment na walimpinga wazi wazi na kuitwa majina lukuki lakini hilo halikuwazuia wananchi kumpa kura. Bernie Sanders hakuwa Democrat lakini establishment ingawa awali hawakumuunga mkono waliachia wananchi waamue wenyewe kama anafaa kulingana na sheria na kanuni walizojiwekea katika kila jimbo.

Mwaka 2008, ushindani ndani ya Democratic Party ulikuwa mkali kuliko wa mwaka huu na tofauti ya wajumbe ilikuwa ni ndogo kuliko sasa. Ingawa Hillary Clinton alionekana kuungwa mkono zaidi na establishment kuliko Barack Obama lakini hilo halikuzuia wananchi kumpa Obama kura na hivyo kulazimisha Clinton kujitoa na kumuunga mkono mshindi.

TUJITEGEMEE, leo wajumbe wote watatakiwa kupiga kura inayoitwa roll call vote kutoka kila jimbo na kama kura za Hillary Clinton hazitafikia idadi inayotakiwa kura zitarudiwa...hiyo ndiyo demokrasia tunayoongelea. Mwaka 2008, kura hii haikupigwa kwa sababu hakukuwa na haja baada ya Hillary Clinton mwenyewe kuamua kumpendekeza Barack Obama.

Swali kwa sasa ni je, Bernie Sanders atakuwa tayari kumpendekeza Hillary Clinton na hivyo kutokuwa na haja ya kupiga kura ama atataka ipigwe ili ajue idadi ya wajumbe wanaomuunga mkono kama alivyosema jana? Lazima ukumbuke kwamba bado Bernie Sanders anayo nafasi ya kusonga mbele kama atapata kura zaidi ya nusu ya wajumbe wote 4,764.
 
Hoja ya Sita

Hata kabla ya matokeo kuna exit poll zinazoonyesha nani anaongoza na wapi
TV zinaweza kubaini rigged elections kwasababu nazo zina system ya kubaini

Ingeshangaza sana Clinton kana angeshinda North Dakota, na ingeshangaza kama Sanders angeshinda Luisiana. Kila kitu kipo wazi na waandishi wangechunguza tu

Kwa taarifa ni kuwa tume ya uchaguzi wa Marekani ipo kama 'symbol' tu na hufanya kazi likitokea tatizo kubwa kama la Al Gore na Bush. Kinyume chake, kituo cha uchaguzi , county na state ndizo zina dhamana ya uchaguzi. Ndiyo msingi wa wenzetu kutanagaza matokeo kupitia TV kwasababu hesabu zipo wazi

Kwa mtazamo huo, tukubali kuwa wenzetu wametuacha.
Mapungufu yao hayawezi kuwa sawa na ububusa, uzembe, ututusa na viroja vya nchi masikini.

Tukijilinganisha nao kwa demokrasia ni sawa na perege au sato kusimam toe to toe na Nyangumi

Tusemazane
 
TUJITEGEMEE, nadhani Nguruvi3 Swali kwa sasa ni je, Bernie Sanders atakuwa tayari kumpendekeza Hillary Clinton na hivyo kutokuwa na haja ya kupiga kura ama atataka ipigwe ili ajue idadi ya wajumbe wanaomuunga mkono kama alivyosema jana? Lazima ukumbuke kwamba bado Bernie Sanders anayo nafasi ya kusonga mbele kama atapata kura zaidi ya nusu ya wajumbe wote 4,764.
Katika hotuba ya Sanders kasema hili la roll call na kusema kesho itapigwa na wajumbe wake wapo

Ukimsikiliza kwa makini,anataka roll call akiamini wajumbe kubadili mwelekeo.

Hilo ndilo kubwa kwa siku ya leo , kwamba idadi itatimia?

Je, atajitoa mapema kuliepusha? Au nini kinafuata

Tunarudi pale pale demokrasia inafanya kazi yake
 
Hoja ya Sita

Hata kabla ya matokeo kuna exit poll zinazoonyesha nani anaongoza na wapi
TV zinaweza kubaini rigged elections kwasababu nazo zina system ya kubaini

Ingeshangaza sana Clinton kana angeshinda North Dakota, na ingeshangaza kama Sanders angeshinda Luisiana. Kila kitu kipo wazi na waandishi wangechunguza tu

Kwa taarifa ni kuwa tume ya uchaguzi wa Marekani ipo kama 'symbol' tu na hufanya kazi likitokea tatizo kubwa kama la Al Gore na Bush. Kinyume chake, kituo cha uchaguzi , county na state ndizo zina dhamana ya uchaguzi. Ndiyo msingi wa wenzetu kutanagaza matokeo kupitia TV kwasababu hesabu zipo wazi

Kwa mtazamo huo, tukubali kuwa wenzetu wametuacha.
Mapungufu yao hayawezi kuwa sawa na ububusa, uzembe, ututusa na viroja vya nchi masikini.

Tukijilinganisha nao kwa demokrasia ni sawa na perege au sato kusimam toe to toe na Nyangumi

Tusemazane
Na si hivyo tu, madai ya rigged elections Marekani mara nyingi hayana msingi na kwa Democrats imetumiwa tu na wapenzi wa Bernie Sanders kama tuhuma zisizo na uthibitisho. Dai lao kubwa ni kwamba sheria zilizopo na ambazo zimetumika miaka yote zinahitaji marekebisho ili kuruhusu watu ambao si wanachama nao wapate fursa ya kupiga kura kwa urahisi. Tatizo hapa ni kwamba si uongozi wa juu wa Democrats unaotoa maamuzi haya, ni uongozi katika majimbo husika na establishment ya chama inalazimika kuyaheshimu.

Bernie Sanders aliingia kwenye kinyang'anyiro akizijua hizo sheria na kanuni na sehemu alizoshinda hakukuwepo na lawama ila zile aliposhindwa alitaka kuhamisha magoli. Mfano mzuri ni jimbo la California...aliamini fika kwamba angeshinda kulingana na ripoti zilizokuwa zinatolewa na wapenzi wake mtandaoni. Hata mimi na Nguruvi3 tulitofautiana...
Nguruvi3 said:
June 6, 2016 - California: Mshindi atakuwa Sanders
New Jersy: Mshindi atakuwa Hillary Clinton
Mag3 said:
June 6, 2016 - Mkuu Nguruvi3, hapo kwa California naomba nitofautiane nawe kidogo; kwa mambo yalivyo nadhani bado Clinton anayo nafasi ya kushinda California
Huu ni mfano tosha kwamba hata sisi humu JF tulitofautiana kulingana na ripoti mitandaoni.

Pamoja na hilo linapokuja kwenye swala la matokeo, si rahisi kuyachakachua kama wengi wanavyodhani. Vyombo vinavyofuatilia vikitoa projection na results viko lukuki na havibanwi na sheria za ajabu ajabu kama hapa kwetu Tanzania. Kura zinakuwa streamed live zinavyotoka na sijui kuzichakachua itawezekana vipi. Na kama mgombea haridhiki na zilivyohesabiwa na kujumlishwa ziko njia na hatua za kuchukua. Kwa mfano katika malalamiko yote yaliyowasilishwa na Sanders hakuna hata moja lililogundulika kuwa si sahihi.
 
"Mag3, post: 16983876, member: 10873"]Na si hivyo tu, madai ya rigged elections Marekani mara nyingi hayana msingi na kwa Democrats imetumiwa tu na wapenzi wa Bernie Sanders kama tuhuma zisizo na uthibitisho.
Katika kutibitisha hilo, tuhuma za emails zinahusishwa na uteuzi wa VP.
Wafuasi wa Sanders wanataka ateuliwe mtu wao kama si Warren basi Brown wa Ohio. Sasa hapa kuna uhausiano gani? Na mara zote 'pundits na surrogates' wameulizwa watoe ushahidi wa kuvurugwa uchaguzi , hakuna! Madai yao mengine ni kuzingatiwa sera za Sanders ambayo ymaezingatiwa
Dai lao kubwa ni kwamba sheria zilizopo na ambazo zimetumika miaka yote zinahitaji marekebisho ili kuruhusu watu ambao si wanachama nao wapate fursa ya kupiga kura kwa urahisi.
Tatizo hapa ni kwamba si uongozi wa juu wa Democrats unaotoa maamuzi haya, ni uongozi katika majimbo husika na establishment ya chama inalazimika kuyaheshimu.
Hii ni point muhimu sana.
Kwamba kila state ina utaratibu wake.
Ndio maana kuna caucus, open, closed and mixed elections.

Sheria za uandikishaji zinabadilika state moja hadi nyingine, za advance voting zinabadilika

Inapotokea tatizo, kwanza msimamizi wa kituo anaeleza, ikishindikana ni wa county, ikishindika ni wa state husika kutokana na sheria zao.
Bernie Sanders aliingia kwenye kinyang'anyiro akizijua hizo sheria na kanuni na sehemu alizoshinda hakukuwepo na lawama ila zile aliposhindwa alitaka kuhamisha magoli. Mfano mzuri ni jimbo la California...aliamini fika kwamba angeshinda kulingana na ripoti zilizokuwa zinatolewa na wapenzi wake mtandaoni. Hata mimi na Nguruvi3 tulitofautiana...
Na alisaini kuzifuata.
Hakuwa na malamiko New Hampshire au Iowa. Wala hakulalamika Michigan.

Kumbuka, alishinda caucus zaidi ya 7 mfululizo bila malalamiko.

Wakati huo alikuwa anasema wananchi wanamwelewa na ana momentum.
Iweje malalamiko yaanze baada ya kupoteza ?

Kuhusu kutofautiana , ninakumbuka sana. Nilisema California ni open, ina watu mchangiko zaidi na imeathirika kwa kiasi na mambo ya trade. Uwezekano wa kushinda Sanders kwa margin ya 1 au 2 upo, na nilisema hilo lingetokea. Mag3 kwa kuangalia vigezo vyake akasema hapana, itakwenda kwa Clinton

Ni kweli Clinton alishinda kwa point zaidi ya 10. Nilifuatilia kwa ukaribu matokeo yalivyoletwa, yaani yalikuwa mtaa, county , district hadi state yakinyumbulishwa bila ubishi. Sasa wizi ungefanyikaje katika mazingira ambayo media ilikuwa inatoa namba kwa tafiti na kazi zao?
Pamoja na hilo inapokuwa kwenye swala la matokeo, si rahisi kuyachakachua kama wengi wanavyodhani. Vyombo vinavyofuatilia vikitoa projection na results ziko lukuki na hazibanwi na sheria za ajabu ajabu kama hapa kwetu Tanzania. Kura zinakuwa streamed live zinavyotoka na sijui kuzichakachua itawezekana vipi. Na kama mgombea haridhiki na zilivyohesabiwa na kujumlishwa ziko njia na hatua za kuchukua. Kwa mfano katika malalamiko yote yaliyowasilishwa na Sanders hakuna hata moja lililogundulika kuwa si sahihi.
Ndio msingi wa media kufanya projections hata kama kura zimehesabiwa 10%. Kwanza kuna polls, halafu kuna exit poll. Zote zinaangaliwa kwa takwimu 'demography' ya eneo husika.
Hakuna mahali palipokuwa na malalamiko.
 
Katika hotuba ya Sanders kasema hili la roll call na kusema kesho itapigwa na wajumbe wake wapo

Ukimsikiliza kwa makini,anataka roll call akiamini wajumbe kubadili mwelekeo.

Hilo ndilo kubwa kwa siku ya leo , kwamba idadi itatimia?

Je, atajitoa mapema kuliepusha? Au nini kinafuata

Tunarudi pale pale demokrasia inafanya kazi yake
Kama tulivyosema jana, Sanders ni kama vile alifungua pandora box na jini limeshatoka hivyo, hakuna namna hata Sanders anavyoweza kulirudisha jini ndani ya chupa. Wapo wafuasi wa Sanders wameapa kutomuunga mkono Clinton hata wakiombwa na Sanders mwenyewe na hivi sasa wanahamasishana kwa kauli mbiu ya Bernie or Bust. Hii ina maana kuwa ama wako tayari kukaa nyumbani bila kupiga kura mwezi November au kama watapiga, watampigia Jill Stein wa Green Party.

Bahati nzuri kwa Clinton ni kwamba idadi ya wenye msimamo huo ni wachache kuliko ambao wako tayari kumpigia kura mgombea wa Democrats...ila wako wachache zaidi ambao wamesema heri kumpigia kura hata Donald Trump kuliko Hillary Clinton. Hali hii imemfanya Sanders kusita kumpendekeza Clinton kuwa mgombea ila alichokubali Sanders ni kuwashawishi wajumbe kutoka jimboni kwake Vermont ndio watoe hilo pendekezo lakini baada ya kura kupigwa na matokeo kutolewa.
 
Nguruvi3 na Mag3 nawashukuru sana kwa kulitendea haki dukuduku langu. Natamani watu wengi wangepitia mabandiko haya mliotoa juu ya dukuduku langu. Ninakubaliana nanyi mambo karibu yote mliyoeleza.

Mbali na maelezo hayo mliyoyatoa, nitolee maelezo kidongo kuhusu baadhi ya mambo nilivyoelewa na ninavyoyaona juu ya mchakato mzima wa uchaguzi marekani. Kumradhi kama kutakuwa na mengine nimeuliza mtakuwa mmeisha yatolea ufafanuzi huko nyuma. Mwaweza kuniwekea ya uzi husika na mkanielekeza pages zenye maelezo.

1. Nguruvi3 umeandika kuwa

"Kinachofanywa na FBI si kuchunguza nani ametoa habari kama unavyosema; Wao wanachunguza nani amefanya 'hacking' wakitaka kujua nani ameingilia mawasiliano"

Mimi nilimaanisha huyo huyo hacker/mdukuzi, maana aliyetoa habari tayari anajulikana (Wikileaks). Ninachoshangazwa, ni kwa nini FBI wanashindwa kuendelea mbele zaidi kufuatilia watuhumiwa wa 'ku-rig' ili Sanders ashindwe, kwani watu hao wanaweza kusabisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe (ingawa ili laweza lisitokee)! Ni kweli umuhimu wa kumjua hacker na njia alizotumia hauwezi kupuuzwa kwa maslahi ya nchi yao(Marekani). Hata hivyo kwa kuwa sijaisoma sheria iliyoiunda FBI na iliipa majukumu gani ngoja nipunguze kuilaumu FBI

2. Pia (Nguruvi3) kuna mahali umefafanua vizuri kuwa demokrasia inalenga hasa kuimiza jamii kutekeleza kile ilichokubaliana kukitekeleza kulingana na mahali jamii ilipo. Ukasisitiza demokrasia yetu si sawa na ya kwao. Hivi huoni kwamba 'suala' la zenji yawezekana tunawashinda wao kwa kuweka 'figisufigisu' zetu wazi wakati wao wanashindwa kujizuia kuwa wanafiki ndiyo maana wanazo mbinu kabambe za kuzuia 'figisufigisu' zisiwe wazi mpaka hackers wahusike?

Pia sijawelewa (Nguruvi3 na Mag3) vizuri kuwa kumekosekana ushahidi wa madai ya kuonewa Sanders wakati 'shehena' ya emails za staffers wa DNC zinawatia hatiani !! Au email ni 'fake' zile...!? I am just curious on this!

3. Mag3 Trump alipata madhila kama ya Sanders, kuna jimbo kama Utah, hao vote streamers (Microsoft) na wengine wakishirikiana na wenye fedha (soro) na walivuruga sana 'trend' ili kumbeba Ted Cruz.

Did George Soros Rig The Utah Vote To Help Ted Cruz Defeat Donald Trump?

Visanga vya Colorado navyo haviwezi kusahaulika kirahisi. Ted Cruz alibebwa, ni uhodari wa Trump katika kucheza 'karata' zake vizuri ndiyo kumemuwezesha kufika hapo alipo vinginevyo Ted alikuwa aiwkilishe Republican. Wakubwa wa Republican walimuogopa Trump, kwani 'kumkata' Trump kungeua chama.
Ted Cruz Defends Colorado 'Election': '65,000 Voted' - Breitbart

4. Ni kweli wanatuzidi 80% sisi tuna 40% kwenye demokrasia lakini wakimulikwa zaidi na tukafumua mbinu zao za kuficha 'figisufigisu' tunaweza kuwashusha asilimia zao.

Tafadhali msinichoke endelea kunielewesha haya mambo. Ninaimani wengi wanafidiaka na melezo yenu.
 
"
TUJITEGEMEE, post: 16984983,

1. Nguruvi3 umeandika kuwa

"Kinachofanywa na FBI si kuchunguza nani ametoa habari kama unavyosema; Wao wanachunguza nani amefanya 'hacking' wakitaka kujua nani ameingilia mawasiliano"

Mimi nilimaanisha huyo huyo hacker/mdukuzi, maana aliyetoa habari tayari anajulikana (Wikileaks). Ninachoshangazwa, ni kwa nini FBI wanashindwa kuendelea mbele zaidi kufuatilia watuhumiwa wa 'ku-rig' ili Sanders ashindwe, kwani watu hao wanaweza kusabisha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe (ingawa ili laweza lisitokee)! Ni kweli umuhimu wa kumjua hacker na njia alizotumia hauwezi kupuuzwa kwa maslahi ya nchi yao(Marekani).
Mkuu FBI Marekani wana taratibu zao za kazi tofauti na sisi. Kuna mahali wanaingia bila kuombwa(mfano tukio la kigaidi), kuna maeneo ya state wanaingia wakiombwa kwani huko kuna sheriff na vyombo vya state husika.

Likewise, kama Sanders ana ushahidi anaweza kuwasiliana na vyombo husika uchunguzi ufanywe kuanzia state level hadi federal kutlingana na madai.
Ndiyo msingi wa kusema, mbona madai ya rigging hayapo wazi?

Kuna uwezekano ilitokea, lakini lazima kuwe na proof kwamba ilitokea na ushahidi wa kutosha. Katika mazingira ya sasa, hakuna.
2. Pia (Nguruvi3) kuna mahali umefafanua vizuri kuwa demokrasia inalenga hasa kuimiza jamii kutekeleza kile ilichokubaliana kukitekeleza kulingana na mahali jamii ilipo. Ukasisitiza demokrasia yetu si sawa na ya kwao. Hivi huoni kwamba 'suala' la zenji yawezekana tunawashinda wao kwa kuweka 'figisufigisu' zetu wazi wakati wao wanashindwa kujizuia kuwa wanafiki ndiyo maana wanazo mbinu kabambe za kuzuia 'figisufigisu' zisiwe wazi mpaka hackers wahusike?
Hapana , Marekani ufute uchaguzi wa jumla tu kwasababu ya Ujecha, halitokei. Wenzetu wamekomaa sisi ya kwetu ni uozo.
Fikiria Cameron amejiuzulu kwa kushindwa tu kura ya maoni!
Kuna mahali wenzetu wamevuka

Kuna wakati Republican wanashinda, kuna nyakati Dem, unadhani ni kwa nini
Kilichotokea Zanzibar,hata waafrika wenyewe wanaona haya isipokuwa tu wale ambao mtima wa haya haupo!Lakini si znz tu hata bara.

Mwenyekiti wa 'Neki' alisema tume si huru akitoa maoni ya katiba, majuzi anasema ni huru sana. Kwa wenzetu wasingekubali kubabaishwa hivi!

Chaguzi zetu ni mfano, chaguzi ni kama za hizi tunazoona sasa, mchezo unachezwa uwanjani. Siasa inafanywa na kuwa burudani

Mkuu sisi hatupaswi ku-question demokrasia ya US , tupo porini kabisa!
Pia sijawelewa (Nguruvi3 na Mag3) vizuri kuwa kumekosekana ushahidi wa madai ya kuonewa Sanders wakati 'shehena' ya emails za staffers wa DNC zinawatia hatiani !! Au email ni 'fake' zile...!? I am just curious on this!
Emails zinaeleza mawasiliano yaliyokuwepo. Je, ni ushahidi wa uchaguzi kuwa rigged? Kuna uhusiano gani wa kampeni na mawasiliano ya ofisini. Na kama emails zipo za kuthibitisha hilo ni jema, ndio ushahidi wenyewe , kwanini wasizitumie kutengeneza kesi, bali wanatumia hoja za kutaka VP?

Hoja za Mkuu Mag3 atatusaidia kuzieleza

Na mwisho,hakuna kuchokana, ni katika majadiliano mkuu, tunafurahi watu wakichanganyika namna hii. Tunajifunza kutoka kwa kila mmoja wetu
 
Breaking news

Hillary Clinton ameteuliwa rasmi kuwa mgombea wa Democrats

Mkutano unaendelea
 
JIMMY CARTER

Anaongea kupitia video baada ya kukaribishwa na mjuu wake Jason

Anasema
-Anamjua Hillary kwa miaka 40 akiwa mwanasheria

-Hillary ana 'take difficult job and yet done'

-Clinton ana support yangu na natumaini nanyi pia

Anamaliza
 
Seneta C.Shumer wa NY

-Obama amepigana kila siku kulinda haki za Waamerika, bado tuna kazi kubwa

-Tunataka tuwe na level field kwa kila mmoja, ikiwemo ushindi wa Clinton na senate majority. Namjua Hillary tumefanya kazi pamoja kwa miaka 8 kama maseneta. Natoka Brookly, namjua akisema jambo ana maanisha hivyo

- Hillary anasikiliza wafanyakazi katika viwanda, akipigania viwanda visifungwe

-Alikuwa sehemu muhimu ya 9/11 kwa firefighter akiwapigania kupata huduma za afya. Ndio uongozi

-Uchaguzi huu ni vision mbili za Amerika, Trump anaona hofu na kutisha washirika wetu nje. Hillary anaamini kila mmoja ana uhuru na haki sawa

-Tofauti zetu zinatuweka pamoja, na Clinton ana vision. Hawezi kufanya hayo peke yake, anahitaji majority katika seneta

-Senti itakayoongeza ujira, kupitia reform za uhamiaji, na kutoa fursa kwa wanafunzi. Ataangalia mikataba ya biashara

-Tukiwa na Hillary tutaweka ndoto za Waamerika 'live'

Anamaliza
 
Donna Brazil

-Nimeishi katika zama za ubaguzi

-Kama mtu mzima nimebahatika kuona Rais Mweusi

-Na sasa nategemea kuona Rais mwanamke

-Hillary amefanya mengi kwa walemavu na wasio na fursa

- HC ha mess around, ana mean business, na hajabadilika kuanzia nilipomujua nikiwa na miaka 22

-Anasimama kwa akina mama na watoto duniani. Hajasahau kazi zake za kutetea watoto. Anataka kila mtu aishi kwa fursa aliyo nayo

-Nikiwa VP wa DNC tutahakikisha pamoja tunasherehekea kutawazwa kwake

Anamaliza

** Huyu ni commentator katika TV na VP wa DNC kitaifa
 
DAVID BANKS

Anawakilisha academy moja ya NY (Eagle academy)

- Kuna kiongozi alikuwa nasi katika kuanzisha academy. Mtu aliyeamini katika academy yetu inayotoa elimu kwa watoto

-Nipo na HC kwasababu yupo nasi. Leo tuna future leader, brilliant and full of promise.

**** Hii ni academy kwa watoto waliofungwa na sasa wapo huru***
 
Barnie Sanders protester wanaonekana nje ya ukumbi

Wanazuiwa na Polisi
 
ERIC HOLDER

Huyu ni AG katika Obama Adm

-Anazungumzia usalama wa Polisi na mtu atakayezuia incarceration

-Nikiwa AG tulikata kiwango cha uhalifu kwa miaka mingi. Tofauti na mnavyosikia violence imepungua wakati wa Obama

-Katika nyakati haki ya kura ilipotekwa na GOP kwa kufunga vituo, tunahitaji Rais atakayesimamia hilo atakayesimama na haki ya kura kwa modern politic

Ndugu zangu waamerika HC ndiye mwenye. Atabdili voting system, ukiwa na 18 automatic unakuwa rgistered

-Tupo katika mapinduzi ambayo ni Zaidi ya siasa. Anasimamia haki, usawa na fursa na ndizo tunu atakazosimamia akiwa Rais

Anamaliza
 
POLICE CHIEF KUTOKA PITTSBURG

-Polisi wanafanya kazi ngumu, mwanzo wa siku hawajui watakumbana na nini

-Kuna crisis katika community za color

-Kuna crisis katika justice system

-MLK alisema Amani si kutokuwa na tension bali kuwa na sharia thabiti

-Utata wa mauaji ya Ferguson yamesababisha tension kati ya Polisi na jamii
Tunafanyia kazi pamoja

-Pitts tunafanyika kazi kuhakikisha haki inatendeka

-Mauaji mawili ya siku mbili yenye utata na mauaji ya Polisi yanatatiza na ni ya kweli. Criminal justice yana impact katika community za color

-Kupungua kwa fursa za kiuchumi na maradhi ya akili yanachangia

-Kama Polisi niliyefanya kazi miaka 30, tunaunga mkono Polisi na kusukuma criminal justice reform

-Ni lazima tushinde hisia zetu na kutafuta muafaka wa kutengeneza US kama ilivyo yenye uhuru kwa kila mtu

Anamaliza
 
Back
Top Bottom