Duru za siasa: Uchaguzi Mkuu USA

TED CRUZ NA PENCE WAKAMPENI

Kuelekea mwisho wa kampeni kumetokea tukio la hasimu wa Trump na mgombea Ted Cruz kufanya kampeni na VP Mike Pence. Ted alisema anafanya kampeni na kupigia kura Republican.
Hakusema anampigia Trump.

Cruz amekuwa hasimu namba moja wa Trump. Kitendo cha kuingia katika kampeni kinaturudisha nyuma katika bandiko moja tuliloeleza kwanini Mike Pence hakutaka kujitoa kama shinikizo la Trump kuachia ngazi lililowekwa na Republican miezi miwili iliyopita

Tulisema katika bandiko hilo kuwa wanasiasa wana short and long term plan

MIKE PENCE
Huyu anatarajiwa kuwa VP kama Trump atashinda. Hiyo ni nafasi ya juu sana ambayo itamapa uwezo mkubwa wa kugombea siku za mbele kama ilivyokuwa kwa Al Gore au George Bush Senior.

Pili, kwasasa anatumia resource za bure kuzunguka nchi nzima akikampeni. Ikitokea hawatashinda uchaguzi huu, Pence atakuwa na mambo mawili. Kwanza, atakuwa amejitambulisha katika jukwaa la Taifa. Ataendelea kuwa tegemeo la Republican siku zijazo na anatumia fursa kujenga mtandao kwa siku ziajazo

Kwahiyo kwake kushinda au kushindwa bado ni ushindi kwasababu ima anakuwa VP au anajenga platform ya siku za baadaye.

TED CRUZ
Ted ana matumaini ya kugombea tena hasa kwa kuzingatia alikuwa wa pili na alionekana kukubalika kwa baadhi ya wapiga kura. Tatizo lake ni 'vita' na wenzake wa Washington

Plan yake ya muda mrefu itakuwa na madhara kama atasusia kampeni zinazoendelea
Ndiyo maana amaemaua kukampeni kwa maseneta ili siku zijazo wamuunge mkono

Lakini muhimu ni kundi linalomuunga mkono Trump. Kundi hili atalihitaji mbele ya safari.

Anachokifanya Ted ni kutafuta ushahidi kuwa alishiriki kumpigia kampeni Trump siku atakapokabiliana na kundi hilo mwaka 2020

Tusemezane
 
Sheriff David Clarke wa Milwaukee leo kawashangza na kuwaudhi wengi kwa kumfananisha mgombea wa Urais kutoka GOP, Donald Trump na Martin Luther King! Sheriff Clarke, mweusi na mfuasi wa Trump, amesema hayo akiwa mjini Cleveland, Ohio, kwenye kampeni ya kumnadi mgombea huyo.

Akiendelea zaidi, amedai asilimia 20% ya weusi nchini humo watampigia kura Trump kwani wanampenda na kumuona kama mkombozi wa weusi na hivyo wako tayari kumpa heshima kama anayopata Martin Luther King. Maajabu hayaishi.

Hilo jambo limezua tafrani kubwa miongoni mwa weusi ikizingatiwa kwamba polls zinaonesha anaungwa mkono na asilimia isiyofika hata 5% ya weusi! Hali hii inaweza kuongeza hamasa kwa weusi kuzidi kumkataa Trump.

Kesho wakazi wa Cleveland wakiongozwa na mcheza mpira wa vikapu maarufu mjini humo, LeBron James wataungana na Clinton kwenye kampeni. Tutegemee kuwaona viongozi wengi wa weusi wakijitokeza kulaani vikali kauli hiyo ambayo inatafsiriwa kama ya kumdhalilisha MLK Junior.
 
Kulikoni? Donald Trump rushed off stage at Nevada Rally by secret agents!
 
Kulikoni? Donald Trump rushed off stage at Nevada Rally by secret agents!
Yes amekuwa rushed off the stage, nimeona clip kwa ufupi

Habari zilizopo si rasmi n kutoka kwa watu tu, bado vyombo vya umma havijasema lolote
Kuna mtu mmoja ameshikiliwa ingawa hana silaha kwa mujibu wa walioko huko

Bado information ni vague, lakini ni kweli Trump aliondolewa kindaki ndaki

Tukio hili linakumbusha jana wakati Obama akiwa NC.
Katika mkutano alitokea mfuasi wa Trump na kuanza kuleta rabsha.

Obama akawaambiwa wahudhuriaji mtu huyo hana kosa nchi ya Marekani ina freedom of expression, na mtu huyo anaonekana kuwa veteran na mtu mzima hivyo asizomewe

Jana hiyo hiyo Trump katika mkutano akasema Obama alimshambulia yule mzee jambo lililokuwa kichekesho kwa vyombo vya habari.

Sasa kwa ya Nevada na tunavyomwelewa Trump kesho kunaweza kuwa na link na crooked Hillary n.k.

Katika habari nyingine VP wa Clinton , Tim Kaine kapata ajali ya basi katika msafara.
Haionekani kama kuna serious issue katika hilo

Tunafuatilia na tuta update kila mpya
 
Asante sana wadau tu aendelea kuwafuatilia na kuchangia tunapoweza.

Nguruvi3 na wadau,
Tumeona issue ya email iliyoibuliwa na Comey director wa FBI kama imempa hedge Trump na kumkandamiza sana bibi Hillary na kampeni yake, najiuliza timing yake huyo bosi ni sahihi kweli kwa alichokifanya na je maamuzi yake si yana influence uchaguzi, je ametumiwa au kafanya kwa utashi wake, maana ni kama kesi yake ilikuwa imeshaisha na emails zilionekana sio classified na hazina atahari kwa serikali, japo sio sahihi kutumia server binafsi.

Sasa je baada ya uchaguzi huyu jamaa mustakabali wake upoje?? Atajiuzulu mwenyewe, atshitakiwa kwa kosa lake la kuingilia within 60 days au kuavoid kuonekana anaonewa atabaki salama??

Vp kuhusu impact yake kwenye uchaguzi?? Maana wenzetu ni information age tofauti na hapa kwetu tungesikia kigu kama hicho karibu na uchgauzi wala kusingekuwa na athari, mm nimefuatilia karibu polls zote kama mama kadrop mno na wamekaribiana mno. Huyu jamaa kamwathiri sana Hillary in favour of Trump, na nianoana kama uchaguzi tite mno kuliko awali kabla ya email, na hali ni mbaya zaidi kwa Bi Hillary.
Tusemezane wadau, naona kama mama ana hali mbaya sana kwasababubya Comey.
 
Mkuu
Asante sana wadau tu aendelea kuwafuatilia na kuchangia tunapoweza.

Nguruvi3 na wadau,
Tumeona issue ya email iliyoibuliwa na Comey director wa FBI kama imempa hedge Trump na kumkandamiza sana bibi Hillary na kampeni yake, najiuliza timing yake huyo bosi ni sahihi kweli kwa alichokifanya na je maamuzi yake si yana influence uchaguzi, je ametumiwa au kafanya kwa utashi wake, maana ni kama kesi yake ilikuwa imeshaisha na emails zilionekana sio classified na hazina atahari kwa serikali, japo sio sahihi kutumia server binafsi.

Sasa je baada ya uchaguzi huyu jamaa mustakabali wake upoje?? Atajiuzulu mwenyewe, atshitakiwa kwa kosa lake la kuingilia within 60 days au kuavoid kuonekana anaonewa atabaki salama??

Vp kuhusu impact yake kwenye uchaguzi?? Maana wenzetu ni information age tofauti na hapa kwetu tungesikia kigu kama hicho karibu na uchgauzi wala kusingekuwa na athari, mm nimefuatilia karibu polls zote kama mama kadrop mno na wamekaribiana mno. Huyu jamaa kamwathiri sana Hillary in favour of Trump, na nianoana kama uchaguzi tite mno kuliko awali kabla ya email, na hali ni mbaya zaidi kwa Bi Hillary.
Tusemezane wadau, naona kama mama ana hali mbaya sana kwasababubya Comey.

Mkuu King Suleiman, kabla sijajibu naomba uitafakari hii scenario...
  • To win, Trump needs a lot to go right.
  • To lose, Clinton needs a lot to go wrong.
Kwa sasa kuna maswala mengi yameibuibuliwa na Trump...
  1. Rigged elections
  2. Classified Emails
  3. Clinton indictment
  4. FBI leaks
  5. Wikileaks
  6. Russsian hackings
  7. Establishment stupidity
  8. Tax returns
  9. Assassination attempt
  10. Rise of alt-right.
Je katika haya yapi ni right kwa Trump na yapi ni wrong kwa Clinton.
Amini usiamini, baada ya Uchaguzi yako mengi yatahitaji uchunguzi.
 
King Suleiman ,

..sheria za Marekani zinaelekeza kwamba Dir Gen wa FBI atatumikia kwa kipindi kimoja cha miaka 10.

..kwa hiyo si Clinton wala Trump mwenye uwezo wa kutengua uteuzi huo kama inavyofanyika hapa Tz.
Naam sheria za Marekani inasema hivyo lakini inategemea pia na uzito wa tuhuma. Congress inaweza kumshitaki (impeach) kulingana na article 2 section 4 ya katiba ya Marekani na hii imewahi kutokea mara moja katika historia ya Marekani.

Pamoja na hayo yako makosa yanayomwezesha Rais kumuomba ajiuzulu lakini akikataa Rais anaweza akasitisha muda wake kama alivyofanya Rais Bill Clinton mwaka 1993 alipomuondoa William Sessions kabla ya muda wake wa miaka kumi.
 
james-comey-fired-fbi-director-hillary-clinton-email-private-server-bill-president.jpg


President Bill Clinton (l) and Attorney General Janet Reno announce the firing of FBI Director William Sessions in 1993.

Under a United States statute that first went into effect in 1968, FBI directors are nominated by the president and must be confirmed by the Senate — a process similar to the nomination and confirmation of Supreme Court justices or presidential cabinet officials.

Unlike the justices, who are appointed for life and cannot be fired — but can be impeached by congress (which has happened only one time in American history) — or cabinet officials who have no set terms, the FBI director is appointed to a single term of 10 years.

The statute establishing the 10-year term limit was passed in 1976, four years after the death of legendary FBI director J. Edgar Hoover, who held on to the job for 48 years.

But according to a 2014 report by the Congressional Research Service, “there are no statutory conditions on the President’s authority to remove the FBI Director.” In other words, the President can indeed fire the FBI director. An FBI director can also be removed by congress, through the impeachment process.
 
King Suleiman
Kuhusu Comey majibu ni kama aliyosema JokaKuu na Mag3

Kwa wenzetu Bosi akikuita na kusema anapata ugumu wa kufanya kazi nawe, mara nyingi ni kujiuzulu

Kuhusu timing , hili ndilo mjadala kwasasa kuliko emails zenyewe.
Kwanza, barua aliandika kwa Republican bila ku copy minority Dem au mhusika.

Pili, barua haikuwa na details na Dir alikiri hajajua nini kimeonekana na kama ni relevant or no

Timing haipo katika siku 60 za kutoingilia uchaguzi na hili limefanyika kukiwa na habari za ushiriki wa Rudi Guillin ambaye ni mshauri wa Trump. Kwahiyo si timing tu, kuna leak za information

Kwamba, hili jambo limeathiri kampeni ya Hillary hilo ni wazi. Kwa mfano, wiki nzima Trump anasema Clinton atakuwa indicted na sehemu nyingine anasema ni looming indictment.

Kwa independents hili lina impact kubwa. Hivyo barua ya FBI imeathiri uchaguzi kwa sehemu kubwa
 
HABARI ZA KUVURUGA UCHAGUZI
Kuna taarifa za serikali ya Marekani kuwa Russia itafanya hacking ya system za uchaguzi

Hili ni ku undermine uchaguzi wa Marekani na kuthibitisha kauli ya uchaguzi ni rigged

Vyombo vingi vya habari vinaonyesha wasi wasi na azma ya Russia ya kuingilia uchaguzi

Concern hii inatokana na WikiLeaks, kuna msemo wa kiingereza unosema 'Chicken are coming home to roost'

Tunafuatilia zaidi
Asante kwa maelezo mazuri juu ya kile kinachoendelea huko US kuhusu uchaguzi.

Hapa Mwalimu wangu pamoja nawengine mmeniacha njia panda. Kwa mara ya kwanza nilipoleta humu habari za rigging ya uchaguzi kutoka kwa Trump, mnilipinga vikali na kubeza suala hilo.
Sasa wakati huu mnasema kuna uwezekano wa kuvuruga uchaguzi kwa njia za udukuzi, Je. hiyo hiyo hacking tutaamini vipi kuwa imefanywa na nchi za nje? Na sasa kama hacking inawezekana, hapo "ujecha jecha "unashindikanaje kufanywa na wenye nguvu(White power in white house) kumuweka wanayemtaka?
 
Asante kwa maelezo mazuri juu ya kile kinachoendelea huko US kuhusu uchaguzi.

Hapa Mwalimu wangu pamoja nawengine mmeniacha njia panda. Kwa mara ya kwanza nilipoleta humu habari za rigging ya uchaguzi kutoka kwa Trump, mnilipinga vikali na kubeza suala hilo.
Sasa wakati huu mnasema kuna uwezekano wa kuvuruga uchaguzi kwa njia za udukuzi, Je. hiyo hiyo hacking tutaamini vipi kuwa imefanywa na nchi za nje? Na sasa kama hacking inawezekana, hapo "ujecha jecha "unashindikanaje kufanywa na wenye nguvu(White power in white house) kumuweka wanayemtaka?
Rigged election ya Trump hakuwahi kuieleza kwa system.

Alichosema ni rigged election kwasababu ya media.
Hilo ndilo tumezungumzia muda mrefu na kusema hakuna mahali alipo justify system nzima tofauti na wewe uliyesema rigged system ipo kwa mujibu wa Trump.

Kwa maana kuwa mlikuwa na hoja moja mkisoma page tofauti. Hilo ndilo tulisema si kweli

Kuhusu interference, homeland security imebaini kuwa Russia kwa mujibu wao wanataka kufanya hacking. Hapo madai ya Trump yatakuwa halali hata kama yalikuwa ya media.

Wlichokusudia ni kuvuruga zile voting system majina kuonekana tofauti na kuleta vurugu

Vyama vyote vimeelezwa kuhusu hali hiyo . Wataalam wanasema uchaguzi wa Marekani ni localized, kama rigging itakuwa localized na si nationwide. Leo wamaongelea sana hilo

Tulikueleza pia kuwa uchaguzi ule ni ngumu ku rig as whole kwasababu upo localized

Sasa sioni hoja yako ni ipi baada ya hilio, siioni kwasababu hawana utaratibu wa kukusanya matokeo na kutangaza kama Tz.

Kesho media zinapata matokeo right away na penye matatizo yanashughulikiwa kama ilivyotokea North Carolina na Iowa

Iowa mfuasi wa Trump amekamatwa akitaka kupiga kura mara 2, na sasa anakabiliwa na kosa la felony ambalo adhabu ni miaka 5 au faini ya 5000 kama sijakosea

Utajitahidi sana kuufanya uchaguzi wa Marekani uonekane sawa na wa Tanzania, katika hilo utajichanganya mwenyewe au wanasema fool yourself kwasababu ni vitu visivyoweza kulinganishwa hata kidogo.
 
Utajitahidi sana kuufanya uchaguzi wa Marekani uonekane sawa na wa Tanzania, katika hilo utajichanganya mwenyewe au wanasema fool yourself kwasababu ni vitu visivyoweza kulinganishwa hata kidogo.
Huyo TUJITEGEMEE sijui hata anataka kusema nini hapa na sina hakika kama anafuatilia vizuri yanayoandikwa humu. Matokeo ya uchaguzi Marekani yanatangazwa live kama yanavyohesabiwa kutoka kila kituo na hakuna kiumbe chochote ama kinachozuiwa au kinachohodhi matangazo ya matokeo vituoni kama yanavyotolewa.

Magazeti, vituo vya redio na television na vyombo vyote vya habari viko huru kutangaza matokeo wanavyoyapata bila pingamizi kutoka kwa yeyote. Rais na wateule wake hawana mamlaka yoyote katika uchaguzi, wenye mamlaka ni viongozi waliochaguliwa na wananchi kwa kupigiwa kura na kwenye majimbo wengi wao ni Republicans.
 
Nawawhukuru sana Nguruvi3, Mag3 na Jokakuu, nimepata shule ya muhimu sana. Kimsingi nimetambua kwamba wenzetu wapo mbali sana kwenye mambo mawili kwanza uwazi na clear processing za kila wafanyacho, yaani kuna miongozo kwenye kila jambo, kiasi inaonekana kabisa wapi pana kosa au wapi pana kasoro, hakuna upendeleo kabisa wa vyombo vya dola dhidi ya mpinzani, ndio maana Comey amefanya yake kumuathiri mgombea wa chama tawala, kwetu nadhani sasa angekuwa kijijini anaangalia mashamba yake.

Pili nimejifunza wenzetu wapo information age, yaani taarifa yoyote ile au kashfa yoyote ina madhara makubwa sana kwenye uamuzi wa kupiga kura, kwa lugha Nyepesi taarifa zinawafikia Kwa wakati watu wengi na wanafanya maamuzi wakiwa well informed kwamba wanamchagua mtu wa aina gani. Hapa kwetu sio ajabu kabisa ukasikia mtu analalamika sijui tulimchagua mathalani raisi au mbunge au diwani ila sasa ametugeuka au hatufanyii vizuri, na uchaguzi ujao utashangaa wanchagua the same, tatizo hapa sisi information parten hatupo vizuri ndio maana nj rahisi sana kupotoshwa na kuaminishwa vitu vingi ndivyo sivyo.

Kwa kweli nimefuatilia uchaguzi huu na shule nimepat sana, asanteni team nzima ya uchambuzi, mnatuelimisha mno
 
Naam sheria za Marekani inasema hivyo lakini inategemea pia na uzito wa tuhuma. Congress inaweza kumshitaki (impeach) kulingana na article 2 section 4 ya katiba ya Marekani na hii imewahi kutokea mara moja katika historia ya Marekani.

Pamoja na hayo yako makosa yanayomwezesha Rais kumuomba ajiuzulu lakini akikataa Rais anaweza akasitisha muda wake kama alivyofanya Rais Bill Clinton mwaka 1993 alipomuondoa William Sessions kabla ya muda wake wa miaka kumi.

..i am 100% ktk post yako hii.

..kuongezea tu, FBI Dir William Sessions alipatikana na makosa ya kutumia madaraka yake vibaya, pamoja na makosa ya kukwepa kulipa kodi.

..uchunguzi uliomkuta na makosa hayo ulifanywa na Justice Department na AG Janet Reno baada ya kujiridhisha na matokeo ya uchunguzi huo akashauri FBI Dir William Sessions aachie ngazi.

..kwa hiyo utaona kwamba kwa wenzetu hakuna aliye juu ya sheria.

Cc King Suleiman
 
FBI wamemsafisha bi Hillary ba saga la emails siku tatu kabla ya uchaguzi,

FBI Director James Comey told lawmakers Sunday the agency hasn't changed its opinion that Hillary Clinton should not face criminal charges after a review of new emails.

Comey had dropped a bombshell 11 days from the election when he informed Congress that the FBI had discovered emails in its separate investigation of Anthony Weiner, the estranged husband of top Clinton aide Huma Abedin, that could be connected to its investigation of whether Clinton mishandled classified information by using a private email server.

It's impossible to know before results are tallied what impact Comey's actions -- first raising a vaguely worded red flag 11 days out, and then lowering it two days from the election -- will have on the contest. But the news could help Clinton put to rest a controversy that has dogged her in the 2016 race's closing days, helping Donald Trump narrow a polling gap nationally and in key battleground states.

Election 2016: Emotions run high in final days of the campaign

"Based on our review, we have not changed our conclusions that we expressed in July," Comey said in the letter to top Republicans on the House Oversight Committee.
 
Back
Top Bottom