Duru za Siasa: 'Safari ya Dodoma'

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,406
31,387
SAFARI YA DODOMA

Uamuzi wa kuhamia Dodoma ni tukio la 'kushtukiza' lililopokelewa kwa mshawasha na hisia

Ni tukio lilozua taharuki kwa taasisi, watendaji ,wafanyakazi na jamii kwa ujumla

Kadri siku zinavyosonga mbele mengi tuliyojadili yanajitokeza kwa sura tofauti

Hoja kubwa si kuhamia Dodoma, bali utaratibu wa kuhamia Dodoma

Wengi wanadhani ni suala jepesi kuhamisha makao makuu ya nchi

Kuna kuchanganya mambo kati ya kuhamia Dodoma kama makao makuu ya nchi/serikali
Halafu kuna kuhamia Dodoma kama kitovu cha shughuli za nchi ikiwemo biashara

Makao makuu ya nchi na serikali ni sehemu maamuzi mengi ya kisera na utekelezaji hufanywa.

Ndio msingi wa kuhamisha wizara na idara za serikali pamoja na mihimili mingine ya dola

Haina maana ya kuhamisha shughuli za biashara. Dar es Salaam itabaki kuwa kitovu cha biashara kutokana na miundo mbinu yake na hata nafasi yake kijiografia ua idadi ya watu

Tunaanza kuona ugumu wa kuhamia Dodoma kwa namna tofauti

Maswali yanayojitokeza;
Je, maamuzi ya kuhamia Dodoma yalifanyiwa marejeo na kuhakiwa kabla ya kutangazwa?
Je, vyombo husika vilishirikishwa katika kupanga au kuonyesha 'concern' zao
Je, ilikuwa suala la kuhamia Dodoma kwa haraka, au lilikuwa na plan za muda mrefu?
Je, Mji wa Dodoma upo tayari kupokea ugeni utakaoongeza 'strain' huduma za umma?

Kwa umuhimu wa suala hili, uzi utakuwa endelevu kujadili nini kinachoendelea

Kwa kuanzia, tutarejea tuliyowahi kuyajadili nyuma

Tusemezane
 
KULIKUWA NA MAREJEO KABLA YA KUPANGA SAFARI?

Uamuzi wa kuhamia Dodoma ulifanywa miaka karibu ya 40 iliyopita na awamu ya kwanza

Kwa mujibu wa wazee waliokuwepo, mpango huo ulikamwa kutokana na kuingilia na masuala mengine ya kipaumbele kwa Taifa kama uwepo wa vita ya Kagera

Kutokana na hyo, uwezo wa kiuchumi ukawa tatizo na kila awamu ilikwepa jambo hilo

Miaka 30+ ni mingi sana katika dunia hii inayokwenda kasi.
Yapo mabadiliko ya kicuhumi, kisiasa na kijamii ambayo hayakuwepo uamuzi unatolewa

Hii ni pamoja na mabadiliko katika eneo la teknolojia ambalo limekuwa na athari chanya au hasi katika sekta zote, iwe ujenzi, afya, mawasiliano, elimu n.k.

Urefu wa muda na mabadiliko yaliyotokea yanatueleza jambo muhimu.
Kwamba, tulitakiwa kufanyia marejeo hoja kujiridhisha uwepo wa umuhimu au la

Tulipaswa tuwe na mjadala mpana wa Kitaifa kwa haraka ili kutupa mwanga kama bado tupo katika njia sahihi au tunahitaji marekebisho au mpango mzima hauna tija

Tuna uhakika suala lisingekuwa na urasimu kwani ni kwa masilahi ya kila mmoja

Taharuki iliyowakumba watendaji, tunahoji kama ngazi za juu zilishiriki mjadala mfupi?

Tunauliza kulikuwa na marejeo au tulikwenda na maamuzi ya miaka 30 iliyopita?

Na je, hakukuwepo haja ya mjadala wa kitaifa au kupitia wawakilishi kufikia uamuzi?

Tusemezane
 
JE, KULIKUWA NA USHIRIKISHWAJI WA VYOMBO VINGINE

Tarehe 31 JULY 2016
Tuliandika kuwa CDA imekuwepo kisheria kwa muda wa uhai wa tangazo la kuhamia Dodoma. Jukumu kubwa lilikuwa kuandaa mji kwa ajili ya kupokea serikali

CDA ilipata fungu la kazi ya kuendeleza makao makuu.
Katika kipindi hicho hatuoni ufanisi kwa taharuki iliyotokea baada ya tangazo kutolewa

Tukauliza, kama CDA haikuweza kufanya maandalizi ni muujiza gani unaooweza kusaidia serikali kuhamia huko mwezi huu ?

Swali hilo limepata jibu karibuni kwa ofisi ya waziri mkuu kushindwa kuhamia kama ilivyosemwa

Makazi ya waziri mkuu hayajakamilika, na kwa mujibu wa gazeti moja la Sept 10 2016 waziri mkuu amesema uhamaiaji utakuwa wa awamu tofauti na haraka iliyokuwepo

Wakati huo huo, taasisi za huduma za jamii kama Hospitali na idara ya maji zimeonyesha wasi wasi kuhusu ujio, kwamba huduma hazitakidhi mahitaji

Hatuna uhakika maeneo ya huduma za miundo mbinu (sewerage) barabara, masoko, makazi ya wananchi , shule n.k. yapo tayari kwa ugeni tarajiwa

Hili linatueleza jambo moja, kwamba hakukuwa na ushirikishwaji wa vyombo vingine na hivyo kujikuta katika hali ya ''kufumaniwa' kama lugha ni sahihi au 'off guard' kwa lugha zao

Kutangaza kuhamia, kisha kubadili ratiba ni dalili kuwa ''mkokoteni umewekwa mbele ya farasi'' (Cart in front of the hose)

Pengine kungekuwa na mjadala japo kidogo, ushirikishwaji wa taasisi na idara na upangaji wa mipango ya kuhamia ungekuwa katika ratiba inayoeleweka ukiwa na rasilimali

Hili linaleta hoja nyingine

SHERIA
Kwamba kuhamia Dodoma ni sera tu au ni sera yenye sheria? Tunauliza hivi kwasababu wakati wa kuomba rasilimali fedha, suala litatinga bungeni. Fungu linatokaje? Ni swali tu wajuzi watusaidie
 
JE, LILIKUWA NI SUALA LA HARAKA AU LILILOHITAJI MIPANGO?

Tunaendelea kupitia hoja za bandiko la kwanza

Kuhamia Dodoma limekuwa suala la haraka, hata hivyo linahitaji mipango ya muda mrefu

July 31 2016 tulisema, ni bora serikali kutoa muda kwa mashirika/taasis zinayohusiana na shughuli za jamii kutengeneza mazingira ya ' ugeni' kutopata mawaa wakti ukifika

Serikali ingeliagiza CDA kuhakikisha miundo mbinu inakamilika, makazi na huduma
Shirika la nyumba lisitishe miradi mingine ili kuongeza nguvu kwa CDA kwa lengo hilo

Mifuko ya jamii iombwe kushirikiana na mashirika kama CDA na NHC kutengeneza miundo mbinu na hasa suala la makazi na ofisi za umma

Ujenzi wa reli ya SGR upewe kipaumbele kuunga Dar es Salaama na Dodoma.
Hii ni kwasababu shughuli nyingi ikiwemo familia zitabaki Dar es Salaam kwa muda

Wizara zihamie kwa nafasi ili kutoa muda kwa Mji wa Dodoma kuji 'adjust' kwa utaratibu
Yote yanahitaji muda uliopangwai. Msingi wa hoja ni kuwa na ratiba na taratibu

UHARAKA

Uharaka una madhara makubwa kwa serikali na wananchi kwa ujumla wake

Tulinukuu gazeti lililokuwa na kichwa cha habari ' Urahisi kuhamia Dodoma'
Gazeti lilitoa takwimu za NBS zikionyesha nyumba katika baadhi ya maeneo ni za udongo

Gharama ni kati ya 15,000-20,000 za kupnga kwa kuchangia huduma kama vyoo
Kwingineko kama Area C na Uzunguni ni 300,000+

Athari za uharaka zipo katika maeneo mengi

1. Kuongezeka kwa gharama za kuendesha serikali. Dar itabaki kitovu cha biashara, kuna ofisi zitalazimika kuwa na ofisi ndogo ili kukidhi haja za kibiashara, kikazi n.k.

Kwa mfano, hatutegemei Wanadiplomasia kuhamia Dodoma ambako makazi ya waziri mkuu yamekuwa tatizo na nyumba zinazoelezwa ni hizo za udongo huko Mlimwa

Usafiri wa anga utabaki Dar es Salaam ukiakisi uwepo wa ofisi za kidilomasia, mashirika ya biashara, ofisi za umma zenye mahusiano na biashara kubwa n.k.

Serikali haiwezi kujitenga na 'network' hiyo.

2. Mji wa Dodoma utakabiliwa na ongezeko la ghafla la wakazi.
Huduma za afya, elimu, miundo mbinu n.k. zitaathirika. Haya yatachangia kuongezeka ghafla kwa gharama za maisha kwa wakazi wa Dodoma bila kutarajia

3. Wafanyakazi watakaohama wataathirika kisaikolojia.
Wengi wana makazi ya kudumua Dar ambayo ni sehemu ya maandalizi ya kustaafu.
Kuwahamisha katika mwendo wa haraka kama ilivyo kuna maanisha mambo mawili

a) Wachague kwenda na ongezeko la gharama za maisha kwa familia mbili, au kuacha familia wakiwajibika kwa familia hizo wakiwa Dodoma au kuacha kazi

b) Baadhi wapo hatua za mwisho za utumishi. Mstaafu mtarajiwa miaka 1, 2, 3, 4 ijayo anapoambiwa achague kwenda au kuacha kazi ni 'teso' la kisaikolojia bila sababu

Haya yanajibu swali, uharaka uliopo umezingatia hali halisi au ni kuhamia kwa haraka?

Inaendelea
 
JE ,DODOMA IPO TAYARI KWA 'UGENI'

Ipo dhana hafifu kuwa uwepo wa Bunge Dodoma na mikutano mikubwa ni ishara za utayari wa Dodoma kupokea ujio. Ipo dhana Dodoma ikiunganisha mikoa mingi ipo tayari kimiundo mbinu

Dhana hizi ni potofu kwa kuzingatia kuwa uwepo wa Wabunge na watumishi ni wa muda tu.

Wabunge na familia zao wanaishi nje ya Dodoma, kilichopo ni makazi au ofisi za muda

Hili linathibitika kwa ukweli kuwa makazi ya waziri mkuu hayajakamilika, kwa maana kuwa uwepo wake Dodoma ni kwa nyakati tu na hivyo anahitaji makazi ya kudumu

Wageni wanaofika Dodoma ni wa muda tu ambao huenda kwa shughuli maalum kwa muda maalum na hivyo hawawezi kueleza utayari wa mji kupokea wakazi wa kudumu.

Ongezeko la watu linatarajiwa kuwa kubwa zikiwemo familia za watumishi, familia za wafanya biashara na family za watu wengine wanaohusiana na mzunguko wa jamii.

Kwa muda mfupi Dodoma itakuwa na ongezeko la ghafla la wakazi

Hii maana yake, mji unatakiwa uwe na miundo mbinu ya kutosheleza ongezeko hilo

Idara ya maji imeonyesha wasi wasi wa ongezeko na upatikanaji wa maji
Hospitali ya mkoa nayo imeonyesha wasi wasi katika huduma zikiwem o za kuhifadhi wafu

Dodoma inahitaji mfumo wa majitaka(sewerage) ambao si kuwa unatakiwa kujengwa katika mabomba bali katika kupokea tofauti na Dar ambako sehemu kubwa huishia baharini

Miundo mbinu ya barabara , mashule itakuwa na msongamano mkubwa

Tukiuangalia Mji wa Dodoma, wasi wasi wa upatikanaji maji safi, usafirishaji maji taka na overcrowding katika huduma kama za shule na hospitali hizo ni precursor kwa maradhi ya milipuko

Kushindwa kwa ofisi ya waziri mkuu kuhamia sept mosi kama ilivyokuwa kunaeleza ukubwa wa tatizo na changamoto zake. Kwa bahati mbaya haionekani kama kuna 'organization' katika hili

Kusipokuwa na plan nzuri, kushirikisha wadau, kutoa vipaumbele na kupanga kwa pamoja, tutahamia Dodoma kwa kuzua matatizo makubwa mbele ya safari

Ili kufanikiwa katika uratibu wa shughuli ni lazima yawepo mamlaka ya kushughulikia.
Kwasasa hilo ni jukumu la CDA, kwa jinsi CDA ilivyofeli kwa miaka mingi hatutarajii mapya.

Kwa kuanzia ni kuifumua CDA, kuweka watu wenye uwezo na maono ya kukabiliana changamoto
 
SAFARI YA DODOMA NA 'TETEMEKO'

Dodoma ni eneo linalojulikana kuwa katika ukanda wa bonde la ufa

Kumekuwa na matukio ya tetemeko la ardhi mara kwa mara

Tunakumbuka tetemeko la kuahirisha bunge wakati wa Spika Msekwa

Hatujui ni lini au wakati gani, tunachojua eneo hilo lipo 'prone' kwa tetemeko

Ongezeko la watu halina uhusiano na tetemeko la ardhi

Hata hivyo,madhara ya tetemeko kwenye wengi ni tofauti na kwenye wachache

Je, miundo mbinu ya Dodoma imetengenzwa kukabiliana na hali kama hiyo?

Je, majengo yaliyopo na yajayo yapo katika hali ya tahadhari?

Tetemeko lililoikumba Kagera limetufundisha mengi

Kwanza, utayari kwa majanga ya asili ni mdogo sana kama upo

Pili, uwezo wetu unatia shaka

Juzi waziri mkuu alikutana na wafanyabaiashara na mabalozi kuchangia maafa

Kiasi kilichokusanywa na ahadi ni chini ya Bilioni 5 kwa taarifa za awali

Je, ipo haja ya michango ikishirikisha nchi, mashirika na wafanyabiashara?

Ikiwa ofisi ya bunge ilirudisha bilioni 6 serikali, tume ya uchaguzi bilion takribani 12, kulikuwa na sababu zipi za kutafuta michango kutoka kwingineko?

Hii ni kuonyesha tu kuwa tuna rasilimali zilizokolewa za kutosha ikiwemo watumishi hewa n.k. Kwanini hatukuwa tayari kabla na wakati wa tukio?

Hatumaanishi michango haikuwa mizuri, la hasa, hilo ni jukumu letu wananchi

Lakini madhara yanayohitaji uharaka yakisubiri michango ya wafanyabishara na mabalozi inatia shaka na kwa kiasi kinachosemwa kilichangwa inafikirisha

Hapa ndipo tujiulize tena, je, safari ya Dodoma ityakayohitaji rasilimali zaidi itakuwa katika hali tarajiwa au itakuwa bora twende?

Je, mji upo tayari ku handle majanga kama ya Kagera kwa kuangalia jiografia?

Tusemezane
 
KAULI YA WAZIRI MKUU

TANGAZO LILIVYOPOKELEWA NDIVYO SIVYO

Waziri mkuu(PM) ameeleza mpango wa serikali kuhamia Dodoma

Kwanza, ameeleza jambo moja muhimu 'kwamba miundo mbinu iliyopo Dodoma inatosheleza mahitaji ya serikali kwa kuhamia kwa awamu''

Kwa lugha hiyo PM anasema, haiwezekani kuhamia Dodoma kwa mkupuo.
Hili tumelijadili katika hapa tukisisitiza kuwa si suala la kuhamia tu bali utaratibu na miundo mbinu

PM akasema kuna master plan inayopitiwa ili kuifanya Dodoma ikidhi vigezo vya kimataifa

Kwa maneno hayo, master plan haikuwa imepitiwa kwanza kabla ya kutangaza kuhamia

Akasema zimeundwa kamati za kitaifa kama ile ya makatibu wakuu, na kwa kushirikiana na CDA na ofisi za mkoa kuratibu shughuli nzima

Kwa maneno mengine, kamati hazikuwepo kwanza, tangazo lilipotoka

PM- shughuli ya kuhamia itashirikisha sekta binafsi na jamii.
Hii ni pamoja na kuhakikisha Dodoma inakuwa na miundo mbinu kama bandari kavu, mahoteli mazuri na makazi ya kuishi

Hapa PM ameliona tatizo la makazi tuliloongea siku za nyuma.
Kwamba Dodoma haikuwa tayari kupokea wageni kwa miundo mbinu yake, na hilo lingeumiza sana wafanyakazi . Lingeongeza gharama za maisha kutokana na demand and supply n.k.

Kilichoshangaza ni ujenzi wa bandari kavu. Tunadhani haikuwa sahihi kusema 'ujenzi' wa bandari kavu. Dodoma ni mji wa serikali na si biashara, kwanini kuwepo na bandari kavu?

Hapa kunaonyesha kuwa wataalam bado wanatakiwa kushauri ili kuepuka maamuzi ya wanasiasa

HARAKA YA NINI?
Baada ya tangazo la Rais tuliona viongozi wakihaha na mikakati ya kuhamia Dodoma.
Ilikuwa vurugu , vikao , matamako n.k. bila chembe ya tathmini kutoka kwa viongozi

Zoezi la kwanza kushindwa ni ofisi ya PM kuhamia sept 1. Hili ndilo limeamsha viongozi 'wape up call' kuwa tatizo lipo mbeleni

Hakuna aliyejiuliza kama kweli tupo tayari, sababu zile za 1973 zipo na kama tuna rasilimali

HARAKA ZA TAASISI BILA TATHMINI. NI KATIKA KU 'IMPRESS'?

Mfano mzuri ni tume ya uchaguzi. Hii ilitangaza kutafuta eneo la kiwanja na kuanza ujenzi wa ofisi

Tume ya uchaguzi ni ofisi ndogo tu ambayo shughuli nyingi huratibiwa wilayani na mikoani

Inaweza kukodi jingo zuri na kuendesha shughuli zake

Muda utakavyosonga mbele ndipo inaweza kujenga makao yake ya kudumu

Huu ni mfano tu wa viongozi waliopokea tamko kwa kulitafisiri vibaya na bila kulifanyia tathimini

Kazi ya tume si kujenga majumba, inaweza kukodi ofisi kutoka taasisi za umma kama NHC, Mifuko ya umma n.k. ambazo zitajenga majengo kadri muda unavyosonga mbele

Haraka ya kutafuta viwanja kukiwa hakuna ratiba ilikuwa ya nini? Kwani ni lazima wajenge ofisi?

Wizara nyingi zinatumia majengo ya mashirika, je, NEC walifanya tathmini kati ya umiliki na kukodi majengo kipi ni bora? Ilifanyika tathmini?

Inaendelea
 
WAMEKWAMA DODOMA

WASITUITE WATABIRI AU WAPIGA RAMLI

Katika mabandiko ya uzi huu tumeeleza kwa kiasi tatizo la kuharakisha safari ya kuhamia Dodoma

Moja ya mabandiko tumeuliza , Je, Dodoma ipo tayari kwa ugeani?

Bandiko lingine tukahoji, haraka hizi za nini?

Na jingine tukasema taasisi kama tume iliyosema ina kiwanja, ilikuwa ku impress tu

Jana Bungeni, waziri amekiri wizara moja kutumia majengo ya UDOM kama ofisi

Hilo la kutumia UDOM si kubwa, bali ni dalili za kuonyesha ukubwa wa tatizo

Serikali inapokosa makazi, sijui makazi ya wafanyakazi yapo katika hali gani

Serikali inapokosa makazi, hali za huduma za jamii zipo katika hali gani

Safari ya Dodoma inahitaji maandalizi ya kitaalam na si ya kisiasa ya kufurahisha

Tumeeleza kuhamia Dodoma ni jambo jema, lakini wema wake utendwe kwa wema

Hakuna bajeti inayoonekana inayowezesha ofisi za umma zinazotengeneza makao ya nchi

Ingalikuwa busara serikali kupitia mapato kutenga fungu kukamilisha wizara moja kabla ya kuhamia nyingine. Hilo lingewezekana kwa kuanza na wizara ndogo

Pili, kungekuwa na kuhamasisha wawekezaji katika huduma na sekta ya ujenzi

Ingebidi,wangetoa incentive kwa wanaojenga Dodoma ili kuharakisha ukuaji wa mji

Kinachoendelea sasa hivi kinasikitisha.
Ni kama watu waliamka asubuhi na kupakia mizigo bila kujua wanakwenda wapi.

Haya ndiyo madhara ya kutanguliza siasa kisha utaalam na si kinyume chake

Tunayoona ni mwanzo tu, watumishi wajiandae kwa wakati mgumu zaidi mbele ya safari

Asijetokea awaye akadhani ni 'watabiri au wapiga ramli' kila kitu kipo wazi kwa wenye macho

Tusemezane
 
Je, tulikuwa na nafasi ya kutokurupuka? Je, tuna nafasi ya kusubiri/kujipanga kwa usahihi kabisa? Mangapi bado yapo kwenye mipango?
Nguvu yetu leo ni Kuthubutu, na katika hilo hatuwezi kukwepa gharama zake, tushikamane tufanye. HATUNA NAFASI YA KUJIPANGA KATIKA MENGI, NA KWA AJILI HIYO HATUNA HAKIKA YA MATOKEO YA MAAMUZI YETU, ILA KILE CHA THAMANI KWETU NI ILE DHATI MIOYONI MWETU. Hatuna nafasi ya Kutokurupuka!
Anaita sasa!
 
Je, tulikuwa na nafasi ya kutokurupuka? Je, tuna nafasi ya kusubiri/kujipanga kwa usahihi kabisa? Mangapi bado yapo kwenye mipango?
Nguvu yetu leo ni Kuthubutu, na katika hilo hatuwezi kukwepa gharama zake, tushikamane tufanye. HATUNA NAFASI YA KUJIPANGA KATIKA MENGI, NA KWA AJILI HIYO HATUNA HAKIKA YA MATOKEO YA MAAMUZI YETU, ILA KILE CHA THAMANI KWETU NI ILE DHATI MIOYONI MWETU. Hatuna nafasi ya Kutokurupuka!
Anaita sasa!
Kuthubutu maana yake si kuingia kichwa kichwa.

Kuthubutu ni kutenda kwa maarifa, weledi na mkakati.

Huwezi kuthubutu kuingia Pori lenye simba bila kujua idadi yao ni kiasi gani, wangapi ni madume wangapi ni majike. Wanajificha wapi na kwa wakati gani.

Kuna silaha za kutosha kukabiliana nao! Plan B kama plan A itashindwa ni ipi, terrain ipoje, wakati gani mzuri wa kuingia pori, kuna wanyama gani wengine hatari.

Ni kipi kinaweza kuwavutia simba kutoka walipo n.k.

Ukishajibu hayo, ndipo unakuwa na uthubutu.

Je, tuna muda wa kusubiri ? Jibu ni hapana, lakini kama tumesubiri miaka 40 hatuwezi kushindwa kujipanga kwa miezi 12

Kukurupuka ni kufanya mambo bila mpangilio.

Hatuwezi kuhama kwasababu tunataka kuhama.
Tunaweza kuhana kwasababu tuna sababu za kuhama na tumejipanga kuhama.

Kwa hili la Dodoma, mambo yaliongozwa kisiasa badala ya kitaalamu
Kulikuwa na nafasi ya kuhama kwa mpangilio na si kukurupuka

Kuhama na kufikia chini ya mwembe ukijinasibu umehama,ni ''unajisi'' wa akili

Kuinajisi akili kwa maana ya kushindwa kutambua hata vitabu vyote vitakapokuwa wazi

Tulisema mapema tukaonekana porojo, muda ni mtetezi wetu mzuri na yanatokea

Tusemezane
 
Kuthubutu maana yake si kuingia kichwa kichwa.

Kuthubutu ni kutenda kwa maarifa, weledi na mkakati.

Huwezi kuthubutu kuingia Pori lenye simba bila kujua idadi yao ni kiasi gani, wangapi ni madume wangapi ni majike. Wanajificha wapi na kwa wakati gani.

Kuna silaha za kutosha kukabiliana nao! Plan B kama plan A itashindwa ni ipi, terrain ipoje, wakati gani mzuri wa kuingia pori, kuna wanyama gani wengine hatari.

Ni kipi kinaweza kuwavutia simba kutoka walipo n.k.

Ukishajibu hayo, ndipo unakuwa na uthubutu.

Je, tuna muda wa kusubiri ? Jibu ni hapana, lakini kama tumesubiri miaka 40 hatuwezi kushindwa kujipanga kwa miezi 12

Kukurupuka ni kufanya mambo bila mpangilio.

Hatuwezi kuhama kwasababu tunataka kuhama.
Tunaweza kuhana kwasababu tuna sababu za kuhama na tumejipanga kuhama.

Kwa hili la Dodoma, mambo yaliongozwa kisiasa badala ya kitaalamu
Kulikuwa na nafasi ya kuhama kwa mpangilio na si kukurupuka

Kuhama na kufikia chini ya mwembe ukijinasibu umehama,ni ''unajisi'' wa akili

Kuinajisi akili kwa maana ya kushindwa kutambua hata vitabu vyote vitakapokuwa wazi

Tulisema mapema tukaonekana porojo, muda ni mtetezi wetu mzuri na yanatokea

Tusemezane
Unenayo ni sahihi kabisa, na ndivyo ilivyopaswa kuwa. Lakini pia ni vyema kujiuliza, kama 40 yrs ilishindwa kutupatia mpango, aje miezi 12 na sisi walewale? JE TUNA NAFASI YA KUTOKURUPUKA? Ni lini tulijipanga kutokurupuka leo? Hatujawahi. NI LAZIMA TUPANGE LEO ILI TUSIKURUPUKE NA KESHO. Leo kilicho cha thamani kabisa na mtaji pekee tulionao ni DHATI katika maamuzi yetu, ni wazi hatuna hakika ya matokeo yake kesho, yaweza kuwa shimoni, lakini ni wazi hatuna nafasi hiyo.
Jiulize pia ni lini ulimuundaa yule aliyekuwa katika nafasi ya maamuzi? Kama kilichomfikisha alipo ni jitihada zake binafsi, wewe utamfunga na nini? Hapo ndipo tunapobaki na tumaini moja tu, DHATI YAKE YULE KATIKA MAAMUZI, NA HAKIKA NDIO MTAJI PEKEE KWA SASA HIVI. KUTHUBUTU NI KUTENDA hata pasi na mpangilio, ni kutenda tu. Tumaini pekee kwetu kwa waendao Dodoma ni kwamba hawatarudi Dar, wanaishije, shida wapatazo, ni gharama ya uzembe wako na wangu, hatuwezi kukwepa, labda tusubiri miaka 40 mingine... walau tumethubutu.
Anaita sasa.
 
JingalaFalsafa, post: 19618571, member: 81123"]Unenayo ni sahihi kabisa, na ndivyo ilivyopaswa kuwa. Lakini pia ni vyema kujiuliza, kama 40 yrs ilishindwa kutupatia mpango, aje miezi 12 na sisi walewale?
Nipo katika rekodi nikisema kuhamia si jambo baya in fact it's long coming.
Uthubutu wa kuhamia ndicho kilichotakiwa
Uthubutu si kuamka na kusema tunakwenda.
Ni dhamira ya kwamba sasa tunakwenda

Swali muhimu baada ya kuthibitisha uthubutu ni , je, tunakwenda kwa mpango na utaratibu gani? Nani atusaidie katika kuandaa mpango mzima na utekelezaji wake?
Hapa ndipo tatizo lililpoanzia
JE TUNA NAFASI YA KUTOKURUPUKA? Ni lini tulijipanga kutokurupuka leo? Hatujawahi. NI LAZIMA TUPANGE LEO ILI TUSIKURUPUKE NA KESHO. Leo kilicho cha thamani kabisa na mtaji pekee tulionao ni DHATI katika maamuzi yetu, ni wazi hatuna hakika ya matokeo yake kesho, yaweza kuwa shimoni, lakini ni wazi hatuna nafasi hiyo
Dhati tunayo lakini je,is that the right way to do the right thing?

Kwenda shimoni kwasababu tu tunataka uthubutu ni kutenda kwa njia mbaya
Nafasi ya kufanya vizuri tunayo, tulichokosa ni watu wa kutuongoza kufanya vema
Jiulize pia ni lini ulimuundaa yule aliyekuwa katika nafasi ya maamuzi? Kama kilichomfikisha alipo ni jitihada zake binafsi, wewe utamfunga na nini? Hapo ndipo tunapobaki na tumaini moja tu, DHATI YAKE YULE KATIKA MAAMUZI, NA HAKIKA NDIO MTAJI PEKEE KWA SASA HIVI. KUTHUBUTU NI KUTENDA hata pasi na mpangilio, ni kutenda tu.
Kuishi kwa dhati ya mtu na si watu nalo ni tatizo.

Sikubaliani kuwa kuthubutu ni kutenda tu.
Unaingia katika pori kwa kutenda bila kujali dhahma ndani ya msitu.

Ni ili watu wabaki katika majamvi wakiomboleza, alithubutu.

Hapana tuna fursa hatuitumii vema. Tuna kila kila hatujui kupanga.

Tumebaki kuwa kiosk na siyo super market. Tunachukua dakika 45 kutafuta chupa ya maziwa ndani ya kiosk, hatujui kuwa kule mall na super market unaiona kwa dakika moja.

Super market walithubutu kuwekeza, uthubutu uliongozwa na weledi na
maarifa
Tumaini pekee kwetu kwa waendao Dodoma ni kwamba hawatarudi Dar, wanaishije, shida wapatazo, ni gharama ya uzembe wako na wangu, hatuwezi kukwepa, labda tusubiri miaka 40 mingine... walau tumethubutu.Anaita sasa
Tumeridhia askari wakafie vitani kwasababu huko ndiko makazi yao yalipo.

Hatuna sayansi ya kisasa kuwa kushinda vita si kupiga mabomu ni kuhakikisha askari waliokwenda wanabaki salama ili wajao wakute makazi yenye furaha.

Tunajivuna askari hawarudi, hatuangalii gharama itokanayo.

Tumeshindwa kupanga, tunawezaje kuthubutu?

Tusemezane
 
Dhamira pasipo matendo hata kama utakuwa una mpangilio sahihi bado hujathubutu. Lakini kutenda hata pasi na mpangilio ni KUTHUBUTU. Tunasema kuwa ni kwa mara ya kwanza TUMETHUBUTU KUANZA SAFARI YA DODOMA, hata kama hatuna mpango mzuri. Tulichonacho mkononi ni ule Uthubutu unaodhihirisha Dhati ya mtu.
Lakini ni ukweli kuwa, tumethubutu pasi na hesabu, ndio maana hatuna hakika ya matokeo ya uthubutu wetu.

Nafikiri nafasi ya kufanya vizuri haiwezi kuwepo nje ya watu wazuri wa kutuongoza, ndio maana niliuliza Je, tuna nafasi ya kutokurupuka? Je, tuliandaa nini jana yetu ili tusiwe wakurupukaji leo? Kama hakuna, basi kuweza tu kuthubutu kuanza safari ni ushindi kwetu, na hasara zao la uthubutu huo usio na mpangilio i juu yetu kwa kushindwa kuandaa hii leo yetu.
Tuna nafasi ya kutokurupuka kesho, lakini si leo. Ndio maana nikasema Tumaini pekee kwetu la maamuzi ya namna hii ni ile Dhati, inayodhihirishwa na Uthubutu tuuonao leo. Na itabaki kuwa dhati ya mtu binafsi mpaka pale tutakapoamua kuandaa dhati ya umma kushika hatamu... Walau tunaona kuthubutu. Kama hukuandaa jeshi lako kwa vita na vikatokea, ni heri kupeleka wanajeshi haohao wazembe kuliko kumpisha adui chumbani.
Anaita sasa.
 
JingalaFalsafa

Kuna nadharia mbili zinazotutofautisha hapa

Kuhamia Dodoma tunakubaliana sote. Hiyo ndiyo dhamira

Tunakwendaje, hili tunatofautiana

Niliposema miezi 12 sikumaanisha ya 'idle'. Nilimaanisha kuhama kwa utaratibu
Ni upi huo?

Kwanza, kufanya assessment nani atangulie kwa mazingira yaliyopo Dodoma

Pili, kufanya stress test baada ya kuhamia kwa awamu kubaini mapungufu

Stress test inahusisha miundo mbinu, social services, accessibility of services n.k.

Halafu adjustment inafanyika wakati maandalizi ya awamu nyingine yakiendelea

Hiyo ni sehemu ya planning ambayo haikufanyika

Uthubutu uliofanyika ni kupakiza mizigo katika magari ya jeshi na kutua UDOM

Ni uthubutu kwasababu wameondoka, si uthubutu wenye weledi kwasababu hakuna plan

Ni kituko kuweka mkokoteni mbele ya farasi.
Imeundwa tume ya kutembelea majiji mengine ili kuona upangaji.

Tume imeundwa baada ya wizara kuhamia UDOM

Kipi kilipaswa kutangulia? Farasi halafu mkoteni au kinyume chake?

Hili tu lianonyesha uthubutu butu hata kama ni uthubutu.

Tusemeza
 
Mkuu, nafikiri hicho ndicho nilichokuwa nakisisitiza kwa kila post humu.

TUMETHUBUTU KUANZA SAFARI YA KUHAMIA DODOMA, LAKINI KWA VILE TUMEKURUPUKA, HATUNA HAKIKA NA MATOKEO YAKE, ILA TU KILE KITUPACHO TUMAINI NI DHATI INAYODHIHIRISHWA NA UTHUBUTU KATIKA HILI.

Imekuwa sawa na bahati nasibu, ni kwa vile hatujafafanya hesabu, na itatugharimu vikubwa na hatuna nafasi ya kukwepa gharama hiyo, kwani jana yetu haikuaandaa leo yetu kutokurupuka. Ndio maana Hatuna Nafasi ya Kutokurupuka, na ni heri kwa maana tunaloweza kupanga vizuri kwa sasa ni ubatili tu.

Ni heri kuthubutu kufanya yale yaliyoonekana kuwa ni mema, hata kwa kukurupuka, kuliko kuvuta subira usiyoihangaikia na kukomaza ubatili.

Anaita sasa.
 
INAWEZAKANAJE NA INASHINDIKANAJE?

KWANINI UDSM IWEZEKANE, MAKAO MAKUU ISHINDIKANE

Katika mjadala huu tumetofautiana na ndugu JingalaFalsafa kuhusu kuhamia Dodoma kwa hoja
Sote tunakubaliana kuwa kuhamia ni jambo muafaka, tunatofautiana kwa namna gani tunahamia

Msimamo wetu wengine ni kuwa lazima kuwe na mipango madhubuti na si ya zimamoto
Kuhamisha makao ya nchi si sawa na kuhamisha makazi ya mtu.

Tumeona tafrani ya waliohama kufikia katika Hosteli za chuo kikuu cha Dodoma
Kuhama huko haiyumkini kumeleta athari kwa namna fulani katika eneo la kitaluma

Tumeshuhudia uzinduzi wa hosteli mpya za wanafunzi pale chuo kikuu cha Dar es Salaam
Inakadiriwa gharama zilizotumika ni Bilioni 10 katika kujenga flat 20. Hili ni jambo jema na la kheri

Flat moja ina ukubwa zaidi ya jengo la Wizara ya afya au wizara nyingine kwa mifano michache
Kama Bilioni 10 ziliweza kujenga flat 20 na serikali ina wizara takribani 16, kuna maswali yanajtokeza

Ni kwanini basi zisitengwe bilioni 10 nyingine kujenga flat 20 pale Dodoma kwa ajili ya wizara?

Katika hotuba yake ya kwanza kwa mhimili wa sheria, Mh Rais alisema zipo takribani trilioni moja ambazo kesi zake zikimalizwa atawapa idara ya mahakama bilioni takribani 200

Makusanyo ya mwezi tunaambiwa ni katika Trilioni.

Na wala si mara moja Mh Rais ameidhinisha pesa katika kiasi cha bilioni 10 au zaidi kwa miradi

Ni kwa vipi basi bilioni 10 ambazo hata kwa dharura zinaweza kuidhinishwa na bunge zisiombwe na kupewa wakala wa majengo kujenga flat 20 Dodoma kama wizara?

Kama kweli Bilioni 10 zimejenga flat za UDSM nini kinakwaza Bilioni 10 zingine kujenga makao makuu japo kwa kuanzia ili kuepusha wizara kufanya kazi katika hosteli za chuo?

Tusemezane
 
Mkuu unachosema si kwamba hakiwezekani, uwezo uko wazi kabisa, tatizo ni bado Hatuna nafasi ya Kupanga.

Chukulia mfano wa hizo Hosteli, hazikujengwa kwa kufuata Mpango fulani, ni Uthubutu tu wa serikali uliofanikisha, SISEMI KWAMBA SERIKALI INAPASWA KUFANYA KAZI KWA MTINDO HUO WA KUKURUPUKIA TU MAMBO, ila kwa wakati huu binafsi NINABARIKI MAAMUZI AINA HII. Hasa yanapoonesha nia njema.

Siamini kama kuna Wizara itafikia Chini ya Miti huko Dodoma, ni wazi kuwa zote zilizoenda zimepata mahali pa kufikia. Hoja, ni kwa gharama ipi? Athari zipi? Tusizikimbie, tumezitengeneza wenyewe.

Kwangu mimi kwa sababu ya Uzembe wetu wa kushindwa kupanga na kutekeleza mambo mengi hapo nyuma, hasa katika hili, hakuna option ya kusubiri. Yeyote aliyefungasha tayari, aende Dodoma. TUNAPASWA KUJIULIZA TU NI KWA NAMNA GANI TUTAPUNGUZA ATHARI ZA KWENDA KWETU DODOMA BILA KUJIPANGA, sio Kusubiri.

Bahati nzuri Udom ina miundombinu mizuri, sijajua ni wapi na kwa namna gani wizara zetu zimekuwa alocated, ila naamini kabisa, Udom ina uwezo wa ku-accomodate wizara zilizoenda pasipo kuathiri taaluma chuoni. Inawezekana kabisa.

Matumizi ya Bil. 10 nyingine kwa ajili ya majengo ya wizara si ya dharura kubwa hivyo, japo INAWEZEKANA. Ni suala la Vipaumbele na Udharura wa jambo. Ndio maana nilisema ninaamini atakayeenda hatarudi Dar, na mwishowe ata-settle Dodoma. Maisha yatasonga.

HATUNA NAFASI YA KUKWEPA GHARAMA KUBWA.

Anaita sasa.
 
Back
Top Bottom