Duru za siasa - Mgongano wa mawazo

Watu wa Magharibi wana sera isiyotangazwa inaitwa FACTS ON THE GROUND. Watakudunda au kukupora rasilimali ili mnegotiate kwa maslahi yao mfano mafuta ya Libya na kuwepo na taifa la Israel nchini Palestina.
"Mapanya" wa Libya wamedhibiti sehemu kubwa ya nchi lakini tusubiri kama wataweza kuiongoza Libya kama nchi huru ya Walibya na yenye maslahi kwa walibya.

Katika mstakabali wo wote endelevu ebu jiulize maswali machache.
1 Lengo (la muda mfupi, wa kati na mrefu) ni nini?
2. Mkakati wake unatekelezeka?
3. Kuna rasilimali za kutekeleza mkakati huo?
4. Mfumo wa tathmini upo katika kila hatua?
5. Madhara na changamoto zinatatulika?nani?
6. Manufaa (ya muda mfupi, wa kati na mrefu) yanatambulika na yanamnufaisha nani?

Naamini kwa tukio la NTC huko Libya ni sawa na kuingia kwenye awamu mpya ya ukoloni mambo leo. Kwa kwetu hilo pia ni lakujifunza lakini nani ajifunze nini ndiyo issue.
Watawala hawakubali ya NTC Libya kwa sababu walinufaika na Gadafi, halafu athari za mabadiriko kwao ni suicide (angalia ya Igunga)
Nikushukuru kwa maoni yako. Ni kweli kuwa gharama za ushiriki wa Gadafi katika vita ya Kagera umetugharimu.

Sisi kama taifa hatukuwa na chaguo na wala hatukuwa na tatizo na Libya. Tutakumbuka kuwa kwa mara ya kwanza Idd Amin aliishambulia Tanzania mwaka 1973 kwa ndege kule Mwanza na busara za Mzee Haile Selasi (RIP) na Mwalimu Nyerere(RIP) ziliepusha balaa hilo. Amin akadhani Tanzania ni wadhaifu hadi alipoamua kuchukua kipande cha Ardhi.

Mbinu aliyotumia Idd Amin ni kutangaza kuwa kulikuwa na njama za kuuhujumu Uislam jambo ambalo Wazanzibar wengi wanadhani ni kweli katika kujenga hoja za chuki dhidi ya muungano. Ni hapo ndipo alimuomba msaada na Gadaffi kukubali hilo kwa misingi ya utetezi wa kidini.
Hizi zikawa ni dalili za mwanzo za ubabe wake aliouendeleza hadi kufikia kipigo cha Rais Reagan.

Gadafi akachukua mwelekeo mpya pale alipokosana na wenzake katika Arab League, hili lilitokea kwa sababu ya msimamo wake juu ya Palestina akiamini kuwa umoja huo umekuwa mamluki na kuwatelekeza Wapalestina. Inaweza kuwa alikuwa na hoja ya msingi na maana zaidi tukiangalia Arab league inavyofanya kazi kama mhuri wa nchi za Magahribi.

Libya ikahamishia nguvu zake AU na alisaidia sana katika makundi ya uasi na ukombozi. Ndiyo maana ANC wamechukizwa sana na kitendo cha NATO. Hata pale ilipokuwa katika vikwazo vya uchumi Mandela alithubutu kwenda kwa Gaddafi kumshukuru kwa misaada akiwaambia nchi za magharibi kuwa wakati wa dhiki Libya ilikuwa nao na hawakubali kuchaguliwa Rafiki.

Wakati AU ikipita katika kipindi kigumu sana kiuchumi na kisiasa Gadaffi alitumia rasilimali zake kuendesha umoja huo. Ikafikia mahali akataka awe mwenyekiti licha ya historia yake yenye utata. AU hawakuwa na chaguo ila kukubaliana na mfadhili wao.
Gadaffi akataka umoja wa Africa U.S.A akitaraji kuwa rais ndoto ambayo haikutimia na ilijengwa katika ubabe tu.

Licha ya kwamba alifanya mambo mchanganyiko mazuri na mabaya, huko nyumbani hali haikuwa shwari.
Kile alichokipigania kuondoa ufalme ndicho alichokirejesha ingawa si rasmi ni kwa mgongo wa demokrasia ambayo haikuwepo bali serikali ya familia.
Libya ikawa haina taasisi za kisiasa (alternative political institutions) kama ilivyokuwa kwa Misri n.k.
Mfumo wa demokrasia ukabaki kwenye majukwaa na karatasi ukweli ukiwa ni mfumo wa kifalme.

Ni kutokana na kukosekana mbadala wa kisiasa, yalipotokea maasi Libya ikabaki kuwa kama taifa lililopata uhuru leo.
Lengo la kwanza la 'mapanya' lilikuwa kumuondoa Gaddhafi kwani hiyo ndio ilikuwa kazi kubwa kuliko nyingine.
Maasi hayakuanza kwa watu wa kaliba ya juu bali wananchi wa kawaida bila kuwa na mkakati wa muda mfupi, wa kati au mrefu lengo likiwa kumuondoa kwanza.

Tutakumbuka walivyokuwa wanapigana bila mpangilio wakisaidiwa na ari hadi NATO ilipowasaidia. Inaweza kuwa kulikuwa na mkakati wa NATO, ukweli wa mageuzi ya Arab spring hatuwezi kuupuza hata kidogo. Hata wa Israel wanajua impact ya Arab spring kwa mustakabali wao ndiyo maana Mahamoud Abas wa Palestina amekuwa na 'guts' hadi kupelekaea Israel kunywea katika baadhi ya misimamo.

Ni ukweli ya kuwa kuna changamoto nyingi sana zilizopo mbele ya Libya. Tunachokiona sasa ni post war honeymoon.
Moja ya changamoto ni kujenga taasisi za kisiasa zitakazoleta utengamano jambo ambalo si rahisi kama inavyodhaniwa.
Ukweli unabaki kuwa yatakuwepo mapambano ya ndani 'power struggle' kati ya waliojitoa mhanga na kundi lililofaidika na Gadhafi.

Malengo ya muda mfupi moja lilikuwa kumuondoa Ghadafi, ya muda wa kati ni kujenga taasisi za kisiasa na muda mrefu ni kuwa na taifa moja huru.
Haya hayataweza kupatikana katika sahani ya fedha ' silver plate' yatakuja na gharama kubwa na hilo lazima wajiandae nalo.

Je wana rasilimali za kufanya hivyo? jibu ni ndiyo kuanzia rasilimali watu hadi fedha, ingawa watalazimika kulipia gharama za vita hasa tukizingatia kuwa Libya ina mafuta safi dunia na kwa wingi kwahiyo macho ya wakubwa hayataondoka hapo leo au kesho.
Sijui investment ya elimu aliyoifanya Gaddhafi itawezaje kusaidia katika mikakati kwani ni dhahiri kuwa wasomi hasa wa nchi za kiafrika hawaaminiki hata kidogo. Nchi kama yetu inamalizwa na wasomi sio wafugaji au wakulima. Je wasomi wa Libya ni 'half baked' kama wetu, linabaki kuwa swali gumu.

Mfumo wa kutahmini changamoto na maendeleo utategemea uimara wa serikali nayo ni changamoto kubwa sana.
Changamoto zinatatulika ingawa itachukua muda mrefu kutokana na kutokuwa na mbadala wa kisiasa ulioachwa na Gadhafi kama tunavyoona Misiri pia. Libya ina uwezo kinachotakiwa ni utashi wa kisiasa.

Manufaa hayataweza kutambulika katika kipindi kifupi, muhimu ni pale nchi itakapokuwa imejenga mfumo thabiti wa kujitawala kwa vizazi vijavyo.
Tunao mfano wa Rwanda iliyokuwa majivu 'reduced to ash' na sasa tunaiona inachanja mbuga. Haya hayakutokea katika muongo mmoja bali miwili na bado ina safari ndefu.

Tatizo ninaloliona ni siasa za nchi za kiarabu zisizo tabirika na zinazotawaliwa na hisia kali.
Hatuwezi kukataa uwepo wa ukoloni mambo leo kwa ajili ya rasilimali, nakuhakikishia kuwa nchi za kiarabu zina 'compicated political sphere' na hivyo hakuna gurantee.

Tunaona jini lililokuwa kwenye chupa Misri linavyoumiza vichwa vya nchi za magharibi. Usijeshangaa ukisikia Islamic brotherhood wanaongoza nchi kama Hamas walivyowashangaza katika uchaguzi huru na wa haki pale Palestina na si dhani Libya inaweza kuwa tofauti sana, tatizo ni kuwa hatujui mbadala ni upi kule Libya.

Bado naamini Libya ina somo zuri sana ukilinganisha na yaliyotokea Arab spring. Tunaona maana halisi ya uhuru na si kuwa na kila kitu, tunajifunza kuwa nguvu ya utawala haipo jeshini bali ndani ya umma, tunajifunza ni kwanini tunatakiwa tuwe na taasisi za kisiasa mbadala, tunaona jinsi rasilimali zinavyokodolewa macho, na kikubwa zaidi ni kuwa utu wa mtu si chakula na malazi tu ni pamoja na ushiriki wake katika kuamua mustakabali wa taifa lake.
 
Ogah;2546956]Nawaomba pia mzungumzie ni namna gani SUALA LA WAGOMBEA BINAFSI litakavyowezesha wananchi kuamua walitakalo............kwa sababu sehemu ya mazungumzo/maandishi yenu mmegusia mabadiliko ya vyama kwenye nchi zingine Vs matarajio ya wananchi (e.g in Kenya).......nafikiri kuna mambo ambayo tunaweza kushawishi wananchi wakayafanya bila kusubiri overhaul ya katiba au mabadiliko ya chama na kuchukua nchi na hatimaye kushika hatamu (risk)!!
Ahsante Ogah kwa kuchokoza mada muhimu kama hii.

Nikumbushe kuwa mfumo thabiti wa demokrasia hauna shaka na mabadiliko yoyote yale,na ikitokea mahali kuna wasi wasi basi mfumo wa demokrasia una matatizo fulani. Hakuna demokrasi iliyo kamili 100% lakini zipo zilizovuka viwango vya ufaulu.

Uingereza na mfumo wao wa kifalme mwaka jana waliweza kukaa zaidi ya wiki mbili bila serikali na hakukuwa na tatizo.
India iliwahi kukaa mwezi na nusu bila kiongozi na nchi iliendelea bila matatizo. Haya yalitokea baada ya chaguzi zilizoshindwa kutoa mshindi wa moja kwa moja, na wakati huo majadiliano yalikuwa yakiendelea.

Japan katika miaka 5 wamekuwa na mawaziri wakuu 5 kwa wastani wa miezi 9 kila mmoja bila nchi kuyumba au kutetereka.
Nchi ya brazili inaweza kufanya chaguzi za kumweka kiongozi na serikalli katika siku moja licha ya kuwa na watu zaidi ya milioni 203 kwa makadirio ya july 2011.

Mfumo wetu wa siasa ni wa kichotara na hakika ni vigumu kuufungamanisha na pande moja. Hilo si jambo baya, ubaya ni pale tunapofanya mambo vibaya kwa kisingizio cha mifumo mingine duniani kana kwamba inafanan na yetu.
Tunasema ni mfumo wa west minster ya Uingereza. Tofauti ni kuwa Waziri mkuu ndiye mtendaji wa serikali wakati kwetu ni kiongozi wa serikali bungeni na nguvu yake kiutendaji inawajibika kwa mkuu wa nchi.

Waziri mkuu wa UK anapatikana kutokana na viti ndani ya bunge mfumo ambao kwetu mkuu wa nchi anapatikana kwa kura.
Rais wetu anachaguliwa moja kwa moja na wananchi kama kwa wabunge.

Uchaguzi wa Rais unafanana na wa Marekani kidogo sana ingawa marekani rais anapatikana kwa kura za majimbo (electorate college) na idadi kutokana na kura inaitwa popular vote ambayo si muhimu kuamua nani awe rais.Tunapofanana ni kuwa marais wote ni wakuu wa nchi
Vivyo hivyo ukiangalia mataifa mengine utaona tunaingiliana kwa baadhi ya mambo mfano South Africa, Inida n.k. kwa namna fulani
Ni kwa mantiki hiyo ndiyo maana nimeuita chotara, na hata uchotara wake haujulikani ni wa mchanganyiko wa nini!!!

Tatizo letu ni kuwa wananchi wana nguvu ya kumchagua kiongozi na baada ya hapo hawana nguvu ya kumuondoa.
Anakua mali ya chama na anawajibika kwa chama na ni chama kinaweza kutengua uchaguzi wake. Tumeyaona haya CCM na hivi karibuni Chadema. Utaratibu wa kumuondoa kiongozi kama mbunge au rais una mlolongo wa kuchanganya na labda niseme ni 'impossible' kwa mfumo wa sasa.Chama gani kinaweza kuondoa rais ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho? Mbunge ambaye anawajibika kwa chama? na Wabunge watakaaje kuamua hukumu dhidi ya boss wao kabla hajawashukia?

Ni kwasababu hizo ndiyo maana suala la mgombea binafsi linaonekana kuwa gumu kukubalika. Mathalani utakapokuwa na wabunge wanaoweza kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali inawezekana rais akapoteza kibarua. Unapokuwa na wabunge wanaoweza kukwamisha miswaada au kuleta hoja za kuisulubu serikali, hapo serikali itakuwa matatani.

Kutokana na hofu hiyo, serikali zisizojali maslahi ya wananchi kama zetu ni rahisi kuizuia hoja yenye kutishia maslahi yao.
Lakini kuna hofu pia kama rais akitoka kwa mgombea binafsi itakuwaje, hofu inayojengwa na hoja yangu ya awali kuwa mfumo wetu si imara kama ilivyo India au UK. Na wala hofu hii si kubwa zaidi ya hofu ya masilahi binafsi

Mgombea binafsi ni haki yetu kama ilivyoainishwa katika katiba(haki ya kugombea na kuchagua). Bahati mbaya mfumo wetu kikatiba umejengwa kiasi kwamba mizunguko yote itarudi pal pale kuwa ni suala la kikatiba na lishughulikiwe kwa taratibu za nchi zinazoongozwa na wale wale wasioutaka mfumo huo, vingenevyo ni kuvunja sheria. Kioja!

Tulifanya makosa makubwa pale mahakama ilipoamua na sisi tukasita kushinikiza uwepo wa mgombea binafsi. Ni wakiati ule wapinzani wakiongozwa na CUF walijikita kumtafutia maalimu ulaji badala ya kuongoza taifa katika mambo ya kitaifa.

Serikali ikatumia mwanya huo kuzuia amri ya mahakama kisheria kwa kupeleleka suala mahakama za juu, mahakama ambazo licha ya kuaminishwa ni huru si huru kwa maana ya huru. Wakuu wake wanawajibika ikulu wanakoteuliwa ndio maana suala hili linapigwa dana dana za kisheria kana kwamba linahitaji DNA na rocket science. Kama serikali haikuweza kutetea hoja zake mahakama ingetoa hukumu au kushinikiza hoja kuletwa.sivyo!

Tatizo si mgombea binasi tu bali mfumo mzima wa kiutawala na kisheria. Kama bado tunaamini kuwa kuna mihimili mitatu huru ya nchi ni kujidanganya. Leo tumenyanganywa haki yetu na tumbili na sasa tunasubiri nyani atoe hukumu!! sasa nyani amekalia mafaili twende wapi?

Kwa sasa hivi uhalali wa kudai mgombea binafsi upo kihalali lakini unakosa nguvu ya uhalali kwa hoja ya katiba inayopigwa dana dana ili kuleta 'suprise'. Kwa vyovyote vile hoja itajibiwa kuwa suala hilo ni la kikatiba na kwa vile katiba ipo mbioni kuandikwa upya basi lijadiliwe humo.

Ukweli ni kuwa CCM hawataki suala hili kwasababu ndani ya chama kuna uasi 'rebellion' na kuliruhusu ni kukimaliza chama kwasababu uwezekano wa kuwa na wabunge binafsi na wa upinzani kuunda bunge ni mkubwa sana. Kwa hali ilivyo ndani ya chama robo ya wabunge wake wanaweza kusimama wenyewe na kushinda, hilo litakimaliza chama kabisa.

Kama wananchi wanadhani hoja nzito kama hizi zitaachiwa kuongozwa na CCM kimabadiliko ni ndoto ya mchana. Swali ni kuwa baada ya ku miss first opportunity ya mahakama wapi tutasimamia kudai tena bila hoja zetu kuvunjwa vunjwa na ujio wa katiba!
Je, mbona hatusikii wapinzani wakilivalia njuga hili jambo, inaweza kuwa ni woga ule ule wa CCM mambo yakiwanyookea au tusemeje!

Kwa sasa ambapo mstakabali wa taifa unategemea uzalendo zaidi, mgombea binafsi ni muhimu sana. Tutafiakje huko?

Tujadili.
 
IGUNGA- USHINDI WENYE MASWALI/MASHAKA

Uchaguzi wa Igunga umekwisha kwa CCM kutangazwa washindi wa kiti. Ni moja kati ya chaguzi zilizokuwa na msisimko sana nchini kwa siku za karibuni.

Msisimko ulitokana na uchaguzi kuchukua sura ya kipima joto kwa chama tawala na upinzani. Igunga ni jimbo mali ya CCM kama ilivyo mikoa ya Tabora, Tanga, Mtwara, Ruvuma, Lindi, Morogoro ambayo haijawahi kuchagua mpinzani. Igunga imekuwa chini ya RA kwa miaka zaidi ya 10 ikisemekana kuwa mbunge wake RA alisaidia sana maendeleo. Hilo ni swali kwa wana Igunga na majibu wanayo.

Kilicholeta msisimko zaidi ni pale mwenyekiti wa CUF akitokea mkoa huo, wapiganaji kama Sitta nao wakitokea huko na ikiamika kuwa CCM na CUF walikuwa na makali 'edge' ya ushindi huku Chadema wakiwa underdog. Maswali yalikuwa, je, baada ya ndoa ya CCM/CUF nini kingetokea katika kampeni ili hali wana ushirikiano wa kisiasa!

Msisimko mwingine ulihusisha mazingira ya kujiuzulu kwa RA ambaye inasemekana kwa kupitia kijana wake ndani ya UVCCM ambaye pia ni mwajiriwa walionekana kuchukizwa sana na tuhuma za akina Nape na Mkama. Watu walitaka kuona kama kuvua magamba kulikuwa serious au ni danganya toto ya kila siku.

Ingawa ni mapema sana kuongealea hali halisi ya uchaguzi bado tunaweza kudodosa mambo mawili matatu.
Kwanza ni dhahiri kabisa kuwa uchaguzi haukuwa baina ya vyama vya siasa bali vyama vya siasa na serikali ikisaidiwa na viongozi wa ofisi za umma, tume ya uchaguzi na msajili wa vyama.

Huko nyuma, CUF walipotoa kauli ya jino kwa jino tuliona msajili wa vyama aking'aka na kutoa mapovu kuwa chama kitafutiwa usajili kwa kauli za kuhatatrisha amani. Kumbuka kwa kauli tu. Aden Rage akapanda jukwaani Igunga akiwa na silaha kiunoni, ikachukua siku 3 msajaili kwa aibu na haya kutoa kauli ya kulaani vurugu kwa ujumla na si Rage.

Kuna malalmiko ya masanduku kupelekwa kabla, tume ya uchaguzi imekaa kimya kama hakuna lililotokea kwasababu limefanywa na mwajiri wao CCM.

Tukasikia mkuu wa wilaya akifanya mikutano na 'watendaji' bila hata kutumia akili ya kusoma mazingira ya kazi yake, wazalendo wakamuumbua.
Tukaona mawaziri na wastaafu wakienda Igunga kwa kodi zetu bila kujali hiyo ni shughuli ya chama na si serikali
Ikifika hapo wapinzani walikuwa tayari wameshashindwa licha ya kushindwa kutokana na kugawana kura wenyewe kwa wenyewe.

Matokeo na muundo wa siasa wa Igunga yameshtua nchi. Chama cha Chadema ambacho hakikupewa nafasi sana kimeibuka 'mshindi'. Ni ushindi usio na mwakilishi lakini ni wa kishindo.

CCM na washirika wake akina msajili na NEC achilia mbali Polisi kimelazimika kuita kundi la viongozi wastaafu, hata kumwita gamba RA na kujidhalilisha ili kuweza kupata tofauti ya kura 4000. Licha ya CCM kutumia mbegu za udini ngoma ilikesha roho zikiwatweta. Nitamshangaa sana mwana CCM atakayejivunia ushindi huu. Wana CCM wanapaswa kulia kwasababu unapotoka ufaulu wa 80% ukafaulu kwa 49% na mwenzako akaanza kutoka 0 hadi 45% bila msaada inasikitisha na ni dalili mabya siku za usoni.

Uchaguzi ungeitishwa leo Chadema wangechukua nchi, kwasababu CCM isingeweza kugawanya rasilimali zake nchi nzima, kwani Igunga tu imekuwa taabu, je Musoma, Arusha, Moshi, Iringa, Mbeya, Kigoma, Kagera, Dar, ingekuwaje.

'Uasi' ulioanza Karatu, Tarime, Moshi, Kigoma, Singida, Iringa unaonekana kusambaa kama moto wa nyikani, na hatari zaidi wanaosasambaza moto huo wana umri wa miaka 16, 17 ambao mwaka 2012 ni wapiga kura.

Ninaandika kwa uhakika kabisa kuwa pamoja na kutokuwa na katiba mpya na tume mpya ya uchaguzi ,mwaka 2015 kuna mambo mawili yatajitokeza.

1. Upinzani kuchukua nchi au 2) Kutakuwa na serikali ya CCM na Bunge la Upinzani au kinyume chake. Kimoja kati ya hivyo hakiepukiki kwa mtazamo na duru za siasa za leo.

Hata hivyo chama cha CUF sasa ni wazi kimepoteza mvuto na mstakabali wake kisiasa upo matatani.
Ninahisi wimbi kubwa la wanachama na viongozi wao kutimka katika kipindi cha miezi 6 ijayo kwa kupoteza matumaini na kujijengea mazingira ya kuaminika ndani ya vyama kama Chadema.

Matokeo ya siasa za haiba 'personality' yanajidhihiri na matokeo ya viongozi kuongozwa na wanachama na si wao kuwaongoza yanaoneka kwa CUF. Ndoa iliyompa mtu mmoja ulaji na si taifa sasa imetumbukia nyongo. CUF imefikia mahali tunapopaita 'Point of no return' na kama yupo asiyeona anguko lake basi yumo ndani ya jengo asilojua linaporomoka.

Kwa upande wa Chadema, wanatakiwa waelewe mafunzo yatokanayo na uchaguzi huu;

1. Kukubalika kwao Igunga ni ishara njema na wanapaswa wasilitose jimbo hilo bali walifanye moja ya 'hot cake' kama walivyofanya ubungo.
Wanapaswa kurejea na kuimarisha chama kwa mikutano na ufunguzi wa matawi pamoja na kuwashukuru wapiga kura

2. Waelewe kuwa kutofika maeneo kama Lindi, Tanga na Mtwara ni uzembe na kukata tamaa na kwamba watakapofika huko na moto wa Igunga wataambulia 45%, kumbe kama wangejizatiti wangekuwa katika 60%.

3. Wajiulize kwanini kuna wanaojiandikisha na hawaendi kupiga kura? Je, biashara ya ununuzi wa shahada imekwisha.
Suala la uchaguzi ni 'trick' na si kuibiwa kura za masandukuni tu.

4. Waache uzembe wa kujibu tuhuma. Jana msimamizi wa Uchaguzi bwana Magayane amenukuliwa na Daily news akisema watu waliojiandikisha ni 171,000 na waliopiga kura ni 50,000 kwasababu ya vurugu za Chadema na vitisho.

Tataizo la kutopiga kura limetokea mara nyingi tu, mfano kule Mbeya. Si tume ya uchaguzi wala wasomi wa TEMCO/SYNOVATE/REDET waliolitolea majibu, ingawa wanaweza kuwa nayo. Data zipo wazi na Chadema hawahitaji research au kikao cha kamati kuu kukanusha uongo wa Magayane.

Kwa bahati mbaya Chadema kama ninavyosema kila siku ni wazito sana wa kujibu mapigo 'rebuttal' hadi uharibifu utakapowamaliza 'damage' na suala la damage control kwao ni msamiati. Umma ukiaminishwa kuwa wao ni chanzo cha vurugu inatumika nguvu nyingi sana kukanusha badala ya kutumia data zilizopo kumuumbua Magayane. Hili ni tatizo kubwa ndani ya Chadema na gharama zake kisiasa ni kubwa ingawa haipimiki kwa mizani au pesa.

Na muhimu ni wapinzani kujiuliza wataingia katika uwanja huku refa na washika vibendera wakiwa timu pinzani wategemee nini. Ile ajenda ya katiba haina umuhimu kwa sasa kuliko wakati mwingine!!!!

Ahsanteni
 
MISAADA NA ATHARI ZAKE (Sehemu ya 1)

Tumekuwa tukisikia viongozi wetu wakienda nje au kukaribisha wageni wanaokuja na misaada. Tunadhani misaada ni neema na kusahahu kuwa kuna wakati inakuwa shubiri. Hakuna taifa linaloweza kutoa misaada tu bila kuwa na masilahi. Misaada inapotolewa huwa inafunikwa na kauli kadhaa kama kudumisha uhusiano, kusaidia wasiojiweza na wa hali ya chini n.k.

Wajapan wanapojenga bara bara zetu wanaangalia biashara zao, ingawa inaonekana ni soko dogo sana lakini ukijumlisha nchi zote za Afirca au Asia ni soko zuri tu. Wanapouza magari yao hawategemei sana faida ya magari bali faida inayotokana na uuzaji huo ikiwa ni pamoja na uagizaji vipuri wa miaka zaidi ya 10 gari liatakapokuwepo bara barani.

Wachina wanajenga miundo mbinu na viwanja vya michezo, si kwasababu wanatupenda sana bali masilahi ya muda mrefu. Walipojenga Tazara ilikuwa ni mamombi ya viongozi wetu, lakini nao waliangalia faida za muda mrefu ambazo hazikuonekana mara moja. Juzi tu wametoa mabehewa kusaidia Tazara. Pengine ni katika mkakati wa kuimarisha usafiri wa shaba kutoka Zambia na Congo pamoja na rasilimali nyingine.

Nchi za magharibi kama marekani wao ni usalama wao zaidi na masilahi ya kiuchumi. Asijedhani mtu kuwa millenium challenge ni kwa waafrika kama inavyosemwa. Asijedhani mtu kuwa wao kugawa vyandarua ni sehemu yao ya mambo ya kiroho.

Hivyo ndivyo ilivyomtokea Mpakistani aliyezoea kupokea dola bilion 10 kila mwaka. Akapewa jukumu la kusaka magaidi akiwemo Osama.
Jinsi gani Osama aliuawa bado ni siri kubwa ya CIA na itatuchukua miaka mingi kuijua kwa ukamilifu wake. Hata hivyo yapo machache tunayoyajua kutokana na hali iliyotokea.

Inasemekana kuwa Mohamed Sheikh Khalili, mshiriki mkubwa wa Alqaeda ndiye aliyetoa siri za nani anafanya mawasiliano kati ya Osama na dunia ikiwa ni pamoja na wafuasi wake. Marekani ilipopata habari hizo kwa undani ikaamua kutomshirikisha Mpakistan kwa hofu kuwa ndani ya serikali ya Pakistan kuna wasaliti na habari hizo zingevuja kabla ya mapAngo mzima.

Osama alikuwa ni mtu mwerevu sana, hata alipoamua kuishi Abotabad haikuwa bahati mbaya. Alijua kuwa karibu na chuo cha kijeshi na kituo cha polisi mita 500 si rahisi mtu kuhisi uwepo wake. Alianza kutotumia technology ya aina yoyote kwa kujua udhaifu wa technology na inavyoweza kukaribisha maadui.

Jumba aliloishi Abotabad lilikuwa la kawaida lakini lenye 'feature' zisizo za kawaida kama kutokuwa na simu au internet. Ukuta ulikuwa mkubwa na taka zilikuwa hazitupwi bali zinachomwa. Hili lilikuwa ni kosa ambalo hakutarajia lingezua maswali kuliko majibu.

Ilipobainika kuwa mchukuzi wa habari anaishi jumba hilo ilikuwa rahisi kuanza kulichunguza. Kila lilipochunguzwa ndipo hoja zaidi zilipoibuka. Haiwezekani mtu mwenye jumba zuri kama hilo na magari ya fahari asiwe na simu au internet!!

Mchukuzi wa habari wa Osama aikuwa anafunga simu yake na kutoa betri kila alipokuwa KM 50 karibu na nyumbani. Alikuwa mkarimu sana kwa majirani lakini hakushiriki mambo ya kawaida ya ujirani mwema. Nalo likazua maswali.

Hata ilipobainika kuwa kuna mtu asiyejulikana anaishi pale ilikuwa ni vigumu kuthibitisha kuwa alikuwa ni Osama. Marekani walikuwa na vinasaba vya Osama kutoka kwa nduguze(DNA), lakini wangeoanisha vipi na vya Osama asiyekuwepo na ambaye hisia za anapoishi zilikwazwa na ukweli kuwa hata ganda la ndizi halikutoka ndani ya nyumba(chomwa moto).

Ndipo ukaandaliwa mpango maalumu wa kuingia ndani ya jumba hilo. Ukazushwa mradi wa chanjo kwa watoto jimbo zima. Mpango huu ulimshirikisha daktari wa Kipakistan na hivyo kuondoa shaka. Zikaandaliwa chanjo za msaada ambazo ni fake. Watu wakafanikiwa kuingia ndani ya jumba kuchanja watoto. Osama hakuwa na hofu kwasababu hakuelewa kilichokuwa kinatafutwa ni DNA. Kosa la pili.

Ilipobainika kuwa vinasaba ni sawa, swali likazuka je Osama anaishi hapo kila siku au anasafiri? Wakatafutwa watu wa ku monitor mwenendo wa jumba lile ambao ni Wapakistani wenye uraia wa marekani. Kwa vile ni wenyeji hakuna aliyewashuku. Ikathibitika kuwa Osama anaishi pale.

Likazuka swali, je, kama wakishambulia na kumkosa kama ilivyowahi kutokea, hiyo haitaathiri taswira ya marekani kimataifa hasa kukiwa na kumbukumbu za Iraq. Je, kushambulia jumba lile na kuua watu wote ingeleta picha gani duniani na ingethibitika vipi kuwa aliyeuawa ni Osma?
Swalilikazuka tena, je akamatwe na kupelekwa marekani? Huko atashtakiwa wapi endapo Khalili sheikh Mohamed imeshindikana? Je hilo halimleteai umaarufu zaidi duniani kila anapopelekwa mahakamani?

Maswali zaidi, je ni salama kwenda kumkamata bila askari kufa endapo atajilipua na mabomu? Hatima ya maswali yote ikawa ni kumuua ikithibitika yupo na kumzika haraka sana mahali ambapo hapatageuzwa kama sehemu ya makumbusho ya Osama na wafuasi wake.
Sehemu ya 1
 
MISAADA NA ATAHRI ZAKE (SEHEMU YA 2).
Mpango mzima wa kuvamia Abotabad ulipangwa kwa uangalifu wa hali ya juu sana. Inasemwa kuwa ni viongozi wachache sana walikuwa na taarifa hizo. Ikumbukwe kuwa wiki hizo kabla, marekani iliendeleza mashambulizi sana Afghanistani ili kumghilibu yoyote anayehisi na kumdanganya Osama kuwa alikuwa salama.

Ni wiki kama mbili kabla ya uvamizi, hoja ya cheti cha kuzaliwa cha Rais Obama ilipopamba moto sana. Watu kama Donald Trump waliifanya kama kampeni na kumbana sana Obama. Obama aliwahi kugoma kutoa uthibitisho lakini pressure ilikuwa kubwa sana. Ndipo alipotoa cheti hicho hadharani. Siku alipokitoa alisema maneno haya '.....habari za cheti changu zinavuruga majukumu makubwa sana tuliyonayo kitaifa na kimataifa'. Hakuna aliyehisi ni majukumu gani zaidi ya yale ya urais. Alionekana mnyonge sana siku hiyo. Wengi wakahisi amedhalilishwa. Hata hivyo hiyo ikakata kidomo domo cha republican daima dawamu.

Wiki hiyo alipotoa cheti cha kuzaliwa alionekana akiwa na shuguli za nje zaidi kuliko white house. Alionekana mwisho wa wiki akicheza gofu na wengi wakijua alikuwa anajiliwaza.

Jumamosi ilipangwa kuwa siku ya Obama kukutana na wanahabari kama ilivyokawida katika chakula cha jioni( annual Press dinner). Siku hiyo ni siku ya utani kati ya wana habari na serikali na huwa kuna mizaha ya kila aina. Ni siku rais wa marekani anaitwa 'comedian in chief' yaani mchekeshaji mkuu.

Siku hiyo aliitumia vema kumshambulia Donald Trump kwa mzaha wa cheti chake cha kuzaliwa. Hata hivyo ijumaa kabla alishanya uamuzi wa mwisho wa kuvamia Abotabad na mipango yote ya mauaji na mazishi ya Osama itakayomaliza suala hilo kwa uharaka bila kuzua mjadala kimataifa.

Jumapili ilipangwa makusudi kwa kujua kuwa viongozi wengi wapo mapunzikoni kwa matayarisho ya jumatatu na kwamba mambo mengi hutokea siku za wiki na hakukuwa na dalili yoyote ya jambo kubwa kutokea duniani.

Swali likazuka, je, jeshi la Pakistani lita react vipi na kwamba hakuna hatari ya kushambulia ndege za marekani?
Jibu lilishapitikana kwa kutumia kikosi maalum 'Seal' na matumizi ya ndege zisizoonekana kwa rada 'stealth'. Pia kikawepo kikosi maalumu endapo Pakistan ingeshambulia. Mpango mzima ulikuwa wa dakika 25 kutokana na mazoezi, lakini ulidumu kwa dakika 38 kutokana na ndege moja kupata matatizo.

Hayo yote yakiendelea white house ilikuwa inayafuatilia kwa muda' real time' kukiwa na mawasiliano kati ya jeshi na ikulu.
Ilichukua zaidi ya masaa 2 Pakistan kutuma ndege huku mpango mzima ukiwa umekamilika. Tatizo ni pale mabaki ya ndege yaliposhindikana kuondolewa na tuliona ujumbe wa senate ukienda Pakistan na kisha mabaki hayo kurudishwa. Hili lilisumbua sana marekani kwani mchina alikuwa karibu ili kuiba technology kama kawaida yake.

Ndipo Jumapili jioni, muda usio wa kawaida wa rais wa marekani kuhutubia taifa ulipowadia na Obama kuitangazia dunia kifo cha Osama. Hii ilikuwa ni baada ya kuthibitisha pasi na shaka kuwa alikuwa Osama ili kutoleta sintofahamu.

Kazi hiyo aliifanya kwa kuanza na mawasiliano na marasi wa nchi husika.
Kukatokea shinikizo la picha za Osama. Hili lilifanywa kwa nia mbili, kwanza watu waamini kifo chake na pili, lipo kundi la waislam wenye msimamo mkali waliotaka picha hiyo ambayo aliharibika vibaya itolewe ili kuchochea hisia zaidi. Yote yakaonekana hayawezikani ili kutoleta mjadala wa Osama na hakika wamarekani wamefanikiwa.

Suala la kuuawa osama liliwaudhi sana Pakistan, in fact kuwaumbua sana. Wamekana mara nyingi uwepo wa Osama nchini mwao na sasa wageni wameingia bila hodi na kumtoa. Ni aibu kubwa sana.

Wiki iliyopita Daktari aliyehusika amekamatwa eti kwa usaliti wa nchi huku marekani ikimtetea.

Dhalili iliyopata Pakistan ni kwa sababu ya kudhani kuwa taifa huru ni kutegmea misaada. Ni tatizo linalotukabili na ipo siku tutalipa gharma zake. Misaada si njia nzuri ya kujiletea maendeleo bali ukoloni na utumwa usio katika maendeleo. Rais au waziri au katibu mkuu anapotia saini mkataba si jambo la kupiga makofi ni jambo la kusikitika kwani nyuma ya misaada hiyo yapo mengi tusiyoyajua.
 
TUGEUKIE DURU ZA SIASA ZA NYUMBANI

Kikao cha bunge kimepitisha sheria ya uundwaji na uanzishwaji wa machakato wa katiba mpya. Hayo yametokea kukiwa na upinzani mkubwa wa kisiasa kati ya vyama vya Chadema na CCM kana kwamba suala hilo limepoteza maana ya utaifa.
Katiba ni sheria na muongozo wa mtanzania yoyote bila kujali itikadi zake.

Sakata ni la CCM wakiunga mkono serikali na Chadema wakipinga mchakato huo.
Wapinzani wengine ukiacha NCCR wao wameamua kuungana na CCM.
Inasikitisha kuona CUF waliokuwa wa kwanza kupeleka rasimu ya katiba kabla ya kujua mchakato nao wamefungwa katika ile ndoa iliyofungwa Zanzibar.

Kuna jambo ambalo pengine halieleweki au linaeleweka lakini linafanyiwa makusudi. Watu wengi wanakataa mchakato si kwasababu ya maudhui kwa vile hatua ya kujadili maudhui haijafikiwa.
Kinachojadiliwa ni jinsi gani tunaandaa mazingira yatakayo kuwa huru na haki ya kila mmoja wetu kuwakilishwa au kuwakilisha mawazo yake.

Tunakumbuka Kenya lilileta matafaruku hadi pale walipoafikiana na serikali ikawa mshiriki wa uundwaji wa katiba na si msimamizi.
Hivi ndivyo intakiwa iwe. Mchakato utokane na wananchi ili watengeneze kitu cha wananchi.
Ilivyo sasa mchakato umempa Rais madaraka makubwa sana kiasi kwamba anaweza kukaa na familia yake wakaandika katiba. Anachotakiwa ni kusema sehemu ya familia au marafiki zake ni wateuliwa.

Tumeona haraka haraka mambo yalivyozuiliwa yasijadiliwe hata yale yanayolisumbua taifa kama muungano.
Rais hawezi kusema hili lijadiliwe na hili hapana kwani kufanya hivyo tayari ana katiba yake na anachotaka ni saini ili iweze kutumika.

Haiingii akilini kuwa tume atakayochaua Rais itakuwa huru hata kwa kufikiri kidogo tu ya kuwa tume ya uchaguzi si huru na tunaona inavyofanya kazi kama sehemu ya Ikulu.
Tumeshuhudia msajili wa vyama akifanya kazi kama katibu mkuu wa CCM.
Lakini tujiulize, hivi tume gani iliyowahi kuteuliwa na Rais ikafanya kazi tuliotarajia?

Mzee Mwinyi baada ya joto la mageuzi akaiteka nyara hoja ya kuanzishwa vyama vingi.
Alichokifanya si kuwauliza wananchi kupitia wawakilishi wao bali kuunda sheria iliyoidhinishwa na wabunge halafu akaendelea na uchochoro wa tume yake. Hakuna anayeweza kusimama na kusema 80% walisema hapana na 21 ndiyo.
Tunaaminishwa hivyo tu, taarifa ya nini kilijiri ni siri ya mwinyi ingawa matokeo ni yetu.

Haya yalitokea wakati wa Mkapa na tume ya Warioba ambayo ilikuja na maoni tu na kumtoa mtu mmoja kafara kana kwamba yeye ndiye alikuwa tatizo(Kiula). Kama tume ile ingekuwa na tija akina Kingunge wasingepata mianya ya mambo waliyoyafanya.

Tume ya Nyalali ikaja na sheria 40 mbovu, leo hii bado zipo na hata nusu ya mapendekezo hayajafanyiwa kazi. Hii si kwa uonevu bali kwa haki kwasababu tume inawajibika kwa aliyeiteua na si bunge au chombo kingine.
Ikaja ya Jaji Kisanga na matokeo yale yale.

Mifano ipo mingi sana na inatosha kusema kuwa, tume itakayoundwa haitafanya kazi wala kuwajibika kwetu hata kama imetungwa na sheria za bunge. Kwani bunge letu lina nguvu? Lingekuwa na nguvu RECHEL wasingekuwa katika ulimwengu wa siasa.
Na bado ze comed inaendelea kwa Jairo, n.k.

Kwahiyo tatizo si maudhui bali ni njia zinazotumika kuajdili maudhui ya katiba.
Kwa mwendo uliopo ni ujinga wa hali ya juu kuanza kujadili nini kiwe ndani ya katiba na kipi kisiwepo. Ni ujinga kwasababu inawezekana unachokitaka au usichokitaka vikawa tayari vimejadiliwa na kuna katiba imeandikwa na inasubiri bunge la katiba, kura ya maoni na kuwa sheria mama.

Huu ndio msingi mkuwa wa madai ya Chadema ambayo ni wazi yapo pamoja na sehemu kubwa ya jamii isipokuwa ile inayonufaika na mfumo uliopo.

Ukiniuliza saa 9.34 usiku jibu langu halitabadilika nalo ni kuwa, je tutatendewa haki ya kusikia na kusikilizwa kwa utaratibu unaosimamiwa na yule yule tunayemlalamikia?

Kwa hali yoyote hakuna sababu ya wananchi kuanza kujadili nini cha kuweka au kuondoa, ni muhimu wakasimama na kusema hii ni katiba sio dhifa ya taifa. Tunatakiwa tujiridhishe kuwa maoni yetu yanayoafikia au kupingana yanapewa haki 'Fair trial' na chombo huru. Vingienvyo turakurudi kwenye tume ya Nyalali, Kisanga, Warioba na white paper na hapo tutasaga meno kwa miaka mingi ijayo.
 
DHANA YA 'DAMAGE CONTROL'

Kwa mara ya mwisho tuligusia namna ambayo siku 14 zilipita bila uongozi wa Chadema kutoa ufafanuzi , maelezo au majibu sakata la AR.
Siku 14 ni nyingi sana kuachia mada ijieleze na kujijibu yenyewe. Ndipo tulisema dhana ya damage control haikutumika kwa gharama kubwa kisiasa.

Hili halikuwa tukio la kipekee kwa Chadema, vyama kama CUF, NCCR vimepita katika majaribu kama hayo na vimeumia sana.
Kwa ukongwe wa kisiasa, CCM wameweza kufanya damage control ingawa kutokana na siasa za chuki na makundi kazi hiyo inakuwa ngumu. Mfano, waliunda kamati ya mzee ruksa kutafuta muafaka wa chuki baada ya mashambulizi yenye hasira kutoka pande zinazohasimiana.
Ilifika mahali siri za chama na viongozi zinamwagwa hovyo na kukidhalilisha Chama, ndipo kamati ikaundwa kuepusha malumbano.

CCM imekuwa ikijitenga haraka na watu au mtu wenye kashfa, ndiyo maana mara zote wanatoa matamko kama yale yasemayo chama si fisadi ila ufisadi ni wa watu binafsi, wakati mwingine kufikia hatua hata za kuwachachafya watuhumiwa ili kupata 'damage control' mapema kabisa.

Damage control inatumika katika serikali, taasisi na mashirika katika ngazi zote za kitaifa hadi kimataifa. Inafanyika kwa njia nyingi.
Kwa mfano Obama alipoandamwa na tuhuma za mchungaji 'Right' ilimchukua muda mrefu kujibu tuhuma kiasi kwamba kampeni yake iliyumba sana. Bahati nzuri Obama ni Orator mzuri aliugeuza uharibIfu kwa manufaa katika hotuba yake Pennyslavania.
Hata hivyo kuzembea kujibu shutuma, tuhuma au kauli umekuwa ni udhaifu mkubwa sana wa kampeni za Obama na humgharimu.

Tofauti na Obama, Hillary alizusha yake aliposema akiwa Bosnia alipokewa uwanja wa ndege risasi zikivuma angani.
Ukweli ni kuwa alipokelewa na maua na ilionekana kuwa kama kashfa kubwa ya uongo. Hillary alikwenda kwenye vyombo vya habari na kutetea kauli zake na kuhudhuria vipindi 'talk show' ambapo aligeuza tuhuma kuwa mzaha akiwa na comedians na kupoteza nguvu.
Wakati hayo yakiendelea watu wanaojulikana kama Political pundits walikuwa wanatafuta hoja mbadala itakayokuwa na nguvu.

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza bw.Godon Brown alinaswa na vipaza sauti kabla hajavivua vikimkariri akimwita mwanamke mmoja Bigots.
Ilipotokea katika vyombo vya habari asubuhi akaenda nyumbani kwa yule mama kumtaka radhi. Alifahamu uharibifu utakaotokana na maelezo au malumbano yasiyoisha ni mkubwa sana kuliko kusema samahani.

Tunakumbuka mwandishi aliyemwagiwa tindikali, baada ya minong'ono iliyohusishwa na habari za ufisadi, siku iliyofuata Rais aliagiza serikali igharamie matibabu je! hii ilifanyika ili kuua minong'ono kwani ni wakati huo shauri la marehemu Bilali lilikuwa moto.

Mwandishi alipokuwa anakaribia kurudi alisema ataweka wazi waliohusika akifika Dar. Baada ya muda wakakamatwa vibakwa kwa kubambikiwa shitaka. Hapo shitaka likawa mahakamani na hakukuwa na uhalali wa kuliongelea.Baada ya miaka 3 nguvu yake ikapungua vibaka wakaachiliwa.
Hii ilikuwa ni sehemu ya mkakati wa damage control kwasababu ni kipindi hicho EL alikuwa na Richmond na hili la mwandishi lingefunua mambo makubwa kama lingeachiwa kuongelewa hovyo.

Katika taasisi au mashirika nayo hujikuta katika gharma kubwa ima za kuwalinda au kuwaweka sawa watumishi wao ili pamoja na mambo mengine wasijehusishwa na uharibifu wa heshima(reputation). Hakuna shirika litakalofurahi kusikia manager au CEO ameokotwa chakari mitaani, au CEO anahusishwa na biashara chafu kama za madawa au umalaya. Taasisi na mashirika huchukua hatua za awali kuzuia kama njia ya awali ili wasifikie hatua ya damage control ambayo si njema na ni ghali .

Nimelitolea mfano hili kwasababu gharama zake zilikuwa kubwa kwa chama cha CUF kilichokuwa na wafuasi wengi wa ukanda wa pwani.
CUF waliposhutumiwa kuwa chama cha Kidini( Kiislamu) badala ya kufanya damage control (hata kama haikuwa kosa lao) wao wakaacha kwanza jambo hilo likaaminishwa vichwani mwa watu kwa muda mrefu sana. Walipotakiwa kujibu walichofanya ni kuchochea uharibifu kwa kusema CCM nayo ina viongozi wengi wakristo, ni chama cha Kikirsto. Hawakuwa na political strategists, pundits, observers au analysts kwasababu chama kilijengwa kwa personality hasa ya maalimu Seif na si idara au wanachama.

Kwa kukosa watu muhimu kama Pundits, Observers, commentators n.k katika idara za CUF, makosa yakaendelea kufanyika na kuharibu zaidi.
Chama kikawa kinafanya mikutano siku ya Ijumaa baada ya swala! Hii ikashadidia hoja iliyokuwepo awali hata kama ilikuwa ni ya uongo. Uharibifu huo ukawa mkubwa sana na damage control haikuwezekana na kupelekea chama kubaki katika vitabu vya historia.

Chadema, chama cha upinzania ni makini sana lakini bado hawajajifunza kutoka CUF au NCCR kwa undani. Nasema hivi kwasababu chama kimekuwa kama mtu au watu na si idara. Haiwezekani Dr Slaa awepo kila mahali kutoa kauli hata kwa mambo madogo.
Ni mara chache kumsikia msemaji wa chama, au watu wanaolinda maslahi ya chama( pundits, strategists etc) wakitoa ufafanuzi au kauli. Matokeo yake siku zote watu husema Dr mbona hajasema au kasemaje! Hiki ni chama na idara zake ni lazima zifanye kazi kikamilifu.
Kwani tatizo la Chadema ni ukosefu wa watu wenye sifa au kutokuwa tayari kuajiri wenye sifa au kutoona umuhimu tu!!!

Chadema wapo Slow katika ku-seize opportunity hasa CCM wanapobofoa. Ni slow katika kujibu tuhuma, na ni slow katika ufuatiliaji.
Inawezekana kuwa ni mkakati wao ndio maana wapo makini sana, lakini in politics timing is very important.
Ndio maana nasema haiwezekani damage control ifanyike baada ya siku 14 halafu useme huo ni mkakati na sio mapungufu.

Hitimisho: CCM wanaijua vema dhana ya damage control, timimg and who is to say what.
Vyama vya upinzania bado dhana hii haieleweki. Hoja ya Nape haijibiwi na Katibu mkuu wa Chadema inajibiwa na 'counterpart wa Chadema'.
Upinzani ujue ku react promptly with precisions na ikitokea kuna dalali li za uharibifu damage control ifanyike mapema sana kuepuka gharma zisizo za lazima kisiasa. Lakini pia wawe innovative si kila jambo wafanye kwa 'template ya CCM'.

Ni wakati tusemezane ili kuviimarisha vyama vya siasa tusijerudi kule kule kwa NCCR au CUF.
Hatuna muda wa kulelea vyama vipya kila msimu, tulee vilivyopo ili tuwe na demokrasi ya nguvu na kweli.

Nimependa hii sana na ni mchango muhimu kwa watu wanaotaka kutengeneza chama kinachofanya kazi kwa kutumia mbinu za kisiasa na mbinu ambazo zinatumika kwa wakati. Mojawapo ya changamoto kubwa ambazo tunaziona leo hii hasa katika upinzani ni kuwa vyama vingi na sasa hivi kweli imebakia CDM inacheza muziki wa CCM na serikali. Sijui hili tutaliondoa vipi kwa kweli.
 
Wiki mbili zilizopita tuliangalia hali ya mambo mashariki ya kati hasa Misri ambako nilieleza mapema kuwa Tahariri square ilikuwa na mkono wa Muslim brotherhood. Kuna rafiki yangu alinipinga na kusema zilikuwa hisia zangu na si ukweli wa mambo. Tunaona zaidi waandishi wengi wakiliongelea jambo hili katika mizania ile ile.

Brotherhood ni werevu na uchaguzi wa leo wanaonekana watazoa viti na huo ndio mwanzo wa kuingia madarakani ingawa ni kimya kimya. Tusubiri matokeo ya uchaguzi wa leo yatatupa nini.

Nikumbushe kuwa Morocco kulikuwa na uchaguzi uliochagizwa na spring revolution ingawa si kwa kasi ya misiri, Libya au Tunisia. Katika uchaguzi huo chama chenye msimamo wa kati (moderate islamists) kimechukua ushindi wa sehemu kubwa.
Inaweza kuwa haina maana ukiangalia kwa mtazamo wa haraka, lakini kama upo Tel avivu, Jeruslame au Washington hili lazima lisimbue watu na vichwa vyao.

Swali kubwa linaloumiza kichwa ni kuwa haya mageuzi mwisho wake ni nini na nani anafuata baada ya! Je, ndiyo ule usemi wa kiswahili umetimia 'jini limetoka ndani ya chupa'!

Asbolutely, utaona hata chombo chao cha kisiasa kwenye kura hakiitwa "Muslims Brotherhood" wanakiita "Freedom and Justice Party" na siwezi kushangaa wakapata wabunge wengi.
 
MSETO (MASHARIKI YA KATI NA NYUMBANI TANZANIA) KATIBA MPYA

Bado tunasubiri habari matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Misri ambayo pamoja na kususiwa na baadhi ya vyama, mamilioni wameshiriki akiwemo aliyekuwa katibu mkuu wa Arab League Bw Amr Mousa.

Wakati hayo yakitokea turejee nyumbani na kuliangalia sakata la katiba mpya. Tumeona madai ya Chadema dhidi ya mchakato na matokeo ya katiba. Hakuna shaka kuwa yale waliyoyaongea yana maana sana kwa mustakabali wa taifa na kama itatumika njia ya mkato kama inayokusudiwa tunaweza kujikuta tunarudi kuandika katiba mpya katika muda mfupi sana kama si kutoana ngeu au roho.

Mantiki hasa ya kuandika ni kutokana na mwenendo wa kile kinachoitwa muafaka kati ya serikali ambayo ni CCM na Chadema. Ikumbukwe vugu vugu lilianzia bungeni na lilipopata joto la umma hali ikaonekana kuwa tete. Pamoja na utete huo kamati kuu ya CCM ikapongeza bunge kwa hatua iliyofikia bila kujali mamilioni ya wananchi yaliyotoka nje kwa kupitia wabunge wa Upinzani.
Wala haikuwa rais Kikwete aliyeshtuka kwa sababu mpango mzima ulikuwa umekamilika, nao ni kuwa na mchakato utakaompa nguvu ya kuandika katiba yake nasi tutie sahihi.

Ni ujinga wa hali ya juu kufikiri kuwa Wabunge wa CCM wanaonufaika na katiba hii (na juzi tu wameongezewa posho) wanaweza au wataweza kuwa na lolote la maana la kuchangia katika katiba hii. Hawa ni wasaliti na kuwaongelea ni kuwapa fursa wasiyostahiki.

Chadema wakaunda kamati ilyokuwa na dhima ya kuzuia utiaji saini hadi pale madai yao ambayo ni ya kweli yatakaposikilizwa.
Huo ndio msimamo uliorudisha nyuma nguvu ya umma iliyokuwa tayari kudai haki.
Niliunga mkono hilo kwani kabla ya kulirejesha mahakama ya wananchi ni lazima zitumike njia zote za kidiplomasia zisizoathri msimamo

Kikao cha siku mbili kikaisha kwa Chadema na Serikali kuandika kitu kinaitwa 'joint statement'. Nasema joint statement kwasababu Chadema hawajakataa au kukanusha habari yoyote.

Magazeti ya CCM likaandika kuwa moja ya makubaliano ni kukubali kuwa katiba iliyopo (ambayo ni mbaya) itumike kusimamia uandikaji wa katiba mpya!!

Gazeti la Daily news likasema makubalino mengine ni kukubaliana kuwa kutakuwa na marekebisho kila mchakato utakavyokuwa unaendelea. Na gazeti lingine likaandika wote wamekubaliana kuwa si rahisi kwa rais kusimamisha utiaji sahihi (accent) huo mswada.

Tumesoma kuhusu kauli ya Mbowe kuwa kama hakutakuwa na marekebisho basi watalirudisha kwa wananchi. Hakukanusha kauli za magazeti. Na ni kuanzia hapo ndipo nayaona matatizo kwa upande wa Chadema.

1. Hakuna mawasiliano na 'base' yao kuhusu 'joint statement' ya kuwa kweli walishiriki kuandika au ilitolewa na iIkulu.
Kwa jinsi ilivyoandikwa ni wazi Chadema wamejifunga kwasababu wamekubali yale yote waliyokuwa wanayakataa, sasa watarudi kuwaeleza wananchi nini wakati wa kulirejesha suala hilo kwa wananchi?

2. Kama wamekubali kuwa katiba iliyopo itumike kusimamia mchakato, kulikuwa na haja gani ya kupinga suala hilo bungeni na kwingineko? Ni katiba hiyo ndiyo inampa rais madaraka yote.

3.Je, walipoamua kukutana na JK tena kwa kusisitiza wapinzani wengine wasishiriki, hiyo ndio ilikuwa haja ya matakwa ya wanachama wao? Je, lengo lao la kuzuia utiaji saini limefanikiwa na kama sio muafaka ndio ilikuw suluhu ya tatizo!

4. Hivi bunge la CCM lililopitisha mswada bila kujali unyeti na malalamiko ya wananchi linawezaje siku za mbeleni kufanya mabadiliko yanayokusudiwa na Chadema?

5. Kikwete aliyewahadaa Chadema kuhusu katiba mpya hapo awali, amejirudi kiasi gani au amebadilikaje kiasi cha Chadema kumpa jukumu la kusimamia mchakato na uandikwaji wa Katiba.

6. Hivi ni kipengele gani cha katiba kinachomlazimisha rais kutia sahihi mswada kwa vile tu umefikia. Je, kama mswada huo ungekuwa wa binafsi au kambi ya upinzani uliopitishwa na bunge na ukaonekana kumkwaza Rais, je, angetia sahihi tu kwasababu umetoka bungeni.

7. Ni nini msimamo wa Chadema kama watawasiliana na wafuasi wao:
a) wanakubaliana na mswada na uendelee kukiwa na marekebisho kama walivyoahidiwa
b) Hawakubaliani na yale yaliyoongelewa ikulu na wanataka mchakato uanze upya
c) Hawakubaliani na wanalirudisha suala hilo kwa wananchi.
 
LOWASSA: MWAGA MBOGA NAMWAGA UGALI
Hatua ya waziri mkuu mjiuzulu Lowassa kutoa kauli ndani ya NEC kwa kumhusisha swahiba yake inaweza kuonekana ni ndogo. Kisiasa ina maana kubwa sana. Kwanza ni kutaka kujisafisha baada ya kuona tuhuma za ufisadi zitakwaza juhudi zake za urahisi.
EL ana pesa za kutosha kuishi raha mstarehe, kinachomsumbua ni kuwa hatua zozote zile dhidi take zinaweza kutumiwa na wapinzani wake kuzima ndoto yake ya kuwa rais kwa kutumia sheria na taratibu za chama.

Ni kwa kuhofia hilo ndipo alipoamua kumuumbua rafiki yake ndani ya NEC. Alichokifanya ni kumtisha JK kuwa yupo tayari kuwaga mboga kama JK atamwaga ugali. Pengine kwa kujua au kutojua EL ametusaidia kujua mengi kuhusu Rais wetu.

Katika mazingira ya kwaida kauli ya Rais huwa na uzito kwani inakuwa imefanyiwa utafiti wa kutosha. Na wala haipendezi wananchi wanapokuwa na mashaka na kauli za kiongozi wa nchi. Kauli ya EL si kuwa imemuumbua rais kwa kumhusisha na Richmond bali pia imethibitisha kuwa kauli za mkuu wa nchi haziamiki kabisa.

Mwanzo kabisa Rais aliwahi kuulizwa kama kuna utata kuhusu suala hili akasema hakuna.
Rais ambaye PCCB inawajibika kwake alipelekewa taarifa 'fake' kabla ya tume ya Shelukindo na yeye kama kiongozi na mamlaka inayowajibisha PCCB akakubali hata kama alijua ukweli tunaojua leo. Alifanya hivyo kama funika kombe.

Bunge likatoa taarifa na kumhusisha Dr Hosea moja kwa moja na uozo wa Richmond. Rais ambaye ndiye mamlaka inayopaswa kumwajibisha akakaa kimya na kumwacha Dr Hosea akiendeleza ngano na hadithi za kipuuzi. Hapa hakuwa Dr Hosea tena bali mamlaka iliyomruhusu kuandika uongo bila kumchukualia hatua.

Rais akaenda Ubungo Plaza kuongea na wabunge wa chama chake akasema kulipa Dowans(ambayo ni Richmond in different version) ilimtia uchungu. Uchungu gani wakati hajawahi kuchukua hatua kuwatia nidhamu akina Hosea waliomdanganya??

Akaenda kwenye sherehe za kuzaliwa CCM, hapo akasema hawajui Richmond au Dowans na wala hawamhitaji katika shughuli zao.

Kauli ya EL kuwa alimtaarifu kuhusu kuvunja mkataba na JK akashauri asubiri kidogo ni ushahidi usio na mashaka kuwa Rais JK alijua suala la Richmond kuanzia 'day one'. Anachokifanya ni kujikosha kwa wananchi wakati ukweli ukiwa pale pale kuwa yeye ni mhusika. Si maneno yangu ni ya EL.

Ni kwa mtitiriko huo sijui rais Jk atatoa kauli gani umma umwamini. Nasema umma umwani kwasababu si suala la Richmond tu kuna mengi kama posho za wabunge ambazo yeye amekuwa akicheza karata za kisiasa badala ya utendaji.
Anawapaka wananchi mafuta kwa mgongo wa chupa kule kwetu pwani tunasema anawalamba visogo.

Ni wakati wa Samwel Sitta wazee wa CCM wa Dar waliandika risala kuzungumzia suala hilo. Yeye akajibu, Wabunge ni watu wazima anategemea wamesikia. Baada ya miezi kadhaa JK akasaini nyaraka za kuidhinisha marupu rupu ambayo kimsingi ni unyang'anyi wa kutumia demokrasi. Mbele ya mungu unabaki kuwa unyang'anyi kama ule wa vibaka wa Mwannyamala au kwa madenge.

Kuna taarifa amegoma kusaini kuhusu unyang'anyi wa posho safari hii. Huyu ni JK baada ya muda atausaini tu. Jitihada zote ni kupendeza kila mmoja. Kiongozi makini hapaswi kufurahisha umma anapaswa kutenda kwa muijibu wa sheria, kanuni na maadili.

Ikifika hapo ndipo nasema ahsante EL, ingawa hutasafishika hata kwa tindikali inajuzu tukushukuru kwa kutufunulia undani wa mshirika wako. Sasa tunajua kauli zake zote ni za kubabaisha na sidhani kama ipo haja ya kutilia maanani tena kauli zake. Haaminiki hata kidogo.
 
LOWASSA: MWAGA MBOGA NAMWAGA UGALI
Hatua ya waziri mkuu mjiuzulu Lowassa kutoa kauli ndani ya NEC kwa kumhusisha swahiba yake inaweza kuonekana ni ndogo. Kisiasa ina maana kubwa sana. Kwanza ni kutaka kujisafisha baada ya kuona tuhuma za ufisadi zitakwaza juhudi zake za urahisi.
EL ana pesa za kutosha kuishi raha mstarehe, kinachomsumbua ni kuwa hatua zozote zile dhidi take zinaweza kutumiwa na wapinzani wake kuzima ndoto yake ya kuwa rais kwa kutumia sheria na taratibu za chama.

Ni kwa kuhofia hilo ndipo alipoamua kumuumbua rafiki yake ndani ya NEC. Alichokifanya ni kumtisha JK kuwa yupo tayari kuwaga mboga kama JK atamwaga ugali. Pengine kwa kujua au kutojua EL ametusaidia kujua mengi kuhusu Rais wetu.

Katika mazingira ya kwaida kauli ya Rais huwa na uzito kwani inakuwa imefanyiwa utafiti wa kutosha. Na wala haipendezi wananchi wanapokuwa na mashaka na kauli za kiongozi wa nchi. Kauli ya EL si kuwa imemuumbua rais kwa kumhusisha na Richmond bali pia imethibitisha kuwa kauli za mkuu wa nchi haziamiki kabisa.

Mwanzo kabisa Rais aliwahi kuulizwa kama kuna utata kuhusu suala hili akasema hakuna.
Rais ambaye PCCB inawajibika kwake alipelekewa taarifa 'fake' kabla ya tume ya Shelukindo na yeye kama kiongozi na mamlaka inayowajibisha PCCB akakubali hata kama alijua ukweli tunaojua leo. Alifanya hivyo kama funika kombe.

Bunge likatoa taarifa na kumhusisha Dr Hosea moja kwa moja na uozo wa Richmond. Rais ambaye ndiye mamlaka inayopaswa kumwajibisha akakaa kimya na kumwacha Dr Hosea akiendeleza ngano na hadithi za kipuuzi. Hapa hakuwa Dr Hosea tena bali mamlaka iliyomruhusu kuandika uongo bila kumchukualia hatua.

Rais akaenda Ubungo Plaza kuongea na wabunge wa chama chake akasema kulipa Dowans(ambayo ni Richmond in different version) ilimtia uchungu. Uchungu gani wakati hajawahi kuchukua hatua kuwatia nidhamu akina Hosea waliomdanganya??

Akaenda kwenye sherehe za kuzaliwa CCM, hapo akasema hawajui Richmond au Dowans na wala hawamhitaji katika shughuli zao.

Kauli ya EL kuwa alimtaarifu kuhusu kuvunja mkataba na JK akashauri asubiri kidogo ni ushahidi usio na mashaka kuwa Rais JK alijua suala la Richmond kuanzia 'day one'. Anachokifanya ni kujikosha kwa wananchi wakati ukweli ukiwa pale pale kuwa yeye ni mhusika. Si maneno yangu ni ya EL.

Ni kwa mtitiriko huo sijui rais Jk atatoa kauli gani umma umwamini. Nasema umma umwani kwasababu si suala la Richmond tu kuna mengi kama posho za wabunge ambazo yeye amekuwa akicheza karata za kisiasa badala ya utendaji.
Anawapaka wananchi mafuta kwa mgongo wa chupa kule kwetu pwani tunasema anawalamba visogo.

Ni wakati wa Samwel Sitta wazee wa CCM wa Dar waliandika risala kuzungumzia suala hilo. Yeye akajibu, Wabunge ni watu wazima anategemea wamesikia. Baada ya miezi kadhaa JK akasaini nyaraka za kuidhinisha marupu rupu ambayo kimsingi ni unyang'anyi wa kutumia demokrasi. Mbele ya mungu unabaki kuwa unyang'anyi kama ule wa vibaka wa Mwannyamala au kwa madenge.

Kuna taarifa amegoma kusaini kuhusu unyang'anyi wa posho safari hii. Huyu ni JK baada ya muda atausaini tu. Jitihada zote ni kupendeza kila mmoja. Kiongozi makini hapaswi kufurahisha umma anapaswa kutenda kwa muijibu wa sheria, kanuni na maadili.

Ikifika hapo ndipo nasema ahsante EL, ingawa hutasafishika hata kwa tindikali inajuzu tukushukuru kwa kutufunulia undani wa mshirika wako. Sasa tunajua kauli zake zote ni za kubabaisha na sidhani kama ipo haja ya kutilia maanani tena kauli zake. Haaminiki hata kidogo.
Nguruvi3, asante nimekusoma, alichosema EL ni tip tuu, alikubali kujiuzulu u-pm to cover for his best friend ambaye ni among benefisharies wa Richmond/Dowans!.

Anachofanya sasa ni kuongeo lolote dhidi ya serikali ya JK ili kuweka mazingira ya kuwaeleza Watanzania kuwa yeye sio sehemu uozo wa serikali iliyopo madarakani ili mwaka 2015 atakapo jitokeza mbele ya wananchi, ajitanabaishe yeye sio "wale wale".

Hoja kuwa JK sio mtu wa kuaminika sana ndio proin ya EL kutokea na nakuhakikishia JK hana ubavu wa kumdhibiti kwa sababu JK as a populist leader amebweteka na umaarufu kuwa anapendwa, hivyo ajajiamisha yoyote atakaye mpigia chapuo ndio lazima awe, lakini EL ni strategist ambaye ameshajipanga kimipango mkakati ndani ya CCM.

My Honest Opinion, EL would have made a better president ten times than JK, ila kwa 2015 EL hawezi!. Juzijuzi nimekutana na kuongea nae mahali, my opinion nadhani afya yake ni mgogoro!.

Kwa vile amefanyiwa maombi na Man of God, TB Joshua, na kama ni kweli Mungu wa Joshua ndiye Mungu wa kweli aliye juu, then nothing can stop him now!.
 
Pasco;2962807]Anachofanya sasa ni kuongeo lolote dhidi ya serikali ya JK ili kuweka mazingira ya kuwaeleza Watanzania kuwa yeye sio sehemu uozo wa serikali iliyopo madarakani ili mwaka 2015 atakapo jitokeza mbele ya wananchi, ajitanabaishe yeye sio "wale wale".

Hoja kuwa JK sio mtu wa kuaminika sana ndio proin ya EL kutokea na nakuhakikishia JK hana ubavu wa kumdhibiti kwa sababu JK as a populist leader amebweteka na umaarufu kuwa anapendwa, hivyo ajajiamisha yoyote atakaye mpigia chapuo ndio lazima awe, lakini EL ni strategist ambaye ameshajipanga kimipango mkakati ndani ya CCM.
Pasco ahsante, EL amekamatwa pabaya. Mbio za 2015 zina makundi na makundi mengine yanafahamu wazi kuwa EL kajipanga ndani ya NEC na Chama in general. Wanachotaka kutumia ni karata ya kisiasa katika mtindo wa 'technical knockout'. Yaani wanataka EL apigwe japo barua ya onyo kama kufukuzwa itashindikana. Ikifika hapo itakuwa imemuondelea sifa tayari.

Anachokipigania EL ni kutopata hata barua ili njia iwe safi. Kwa bahati mbaya anatumia strategy mbaya ima kwa kutojua au kwa hasira. Amegeukia viongozi wa dini wamsafishe. Kwa jinsi nchi ilivyo sensitive sasa hivi anaweza kuona mambo ni rahisi, lakini wakati ukifika NEC au CC zinaweza kugawanyika!!

Inawezekana pia wapinzani wake ndani au nje ya chama wakatumia karata hiyo itakayomuumiza kisiasa. Nadhani unakumbuka jinsi RA na vyombo vyake vya habari vilivyo leta mtafaruku kwa mgombea wa Chadema kwa karata ya udini. Sio jambo jema na wala silipendi litokee lakini ndio ukweli unaojidhihiri leo hii na lazima tuuseme kama sio kuukemea.

Ndani ya Chama wapo watu 'EL Masilahi' na 'EL damu'.
EL masilahi wameshaona ugumu unaomkabili mzee, ingawa bado hawajaamua kwa matumaini kuwa mabadiliko yanaweza kujitokeza kwa maombi n.k ni wazi kuwa wameshaanza kujiunga na makundi muhimu na ni suala la muda 'utiifu' unaweza kuondoka.
Hapo ndipo safari ya EL magogoni napokuwa na mawimbi.
 
MGOGORO WA CUF

Siku za hivi karibuni kumekuwa na mgongano wa kisiasa ndani ya chama cha CUF. Chama hiki kilikuwa ni kikubwa na cha upinzani nyakati hizo. Kama nilivyoeleza katika ' damage control' hapo juu CUF haikujengwa kama chama chenye idara bali personality ya maalimu Seif. Kwamba yeye ndiye chama na chama ni yeye. Muafaka wa Zbar haukuwa na baraka za chama bali maamuzi kati ya Seif na mwenzake Karume ambaye alikuwa na baraka za chama chake.

Ni kutokana na chama kuwa personality na si organization, maalimu alipokatiwa kitumbua basi na chama kinaonekana kuzorota.
Hiyo sio sababu pekee zipo sababu nyingi ikiwemo kukosa watu wa mkakati (strategists, analysits na thinking tank) ambao wangegundua makosa walioyafanya tangu mwanzo.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo maingiliano ya kidini ni makubwa sana na hakuna mipaka ya kijiji au mikoa,ni jambo gumu sana kuanzisha chama cha kisiasa kwa mrengo wa dini na kufanikiwa. Wapo watakaosema mbona kuna kelele za udini, nawahakikishia kuwa hawa ni watu wachache sana ukilinganisha na mamilioni yenye uweledi.

Wala sina maana kuwa CUF ni chama cha kidini, lakini ni lazima wabebe dhima hiyo kwasababu kwa upande wa Tanzania bara waliachia hoja na sera zao zikatekwa na kikundi cha waganga njaa wanaojiita masheikh. Ni waganga njaa maana ni hao hao sasa wapo CCM, chama kile kile walichokilaumu kwa dhulma. Na hapa simaanishi waislam namaanisha kikundi kilichojivika joho la uislam.

Mikuatano ya CUF ikawa Ijumaa baada ya swala, na huko misikitini wakipigiwa upatu wa chama kinachopigania haki sawa. Hili ni kosa kubwa sana la kisiasa katika nchi kama Tanzania. Pengine hali isingefikia hapo endapo chama kingekuwa na wana mkakati , lakini haikuwa hivyo, chama kilikuwa Seif na Seif ndio chama bila Seif hakuna chama.

Kosa lingine ambalo tuliwahi kulisema ni CUF kujiunga na serikali ya mseto. CCM ni chama kikongwe na uwezekano wa CUF kumezwa lilikuwa jambo la wazi. Wapo wanaosema GNU imeleta muafaka wa amani visiwani, hilo ni kweli lakini ni kwa muda mfupi tu. Hakuna maendeleo yasiyotokana na mawazo mbadala na kwa kujiunga na CCM chama cha CUF kilichoundwa na kutetewa kwa gharama kubwa kimefikia ukingoni. Haya pia ni matokeo ya kuwa na mtu na sio chama.

Haya tunayoyaona sasa ni matokeo ya wana CUF kutambua kuwa maalim Seif hakuwa anapigania maslahi ya umma bali kitumbua chake. Wanaopinga sasa ni wale waliominywa muda mrefu na sasa wanaona hawana cha kupoteza tena liwalo na liwe.

Ni makosa kusema CCM imeua CUF, ukweli ni kuwa CUF imejimaliza yenyewe kwa kuwa taasisi binafsi inayoongozwa na mtu na sio chama kama ilivyokuwa NCCR, TLP n.k.

Vyama kama Chadema vinapaswa kujifunza kutokana na makosa ya watangulizi katika vyama hivi vinginevyo historia itajirudia.
CUF ndiyo imefikia ukingoni na ni suala la muda itatoweka katika historia. Chama cha kisiasa kinaongozwa kwa makakati, tahmini, propaganda na kujitathmini kama organization inayoweza kusimama yenyewe bila jina la mtu au watu.
 
Asante sana Nguruvi3, hii ndiyo naiita darasa na siyo yale ya Mohamed Said aka FaizaFoxy aka Topical - huku hawakanyagi katu.. Ni bahati mbaya wengine muda una matatizo na hivyo kushindwa kuchangia mada muhimu kama hizi. Hata hivyo endelea ndugu yangu, kwa namna hii unawaamsha wengi mimi nikiwa mojawapo - asante sana.
 
KAFULILA NA UTETEZI

Sakata la mbunge wa Kigoma kwa tiketi ya NCCR linazidi kupamba moto nje ya chama chake.Wamejitokeza watetezi wa Kafulila kwa kutumia ngao ya Ujana. Hoja wanaoijenga ni kuwa hatua dhidi ya Kafulila ni matokeo ya wazee wasiopenda vijana. Ima watetezi wamejenga hoja kuwa Kafulila ni mbunge na kijana machachari kwahiyo kumweka pembeni ni kurozotesha demokarasia nchini.

Hoja ya Kafulila haiwezi kuangaliwa kwa wepesi na kuundiwa dhana bila kuangalia historia yake na masahibu yanayomsibu.
Kafulila aliondoka mwenyewe Chadema. Kinyume na matarajio ya wengi, Davidi alitoa hoja nzito dhidi ya chama na madai yanayoitafuna Chadema kisiasa hadi leo. Alisema chama hicho ni cha kikabila na kinaongozwa na ukoo.
Hata pale alipotakiwa atoe ushahidi wa madai yake hakuweza kufanya hivyo.

Chanzo cha sakata lake Chadema kinahusishwa na Mbunge Zitto ambaye alikuwa katika ugomvi na Mwenyekiti wake Mbowe kuhusu uchaguzi. Kuna habari kuwa Zitto alikuwa anasaidiwa na kafulila na wenzake kutoka Kigoma. Ni coallition hiyo ya kimkoa ndiyo ilimgharimu Kafulila nafasi ya uongozi. Badala ya kuwa mvumilivu alikimbia NCCR ili apate cheo na fursa ya kugombea ubunge, fursa ambayo angeipata akiwa Chadema. Kauli yake haikuonyesha ukomavu wa kisiasa bali hasira za kutaka kuimaliza Chadema.

Hadi hapo hatukuelewa kama alikuwa mwana Chadema kwa kufuata sera au nafasi yake kisiasa.
Ingewezekana Kafulila kusema ameondoka Chadema kwa kutofautiana na uongozi ingawa anakubali sera za Chama.
Kafulila hakuona hilo na akajikita katika siasa za mwaga unga namwaga ugali.

Yaliyomkuta NCCR ni yale yale ya kutokuwa na imani na uongozi. Safari hii kafulila aliunda kundi lake likiwa na watu wa mkoa wake kama ilivyokuwa Chadema. Ni wazi kuwa Kafulila anapenda siasa za mkoa zaidi kuliko kuwa na coallition ya kitaifa. Mara ya pili anawatumia wajumbe wa mkoa wake kuleta mtafaruku. Nasema mtafaruku kwasababu hakuwa na political strategy.

Ni haki ya kafulila kuhoji uongozi wa Chama kama haridhiki nao. Naamini hiyo ndiyo demokrasia tunayoitaka na kwa hilo hana kosa. Kafulila alifanya hivyo kama kijana,mwananchi, mwanachama na kiongozi. Kwahiyo dhana ya kuwa alifanya hivyo kwa vile ni kijana ni dhana isiyo na mashiko inayolenga kumjengea kinga kwa kutumia ujana kama ngao. Hii ni filosofia ya ajabu inayoanza kushamiri nchini. Kila vijana wanapofanya mambo yasiyofuata taratibu kinga yao ni ujana.

Kwa vile hakuwa na strategy Kafulila alianzisha 'uasi' kwa kutumia wajumbe wa kanda yake na vyombo vya habari. Alichokisahau ni kuwa siasa ni game of timing, kwamba ukifanya kosa mwenzako analitumia kukumaliza. Ndicho kinamsibu sasa.
Mwenyekeiti Mbatia alikuwa na taarifa zote na akaitisha mkutano wa kupiga kura ya maoni. Hapo alikuwa anajenga uhalali wake kisiasa. Baada ya kura kumrejeshea imani akatumia hoja ya kafulila kuongea na vyombo vya habari nje ya utaratibu wa chama.

Ni kweli lazima iwepo nidhamu ya kuendesha chama. Chama hakiongozwi na magazeti bali kanuni na sheria. Kafulila alikuwa na nafasi ya kutumia vikao halali kuleta hoja ya ke ya kutokuwa na imani. Hakuna tatizo kwa hilo na hakika ndiyo demokrasia ya kweli. David akaamua kutumia uasi kama ule aliotaka kuuleta Chadema ili kukwea ngazi ya uongozi. Huu ni ukosefu wa maarifa wa kiwango cha hali ya juu.

Kinachoshangaza ni kusikia eti hakufukuzwa Chadema na Chadema inamkaribisha. Kauli hiyo inatolewa na mtu wa Kanda yake ili kumrudisha kundini. Hatujasikia Zitto akimtaka Kafulila kufuta kauli zake kwanza pengine kwa kuamini zilikuwa halali na za kweli.
Chadema wanayo kazi kubwa ya kutathmini uwepo wa Kafulila ndani ya chama na mustakabali wake kisiasa.

Chadema ina viongozi vijana wengi wenye akili na maarifa na hivyo kudhani uwepo wa Kafulila asiyekubaliana na taratibu za chama na asiyeamini sera bali masilahi yake utaleta mabadiliko ni kujichimbia kaburi. Kaburi kama lile la CUF lililoamini presonality na sio organization. Kitakuwa kituko kwa Kafulila kufunguliwa milango Chadema labda kama atatoka hadharani na kumeza matapishi yake.

Kwa mtu mwenye ndoto za kiungozi kama David, ni lazima akae chini na kujitathmini kama kweli anafuata misingi ya demokrasia na maarifa ya kisiasa. Ni lazima umma uelewe kafulila anasimamia demokraisa gani asiyoweza kuitumia hata pale anapokuwa na haki.
Ni lazima sasa tujue tofauti kati ya viongozi wa siasa wenye kufuata sera na wale wanaotengeneza ulaji wao.

Kwa historia na mambo yanayomkabili Kafulila, nadiriki kusema huyu si kiongozi wa kutumainiwa na taifa, ni mtafuataji anayetaka kuitumia siasa. Kafulila ni hatari kwasababu anaamini ushirika wa kimkoa zaidi na si taifa. Kwa kuunda coallition za uasi ndani ya vyama vya siasa David hapaswi kupewa nafasi katika siasa za nchi hii. Huyu atatengeneza makundi ya kikanda kimkoa,kiwailaya na kikabila. Anazo mbegu hizo zinasubiri mvua ichanue. Kafulila haamini itikadi za kisiasa na taratibu bali uasi ili afike kileleni.

kumkingia kifua kwa jina la ujana na demokrasia ni kutengeneza viongozi wabovu.
Mwacheni kafulia avune alichopanda, ujana na demokrasia havitamvua aibu anayoipata. Tuambizane ukweli na tusiuhadae umma.
 
Mkuu Nguruvi3, asante sana kwa maneno mazito hapo juu............ni kweli kijana kadhihirika kuwa ana tabia mbaya kisiasa.......
 
KIKWETE NA USANII WA UONGOZI

Nimekumbuka baadhi ya visa kutoka nchi za wenzetu halafu nikaoanisha na uongozi wa nchi hii nikabaki najiuliza, hivi Watanzania tumelogwa, ni mazezeta au tuna IQ ndogo?

Scooter Libby na Carl Rove wa chama cha Republican marekani ndio wanojulikana kama 'archtectors' waliomwingiza George Bush white house na kumrudisha mara ya pili. Ghafla ikazuka kashfa ya CIA ku-leak na mmoja wa watuhumiwa alikuwa Libby. Sheria ikachukua Mkondo wake na Bush akaacha natural justice kwa rafiki yake itendeke.

Obama alimkaribisha waziri mkuu wa India katika state banguet. Mkuu wa Itifika wa white alikuwa miss Rice ambaye ni kipenzi cha Obama na Michelle toka Chicago. Bahati mbaya wakatokea wazamiaji wawili katika sherehe hiyo. Ikawa ni kashfa kubwa ikizingatiwa usalama wa rais na white house kwa ujumla.

Uchunguzi ukafanyika na matokeo yakaonyesha Miss Rice hakuwa na mkono katika kashfa ingawa yote yametokea chini ya uongozi wake. Akatoke Senator mmoja na kutaka kufikisha hoja binafsi juu ya usalama wa Rais.
Whitehouse ikaona hilo ni balaa na kabla ya hoja Miss Rice akalazimika kujiuzulu.

Mama Thatcher alipokuwa anabinafsisha kila kitu chama chake cha Wahafidhina kikamuita na kumtaka aachie ngazi.
Kutokana na mauza uza ya Iraq chama cha Labour kikamwambia Tonny Blair aachie ngazi licha ya kuwa kiongozi bora katika nchi hiyo kwa miaka mingi sana.

Fidel Castro baada ya kufikishiwa malalamiko dhidi ya mshirika wake, aliruhusu sheria ichukue mkondo. Rafiki yake alipotiwa hatiani na kuhukumiwa kifo Castro alimwambia ' Sina jinsi ya kukusaidia kwasababu umesaliti mapinduzi'.

Mzee Mtei alipotofautiana na Nyerere kisera, Nyerere alimwambia aachie ngazi.
Mifano ipo mingi sana ya jinsi viongozi wanaopewa dhamana baadhi yao kukutana na mambo yanayokinzana na masilahi, ushirika au urafiki na viongozi wenzao,jinsi wanavyochukua hatua za kulinusuru taifa na si mtu.

Bunge letu liliwahi kutaka seriakli imwajishe Dr Hosea kwa kuudanganya umma mchana kweupe akishirikiana na akina Mwanyika.
Mamlaka iliyopaswa kutekeleza hayo ni Rais Kikwete. Ghafla tukasikia Mwanyika amestaafu na kuondoka na masilahi yake na tunaendelea kumhudumia licha ya uchafu aliyoufanya unaoliumiza taifa hadi leo.
Hosea kaachwa kuendelea kulidanganya taifa na sasa PCCB inaonekana uchafu mbele ya jamii.
Hawa wote ni washirika wakuu wa JMK. Heri taifa liangamie lakini wao walindwe.

Mwenyezi mungu kaibua tena ya Jairo na Luhanjo. Kama ilivyokuwa kwa Hosea na Mwanyika nao pia wameruhusiwa wastaafu ili tuendelee kuwahudumia licha ya uchafu walioliachia taifa. Mamlaka ni ile ile JMK.
Nao pia ni maswahiba kama EL na AC.

Yote haya Kikwete anayafanya mchana kweupe bila haya wala woga akijua kuwa Watanzania hawana 'nyimbo' ni watu wa hewala mzee. Hata wale tuliowapa sauti nao wameufiata Dodoma ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari.
Huku mitaani sisi tunabaki tukitaja majina ya nani amrithi yupi. Kwa maana kuwa Kikwete atarithiwa na Kikwete na hapo ndipo taifa lilipo kwama.

Tunabaki tukisema vijana wabunge wanahujumiwa lakini yanapokuja masuala mkubwa kama haya ya urafiki kazini ni wabunge hao vijana wameufiata.

Kama hatutakuwa na utaratibu wa kuangalia viongozi kwa upana na si uchama basi kila siku tutakuwa na akina Kikwete, Jairo, Luhanjo na Mwanyika.

Kinachouma zaidi ni limbwata ambalo Watanzania wamelishwa kuamini kuwa rais atatoka CCM na si kwingineko.
Kwanini watu wamfikirie kiongozi kwasababu alifanya jambo moja fulani na si historia na uadilifu wake? Hivi Membe na EL wanaotajwa kila siku watakuja na lipi jipya ili hali wao ni sehemu ya 'najisi' inayolinjaisi taifa kila siku?

Kwanini watu wasifikirie kuwa kiongozi anaweza kutoka Chadema, TLP au NCCR au mwantaaluma hadi kufikia mahali pa kuwataja watu wasioweza hata kumkemea rais anayeliumiza taifa kwa uswahiba kiais hiki?

Kama hatutabadili 'vetting' system na mind set tuliyo nayo basi mradi huu wa kuiba na kustaafu utakuwa sustainable.

Ttauangalia usanii huu hadi lini!
 
NCHI KUIGA JAMBO JEMA KUNA UBAYA?
Marekani wapo katika mchakato wa uchaguzi November mwaka huu. Mchakato mkubwa upo kwa wagombea wa Republican wanaowania kumuondoa Obama white house. Wapo walioanza na hawapo tena na wengine wapo hali zao hazina matumaini.
Kwa sasa wamebaki Mitt Romney, R.Santorum, na spika wa zamani Ginrich. Wengine ni Gavana Perry, M. Buchmann na Ron Paul amabao matumaini yao ni hafifu. Hata hivyo kwa siasa za Marekani lolote laweza kutokea

Tofauti na sisi, wagombea wanakuwa na 'plan' za sera zao zikiwa katika itikadi ya vyama vyao. Mfano itikadi ya wahafidhina(conservatives) ni serikali ndogo na usimamizi kidogo wa huduma wakiacha soko huria litawale.
Democrat wao wanaamini katika huduma za jamii kwa umma na usimamizi wa serikali wakitilia mkazo 'regulations'.
Hayo ni kwa uchache sana na ni mifano tu.

Ugumu wa Republican upo katika mambo mawaili.
Kwanza wamegawanyika kukiwa na kile kitawi kinachojulikana kama Tea Party. Hawa ni wahafidhina wenye msimamo mkali wanaoona ubepari wa marekani umeingiliwa. Wao wanaamini 'survival for the fittest'.

Wanapinga sana sera za Obama hasa kuhusu health care. Tea party ndio walioongeza nguvu katika uchaguzi wa kati ya muhula 'mid term election' na Obama kupoteza umiliki wa bunge la chini 'congress'. Hata hivyo wagombea wao kama Sarah Palin hawamo katika kinyanga'nyro na inawapa tabu sana kutambua miongoni mwa wagombea nani anashabihiana na sera zao.
Hili linawagawa sana Republican.

Pili, moja ya nguvu za Republican ni security. Wao wanaamini kuwa wanauwezo mzuri wa kulilinda taifa lao kufuatia historia.
Ni watu wa piga piga kama alivyokuwa Bush na ubabe umekuwa ukiwasadia sana nyakati hizo dunia haijabadilka.
Kwa hili wana wakati mgumu kwasababu Obama amemaliza vita kule Iraq kama alivyoahidi na anaendelea na mipango ya kumaliza Afghanistan. Kubwa zaidi ni kumuua Osama bin Laden ambaye Clinton na Bush walimshindwa.
Hoja ya Republican inafia hapo na sasa wamegeukia suala la uchumi.

Uchumi nao unawapa taabu maana matatizo yalianzia kwao wakiwa na umiliki wa Ikulu na moja ya mabunge mawili. Hata hivyo wanachokifanya ni kuelekeza tuhuma zao kwa Obama kwasababu marekani Rais aliyeko madarakani ndiye anabeba dhamana ya aliyoyakuta. Hakuna excuse kwasababu Rais alichaguliwa ku fix problem na si kujifunza kama sisi ambapo Rais anakiri miaka 5 ya mwanzo alikuwa mafunzoni.

Obama ana hoja nyingine ya kubadili siasa za nje za Marekani kuwa za kidiplomasia na kwa kiasi fulani kurudisha ile heshima iliyoonekana kutoweka kutokana na ubabe. Na sifa mojawapo ni jinsi alivyoshughulikia mgogoro wa mashariki ya kati hasa Libya na Egypty.

Hoja yangu ni kuwa ukifuatilia midahalo na maswali kwa wagombea, utaona wanaongelea matatizo ya nchi kwa ujumla na jinsi gani watayashughulikia. Hapa ndipo tofauti iliyopo na sisi kwasababu wagombea wetu wanapita wakihubiri matatizo moja moja kama ahadi za ujenzi wa bara bara na shule n.k. Kwa Marekani Rais anaangalia nchi kwa ujumla wake na hayo ya madaraja na bara bara wahusika wakubwa ni serikali za majimbo labda kwa mambo yalipo ndani ya federal governement.

Nikifika hapo najiuliza hivi kwanini na sisi tusiwe na mfumo wa majimbo ili kuhakikisha kuwa watu wa jimbo fulani wanajiletea maendeleo kwa jitihada na mipango yao. Matahalani matatizo ya jimbo la kasakazini (Tanga, Arusha, Kilimanjaro na Manayara) hayafanani na yale ya nyanda za kusini (Mbeya, Iringa, Ruvuma). Sasa kwanini kila jimbo lisiamue kufanya kile kinacholingana na mazingira yao hadi tuwafanye 'uniform system' tena ikifanya kazi kwa maelekezo kutoka Dar es salaam.

Pili, kwanini jimbo moja lichangie maendeleo ya lingine na isiwe mapato na matumizi yafanywe jimboni. Sina maana kusiwepo na mchango wa seriakli kuu, nina maana kila jimbo lipewe 'quarter' katika hazina kuu lakini liwe na hazina yake, bunge lao n.k. isipokuwa kwa mambo ya kitaifa kama ulinzi na mahusiano ya kimataifa.

Hili lingesaidia tuwe na viongozi wanaoliangalia taifa na sio wanaopita na kuuza sera za kununua mabomba ya maji, kujenga vyoo vya shule n.k. Haiingii akilini kwanini mgombea asiwe na focus ya mambo ya kitaifa bali ashughulikie ununuzi wa mabomba jambo ambalo lingefanywa na halmashauri au serikali za majimbo. Pengine ndiyo maana hatuoni sera zao kwasababu mfumo wetu umewapa nafasi ya kuzungumzia ujenzi wa madarasa kwa kiongozi anayetegemewa kuliongoza taifa la watu milioni 40.

Chadema wana sera za majimbo, kinachonishangaza ni kuona sera hizo zimebaki katika makaratasi. Japo hawajashika dola lau basi wangeongoza kwa mafano. Mfumo wa chama haufanani na sera zao na hapa ndipo najiuliza, je wapo serious na hili?
Nasema Chadema kwasababu CCM tumeshawaona kwa miaka 50 na sitarajii jipya zaidi ya the same old story.

Nimalizie kwa kusema, hivi kuna kosa gani kwa sisi kama nchi kuiga mema kutoka kwa wenzetu na kuyafanya katika hali inayolingana na mazingira yetu? Kwanini tusiwe na mfumo wa vyama unaoruhusu itikadi za vyama lakini pia mgombea atueleze atafanya nini tofauti akiwa katika itikadi ya chama chake kama wanavyofanya Marekani sasa? Hivi kwanini mgombea apite akaiahidi madaraja na bara bara bila kutuainishia wapi atapata pesa. Kwanini hatuhoji sera za mgombea kuhusu elimu, afya na mambo ya jamii badala ya kusikiliza shida za mtaa mmoja au kata moja?

Kwanini vyama vya siasa havishindanishi wagombea kama tunavyoona wenzetu wanavyofanya? Hivi ni kweli kuwa wajumbe 500 wa mkuatano mkuu wa chama fulani wanaokaa siku moja wanaweza kufanya vetting ya kutosha kutuwekea mgombea makini kama wanavyofanya wenzetu.
Kwanini vyama hasa vya upinzani visiwe na mfumo wa ushindanishi ndani ya chama kwanza ili kutuwekea wagombea makini. Je, utaratibu wa CCM ndiyo formula ya siasa za nchi yetu na hatuwezi kufikiri mbadala hata kwa kuangalia wenzetu kama hatuwezi kubuni wenyewe.
Kwanini tusifikirie mfumo wa majimbo utakaoleta ushindani wa kisiasa na kiuchumi kwa jamii?

Hebu tusemezane kwa hili.
 
NYERERE: HOJA ZISIZOJIBIWA KWA HOJA
Sote tunafahamu aina ya mijadala inayoendelea kuhusu nyakati za mwalimu, mafanikio na kushindwa kwake. Tumekuwa na makundi mawili, la kwanza likimtuhumu mwalimu kama chanzo cha matatizo yetu tuliyoyananyo na la pili likajaribu kutetea hoja dhidi ya mwalimu

Ikumbukwe kuwa mwalimu ametawala kwa kipindi cha miaka 24,na waliomfuata miaka 26 kwa ujumla wao.Katika mambo aliyoyaacha mwl ni pamoja na miundo mbinu na viwanda tukiachilia mbali huduma za jamii kama afya na elimu.Haya yote tumeyaona na kuyachambua katkia mada ya mzee mwanakijiji iliyohusu mpango wa maendeleo wa mwak 1963.

Katika mada hiyo wachache sana wanaomtuhumu walijitokeza kujibu hoja na hakika si kujibu hoja bali kusema Nyerere ‘amefeli' au ujamaa umeshindwa. Baadhi walipohoji hoja za namna gani mwalimu kafeli, hapakuwa na jibu bali kafeli tu.

Tulipohoji ujamaa umeshindwaje na nini mbadala wake ktika miaka 26 ikiwa ni pamoja na miak 10 tangu afariki hakuna jibu. Kwa ufupi hoja za kufeli kwa mwalimu au ujamaa kushindwa hazijajibiwa kwa ukamilifu bali hisia zinzochagizwa na chuki ima za kiiamini au itikadi za kisiasa

Kwa vyovyte vile,lazima tukubaliane kuwa mwl alikuwa mwanadamu na hakika hakuwa mtimilifu kama tulivyo viumbe wote.
Pengine kuna hoja ya msingi kwa wale wenye kushadidia mwalimu kushindwa au kufeli, kwa bahati mbaya hoja zao hazijengwi kimantiki zaidi ya chuki tu. Yaweza kuwa kuna waliolishwa jambo na kutotaka kuhoji, hoja muhimu kwao ni mwl kufeli.

Hata kama mwalimu kafeli ni haki akapewa daraja la kufeli, kwani hatutarajii alifeli o% au alifaulu 100%.
Endapo alipata 51% si haki kusema alifeli na kama ni chini ya hapo basi tuambiwe ni kwa kiwango gani.
Kama hatuwezi kutoa viwango basi tumlinganishe mwl na waliomfuata mmoja mmoja au kwa ujumla wao ili tuweze kutoa hukumu ya haki.

Tuliangalia kwa haraka haraka ni wazi wote waliofuata baada ya mwl hawakuja na kitu kigeni ziaidi ya yale aliyotarajia kuyafanya mwl. Si miundo mbinu, afya wala elimu. Tunapotazama mambo kadhaa tusisahau changamoto alizokuwa nazo mwl baada ya kupokea nchi kutoka kwa wakoloni.

Upo msemo wa kipimo cha uzuri ni ubaya na sasa taratibu tunaanza kuona wapi tupime ili kupata ubaya au uzuri. Baada ya mwl kuondoka likapitishwa azimio la Zbar lililohitimisha kifo cha ujamaa na kukaribisha mfumo wa ubepari.
Mfumo unaoaminika ni mzuri tena kwa jina bandia la soko huria.
Ni mfumo huo huo unapigiwa kelele kule ulikotoka kama tunavyoona occupy wall street n.k.
Ni mfumo huo ndio uliolazmisha viongozi kuwa madalali wa mali zetu kwa kisingizio cha kuboresha.

Hapa ndipo niliposukumwa na mwandishi Florence Mugarula wa gazeti la The citizen aliyetoa makala yake kuhusu taarifa ya ubinafsishaji wa viwanda na kile kilichotokea.

Tuiangalie taarifa ya ubinafishaji wa viwanda na matokeo yake halafu turudi kwenye meza ya majadiliano ili tuweze kutoa hukumu ya nini viongozi wetu wamefanya kuanzia mwl, Mwinyi, Mkapa na Kikwete halafu tujiulize wapi mwl alifeli, na kama alifeli' alifeli kwa kiwango gani ili tulinganishe na matokeo ya waliomfuata.

Soma sehemu inayofuata kuhusu ubinafsishaji wa viwanda, vingapi vingali hai, vingapi ni ‘marehemu' na serikali inafikiria nini kuhusu viwanda hivyo.

Tutaangalia ni kwanini mwl aliwekeza katika viwanda, faida zake za muda mfupi na mrefu na je, ubinafsishaji umekidhi haja kama ilivyotarajiwa?

Itaendelea........
 
Nianze pale nilioishia kuwa mwl alianzisha viwanda kama sehemu ya taifa kujitegemea. Nchi nyingi zinazoendelea kama Asian tigers, India, China na Brazil sehemu kubwa ya mafanikio yao ni kuwa na uwezo wa kuzalisha bidhaa zao wenyewe na ziada ya kuuza.
Hata zile nchi kubwa tajiri bado tunaziita ‘Industrialized' au nchi zenye viwanda kwa maana hiyo hiyo.

Bila kugusia umuhimu wa viwanda katika mambo ya uchumi kwa undani kama import/export na stability ya currency n.k, viwanda vina faida nyingine kijamii.
  1. Ni kutoa ajira na kuinua hali za maisha ya wananchi
  2. Ni kutoa sehemu za mafunzo kwa vijana wanaochipukia iwe katika utawala, biashara, injinia au chemical. Wale wa zamani mtakumbuka jinsi wanafunzi wa UD walivyokuwa wanapata internship na uzoefu mwingine kama sehemu ya mafunzo yao kwa kupitia viwanda kama Moproco, Textiles n.k.
  3. Kuisaidia serikali katika kutoa huduma za kijamii kama shule na afya au hata bima na matibabu kwa wafanyakazi na familia zao na hivyo kuipunguzia serikali mzigo indirectly kama sehemu ya mafao ya wafanyakazi wa viwanda.
  4. Kuongeza thamani za bidhaa hasa za kilimo hadi ngazi ya chini kabisa. Kwamba mkulima ni sehemu ya wafanyakazi wa viwanda na hujipatia mapato yake kama ilivyokuwa kwa Gineries kama zile za Mgango kule MUsoma na Shinyanga, Usindikaji wa matunda kule Korogwe, na Maziwa kule Musoma.
Orodha ni kubwa na inategemea mtu ataiangalia kwa mtazamo gani lakini tunakubaliana kuwa kuna faida zaidi ya hasara.

Nitahadharishe kuwa hata kama viwanada vyetu vilikuwa havijafikia hadhi ya viwanda vya nchi zilizoendelea, bado ilikuwa ni hatua muhimu sana kwani nchi kama India hazikuanza na viwanda vikubwa. Kwa muktadha huo nadhani tuchukulie viwanda kwa maana ya viwanda katika viwango vyetu.

Tukumbuke kuwa ujenzi wa viwanda hivyo haukutokana na misaada tu bali pia mikopo ambayo leo hii tunaendelea kuilipia hata kama Paris club ilifuata baadhi.

Mwalimu alipoomba misaada hiyo hakuwa na maana ya kugawa viwanda vya wananchi kwa rafiki zake, bali kuvifanya viwe mtaji kwa vizazi vijavyo. Deni la kulipia pengine lilionekana dogo sana ukilinganisha na faida za muda mfupi na mrefu zitokanazo.

Kwahiyo uwekezaji wake ulikuwa wa gharama na swali ni je, uwekezaji ule umeleta tija iliyokusudiwa au kutuacha na madeni?

Ikifika hapo naomba tuangalie taarifa ya The citizen hapo chini halafu tutaijadili.
Taarifa naileta kama ilivyo ili kuepeuka tafsiri inayoweza kuleta maana isiyokusudiwa.

Tuiangalie taarifa kama ifutavyo

Inaendelea......
 
Back
Top Bottom