Duru za siasa - Matukio

Makandara Mkuu wangu,

Tunashukuru sana kwa uchambuzi wako marua nimejifunza mengi sana kwenye ili pandiko lako, na pia Mkuu Nguruvi3, msichoke kutupa darsa.

JF Daima.
Mkuu wangu shukran sana na naomba tuvumiliane...Mimi huandika na makosa mengi sana kwa sababu moja kuu. Pengine niwaulize wana JF kina Maxence maana kila napoandika hoja kuna tracing huingia na mara zote znisipokharakisha ku post siwezi tena huwa inaingiwa kiasi kwamba lazima nizime PC kuislafisha na kisha kuanza upya. Hivyo, ni rahisi kuandika haraka na ku post kisha nafanya marekebisho ikisha kuwa hewani. Hapo siingiliwi kabisaaaa!

Tatizo jingine siwezi kuandika pembeni ktk word kisha ndio nirudi hapa na kunukuu nilichoandika ktk word. Nimejaribu hivyo sana na kujiona kama mwandishi wa magazeti ama mtu anayeshindwa kujadili wakati anasoma maelezo ya mtu mwingine. Hata hivyo nitajitahidi kuweka fikra zangu na mnapoona makosa jaribuni kunipa muda..
 
jmushi1,

Kwenye suala la mafuta ni vita vya kidunia Mataifa matano wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Marekani, Uingereza, Ufaransa, China, Urusi, hawa ndio wanaomiliki makampuni makubwa sana ya mafuta duniani.

Makampuni haya yanashikilia sasa soko la mafuta kutokana na mitaji yake mikubwa sana ya mafuta duniani, makampuni haya ni Petrochina, British Petroleum (BP), Royal Dutch Shell, Exxon, Texaco, Gulf, Mobil, makambuni ya Kirusi yaliyo chini ya Ikulu, Yukos, Sibneft, Lukoil, kuna Chevron, Total na mengine huunganisha mitaji ili kulikamata soko la mafuta duniani..

Mataifa ya kiarabu yanatumia mafuta yao kama silaha katika uchumi wa dunia.


Ritz,

..suala la utajiri wa mafuta vs haki za wapalestina.

..inasemekana turufu ya mwisho ya kupatikana kwa uhuru wa Zimbabwe ilikuwa ni Nigeria kutishia kutaifisha visima vya mafuta ikiwa Uingereza haitasitisha misaada yake kwa walowezi wa Zimbabwe.

..inasemekana Nigeria tangu enzi za Murtala Mohamed ilikuwa ikitoa msaada mkubwa sana kwa vyama vya ukombozi na nchi zilizokuwa mstari wa mbele wa ukombozi wa kusini mwa Afrika.

..Waarabu wanapaswa kuungana, na kutumia turufu ya utajiri wa mafuta, kushinikiza Wapalestina wapewe haki yao.
 
Ritz,

..suala la utajiri wa mafuta vs haki za wapalestina.

..inasemekana turufu ya mwisho ya kupatikana kwa uhuru wa Zimbabwe ilikuwa ni Nigeria kutishia kutaifisha visima vya mafuta ikiwa Uingereza haitasitisha misaada yake kwa walowezi wa Zimbabwe.

..inasemekana Nigeria tangu enzi za Murtala Mohamed ilikuwa ikitoa msaada mkubwa sana kwa vyama vya ukombozi na nchi zilizokuwa mstari wa mbele wa ukombozi wa kusini mwa Afrika.

..Waarabu wanapaswa kuungana, na kutumia turufu ya utajiri wa mafuta, kushinikiza Wapalestina wapewe haki yao.

JokaKuu, hili la nchi za kiarabu zenye utajiri wa mafuta kushinikiza Wapestina wapewe haki yao limeathiriwa sana na vita ya Iraq. Pengine hali ya Palestine ingekuwa na nafuu kuliko ilivyo sasa kama hii vita haikuwepo. Sadam Hussein alikuwa rafiki wa marekani kabla hajawa hasimu wao mkubwa. Vita ya Iraq na kifo chake Sadam Hussein kwanza kilitoa mwanya kwa shia majority ndani ya Iraq kushika madaraka makubwa, lakini kubwa IRAN iliibuka kama big brother fulani wa ukanda huu wa Middle East. Iran watu wake wengi ni Shia, na jirani sasa nako wengi ni shia.

Looser number moja wa huu mtafaruku anakuwa Saudi Arabia (na hata UAE). Hawa ni sunni, na kwa muda walikuwa juu (dominance), sasa wanakuwa challenged na Iran ambayo iko kwenye mkakati wake wa Nuclear. Hili la nuclear linazidi kupandisha mashetani wasaudia na marafiki zake marekani. Na hapa ndipo urafiki wa Saudia na mmarekani unazidi kuimarika kwa sababu wote wana common enemy - Iran. Marekani kwa upande mwingine na muisraeli ni kitu kimoja. Na hapa ndipo tunakuja kwa looser number mbili Palestine.

Saudia ina nafasi kubwa sana kuongoza nchi nyingine middle east ili kuisaidia palestina. Lakini vile vile Saudia na wenzake wanamuhitaji sana mmarekani kupambana na Iran. Mmarekani yuko na Israel na kuna fununu kwamba nyuma za pazia Saudia anakubaliana mambo mengi tu na Israel kupitia kwa middle man - marekani.
 
HALI YA MISRI BADO TETE

Rais Morsi alitangaza kurudishwa kwa bunge lililovunjwa na baraza la kijeshi.
Mtafaruku umeendelea baada ya mahakama kupinga agizo la Morsi na kwamba kuliita bunge ni kukaidi amri ya mhimili mwingine. Siku za nyuma tulisema Brotherhood walikaa kimya wakati wa uchaguzi bunge likivunjwa ili wa-focus katika hatua yao ya mwisho ya kuchukua utawala.

Taratibu tunaona kucha za Brotherhood zikichomoza. Ni ukweli usiopingika kuwa Brotherhood walishinda viti vya bunge na Urais. Ni ukweli kuwa baraza la kijeshi chini ya Tantawi halikupaswa kuvunja bunge halali lililochaguliwa na wananchi.

Tunajua kuwa hata uapishwaji wa Morsi ulifanyika mara mbili, moja ikiwa ni mbele ya jengo la mahakama linaloelekeana na Hospitali maarufu ya kijeshi. Hospitali hiyo ndipo alipotangazwa kufariki Anwar Sadat, ndiyo hospitali aliyofia Shah wa Iran na ndiyo anapotibiwa Hosni Mubarak.

Baraza la kijeshi lilitaka Morsi aelewe kuwa kuna mihili mingi ya kikatiba na mingine isiyo rasmi.
Msuguano wa Mhakama, serikali, bunge na baraza la kijeshi unaonekana kupamba moto.
Hili ndilo changamoto tulilosema siku za awali kuwa linamkabili Morsi.

Jambo la kushangaza ni kuwa nchi za magharibi hazijalikemea jeshi kwa kuingilia serikali iliyochaguliwa kihalali.
Huu ni ushahidi kuwa jeshi linaungwa mkono kama lilivyoungwa mkono wakati wa kumuondoa Mubarak.
Bado nchi za magharibi hazijaridhika na uchaguzi halali wa Misri. Wanawajua Brotherhood vema na hakika hawana usingizi

Siku za karibuni tutashuhudia makundi Tahariri Square kumuunga mkono Morsi, na mengine kuunga mkono Jeshi.
Jeshi halitaki kuachia 'utamu' kwasababu linapata msaada wa dola Bilioni 10 kutoka marekani kila mwaka. Hayo ni sehemu ya mkataba wa Camp David.

Uwezekano wa Morsi kupata 'ajali' ya kisiasa ni mkubwa sana hasa kwa jinsi jeshi lilivyochukia kuporwa madaraka.
Ukitaka kujua jinsi jeshi linavyoendesha mambo kichini chini ni pale Mubarak akiwa mfungwa kama wengine bado anatibiwa katika Hospitali ya jeshi. Muda wote wa mashataka alikuwa katika Hospitali ya kijeshi.

Hali ya Misri bado haijatengemaa na tutaendelea kujadili kadri itakavyojuzu

Tusemezane
Nguruvi3

Muslim Brotherhood watasuguana sana na Jeshi.Kilichopo hapa Jeshi linataka kupindua matakwa ya Umma(coup civillien)...wanaandaa sasa precarious situation.Hata kama ningekuwa Morsi nisingekubali ufedhuli huu wa Jeshi

The Egyptian people have spoken and whether we like it or not,its their choice.They first gave the Muslim Brotherhood an overwhelming majority in the legislature and despite all the attempts of the military to impose Shafiq,the will of the people has prevailed.

The option was pretty clear for the egyptian people,a vote for Shafiq was undoubtedly a vote for Mubarak who Shafiq describes as his role model.A vote for Shafiq is a vote that signals that the revolution achieved nothing while a vote for Morsi is a vote for progress(at least in the eye of the average revolutionist).

The Muslim Brotherhood were classified as terrorist by America because of their stance against Mubarak who was their ally.The Muslim Brotherhood risked their lives fighting Mubarak and took the forefront in the revolution,and now the people of Egypt want them to build the bridge to the future and it is my hope that they can.It is my hope that Morsi honours with some sort of reservations in the interest of Egyptians the camp David accord Mubarak gave his life for but i hope he stops assisting in the blockade of Gaza and lets in humanitarian efforts to the repressed people.

True,weapons might be smuggled in but refusing Palestinians access to weapons while Israel receives stockpiles is similar to the Bosnia/Serbia crisis in which the UN and NATO had to lift the arms embargo to allow Bosnia access to weapons.

Pia the United States atatumia kila gharama akishindwa kumshawishi Morsi na Brothehood kujaribu kudhoofisha utawala wake ili akataliwe na umma.Marekani ina hofu juu ya mkataba wa Camp David.Sasa Muslim Brotherhood watabadili sana policy ya US in Middle East and possibly EU Policy uarabuni.

Hamas wanapata nguvu kwa sababu sasa wanapata mshirika.Huko Saudi Arabia Nguvu inapungua kwani serikali Kibaraka nayo imeanza kutikiswa

Nilifurahi sana kuona Muslim Brotherhood wanashinda uchaguzi Egypt na hasa alipowekwa Morsi kuwa mgombea.Mwanzoni kabisa mwaka jana nilikuwa naona hofu kubwa kwa mtu kama El Baradei kuongoza Muslim Brotherhood.He's so soft

Sasa Obama akichaguliwa tena kipindi cha pili atapata kazi nzito sana hapo Middle East.Containment policy and Us policy of Regime change in middle East should now be reviewd
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Joka kuu, FJM na Ritz,
Tatizo lililopo katika Arab world ni kubwa sana na linachangiwa pamoja na mengine, historia ya kuhasimiana na kutowekeza katika elimu.
Ni rahisi sana kuwagawa waarabu katika misingi ya Ushia, Usuni, sufiism kuliko kuwaunganisha kwa misingi ya dini yao.

Marekani walipovamia Iraq jambo la kwanza lilikuwa kuwagawa watu wake. Ilichomekea hoja kuwa Sunni walitawala na kuwanyanyasa Shia wenye utajiri wa mafuta. Kuwachochoea Kurds kuwa wao ni raia wa daraja la pili.
Yote hayo ilikuwa kuvunja nguvu ya umoja ili wapate mradi wao.

Kilichofuata ni kutokea kwa akina Mortada al Sadra wa Shia na upande mwingine Baath Party cha Sadam. Marekani walichokifanya ni kutumia udhaifu uliokuwepo na si kuweka udhaifu. Tumeona yaliyotokea na nchi ilivyoparaganyika.

Ni kwa mwendelezo huo tumeona uasi Bahrain na UAE kwa ujumla, ikitikisa hata falme kubwa ya Saudi Arabia.
Hakuna sababu kwa nchi kama Saudia ambayo ni kitovu cha dini kulimbikiza masilaha ya hatari na nguvu sana.
Saudia ukiacha habari nyingine haiwezi kushambuliwa na mtu mwingine wa eneo la mashariki ya kati, sasa silaha za kisasa za nini? Jibu ni kuwa hakuna kuaminiana kunakotokana na tofauti ninazoweza kusema hazina mshiko hata kidogo.

Nchi za eneo hilo zilizembea kuwekeza katika elimu na kutegemea teknolojia kutoka magaharibi.
Vifaa vyote vya uchimbaji wa mafuta vinatoka magharibi ikiwa ni pamoja na survey ya maeneo ya mafuta na hata uendeshaji wa visima.Silaha zote zinatoka magharibi nk.nk.
Ukichangaya factors nilizozitaja ni vigumu kwa mataifa ya uarabuni kuungana na kutumia mafuta kuwasaidia Wapalestina

Hawawezi kwasababu hawana control ya region isipokuwa kufanyia kazi maamuzi ya magharibi.
Wataweza tu kuwasaidia pale watakapoweka tofauti zao pembeni kwanza na kuwekeza katika elimu na teknolojia.

Ben,
Jeshi la Misri linaungwa mkono na Marekani. Ukweli ni kuwa Marekani haikutaka Mubarak aondoke na ilitaka mtoto wake awe mrithi. Misri ina ushawishi mkubwa sana wa siasa za mashariki ya kati.
Hotuba ya Obama aliyoitoa Cairo ilikuwa ni kuthamini ushawishi wa Misri katika Arab World. Tofauti na nchi nyingine Misri wamewekeza sana katika elimu na hivyo kuwa na upper hand kati decision nyingi za eneo la mashariki ya kati.

Wasi wasi wa Marekani ni kuhusu Brotherhood. Marekani hawagopi Brotherhood kwa lolote lile bali weledi, elimu na maarifa yao. Wanajua kuwa Brotherhood ikifanikiwa itakuwa ni 'template' ya middle East katika siasa za region and international.Lolote ni lazima lifanyike kuwarudisha chini na hata kuwapoteza katika medani za siasa.

Tunakumbuka chama cha FIS cha Algeria kilishinda uchaguzi halali uliothibitishwa na mwakilishi wa Marekani. Kilichofuata tunakijua sote. Tunakumbuka chama cha Hamas kilishinda uchaguzi uliothibitishwa na Jimmy Carter kuwa ni halali kabisa.
Kilichofuata ni kuweka masharti nje ya sanduku la kura na kuwasadia FATAH kubaki Ramallh huku Ismael Haniya akiwa na Gaza. Hayo ndiyo yanayotokea kwa Brotherhood sasa kwamba uwepo mtafaruku ili wasiweze kuleta mafanikio au kutekeleza kile kilichokuwepo katika ilani yao ya uchaguzi.

Kama tulivyosema awali kwa nchi kama Misri yenye uelewa na waelewa zaidi ya wengine mashariki ya kati kazi ya CIA haitakuwa rahisi. Jeshi halina sababu ya kuwa na mkono wa utawala bali ni kwa shinikizo tu la nchi za nje.

Morsi anapaswa ahakikishe kuwa mhimili wa bunge unarudi na unakuwa na nguvu zake kama bunge.
Ahakikishe kuwa mahakama haiendeshwi kwa influency ya jeshi kama tulivyoona katika kesi ya Mubarak na watoto wake.
Hapo ndipo aanze kutengua nguvu za jeshi katika utawala.
Haitakuwa rahisi kwasababu anaweza kujikuta akifuata njia ya Anwar Sadat lakini ndiyo silaha aliyo nayo kwa sasa

Kwa mwenendo wa Marekani hadi sasa naweza kusema uwezekano wa Obama kurudi madarakani ni asilimia 40.
Hili nalo tutaijadili kutokana na habari tulizo nazo kufuatilia harakati za uchaguzi zinazoendelea.
Kwa kuanzia tu ushindi wa Brotherhood umeanza kumuumiza Obama katika kampeni za uchaguzi.

Niseme tu kuwa Rais ajaye iwe Obama au la atakuwa na tatizo kubwa mashariki ya kati.
Ni lazima Israel ilindwe na haiwezi kulindwa Misri ikiwa out of control. Mkataba wa Camp David unaweza kutetereka.
Kumbuka ni Brotherhood waliomuua Anwar Sadat kwa saababu ya Camp David. Sasa nani anaweza kusema Brotherhood wamebadili mtazamo. Ingawa Morsi anaonekana Moderate lakini Brotherhood ni organization siyo figure!

Msuaguano wa mashariki ya kati sasa ni mkubwa sana kuliko ilivyokuwa na nchi za Magaharibi zina hofu sana.
Hali ya Arab world bado ni tete sana na yapo mengi yanayokuja katika medani za kisiasa.
 
Ni suala la kuomba Mungu jukwaa hili liendelee hivi hivi bila kuvamiwa na vijana wetu wasiokuwa na hoja bali viroja. Mpaka sasa nimekuwa na utaratibu maalumu wa kusoma nondo toka Duru za Siasa kabla sijatembelea majukwaa mengine natumaini Mods watalilinda kwa nguvu zote iwapo uvamizi utatokea.

Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wanajamvi wafuatao Nguruvi3 Mkandara jmushi1 FJM JokaKuu Jasusi chama Kakalende Ogah Ben Saanane na Ritz Michango yenu mbali mbali kupitia thread hii imekuwa darsa kubwa sana hakika mwanzisha thread Mkuu Nguruvi3 katurejesha miaka ya nyuma wakati najiunga JF nilikuwa nikipata darsa la uhakika hali ilikuja kubadilika miaka ya karibuni wanajamvi badala ya kujadili hoja za maana wakajikita kushabikia vyama vya siasa misamiati mingi isiyobeba ujumbe wa maana ikazaliwa eg Gwanda, Gamba, Masaburi na nk. Hadhi ya JF ikaanza kushuka kwa kasi ya ajabu wanajamvi mahiri kama hao niliwataja na wengine wengi wakatimua mbio wakakosa sehemu stahiki ya kujadiliana na waTanzania wenzao bahati nzuri kupitia uzi huu naanza kuona dalili nzuri. Mjadala unakwenda vizuri lugha ya heshima na kuheshimiana miongoni mwa wanajamvi inatawala, wanajamvi wajuzi wa masuala mbali mbali wanajitolea kutoa darsa bila choyo.

Mungu ibariki JF,Mungu ibariki Tanzania.
 
Last edited by a moderator:
Duru za siasa,

Bado tupo kwenye siasa za Mashariki ya Kati huku tukitazama Misri kama muhmili mkubwa na mwenye nguvu Mashariki ya Kati, tuangalie Misri tokea enzi za Rais Gamal Abdel Nasser hadi za Rais Anwar Sadat na hatimaye Rais Hosni Mubaraka, kila enzi katika hizo iliifanya nchi ya Misri kuwa na sura ya aina yake.

Wakati wa Nasser, pale nchi nyingi za kiafrika zilipokuwa bado zinatawaliwa na wakoloni, Waafrika waliuona mjini Cairo ni mji ulio mstari wa mbele wa katika mapambano dhidi ya ukoloni, Takriban nusu ya vyama vya ukombozi vya kiafrika vya miaka ya 1960 vilifungua ofisi zao mjini Cairo, kulikuepo na wengine pia hasa kutoka nchi za Kiarabu Yasser Arafat, alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Cairo, aliwachochea Wapalestina wenzake wapiganie haki zao.

Na Cairo ndiko alikokimbilia Saddam Hussein, akiwa kijana kabisa baada ya kuuwa kwa mara ya kwanza alipompiga risasi mwanasiasa mmoja Wakiiraq barabarani Baghdad mwaka 1962 siku hizo hakuna aliyekuwa akijua kwamba Saddam atakuja kuwa Rais wa Iraq na siasa zake za kibabe. Saddam akijificha kwa woga katika vikona vya chuo kikuu cha Cairo na alikuwa akisomea sheria.

Siasa za Nasser ziliwaambukiza wengi kwa hakika, kuna mengi yanayostahiki kuandikwa kumsifu Nasser, na kuna mengi yanapaswa kusemwa kumbomoa, moja ya yanayopaswa kusemwa ni kwamba Nasser alipofariki mwaka 1970 nchi nyingi za Kiarabu zilikuwa zikitawaliwa kimabavu kama yeye alivyokuwa akitawala, tukiacha udhaifu huo ambao uliigharimu pakubwa jamii ya Misri,hamna shaka yeyote kwamba Nasser ailkuwa kiongozi shupavu aliyewavutia wengi barani Afrika, mshirika mkuu wa Nasser kusini mwa jangwa la sahara alikuwa Kwame Nkrumah, Rais wa Ghana walikuwa na msimamo mmoja kuhusu mustakabali wa Afrika, Nasser pia alikuwa na uhusiano mzuri na Mwalimu Julius Nyerere aliyekuwa Rais wa Tanzania.

Nasser alikuwa akijituma sana kisiasa aliugua kisukari pamoja na shindikizo la damu na tangu mwaka 1967 aliapata mishtuko ya moyo mara kwa mara madaktari wake walimuamrisha apunguze kazi lakini hakuwasikiliza, Tarehe 27 Sep mwaka 1970 akiwa na hali dhaifu ya afya na mchovu Nasser aliwaita baadhi ya viongozi wa Wakiarabu mjini Cairo katika juhudi za kumpatanisha Mfalme Hussein wa Jordan na yasser Arafat ambao wakati huo walikuwa kama paka na chui...


Tutaendelea na duru za siasa, Nguruvi3, Mkandara, Kimbunga, Jasusi, Ngongo, JokaKuu, chama.
 
Mkuu Ritz kuna wakati ulikuwa ukizungumzia siasa za mashariki ya kati ukijikita zaidi na siasa za Misri,leo nimesikia Rais Morsi kamtimua mkuu wa majeshi General Tantawi kabla ya hapo alimtimua mkuu wa usalama.Nadhani hizi harakati za Rais Morsi ni jitihada zake za kulidhibiti jeshi la Misri ambalo kwa muda mrefu limekuwa likitawala siasa za Misri.
 
Mkuu Ngongo,
Hapa katikati kulikuwa na mnakasha mkubwa wadau wa duru za siasa wakashauri tuzame kwanza kwenye mada moja.

Ni kweli Rais Mohammed Morsi ametangaza kuwa amemvua madaraka Waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Jeshi Field Marshal Hussein Tantawi pamoja na naibu wake, Rais pia amesema anafuta mabadiliko yote yaliolipa jeshi madaraka zaidi.

Rais Morsi amefanya hayo mabadiliko yasiyotarajiwa kuhusu majenerali wawili wakuu wa Misri, Field Marshal Tantawi, ambaye alishika madaraka ya uongozi baada Rais Hosn Mubarak kuondoshwa madarakani analazimishwa kustaafu pamoja na naibu wake, Waziri mpya wa Ulinzi ni Jenarali Abdel Fatta, Rais Morsi pia amefuta mabadiliko ya katiba yaliyotangazwa na jeshi wakati wa uchaguzi wa Rais.
 
Ngongo

Hao aliowafukuza walikuwa ni powerful kuliko yeye, kwahiyo anataka yeye ndo awe "top dog",hopefully watamove forward bila kuanza kuwindana tena.Toka walipomu assasinate yule Anwar Al Sadaat,rais huwa lazima awe kama yuko chini ya jeshi,sasa naona wanataka kubadili na kurudisha ile mantiki ya kwamba amiri jeshi mkuu ni yule aliyechaguliwa na civilians na kwamba the buck stops with him...
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Ritz Mkandara Nguruvi3 jmushi1 JingalaFalsafa na wengine wote tunaopenda kutembelea Duru za siasa nilikuwa na ombi moja awali tulikuwa tumekubaliana tuzame kwenye mada moja lakini kuna issues nzito zinajitokeza nje ya mada iliyokubaliwa kama mabadiliko ya wakuu wa majeshi nchini Misri si vibaya tukayajadili yakiwa bado ya moto moto.

Naomba kuwasilisha.
 
Kama nilivyoandika katika duru za siasa (core),nimepata usuli kidogo kuhusu sehemu ya matukio yanayojiri ili kuepeuka kuingilia mada endelevu na kuwa na mtiriiko mwanana. Kwa wengine ambao sikupata usuli basi tuchukulie kama tumekubaliana. Hata hivyo bado maoni ya kuboresha yanakaribishwa

Napenda kuwaalika wote katika duru za siasa matukio kwa utaratibu wetu wa kupingana bila kupigana, hoja kwa hoja na kwa stara inayokubalika.Maoni yaheshimiwe hata kama hatukubaliani nayo.

TUZIANGALIE SIASA ZA MASHARIKI YA KATI NA MAREKANI
Kama tulivyowahi kusema siku za nyuma, huko Misri bado hali haijatulia na juzi tu Rais Morsi amemtimua kazi Field Marshal Tantawi na mwenzake. Tukio hili limefuatilia mauaji ya askari wa Misri katika eneo la Sinai ambalo lina mpaka na Israel. Mauji yalikuwa ya askari 16 na hadi sasa hakuna anayejua kiini au chagizo la mauaji (motive)

Hali hiyo ililazimu mpaka wa Israel na Misri (Rafah) kufungwa na hadi sasa bado kuna sintofahamu eeo hilo.
Uamuzi wa Morsi kuwatimua majemadari ni sehemu ya mikakati ya Brotherhood kumiliki utawala wa nchi.
Ikumbukwe kuwa jeshi la Misri lilikuwa na nguvu kumzidi Rais kwa baadhi ya mambo.
Wakati wa Mubarak hilo halikuwa tatizo sana kwasababu yeye mwenyewe alikuwa mwanajeshi.

Jeshi limepanga kukataa rufaa kwenye mahakama ya katiba. Inavyoonekana ni dhahiri wanajeshi hawataki kurudi kambini wakati huo huo Morsi hayupo tayari kuendesha nchi wakiwa na nguvu zaidi yake.
Haya ya jeshi kuwa na nguvu tumeyaona pia Turkey ambako nguvu ya Rais ndani ya jeshi ina ukomo.

Kitu kimoja cha kujifunza ni jinsi hawa Brotherhood walivyo na subra, haikuonekana kama hilo ni tatizo hapo awali kwani licha ya misuguano na akina Tantawi wakati wa kuapishwa Morsi alionekana kukubaliana nao.
Siku zote husema Brotherhood ni werevu sana na wenye subra. Mathalani sasa hivi hawaonekani kuwa na tatizo na Israel, trust me ni suala la muda hata kama ni miaka 10 ijayo lazima watafanya wanachokusudia.

HUKO MAREKANI
Kampeni za uchaguzi zinapamba moto hasa baada ya Romney kupata mgombea mwenza Paul Ryan.
Ryan ni mshiriki wa kundi la tea party na uteuliwa wake umeonekana kama kuthamini mchango wa tea party.
Faida kubwa ni kuungwa mkono na tea party ambao ni machachari sana katika uhamasishaji.
Tutakumbuka uchaguzi wa kati kati ya muhula mwaka jana (midterm election) hawa Tea party waliongoza mashambuli yalipoteza wabunge wengi wa Democrat.

Faida ya pili ni Ryan kuwa mjumbe wa kamati ya fedha na bajeti ya bunge la Marekani. Hiyo inampa uzooefu katika mambo ya bajeti. Tumeona anavyosimama kidete katika Medcare Kwa upande mmoja akimsadia Romney.
Ryan anapendwa tu kwa haiba (charisma) kitu kinachoondoa utando wa tabia ya ujeuri na undava (Arrogance ) ya Romney.

Kwa upande mwingine ujio wa Ryan umewaamsha Democrat ambao walidhani mambo yametulia.
Kilichowaamsha zaidi ni kuona kuwa Ryan wa Tea party ameingia na kama inavyojulikana Tea party inahusishwa sana na ubaguzi wa rangi na wanachama wake wengi ni weupe.

Hiyo ni hasara ya ujio wa Ryan kwasababu kura za blacks na Latino zinaweza kuota mbawa.
Kitakachoamua sasa ni kura za majimbo yanayobadilika (swing state).

Kwa upande mwingine ujio wa Ryan umeonekana kumfunika Romney kihaiba na kisera. Na kwa bahati mbaya sera za Romney na Ryan kuna wakati zinakinzana. Inapofuatiliwa historia ni wazi kuwa watakuwa na wakati mgumu wa kujibu baadhi ya hoja kama timu. Kampeni ni changa na tutaendelea kadri itakavyojuzu.
 
Asante sana Nguruvi3 kwa kuboresha duru za siasa, kwa sisi wanafunzi nadhani tutajifunza vizuri zaidi kwa kufuatilia mtiririko uliotulia.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ritz, suala lako tunalifanyia kazi na tunatumaini Invisible atasaidia. Shukran
 
Mkuu Ritz, suala lako tunalifanyia kazi na tunatumaini Invisible atasaidia. Shukran

Mkuu Nguruvi3,
Tunashukuru nadhani Mkuu Ngongo, pia anasubiri kwa hamu kuna matukio mengi tutayabandika humu kwenye Duru za siasa (matukio)..
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Ritz na Nguruvi3 jana mbunge wa Igunga kavuliwa ubunge na mahakama, na hii huenda ikapelekea uchaguzi mdogo jimboni humo. Kwa mtazamo wangu naona tunajiingiza wenyewe katika gharama zisizo za lazima, ni wakati muafaka wa katiba kuangalia hii ishu. Sina utaalamu sana na haya mambo ya demokrasia, je haiwezekani kuwekwa katika katiba kifungu kuwa anayeshika nafasi ya pili achukue nafasi pale inapotokea kesi kama hii??
 
Last edited by a moderator:
Wakuu na wadau,

Nadhani tumejitahidi sana kufanya mabadiliko tuliyoahidi. Ni kazi kuhamishapost zote kwa namna kila mmoja angependelea na tulifanya utaratibu ili ule mtitiriko uwe sahihi. Niwashukuru sana Maxence Melo na Invisible kwa kulifutailia suala letu kwa ukaribu. Utaratibu wetu wa kukubaliana au kukubaliana kutokubaliana unaendelea.
 
Wakuu Ritz na Nguruvi3 jana mbunge wa Igunga kavuliwa ubunge na mahakama, na hii huenda ikapelekea uchaguzi mdogo jimboni humo. Kwa mtazamo wangu naona tunajiingiza wenyewe katika gharama zisizo za lazima, ni wakati muafaka wa katiba kuangalia hii ishu. Sina utaalamu sana na haya mambo ya demokrasia, je haiwezekani kuwekwa katika katiba kifungu kuwa anayeshika nafasi ya pili achukue nafasi pale inapotokea kesi kama hii??
Katavi ni kweli kabisa unayoyasema. Tatizo ni kuwa utaratibu upi utumike ili kuhakikisha usalama wa kila mmoja wetu.
Kwa siasa za nchi yetu watu wanaweza kufanyiana hiana ili tu mtu aende mjengoni. Tunaweza sikia more of Mabwepande and the likes.

Mimi nadhani suala hilo lingefanya kuwa chama kilichoshinda ndicho kipewe dhamana ya kuchagua mbunge mwingine kwa ushindani within the party. Yaani uchaguzi wa chama na si kama ilivyo kwa viti maalumu kuteua the next.
Hapa pia ni tricky kwasababu mtu wa pili anaweza ku-mabwepande hivyo ni muhimu kuwa na chaguzi ndani ya chama
 
KIFO CHA ZENAWI
Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi amefariki jumanne wiki hii. Zenawi amekuwepo madarakani kwa takribani miaka 20.Maisha yake kisiasa ni ya kutatanisha kwasababu huwezi kumweka katika kundi moja na ukamuelezea.

Pamoja na kuwa inaonekana kuwa mtawala wa kidemokrasia, ukweli unabaki kuwa demokrasia yake ilikuwa na mkono wa nchi za magharibi. Kwa maneno mengine alitumika kisiasa.

Kwa mfano, baada ya kuwepo vita nchini somalia, makundi yanayohasimiana yalikubaliana kuunda serikali ya umoja iliyokuwa chini ya sheria za kiislam. Kundi hilo lilionekana kuwa na wafuasi wengi wa Alshabaab. Ukweli ni kuwa serikali hiyo ilirejesha amani Mogadishu kwa muda fulani kwasababu iliweza kuvunja nguvu za makundi ya koo na kikabila.

Nchi za magharibi hazikupendezwa kwa hoja ya kuwa hiyo ilikuwa kulea Alshaabab, lakini pia hazikuwa tayari kurudi somalia kwa kumbu kumbu ya Black Hawk nyakati za jenerali Collin Powell.

Nchi za magharibi zikatoa pesa kwa Zenawi ili aanzishe vita isiyokuwa yake na alifanya hivyo.
Zenawi amebaki kuwa msumbufu wa amani ya Somalia ili mradi tu kile kinachotakiwa na magaharibi kitimie.
Ethiopia imekuwa inapokea zaidi ya dolla bilioni 1 kama msaada kutoka magharibi.

Kwa upande mwingine Zenawi amekuwa ni rafiki mkubwa sana wa China ambao wanawekeza katika nyanja mbali mbali.
Hilo tu linamfanya awe na pande mbili 'double standard' ndiyo maana tunasema hakueleka kwa uhalisia.

Pamoja na hayo Zenawi amejitahidi kutumia misaada vizuri ilkiwa ni pamoja na mradi mkubwa sana wa umwagiliaji na umeme kwa kutumia sehemu ya mto Nile. Amefanikiwa kuifanya Ethiopia iwe stable kwa kiasi fulani ingawa pia ni mwepesi kutumia FFU kuzima demokrasia.

Wasi wasi uliotanda ni jinsi gani nchi itatawalika baada ya Zenawi. Wapo wanaodai hali inaweza kuwa kama ya Iraq ambapo mkono wa chuma ndio uliokuwa sahihi kuiweka nchi sawa.
Nini kinafuta baada ya Zenawi bado ni kitendawili

Tusemezane
 
Back
Top Bottom