Duniani kuna mambo soma hii!!!

kiparah

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,173
114
Mke anayependa sana ngono amfanya mumewe akimbilie polisi

ISTANBUL, Uturuki
MWANAUME mmoja raia wa Uturuki anayeishi nchini Ujerumani amelazimika kukimbilia polisi kuomba msaada baada ya kushindwa kumvumilia mkewe anayedai haki yake ya kupewa unyumba kila wakati bila ya kumpa mwanaume huyo muda wa kupumzika.

Mwanaume huyo ambaye jina lake limewekwa kapuni, alikimbilia kituo cha polisi kuomba msaada baada ya kushindwa kuyatimiza mahitaji ya kimapenzi ya mkewe wa ndoa yao iliyodumu miaka 18 na kuzaa naye watoto wawili.

Mwanaume huyo aliwaambia polisi kuwa mkewe kila wakati anataka uroda akidai ni haki yake ya msingi kupewa unyumba kila anapojisikia.

Mwanaume huyo alikimbilia kwenye kituo kimoja cha polisi kusini magharibi mwa Ujerumani akisema kuwa kwa miaka minne iliyopita amelazimika kulala sebuleni kumkimbia mkewe chumbani ili angalau aweze kupata muda wa kupumzika.

Mwanaume huyo aliongeza kuwa hata hivyo, mkewe amekuwa akimfuata sebuleni akidai unyumba na kumfanya akose usingizi kutokana na kero kubwa ya kumpa unyumba mkewe kila wakati.

Mwanaume huyo aliwaomba polisi watafute njia ya kumsaidia ili aweze kupata usingizi wa kutosha usiku ili aweze kwenda kazini asubuhi bila ya uchovu mwingi.

"Sasa ameamua kumpa talaka mkewe ili aweze kuendelea na maisha yake na angalau aweze kupata muda wa kupumzika na kwenda kazini mapema asubuhi akiwa fiti bila ya uchovu," ilisema taarifa ya polisi.


SOURCE: Yahoo-news.
 
kama vipi akubali ndoa yao iwe ya watu watatu aongeze kifaa kipya damu changu ya kiume mzigoni wapange roster..
 
haya kutakuwa na sababu tena ya nyumba ndogo?kama mchezo,bwana hauwezi tena.jamani huyo bwana nae hana sauti mpaka akashtaki polisi? kwa kweli inashangaza
 
Back
Top Bottom