Dunia tuliyo nayo leo haukuwa mpango wa Mungu!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Sisi kama binadamu tunajipenda na hakuna awezaye kulizuia jambo hili. Lakini kujipenda kwa ziada kunaweza kuzuilika kama mtu ataamua. Kujipenda kwa ziada ndiko ambako kunapelekea dunia kuwa kama ilivyo leo kwa upande wa uharibifu. Yale yote ambayo hayakwenda sawa kufuatana na mpango wa mungu, yamesababishwa na uziada wa kujipenda kwa binadamu. Mpango wa mungu ni kuwa na dunia ambayo haina makovu wala vidonda.

Lakini leo hii, dunia hii tunamoishi imejaa vidonda na makovu zaidi kuliko uzima. Vidonda na makovu haya kama ambavyo nimesema ni matokeo ya binadamu kujipenda kupita kiasi. Kujipenda huku kunamfanya adhani kwamba yeye anastahili zaidi kuliko mwingine na kumemfanya awe pia mvivu wa kufikiri..

Labda nikumbushe kwamba binadamu hawi binadamu kwa sababu ana magari makubwa na madogo mia moja yenye thamani au ana nyumba za kifahari mji mzima, au ana akaunti zenye vijisenti huko ghaibuni, lakini pia hawi binadamu kwa sababu anashinda na njaa au anatembea makalio yakiwa nje kwa ukosefu. Binadamu anakuwa binadamu kwa sababu kuna sifa ambazo hupatikana kwake na kwa mwingine bila kujali huyo mwingine yukoje kimwili au kihali.

Kushindwa huku ndiko ambako huwafanya binadamu kuwapa wenzao kile ambacho kama wangepewa wao kungezuka balaa kubwa. Binadamu wamejaribu kuridhisha miili yao na pengine nafsi, kama sio tamaa zao kwa kuwafanyia wengine lile ambalo kwao lingekuwa ni gumu sana kulivumilia.

Kuna wale ambao kutokana na tamaa na kutojitosha wameshiriki katika vitendo vya ufisadi na kujichotea mabilioni ya shilingi huku wakiwaacha binadamu wenzao wakihangaika kwa kukosa huduma muhimu, ambapo hizo fedha zingesaidia kuboresha huduma za afya, miundo mbinu, elimu na Nishati.

Kuna wale ambao kwa matumizi ya vyeo vyao huwakosesha wengine haki zao kwa sababu tu wengine hao hawana nguvu na uwezo wa kupambana nao. Hawa kwa makusudi huwafanya watu wengi kuishi katika ulitima wa kudumu wakati wangeweza kuinuka na kuishi kama wao.

Kuna kundi kubwa la binadamu ambalo kamwe halijawahi kufanya jema kwa wengine. Halijawahi kutamka jema kwa wengine na halijawahi kufikiri jema kwa wengine. Kundi hili lina watu ambao wao kila siku wanafikiria ni kwa namna gani watatumia ujinga wa wengine kwa manufaa yao. Hutumia ujinga wa wengine kwa kujipatia ziada na “kutanua” huku wengine hao wakiporomoka na kuingia kwenye shimo la kiza cha ulitima.

Imefika wakati ambapo inabidi kuheshimu ubinadamu katika ujumla wake. Inabidi tujue kwamba kinachotufanya tusimame leo na kujidai, kujivuna na kujiona tu bora sana ni kwa sababu kuna binadamu wengine wanaotuzunguka. Kinachotufanya leo hii tutamani kuonekana wakubwa zaidi, wenye uwezo zaidi, wenye heshima zaidi, ni kuwepo kwa biandamu wengine, Kwa hiyo sisi sio binadamu hata kidogo kama tunavyodhani, bila binadamu wengine kuwepo.

Mbaya zaidi ni kwamba sisi siyo binadamu kamili kama wenzetu siyo kamili. Ukamilifu wao ndio unaotupa sisi ukamilifu. Ukitaka kuthibitisha jambo hili ni rahisi sana.Hebu anza sasa kutenda yale ambayo hata wewe ungependa kutendewa na kuacha kuwatendea wengine yale ambayo hata wewe usingependa kutendewa. Nina imani baada ya muda fulani utagundua ukweli fulani.

 
Nafikiri pia tunateswa na mfumo wa kimadaraja.
Kwamba mmoja ni mtawala wa mwingine na hivyo kuondoa dhana ya usawa. Hakuna usawa ila tulicho nacho ni haki ya ushiriki sawa ambayo nayo ni shida kutekelezwa kwa sababu ya ubinafsi.
 
tunasubiri vita ya tatu ya dunia itakayohusisha silaha nzito za maangamizi mazito,
tunasubiri super volcano itakayorusha vumbi mpaka juu ya mawingu na kuziba hewa inayotusaidia kupumua
wakuu yanakuja hayo .
 
Back
Top Bottom