MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,752
- 5,497
???????
Swali hili ni Muhimu sana hasa dunia ya leo maana limeigawa katika vipande viwili ambavyo havina ukaribu wala ufanano hata chembe.
1:Wanaoamini Dunia iliumbwa(Creationists) - Dunia ina umri wa miaka takribani 6000 (maelfu).Pia kunadhana ndogondogo zinazoendana na hii.
2:Wanaoamini Dunia iliibuka (Evolutionists) - Dunia iliibuka Takribani miaka Bilioni 4.6 na maisha kuanza miaka Billioni 3.5 iliyopita.Pia kuna dhana takribani saba za uibukaji.
Haya ndio Matokeo ya Hii mitazamo miwili.
1: Kama dunia ni changa (Miaka kama 6000) Basi Dhana ya uibukaji EVOLUTION inakufa hapohapo. Somo kwamba tulitokana na Sokwe linafia hapo hapo.
2: Kama Dunia imezeeka na inaumri wa miaka Billioni 4.6 basi, Dunia haikuumbwa na chochote kuhusu uumbaji ni stori zisizo sawa. Na ikumbukwe bila tukio hili ktuokea kwa mabillioni ya miaka tena kidogo kidogo hii dhana inakufa rasmi.
Vipimo Vya miaka.
1: EVOLUTION; Hapa wanatumia Carbon dating au Radiometric Dating (Ni njia ambazo ili zifanye kazi inabidi ujumuishe na MAKISIO/ASSUMPTIONS), Yawezekana kuna mengi zaidi pia.
2:CREATION; Hapa inatumika Umri wa watu hasa waliozaliwa baada ya adam,Historia,Utafiti na nyaraka za kale na kwenda hadi kufika leo tulipo.Yawezekana kuna mengi zaidi pia
Karibuni kwa changamoto fikirishi,
always am a Winner Kiranga gasgas Nyani Ngabu CHARMILTON tejateja Apollo Iceman 3D UHURU JR Kikwajuni One Behaviourist Stefano Mtangoo Hb wa Ilala Kahtan Ahmed Vivax Warrior faiz MALCOM LUMUMBA na wengine wengi...
Dondosha hapa chochote unachoamini au kujua kuhusu haya mawili. Ninaamini hakuna ambaye yuko pande zote mbili kwani hazichangamani.
Ukitoa na reference, illustrations, Quotes, links, chochote kile Kumtetea Adam au Homosapiens na makazi yake tutashukuru