Dunia haiishi vituko ebu sikia njia hii rahisi ya kumnasa mke anayetoka nje ya ndoa!

Kingcobra

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,000
309
Ndg zangu,

Sina maelezo ya kisayansi lakini kuna news nimezipata kutoka maeneo ya Kyela namna wanaume wanavyowadhibit wake zao wasitoke nje ya ndoa na kula uroda na wanaume wengine. Eti teknolojia hii inatumika sana kwenye kijiji kimoja kipo karibu na mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira. Wanaume wengi wa kijiji hicho wana visu vyenye ala au mfuniko unaotunza upande wa makali. Inapotokea mume anaondoka kwa safari au matembezi ya kawaida, humwita mkewe na kumwambia ashike kisu upande wa mfuniko kisha yeye huvuta kisu na kukichomoa na kumwachia mkewe ameshika mfuniko. Baada ya hapo, mwanaume humuaga mkewe na kuondoka zake kwenda safari au matembezini. Kinachotokea hapo ni kwamba mke akitoka nje ya ndoa lazima atashikwa. Eti yule 'mdudu' wa mwanaume mwizi atang'ang'ania ndani mpaka mwenye mali aingilie kati ndipo atoke. Eti imefika mahali tabia ya wana ndoa kutoka nje, imekufa kabisa kwani familia zaidi ya tano zilikumbwa na kisa hicho. Jamani wadau mmewahi kuisikia hiyo???
 
Hiyo niliwahi kusikia maeneo ya Tanga na moja ilitokea hapa Arusha lakini sina uhakika maana naona kama ni la kiimani zaidi
 
vya kawaida hivyo haa musoma ilishatokea ni kwel ukicheza ina kula kwako
 
hahahhahahahhahhaha loooool kweli dunia haishi vioja,,kwahiyo kama safari mume wangu enda kaa wiki mbili???? hahhaha spati picha lool mwagandana tuu hahahah hivi ni vichekesho jamani au kwelii???
 
Ni mchezo wa kudhalilishana, km kutoka nje keshatoka, kagongwa km kawa. Huo mchezo cjaupenda, upo kishirikina!
 
Nimesikia lkn si nzuri! Miaka ya nyuma iliwahi tokea maeneo ya Msimbazi Center! Jamaa walinasana kwa muda wa zaidi ya saa 10. Sio vzr kwa kweli. Bora umwache kuliko kumfanyia mwenzio upuuzi huu
 
haka kamchezo ako vizuri sana maana katasaidia kumkamata mwizi ila pia kwa upande mwingine it's a humiliation situation.......... kula tunda watakuwa wameishakula sasa unakamata nini?
 
Huu mchezo upo sana, nimewahi kuusikia miaka ile ya Tisini mwishoni ilitokea hukohuko Mbeya....
Huu ni udhalilishaji kwa kweli.......lakini ni nzuri kwa kuwa ni funzo kwa wezi wa wake za watu..
 
Acha watumie kukomoana!Sasa hapo sijui huyo mwenye mke akirudi atamchukua mke wake si la maana hapo ni sawa Na kujiambukiza aibu!!
 
Acha watumie kukomoana!Sasa hapo sijui huyo mwenye mke akirudi atamchukua mke wake si la maana hapo ni sawa Na kujiambukiza aibu!!
Akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na la kulia
Dawa ya moto ni moto
Ukimwaga mboga namwaga ugali
 
na ikitokea huyo mume kufariki ajalini na kisu kupotea itakuwa vipi? kwa mawazo yangu, siku waswahili tutakapoachana na imani za kishirikina tutafanikiwa sana kwenye mambo yetu mengi. hata kuvuana magamba tutaweza bila hofu!
 
mambo wadau kuhusu hiyo issue ina ukweli kabisa iliwah kutokea live kabisa at that time nipo mby na nikashuhudia vitu viliumana live wakatoka kyela wakiwa ivyo ivyo na kuja hosptal ya rufaa mby mjin watalaamu wa hosptal wakashindwa tena kibaya zaid walikuwa mke wa mtu na mume wa mtu mpka pale alipotokea yule mume akatoa kisu kny alert yake nao wakaachana live
 
Afrodenzi...nimependa macho yako-a well focused and single ending mind.
Could you please allow me to make a journey through your mind and find the source of this impression?
 
Ndg zangu,

Sina maelezo ya kisayansi lakini kuna news nimezipata kutoka maeneo ya Kyela namna wanaume wanavyowadhibit wake zao wasitoke nje ya ndoa na kula uroda na wanaume wengine. Eti teknolojia hii inatumika sana kwenye kijiji kimoja kipo karibu na mgodi wa makaa ya mawe wa kiwira. Wanaume wengi wa kijiji hicho wana visu vyenye ala au mfuniko unaotunza upande wa makali. Inapotokea mume anaondoka kwa safari au matembezi ya kawaida, humwita mkewe na kumwambia ashike kisu upande wa mfuniko kisha yeye huvuta kisu na kukichomoa na kumwachia mkewe ameshika mfuniko. Baada ya hapo, mwanaume humuaga mkewe na kuondoka zake kwenda safari au matembezini. Kinachotokea hapo ni kwamba mke akitoka nje ya ndoa lazima atashikwa. Eti yule 'mdudu' wa mwanaume mwizi atang'ang'ania ndani mpaka mwenye mali aingilie kati ndipo atoke. Eti imefika mahali tabia ya wana ndoa kutoka nje, imekufa kabisa kwani familia zaidi ya tano zilikumbwa na kisa hicho. Jamani wadau mmewahi kuisikia hiyo???

Thank you for sharing... Mmmmh inapendeza....
 
Back
Top Bottom