Duni Haji mgombea mwenza wa Lipumba awa waziri wa Afya Zanzibar

eliesikia

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
787
755
Hivi hawa CUF ni CHADEMA au CCM walipaswa kuunda nao kambi huyu???
Mgombea mwenza wake kawa waziri wa Afya kule Zanzibar kwa kweli sielewi wanataka nini kwenye kambi ya upinzani...
Mimi nimejaribu kangalia picha kipindi kile kabisa cha enzi za mzee ruksa kwa kweli alipendeza kuasi haikuwa haki yake kabisa... chama tawala cha CUF kipo juu sana kiunde kambi tawala na CCM huku bara tujue moja sio kung´ang´ania tuu upinzani ili hali wao ni watawala.... lipumba ni CCM.jpg
 
Masikini Lipumba, wapambe wenzake wamemegewa mlo (Seif Makamo wa I na Duni Waziri wa Afya. Wamemwacha solemba. Pengine kabla ya 2015 atatambua wapi pa kujiunga baada ya kung'ang'ania CUF ambao tayari imekuwa CCM B
 
subirini baraza jipya la mawaziri au wateule wa jeikei muone sarakasi zinavyoendelea.
nadhani watanzania wanazidi kufumbuka macho yao kuona who is who kwenye siasa za bongo.
 
Masikini Lipumba, wapambe wenzake wamemegewa mlo (Seif Makamo wa I na Duni Waziri wa Afya. Wamemwacha solemba. Pengine kabla ya 2015 atatambua wapi pa kujiunga baada ya kung'ang'ania CUF ambao tayari imekuwa CCM B

Lipumba hajaachwa solemba , atateuliwa na JK viti maalumu then uwaziri kuidhinisha muungano wao unaojionyesha sasa bungeni:rip:cuf
 
Ndoa ya KAFU na THITHIEM iliongelewa mapema sana na wachambuzi wa mambo kabla hata ya kuanza kwa pilikapilika za uchaguzi. Watanzania makini watakuwa wametambua dalili za ndoa hiyo. Hata kwenye bunge la jamhuri dalili zipo wazi. Baadhi wameanza kumcheka Prof. Lipumba kuwa ameachwa solemba na akina Seif na Duni. Ukweli ni kuwa wanaombeza Prof. Lipumba watashangaa watakaposikia ni mbunge wa kuteuliwa na jk. Nchi hii jamani acheni tu!
 
Back
Top Bottom