Shimba ya Buyenze
JF-Expert Member
- Dec 22, 2014
- 178,203
- 1,077,385
Angalau umejitahidi kuwafufua katika andiko lako. Historia huamuliwa na wenye madaraka ndiyo maana historia rasmi iliyochekechwa na kurasmishwa na tabaka tawala mara nyingi usahihi wake hutiliwa shaka; na karibu duniani kote lazima utakuta kundi la watu likilalamika kuwa historia yao imepotoshwa na hata kufishwa kwa makusudi. Sijakisoma kitabu chako na hivyo sijui hoja zako kuhusu kusahaulika kwao kwenye historia rasmi ya taifa letu lakini naweza kubashiri pengine ni sababu ya dini yao; na hata elimu na migongano nafsiya kati yao na Mwalimu.Shimba...
Nadhani Dully anachokusudia ni babu zake hao wawili kusahaulika na mamlaka
ambazo zilistahili kuwaenzi.
Kitabu nilichoandika cha maisha ya Abdul Sykes hakiondoi dhima ya mashujaa
hawa kupewa hadhi wanayostaili katika kuwaleta wananchi wa Tanganyika kuwa
pamoja kwanza katika African Association ambacho kilianzishwa na babu yake
mkuu Dulliy, Kleist Sykes na kisha katika TANU chama walichoasisi babu zake
hao wawili, Abdulwahid na Ally Sykes.
Ni kweli walisahaulika hii inafahamika kiasi siku Nyerere alipomtaja Abdul Sykes
Diamond Jubilee Hall wakati anaaga alisema hakumbuki Abdul alikuwa na cheo
gani katika TAA.
Hizi ndizo siasa zetu za Afrika.
Kuandika vitabu na kujaribu kuinyoosha historia ndiyo njia sahihi hasa kukifanywa kwa kutoegemea chuki za kidini, kikabila na kiitikadi. Umewafanyia jambo jema!