Dully Sykes: Hawa wamesahaullika?

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,216
7,907
472334ce9e642d46542d71c350d4c7f8.jpg

bbc3ab9808e529e198f28b7e431f2182.jpg
 
Labda mwanamuziki Dully anataka iwepo siku ya mapumziko, yaani taifa lisifanye kazi kama vile Karume Day na Nyerere Day. Lakini yeye si mwanamuziki?, si anacho kipaji cha utunzi?.

Kwanini asiwatungie nyimbo maalum ili kupitia mashairi na ubora wa muziki, waweze kuendelea kukumbukwa.

Stevie Wonder na wanamuziki wa Marekani walimtungia nyimbo Barack Obama, anaweza kuiga mtindo huo wa kuenzi wapigania uhuru.
 
Ila Nyerere alikuwa mjanja sana, mlimkaribisha baadaye akawageuka.
Najua mtakimbilia kumlaumu Nyerere kwa kila kitu.

Kama nilimsikia vizuri Nyerere kwa maneno yake ni kuwa alitaka kuanzisha chama akiwa Makerere lakini wakamtumia barua kuwa kwa nini asije tu kuunganisha nguvu kwa chama kilichopo huku (Tanzania/Dar es Salaam)

Na alipotia timu Dar es Salaam hao waanzilishi wenyewe walisalimu amri kwa kijana wa Kizanaki ambaye hata Kiswahili chake kilikuwa sio imara lakini na bado walilazimika kumkabidhi mikoba.

Nyerere alikuwa na kipaji special kwamba hata kama angeamua kuanzisha harakati zake mwenyewe pembeni Watu wangemuelewa yeye zaidi kuliko hata hao waliokuwa wamemtangulia.
 
Wakumbukwe kivipi au wawekwe kwenye wimbo wa taifa? Mchango wa kila aliyesaidia harakati za uhuru ni wa thaman kuu na wote hukumbukwa siku ya mashujaa.
 
Huyu anajipigia promo.
Hawapo kwa hiyo mpewe ninyi?
Hawakukuita kwenye kampeni?
Pole !!
 
Sheikh mkuu na mwanazuoni mashuhuri wa Kiislamu Mzee Mohammed Said ameshawaandikia kitabu. Sasa wamesahaulika kivipi?

Walizidiwa kete na Mzanaki ama? Butiama Baby!
Shimba...
Nadhani Dully anachokusudia ni babu zake hao wawili kusahaulika na mamlaka
ambazo zilistahili kuwaenzi.

Kitabu nilichoandika cha maisha ya Abdul Sykes hakiondoi dhima ya mashujaa
hawa kupewa hadhi wanayostaili katika kuwaleta wananchi wa Tanganyika kuwa
pamoja kwanza katika African Association ambacho kilianzishwa na babu yake
mkuu Dulliy, Kleist Sykes na kisha katika TANU chama walichoasisi babu zake
hao wawili, Abdulwahid na Ally Sykes.

Ni kweli walisahaulika hii inafahamika kiasi siku Nyerere alipomtaja Abdul Sykes
Diamond Jubilee Hall wakati anaaga alisema hakumbuki Abdul alikuwa na cheo
gani katika TAA.

Hizi ndizo siasa zetu za Afrika.
 


Sina hakika Dully Sykes ana maana gani...ila ni kweli akina Sykes walitoa mchango mkubwa katika kupatikana uhuru wa nchi hii...baadhi yetu wakati tunakua katika miaka ya 70 tulikuwa tunawasikia sana akina Sykes kuhusu michango yao kwenye harakati za uhuru...kuna mwingine pia ambaye naye alitoa mchango mkubwa kwa taifa hili...mzee Rupia...Ila kuhusu kusahaulika watu hawa sijui huyu dogo Dully ana maana gani...labda anataka wajengewe mnara, au?????
 
Historia ya kweli inapotezewa sana hasa ambayo haiwapendezi ccm.
Ila sheikh wetu mzee Mohamed ameandika kitabu kuhusu sykes' sasa sijui kama Dully kakipitia au la hasha..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom